Saturday, 7 March 2020

Zielewe sababu unazojipa lakini usikubaline nazo....

Rafiki yangu na mwanamafanikio mwenzangu bilashaka umekuwa na wiki bora sana,na ubora huo unatokana na changamoto,kutekeleza uliyopanga na hata kutoroka kufanikisha kile ulichopanga kufanya na mengi yaliyojitokeza kama surprise yamekuacha mdomo wazi lakini umejifunza na umekuwa imara kama umefikiri kwa kina.

Rafiki yangu sisi binadamu ni watu wa sababu sana, Kila kitu utakipa sababu, kama ni kosa umefanya utajipa sababu na utetezi mwingi wa kwanini umefanya kosa hilo, na kama kuna jambo hukutekeleza utajieleza sababu kibao ambazo zimesababisha usitekeleze,kitu unachotakiwa kufanya ni kuzijuwa na kuzielewa sababu hizo lakini usizikubali kabisa maana hazina ukweli wowote, utetezi mzuri unaopaswa kutoa ni kutekeleza ulichopanga na kutoa matokeo lakini utetezi mwingine haubadilishi kitu chochote.

Swali unalopaswa kujiuliza kabla hujatoa utetezi ni hili. "JE KAMA MFUMO WA UPUMUAJI UNGETOA UTETEZI KWAMBA KESHO SITAWEZA KUFANYA KAZI KWASABABU NIMECHOKA JE UNGEKUWA HAI LEO?

Jiulize swali lingine ukiwa msituni halafu uko peku (hujavaa viatu) halafu ghafla simba akatokea na unakokimbilia kujiokoa kuna miba, Je utatoa utetezi kwamba huwezi kukimbia kwasababu hujavaa viatu?

Hivyo ndivyo yale yote unayojipa sababu hayana ukweli wowote ila hukuyafanya kwasababu moja Tu "Hayakuwa muhimu ndio maana sikufanya"

Hivyo ukiwa unatafakari wiki inavyokwisha jiulize ni mangapi hukuyatekeleza kama ulivyopanga kwasababu hayakuwa muhimu na unakwenda kuyapa umuhimu wiki linaloanza na utayatekeleza.

Asante na uwe na siku njema.Ni Mimi rafiki na mwanamafanikio mwanzako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.

No comments:

Post a Comment