Tuesday, 30 June 2020

Zifahamu aina za maarifa na namna ya kutumia ili kufikia ndoto zako.....


Habari za wakati huu rafiki, hongera kwa mwezi huu mpya kama tunavyopenda kuita na wakati huo huo tunaendelea kufanya mambo yale yale na kukaa kusubiria matokeo tofauti, kama kweli tunataka uwe mwezi mpya basi chaguwa mambo ambayo hayakuwa na tija kwako kwenye mwezi uliopita na achana nayo,kisha peleka nguvu zako kwenye yale muhimu na yatakayokusaidia kufikia ndoto zako kwa wepesi iwezekanavyo.

Rafiki kama ilivyo kawaida yetu siku hii ya jumatano kwenye Kila wiki tunajifunza kutoka kitabu cha Think and grow rich, kitabu ambacho mwandishi anatushauri tunaposoma tusijaribu kuacha hata jambo moja na kutolifanyia kazi, tujifunze na kwenda kufanyia kazi.

Leo tutaangalia umuhimu wa maarifa na aina za maarifa, rafiki yangu utakubaliana na mimi kwamba karne hii tuliyopo ni karne ya maarifa na taarifa sahihi, kama unakwenda kufanyia kazi maarifa au taarifa sahihi basi hakuna atakayekuzuia kufika unapotaka kufika, pamoja na umuhimu wa taarifa na maarifa bado watu wengi wanatumia muda mwingi kusikiliza au kutafuta taarifa zisizo na manufaa yoyote kwao, watu hupenda kusikia habari hasi, kutumia muda mwingi kubishania mambo mbali mbali yanayoendelea na yasiyo na tija yoyote kwao, Leo tutajifunza aina za maarifa na utafahamu ni maarifa gani utapaswa kuyatumia kupiga hatua.

Zipo aina mbili za maarifa, aina ya kwanza ni MAARIFA YA KAWAIDA ambayo hupatikana kwenye jamii na mashuleni, na maarifa haya yanaitwa ya kawaida kwasababu yana mambo mengi sana na wingi huo wa maarifa bado hauwezi msaidia mtu kwenye kumpatia hitaji lake, maarifa haya ni kama njia ambayo itakusaidia kuweza kupata mwanga wa kule unakotaka kufika.

Aina ya pili ni MAARIFA YA KITAALUMA, haya ni yale maarifa ambayo Kila mtu anatakiwa kuyapata, ni maarifa ambayo yanapatikana kwa mtu anayefahamu ni kwa vipi anayapata na kuyatumia na yakamsaidia kwenye kutatua changamoto zake ambazo zinamkwamisha kufikia ndoto zake. Mwandishi anasema ukiyapata maarifa haya na kuweka kazi lazima utapiga hatua kubwa sana.

Mwandishi anasema maana ya elimu ni yale maarifa ambayo mtu unayapata ili kuendeleza kile kilichopo ndani yako,hebu tuone maeneo ambayo elimu hii ya kitaaluma inapatikana.

1.Uzoefu wako mwenyewe kwa elimu uliyopata.

2.Uzoefu na elimu za watu wengine ambao upo nao.MASTER MIND GROUP hili ni kundi la watu ambao mna ujuzi tofauti tofauti na mnasaidiana kufikia ndoto zenu (Kisima cha maarifa ndio mfano sahihi wa master mind group)

3.Kwenye vyuo mbali mbali vinavyotoa taaluma mahususi kwa kozi fulani.

4.Usomaji wa vitabu

Haya ndio maeneo ambayo elimu ya kitaaluma inapatikana,hivyo kama unataka kupiga hatua kubwa kufikia ndoto zako basi pigana kupata elimu kutokana na maeneo hayo.

