Sunday, 29 March 2020

Tatizo lako siyo tatizo, bali hujuwi tatizo ni nini?....



Rafiki yangu habari za wakati huu, Nina hakika kwa wiki nzima umetatua mambo mengi na umesababisha mengi yanayo Fanya dunia yetu kuwa sehemu bora sana ya kuishi, na hii ndio maana ya wewe kuishi, na je unaogopa Corona,kifo au kutokuishi? Maana wapi wanaogopa corona kwa kuhofia kifo kumbe walishakufa siku nyingi wanasubiri kuzikwa tu, kama umekata tamaa na changamoto unazopitia basi umeshakufa subiri siku uzikwe tukusahau,tunachopaswa kuogopa ni kutokuishi pekee na siyo kitu kingine chochote. Karibu tuwe wote......

Rafiki yangu utakubaliana na Mimi kabisa kwamba kama hujuwi tatizo ni nini huwezi litatua tatizo hilo, sababu tatizo litakuwa ni kubwa kuzidi wewe, hapo ndipo Kila siku utajipa sababu nyingi zisizo sahihi na kuona mambo hayawezekani, Leo nataka nikuambie matatizo yako yote yanaanzia kwenye sehemu inayoitwa MAARIFA SAHIHI,siku utakapopata maarifa sahihi kuhusu Fedha ndio utafahamu tatizo halikuwa fedha Bali tatizo ni maarifa yanayohusu fedha,siku utakapopata maarifa sahihi kuhusu mafanikio ndio utajuwa tatizo siyo utajiri,siku utakapo pata maarifa kuhusu biashara ndio utafahamu tatizo siyo ugumu wa biashara ila hukuwa na maarifa ya namna ya kufanya biashara, Je tatizo ni madeni yamekuandama? Tatizo siyo kipato unachopata ila tatizo ni maarifa ya namna ya kutumia kipato chako ili kufikia Uhuru wa kipato, Je rafiki yangu wewe tatizo lako ni nini? Una maarifa sahihi kuhusu tatizo hilo? Amini hakuna jambo lisilo kuwa na ufumbuzi hivyo ukiona unapitia changamoto yoyote ile basi fahamu kuna sehemu hapako Sawa na kama unataka kuondokana na tatizo hilo tuwasiliane nitakuonganisha na mbobezi wa eneo linalokutatiza kwani kupitia Club yetu ya KISIMA CHA MAARIFA kuna tiba ya Kila ugonjwa unaokusumbuwa, biashara,fedha,mahusiano,sheria na mengine mengi, asante na uwe na siku njema rafiki.

Nenda kajiulize Leo nini tatizo? Je una maarifa sahihi kwenye hilo tatizo?kisha chukuwa hatua sasa huna haja ya kuendelea kulalamika.

Ni Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga mtu ambaye Nina amini katika maarifa sahihi kunikombowa, karibu tuwe sote.

Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944

Friday, 20 March 2020

Unapokosa majibu ya maswali uliyo nayo ndipo unapohitaji mtu huyu.......



Habari za muda huu rafiki yangu, bilashaka umesoma na kutekeleza yote yaliyo kwenye makala ya Amani makirita inayosomeka WAKATI DUNIA INAFUNGWA WEWE FUNGUA VITABU........ Kama hujasoma usiendelee kusoma hapa nitafute nikutumie usome kwanza kisha utakuja kumalizia.

Rafiki yangu sisi binadamu ni viumbe wa kuhoji, viumbe wa kutaka kujuwa sababu kwanini jambo fulani limetokea na hapa penye kwanini zako ndipo penye mafanikio au kushindwa kwako, unaweza pata sababu sahihi au usipate sababu sahihi na wakati mwingine ukabaki njia panda usijuwe nini cha kufanya.

Upo usemi mmoja unasema hivi "WANAOLETA MABADILIKO SIYO WENGI BALI WACHACHE WENYE MSIMAMO" huku usemi mwingine wa kingereza unasema hivi "Every generation needs someone hero to answer their questions" misemo yote hii INA maanisha mabadiliko ya kweli hayaletwi kwa kuangalia kile anachofanya Kila mtu Bali kwa kuangalia mashujaa ambao ni wachache wanafanya nini, rafiki unayo maswali mengi sana. Na majibu mengi sana yasiyo sahihi na umeanza kukata tamaa, hapa ndipo unapotakiwa kupata mtu sahihi wa kujibu maswali yako yote kwa usahihi, umekuwa hufahamu kwanini ni masikini?kwanini hupati kazi na umesoma una elimu kubwa? Kila ukianza biashara inakufa? Basi Mimi nitakukutanisha na mtu sahihi ila anza kufanyia kazi kauli hii.

EVERYTHING THAT IS HAPPENING AT THIS MOMENT IS A RESULT OF CHOICES YOU'VE MADE IN THE PAST-DEEPAK CHOPRA.

maamuzi yako ya siku za nyuma ndio sababu ya yale unayopitia Leo, Je yalikuwa sahihi? Basi yanaweza boreshwa na kuwa bora zaidi na shujaa wa kujibu maswali yako na yakafanya Leo uamue sahihi ujishukuru kesho ninamfahamu hivyo Fanya mawasiliano nami nitakuonyesha shujaa wa kizazi chetu na utanishukuru siku moja.

