Saturday, 23 January 2021
Unaitumikia fedha au fedha inakutumikia?
*Je maisha yako yanaweza kwenda kama kawaida hata kama hutafanya kazi moja kwa moja?*
Rafiki yangu maswali ni njia nzuri sana ya kujifanyia tathimini,karibu ujifunze ili fedha akawe mtumwa kwako na kukufanyia kazi......
Kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba kuna siku hutaweza kufanya kazi ili upate fedha kama sasa,pengine kwasababu ya uzee au ulemavu wa viungo ambavyo leo unavyo lakini kesho hutakua navyo kwasababu kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.Hapo ndio unahitaji kuanza maandalizi ya fedha kuwa mtumwa wako.
Njia pekee ya kuweza kuifanya pesa kutufanyia kazi ni kuitumia fedha unayopata sasa kama mbegu kwa kuiwekeza.
Uwekezaji ni pale fedha unayoipata inapokufanyia kazi badala ya wewe kuifanyia kazi kama unavyofanya sasa.
Rafiki utakua shaidi kwamba asilimia kubwa ya wastafu hufa mapema baada ya kustafu kwasababu nguvu za kufanya kazi hawana na pesa zinakua haziwezi kukidhi mahitaji yao,hivyo kama hutojifunza sasa namma ya kuwekeza jiandae kwa maisha ya mateso wakati nguvu na uwezo wa kufanya kazi utakua huna.
Faida nyingine ya uwekezaji unaipata kwa kustafu kazi ya kuajiriwa na kujiajiri kabla ya umri wa kisheria wa kustafu haujafika.
Ninafahamu nikitaja neno uwekezaji unawaza mamilioni ya fedha lakini ukisoma kitabu cha *elimu ya msingi kuhusu fedha* jambo la msingi kwenye uwekezaji ni KUANZA MAPEMA NA KUWEKEZA KILA WAKATI.
Angalia wafanyakazi wanapolipwa mafao yao baada ya kustafu,lakini fedha hiyo ni kidogo ukilinganisha na namna ilivyowekezwa na kuzalishwa.
Rafiki kwa leo ni hayo nenda kayafanyie kazi.
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Subscribe to:
Comments (Atom)