"Any man is educated who knows where to get knowledge when he needs it and how to organize that knowledge into definite plans of action"

Ukishafahamu wapi elimu unayohitaji ili kukusaidia kufikia ndoto zako, kisha kuitumia elimu hiyo kwa kuunganisha na vitendo,basi utapiga hatua kubwa sana, kisima cha maarifa tunaishi kanuni ya PATA MAARIFA SAHIHI+WEKA KAZI KUTOKANA NA MAARIFA ULIYOPATA=MAFANIKIO MAKUBWA, hii inatupa picha kwamba maarifa pekee hayaleti muujiza wowote, bali yanapounganishwa na vitendo kwa kuyafanyia kazi ndio kutatupatia mafanikio makubwa.

Kwenye kitabu hiki kipo kisa kimoja kimeelezwa kinachomuhusu tajiri wa kipindi cha vita vya dunia Henry Ford,mtu aliyekuwa tajiri wa dunia kwa kipindi hicho ambapo gazeti moja la Chicago marekani lilimwandika kama mtu asiye na elimu na kumdhalilisha, Henry aliamua kufunguwa mashitaka dhidi ya wamiliki wa gazeti na moja ya utetezi wake kuhusu kuwa na elimu ndogo,aliulizwa kuhusu idadi ya wanajeshi wa kimarekani waliokwenda kupigana vitani, akajibu hakumbuki idadi kamili ila ni wengi na pale anapoulizwa  maswali  ya kijinga kama hayo, akiwa na maswali ambayo kwa kuyajibu kuna mnufaisha yeye kufikia ndoto zake basi ana vijana wake alio waajiri watampatia majibu ya maswali hayo, hivyo haoni umuhimu wa kujifunza Kila kitu wakati havimsaidii kwenye kutimiza ndoto zake, ila ana uwezo wa kupata elimu yoyote anayohitaji.

Hili linatupa funzo kwamba elimu tulizojifunza darasani zina mambo mengi ambayo hayana umuhimu kwenye kutimiza ndoto zetu na kama umeshafahamu ni elimu gani itasaidia kufikia ndoto zako basi anza sasa kupigana mpaka uipate elimu hiyo.

Asante sana rafiki yangu nikutakie siku njema katika kuuanza mwezi huu mpya wa Julai.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0712161251/0763766944

Monday, 29 June 2020

Tiba ya pili inayokwenda kutunisha mfuko wako ulio sinyaa....


Rafiki yangu habari ya siku hii nyingine, hongera kwa kuweza kuwa miongoni Mwa watu wenye bahati ya kuweza kuifikia siku hii, nina imani Zawadi hii huwezi kubali ikapotea bila kufahamu umefanya nini,Panga na hakikisha unakwenda kukamilisha yote uliyopanga kutekeleza kwenye siku hii..

Leo tunaendelea na uchambuzi wa kitabu chetu cha The richest man in the Babylon na kwa wiki kadhaa tumejifunza mambo mengi sana ambayo nina amini ueyafanyia kazi kabla masomo hayo hayajapoa, Leo tunakwenda kuangalia Tiba nyingine ambayo tunajifunza kutoka kwa Tajiri Arkadi baada ya kuona tiba ya kwanza ya KUANZA KUTUNISHA MFUKO WAKO KWA KUTUMIA SEHEMU TISA KATI YA KUMI NA MOJA KUIWEKEZA, baada ya kufundisha tiba hii ya kwanza mtu mmoja alimuuliza ninawezaje kutenga sehemu hiyo wakati kipato ninachokipokea ni kidogo na hakitoshi hata kwa matumizi muhimu?

Ndipo Arkadi akawajibu kwa kuwauliza swali, Je ni wangapi ambao jana walikuwa na mifuko iliyosinyaa? Karibu watu wote waliopo ukumbini walinyoosha mikono, basi akawaambia kwa kuwauliza inawezekanaje watu wote humu muwe na mifuko iliyo sinyaa wakati mnafanya kazi tofauti tofauti na mna vipato visivyo fanana?