Uwe na siku njema, siku ya kumfahamu shujaa wa kizazi chako ili alete mabadiliko chanya kwenye maisha yako.

Makala hii imeandaliwa na Mwl.Kelvin Kinyaga.
Mpenzi na mtu anayeamini kwenye vitabu na uandishi.

Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944

Saturday, 14 March 2020

Tengeneza changamoto na utatuzi wake kabla hazijatokea......

Rafiki yangu hongera na mapambano unayoendelea nayo hata kama hali ni ngumu kiasi gani lakini wagumu wanadumu na sina shaka na wewe kwani natambuwa uwezo na maarifa unayopata yamekuwa Mwanga kwenye kiza unachokabiliana nacho.

Rafiki kitu kikubwa kinachotutesa ni kupata matokeo ambayo hatukuyatarajia,pengine ulisoma kwa bidii lakini hukufaulu mtihani,umepeleka watoto wako shule nzuri lakini hawakupata matokeo mazuri, umefanya kazi kwa bidii lakini matokeo yamekuwa tofauti na matarajio, haya yote unaweza kuona ni bahati mbaya na hukustahili kuyapitia lakini kuwaza hivyo ni kujidanganya. Ipo njia moja sahihi ya kukabiliana na changamoto hii.

TEGEMEA CHANGAMOTO KABLA HAZIJATOKEA.
Rafiki kama umeajiriwa basi ona changamoto ya kulipwa mshahara usio tosheleza mahitaji, ona manyanyaso unayopata kwa boss wako, ona umeshafukuzwa kazi na huna chanzo kingine cha kipato, kisha kaa chini na ona utazitatuaje changamoto hizo sasa kabla hazijatokea.

Rafiki wakati mzuri sana wa kutatua changamoto zako ni wakati mambo yanakwenda vizuri, Je rafiki ni yapi unahisi yanaweza tokea kama changamoto kubwa kwenye maisha yako? Ona imeshatokea na chukuwa hatua sasa ili likitokea lisikuumize kichwa. Ona miaka kadhaa mbele mshahara unaopokea utakatwa makato na kodi nyingi na utapunguwa na anzisha biashara ya pembeni ili utakapopitia hali ngumu zisiwe sababu ya wewe kuto kuishi. Hayo yote yasiwe sababu ya kutoweka bidii, nidhamu na uadirifu kwenye kazi lakini usiweke matarajio yoyote kwani unachokitegemea na kukitarajia ndio kinakufanya uwe mtumwa.
Haya yote yatawezeana kama una falsafa ya kufuata.Karibu tujifunze falsafa bora ya kutupa utulivu na kufanya maisha yaliyokusudiwa.

Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.

Saturday, 7 March 2020

Zielewe sababu unazojipa lakini usikubaline nazo....

Rafiki yangu na mwanamafanikio mwenzangu bilashaka umekuwa na wiki bora sana,na ubora huo unatokana na changamoto,kutekeleza uliyopanga na hata kutoroka kufanikisha kile ulichopanga kufanya na mengi yaliyojitokeza kama surprise yamekuacha mdomo wazi lakini umejifunza na umekuwa imara kama umefikiri kwa kina.

Rafiki yangu sisi binadamu ni watu wa sababu sana, Kila kitu utakipa sababu, kama ni kosa umefanya utajipa sababu na utetezi mwingi wa kwanini umefanya kosa hilo, na kama kuna jambo hukutekeleza utajieleza sababu kibao ambazo zimesababisha usitekeleze,kitu unachotakiwa kufanya ni kuzijuwa na kuzielewa sababu hizo lakini usizikubali kabisa maana hazina ukweli wowote, utetezi mzuri unaopaswa kutoa ni kutekeleza ulichopanga na kutoa matokeo lakini utetezi mwingine haubadilishi kitu chochote.

Swali unalopaswa kujiuliza kabla hujatoa utetezi ni hili. "JE KAMA MFUMO WA UPUMUAJI UNGETOA UTETEZI KWAMBA KESHO SITAWEZA KUFANYA KAZI KWASABABU NIMECHOKA JE UNGEKUWA HAI LEO?

Jiulize swali lingine ukiwa msituni halafu uko peku (hujavaa viatu) halafu ghafla simba akatokea na unakokimbilia kujiokoa kuna miba, Je utatoa utetezi kwamba huwezi kukimbia kwasababu hujavaa viatu?

Hivyo ndivyo yale yote unayojipa sababu hayana ukweli wowote ila hukuyafanya kwasababu moja Tu "Hayakuwa muhimu ndio maana sikufanya"

Hivyo ukiwa unatafakari wiki inavyokwisha jiulize ni mangapi hukuyatekeleza kama ulivyopanga kwasababu hayakuwa muhimu na unakwenda kuyapa umuhimu wiki linaloanza na utayatekeleza.

Asante na uwe na siku njema.Ni Mimi rafiki na mwanamafanikio mwanzako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.