Hapa tunapata funzo kwamba, waajiriwa huwa tunatabia ya kuongeza matumizi kadri  kipato kinavyoongezeka, ndio maana anayepokea million moja, laki tano na hata kipato kidogo cha laki moja bado inapokaribia na siku anayopokea tena kipato hicho huhakikisha kipato cha mwanzo kimekwisha, hili hata kwa mtu mmoja unaweza kukubaliana na hili, kuna miezi unapata fedha nyingi tofauti na kawaida lakini unazitumia zote na pengine kabla ya kupokea zingine utahakikisha zile za mwanzo umezimaliza, hii yote ni ile nguvu ya tamaa ya kutumia tuliyo nayo.

Baada ya kuwapa ufafanuzi huo Arkadi anawafundisha tiba ya pili ya kutunisha mifuko yako iliyo sinyaa ni DHIBITI MATUMIZI YAKO, haijalishi unapokea nini lazima ujidhibiti kwenye kutumia kipato hicho kwani hayo matumizi unayo yaona ni muhimu hukua kadri kipato chako kinachoongezeka. Hivyo anza kudhibiti matumizi yako.

Mwandishi anafananisha tamaa ya kutumia kipato tunachopokea na magugu yasiyo pandwa shambani, kama hayatadhibitiwa yataendelea kukua na kuathiri mazao yaliyopo kwenye Shamba hilo, hivyo anza sasa kutengeneza bajeti yako kwa Tisa ya kumi na hiyo moja inayobaki hakikisha unaiweka kwa ajiri ya kukikuza kipato chako. Fahamu matumizi muhimu kweli na yapi siyo muhimu na ondokana nayo Mara moja.

Rafiki yangu asante na nikutakie utekelezaji mwema kwa haya unayojifunza hapa yatakufikisha sehemu fulani ya juu tofauti na ulipo sasa, nakupenda na nakutakia siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Sunday, 28 June 2020

Tatizo alipo kwenye unachokipokea bali unachokinunua.


Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka u mzima na buheri wa afya, umeianza wiki hii kwa nguvu na umeshapanga ni nini unakwenda kukamilisha kwenye siku hii, haijalishi nini kitakwenda kutokea ila hutojipa sababu kwanini usifanye bali kwenda kutekeleza yote uliyopanga.

Kama ilivyo utaratibu wetu siku hii ya Leo ya Jumatatu kwa wiki kadhaa sasa tunachambuwa kitabu cha Rich dad poor dad,tangu tumeanza kujifunza tumeona nini tunatakiwa kufahamu kupitia baba hawa wawili, maana hatujifunzi kwa kuwaangalia matajiri wanafanya nini pekee bali kutofanya kile ambacho masikini wanafanya.

Leo tuangalie dhana ya kununua inavyotutenganisha na utajiri, ni kawaida kwetu kuona tunakuwa masikini kwasababu kipato tulichonacho ni kidogo na pale tunapoongezewa kipato iwe kwa kuweka bidii au kulipwa na waajiri wetu bado gharama za maisha zinaongezeka na kuwa kubwa, sasa hapa ndipo pale wanaoshinda bahati nasibu au kuachiwa urithi wa fedha nyingi na utajiri huwa hawaelewi nini kinasababisha fedha zao au utajiri wao kupotea.

Moja ya tofauti kubwa kati ya masikini na tajiri ni kwenye manunuzi, masikini ananunua Mali zisizo zalisha(liabilities) wakati matajiri hununua Mali zinazo zalisha (Assets), Leo ukienda kuongea na mtu mwenye mawazo ya kitajiri utamsikia akiwaza kununua vitu vitakavyomuingizia kipato, biashara au kuwekeza fedha kwenye sehemu ambayo na yeye atanufaika, lakini masikini muda wote huwaza kununua anasa na kufanya starehe, vitu vinavyo vutia machoni na havimuingizii pesa yoyote ile.

Mwandishi anafananisha kutengeneza mali zinazozalisha ili kustaafu ni Sawa na kupanda mti, mwanzo utaupa huduma zote na kuumwagilia na baadaye ukiwa mkubwa na mizizi yake kwenda chini hufikia Maji na kuto hitaji huduma kitoka kwako bali kukupatia kivuli au matunda.

Mwaka 1990 Mike alichukuwa urithi kutoka kwa baba yake (baba tajiri) na aliweza kuzisimamia vizuri na utajiri wao ukakua Mara dufu, huku mwaka 1994 Robert akiwa na miaka 47 na mke wake mwenye umri wa miaka 37 waliamua kustafu na kuendelea kula utajiri wao, na hapa Robert anatupatia dhana ya kustafu kwamba siyo kuacha kufanya kazi moja kwa moja bali kutokuifanya au kufanya hakuzuii fedha kuongezeka, hapa unakuwa umefikia hatua fedha inakufanyia wewe kazi kwa uwekezaji uliofanya huko nyuma.

Lazima Mimi na wewe tuanze kufikiri ni lini tutahitaji kuwa tumefikia hatua ya kustafu na fedha zikitufanyia kazi, kwani nguvu ulizo nazo sasa hazitakuwa Sawa na nguvu utakazo kuwa nazo miaka 10 au 20 ijayo hivyo maandalizi ya kufika huko anza kuyafanya sasa.

Asante sana rafiki nina imani unakwenda kufanyia kazi haya uliyojifunza Leo, uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Mambo matatu yatakayofanya msaidizi wako kwenye kazi ajitume.......



Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri, siku ambayo tunamaliza wiki na kujiandaa kuanza lingine, kama ilivyokawaida yangu na nimekuwa naitumia kukushirikisha kwamba itumie siku hii kujifanyia tathimini ya kipi umefanya wiki hii kuiendea ndoto yako? Na kipi unapanga kukamilisha kwenye wiki unaloliendea? Yapi umefanya sahihi, yapi ulikosea na nimejifunza kupitia makosa hayo? Kwa kufanya hivyo kunakufanya uweze kujifunza na kutorudia makosa, lakini pia kunakufanya uongeze bidii kwenye kusudi lako unalofanyia kazi, karibu tuwe sote.....

Rafiki leo twende tukaangalie changamoto za wasaidizi wetu wa kazi kwenye shughuli zetu, lakini pamoja na majumbani.Kabla hatujaenda kuangalia ni vitu gani unapaswa kufanya ili waweze kujituma zaidi kwenye kazi zao  hebu tuangalie ni kwanini nimesukumwa kuandaa somo hili.

Wakati naangalia changamoto kubwa ambazo nimezipitia wiki hii inayoisha ndipo nikagundua kama familia tuna angaika kupata mtu atakayeweza kukaa na wazazi wetu ambao ni wazee na wako kijijini, kwani wengi wamekuwa wanakaa kidogo na kuondoka lakini pamoja na kigezo na hitaji la wasaidizi hawa kutaka ongezeko la mshahara bado ufanisi wa kazi huwa ni mdogo na usioridhisha, wakati familia tunapitia kwenye changamoto hii lakini wiki hii pia tuliweza kukaa na wana partnership wa biashara tuliona changamoto ya Dada anayetusaidia kazi eneo la biashara kuwa na matatizo mengi yanayopunguza na kuathiri biashara yetu, uchelewaji, kiburi na kuleta mazoea kazini.

Baada ya kuona kwenye familia na kwenye biashara yetu tunapitia changamoto ya aina moja ndipo nikajitafakari kwa kina ni wapi tunaweza kuwa tunakosea, maana kuishia kulalamikia wasaidizi wetu bila ya kuangalia upande wetu ni kazi bure, baada ya kutafakari kwa kina nikakumbuka mwaka jana tulipata semina bora sana kwenye kisima cha maarifa kuhusu namna ya kukuza biashara zetu, hapo tulipata masomo kumi yenye Kila mafunzo kwenye biashara,baada ya kuanza kupitia ndipo niligundua kuna makosa mengi sana bado tunayafanya kwenye biashara na hata kwenye maeneo mengine yanayohusisha wasaidizi wa majukumu yetu, Kwenye semina ile somo la saba kati ya kumi lilisomeka hivi JINSI YA KUAJIRI WAFANYAKAZI WATAKAO WEZESHA BIASHARA YAKO KUKUA.

Wakati napitia somo hili niligundua makosa mengi tunayafanya wenyewe, tunapokuwa na uhitaji wa wasaidizi hakuna vigezo tunavyotumia kupima namna ya kuwapata bali tunaangalia tu kwamba tunahitaji mtu wa kutusaidia, lakini hata mtu huyo akipatikana tunaongea naye bila kuweka utaratibu wa ki maandishi wa orodha ya majukumu yake na namna gani utapima ufanisi wake, lakini pamoja na makosa hayo bado tukiona ameshindwa kutekeleza majukumu yake tunakimbilia kuwaondoa pasipo kuzungumza nao na kuwaambia ni nini tulitarajia kupata kutoka kwao na wapi wanakosea na kisha kuwapima tena kwa kuwashirikisha makosa wanayofanya na hili kupelekea Kila siku kuendelea kubaki kwenye changamoto hii kwa kufanya kwa namna tuliyozoea kufanya. Yako mengi sana nimejifunza hapa lakini twende tuone vitu vitatu vinavyofanya mfanyakazi ajitume zaidi kwenye majukumu uliyompangia.

1.Maamuzi(Autonomy)
Kufanya maamuzi ni kitu ambacho siyo rahisi sana kufanya kwa tulio wengi, watu hawa tunaofanya nao kazi wakigundua wewe msimamizi wao siyo mtu wa kufanya maamuzi bali ni mtu wa kuongea tu na huchukuwi hatua basi analeta mazoea ambayo yanakwenda ku athiri kazi au biashara yako, lakini ukiwa ni mtu mwenye msimamo na maamuzi lazima awe makini na kuweka kazi kwani anafahamu utamchukulia hatua Mara moja, hili linaanzia na namna yeye alivyopata nafasi hiyo.

2.Chenye maana kwake(Meaning)
Kama uliyemwajiri hakithamini kile anachopata kwenye kazi anayofanya iwe ni kwa kujifunza au kumsaidia kwenye maisha yake basi atakipuuza na kufanya kwa mazoea, lakini kama ataona kina maana kwake basi lazima aweke bidii, ipo njia ambayo itakusaidia kumfanya aone thamani na maana ya kile anachofanya ni kwa kumuonyesha manufaa atakayopata kama atajituma kwenye kazi na ukiona hilo anza kumpatia kitu cha ziada na kuonyesha unafurahishwa na jitiada zake.

3.Ukuaji(Growth)
Kama kile anachofanya msaidizi wako hakikui basi anachoka na kutoona kina umuhimu kwake, lakini akiona kinaelekea kukua na kuwa kitu kikubwa anaanza kuona atanufaika na ukuaji huo, hata ungekuwa wewe msomaji sehemu ambayo Kila siku iko vile vile haiongezeki na unapokea kiasi kidogo je utakaa?kaa naye na mshirikishe mwakani biashara itakuwa imefika wapi na je unataka miaka mitano ijayo biashara yako iwe imefika wapi na yeye atanufaikaje na mafanikio hayo, na Kila biashara inapokua na kukua basi iwe na muunganiko wa moja kwa moja na yeye.

Hayo ni machache kati ya vitu vingi ambavyo tumekuwa hatuviangalii kwa watu tunao waajiri na tumekuwa tukibaki kulalamika bila kuangalia upande wetu ni yapi tunayakosea, asante rafiki na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Saturday, 27 June 2020

Namna pekee ya kukaa na watu wenye akili.......



Rafiki yangu kile unachoambatana nacho ndicho kitakachoamua hatima yako, Kama unaambatana na watu wajinga huwezi kuwa mbali na ujinga,na kama ukiambatana na watu wenye akili na uwezo mkubwa wa kufikiri basi na wewe utajifunza na kuwa na akili kubwa, siyo kitu rahisi sana kuhitaji kukutana na watu wenye mafanikio makubwa ili ujifunze kwao, Leo huwezi kusema kesho nahitaji nikutane na bakheresa na ukakutana naye akufundishe nini ufanye ili ufanikiwe kama yeye, hilo litakuwa gumu kwako, lakini ipo njia rahisi ya kukutana na watu kama hao na kuzungumza nao, Bilgate na matajiri wakubwa utakutana nao kwa njia hii ambayo nakwenda kukuambia hapa chini......

"Going straight to seat of intelligence"That's what books are"-Epictetus.

Kama unahitaji kufanikiwa kweli na kuwa na uwezo mkubwa kiakili,kama unataka kukaa seat moja na watu waliofanikiwa basi lazima ufuate upande wa vitabu, jijengee tabia hii ya kusoma vitabu na utakutana na wote waliofanikiwa na watakufundisha nini walifanya wakafikia mafanikio hayo na muda si mrefu utajifunza na kufanikiwa kama utatekeleza ulicho jifunza.

Rafiki labda nikupe shuhuda ndogo kwangu, kabla sijawa na utaratibu wa kusoma vitabu na kujiunga na kisima cha maarifa niliungana na wenzangu kwamba mshahara ni kidogo na hautoshi, hili ni kweli lakini njia pekee niliyoona kwa kipindi hicho ni kukaa kusubiria serikali waniongezee mshahara, kukaa na kuilalamikia serikali ikawa ndio kitu nilidhani ni sahihi, mwishoni Mwa mwaka wa 2017 nilianza kujifunza kupitia Amka Mtanzania ambapo nilijifunza bure na kuanza kuona hali ya kulalamika na kubeba jukumu la maisha yangu likabaki kwangu, mwaka 2018 mwanzoni niliweza kulipa ada na kuwa mwana kisima cha maarifa, hebu fikiria kutoka kutoweza kukutanisha mshahara na mshahara mpaka kufikia hatua ya kuwekeza karibu nusu ya mshahara Wangu sasa na mshahara huo haukuongezwa hata shilingi kumi tangu mwaka huo wa 2018 mpaka sasa lakini nimeacha kulalamika na nina imani kubwa ya kufikia ndoto zangu. Hii ndio nguvu ya vitabu kwenye maisha yetu.

Leo wakati napitia kurasa za Kila siku za ustoa nikakutana na kichwa cha habari kinachosomeka hivi "Why did the slave masters hide their money in books?" Hili likanifanya niendelee kusoma na ndipo nikakutana na kisa kimoja cha kocha wa mpira wa kikapu (basketball) aliyeitwa GEORGE RAVELING aliyeulizwa swali hilo la kwanini wamiliki wa watumwa (slave masters) wanapenda kuficha fedha zao kwenye vitabu?

George anamjibu bibi yake hafahamu ni kwanini ndipo bibi anampa sababu "because they knew slaves wouldn't open them" akimaanisha kwamba kwasababu watumwa hawapendi kufunguwa vitabu na kusoma.

Hivyo rafiki kama unataka kuondokana na utumwa wa fedha, utumwa wa ujinga, utumwa wa ajiri na manyanyaso kazini, utumwa wa fikra zako, utumwa wa hisia zako basi anza kujenga Tabia ya kusoma vitabu,hili litakupa Uhuru wa kutumikia wengine kwani u dhaifu na mtumwa kwasababu umekumbatia ujinga na hutaki kujifunza, kama utaruhusu siku yako ipite bila ya kusoma kurasa kadhaa za vitabu basi tambuwa unakumbatia ujinga na rafiki wa ujinga ni utumwa, hivyo kama unahitaji kufahamu utapataje vitabu vizuri vya kusoma basi wasiliana na Mimi na ukiweza kujiunga na kisima cha maarifa utapiga hatua kubwa sana kwani utazungukwa na watu sahihi. Nakupenda na nakutakia siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Thursday, 25 June 2020

There is no end to relationship-Krishnamunt......



Rafiki hongera kwa siku nyingine nzuri, furahi day kama wengi wanavyopenda kuiita, wengi hufurahi siku hii wakiamini ni siku ambayo wanaanza kufurahia mapumziko ya mwisho wa wiki lakini kwako wewe kama unajitoa kweli kufanikiwa siku za mwisho wa wiki ndio siku zitakazoamua hatima ya maisha yako, usikubali kukaa bila kuwa na kitu cha kujishughulisha nacho......

Rafiki leo tuzungumzie kauli ya Krishnamunt ya kwamba haitafikia hatua ukajiambia huhitaji mahusiano na wengine, hili ni zoezi endelevu kwa maisha yako yote kwani chochote kinaumbwa kwa namna kinavyohusiana.

Pamoja na umuhimu wa mahusiano na wengine kwenye maisha yetu,watu wengi tunasahau kwamba huwezi kuwa na mahusiano mazuri na wengine kama huna mahusiano mazuri na wewe mwenyewe, ndio maana tunaamini wanaofanikiwa wanafanikiwa kwasababu wanafurahia maisha, kama wewe mwenyewe hujikubali kwa kile unachofanya hakuna atakayekukubali, chochote unachotaka kukiunda basi tambuwa lazima uwe na mahusiano mazuri na wengine, hakuna mtu aliwahi kufanikiwa kwa kujiambia hahitaji kuhusiana na wengine, mfanyabiashara ili afanikiwe lazima awe na uhusiano mzuri na wateja wake, mfanyakazi ili awe mfanyakazi bora lazima awe na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzake pamoja na wanao pokea huduma kutoka kwake.

Usiruhusu hisia iongoze mahusiano yako na wengine bali ruhusu fikra zaidi dhidi ya hisia,wengi tunaruhusu hisia iongoze badala ya fikra kwenye mahusiano, na ndio maana kosa lile lile alilofanya mtu unayempenda linakuwa ni kosa dogo, lakini kosa hilo hilo akifanya mtu usiyempenda linakuwa kubwa na kukuzwa na wakati mwingine kutokusamehe. Kutatua changamoto yoyote iliyoko mbele yako jiulize maamuzi ninayotaka kufanya yanahusisha kufikiri au hisia?

Rafiki jiulize kama una mahusiano mazuri na wewe mwenyewe?kwani huwezi wapa watu kile usichokuwa nacho, kisha hakikisha una husiana na wengine vizuri kwa kuhakikisha huna chuki na yeyote kwani hakuna kitakachomuumiza yeyote kutoka ndani mwako halafu wewe kikakuacha salama, kama una hasira na yeyote lazima ikuumize wewe kwanza kabla hujamuumiza unayemchukia, huwezi mfanyia mtu ubaya harafu wewe ukabaki salama, siku zote tambuwa kazi yako kubwa ni kusamambaza upendo kwa wengine.

Kazi yangu ni kuhakikisha maisha yangu na yako yanakuwa bora zaidi Kila tunapopata siku moja ya Zawadi zaidi,tutaendelea kua pamoja rafiki nakupenda daima.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251


Wednesday, 24 June 2020

Umuhimu wa mifereji mingi na mifereji unayopaswa kuwa nayo...



Rafiki karibu tuendelee kuwa sote na tuweze kujifunza pamoja, lengo ni kuhakikisha mateso yetu na ya wengine yanapunguwa kwani hata mwenyezi mungu anatambuwa kukosa maarifa kunatuangamiza, karibu twende pamoja.........

Siku alhamisi ni siku ambayo tunachambuwa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA na wiki hii tutaweza kuona umuhimu wa kuwa na vyanzo vingi vya mapato ambavyo vinakuingizia fedha.

Mwandishi anafananisha hali ya kuwa na vyanzo vingi vya mapato kama mito mingi ambayo inatiririsha Maji yake kuelekea bahari moja.Pale mto mmoja ukikauka basi bahari itaendelea kupokea Maji kutoka kwenye mito mingine, hebu chukulia mfano wa tangu umeanza kusikia bahari ulishawahi kusikia bahari imekauka? Basi pale unapokuwa na chanzo cha aina moja cha kukuingizia fedha basi huwezi fikia utajiri na unakuwa kwenye hatari kubwa pindi unapopoteza kazi hiyo.Mwandishi anaweza kutuonyesha utafiti uliofanywa na waandishi wa kitabu cha THE MILLIONAIRE NEXT DOOR na walibaini kwamba baada ya kufuatilia maisha ya matajiri wenye utajiri wa zaidi ya billion 2 za  Kitanzania walibaini hakuna tajiri aliyekuwa anategemea kipato cha aina moja, waajiriwa na wafanyabiashara wadogo tuko kwenye changamoto nyingi kwasababu ya kutegemea kipato cha aina moja mwandishi anasema ni hatari kubwa sana hii kwenye fedha na utajiri.

MIFEREJI YA KIPATO UNAYOPASWA KUITUMIA
Vipo vyanzo vingi sana vya mapato unavyoweza kuvitumia lakini mwandishi amevigawa kwenye makundi yafuatayo.

1.Kazi au ajira,hapa unaweza kuwa umeajiriwa au kujiajiri na unauza ujuzi na muda wako ili kupata fedha.Hiki siyo chanzo kizuri kwasababu kitakupa ukomo wa fedha na muda. Lakini ni chanzo ambacho wengi wanaweza kuanzia hapa kuelekea safari ya utajiri.

2.Biashara, hapa unauza bidhaa au huduma kwa watu wengi na kuweza kutengeneza faida.kundi hili unaondoka kwenye ukomo wa muda na wewe binafsi,hapa unakuwa na mfumo ambao utakuwezesha kutumia muda wa wengine,nguvu za wengine na ujuzi wa wengine kuweza kutengeneza kipato.

3.Uwekezaji;Hapa unaiwekeza fedha yako sehemu inayozalisha na kisha unapata faida, hii ndio dhana ya fedha kukufanyia kazi,unapata gawio au riba kulingana na uwekezaji ambao unakuwa unafanya. Mbele utaona makundi yaliyogawanyika kwenye kuwekeza.

4.Mrahaba; Hapa unalipwa kwa kazi ambayo ulishaifanya huko nyuma.Waandishi wa vitabu wanaingia kwenye kundi hili, ukishaandika kitabu kazi yako inakuwa kuchapa na kuongeza nakala zaidi. Hivyo mwandishi anashauri acha kufikiria sehemu moja ya kipato,unaweza kuwa na biashara zaidi ya moja, ukawa na uwekezaji kwenye Mali, ukawekeza kwenye hisa na kununua vipande.

Hili ni zoezi muhimu kulifanya kwa Kila mmoja ingawa litachukuwa muda mrefu kulifikia, hivyo unaanza kidogo kidogo, siyo Leo umeanza biashara moja na haijasimama vizuri unaanza biashara nyingine,lazima kile ulichoanza mwanzo kisimame vizuri ndipo uanze kingine,lakini usikubali kuwa na maisha ya chanzo kimoja cha kipato. Asante rafiki tukutane wiki ijayo kuendelea na chambuzi ya kitabu hiki.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Tuesday, 23 June 2020

Hizi hapa hatua tatu za kufuata ili kukamilisha mpango na malengo yako ya kifedha........


Leo kabla hujaendelea kusoma hapa jiulize ni lipi katika niliyojifunza kwenye Ustawi wa fikra nililifanyia kazi? Kisha ukanishirikisha inbox na kama hufanyi hivyo Kila siku unajiambia masomo mazuri nitaanza mipango kamili siku zijazo, hapo unajidanganya mwenyewe kitu ambacho hakitamuumiza yeyote isipokuwa wewe mwenyewe, siwezi kaa chini nikaandika kitu ambacho sina hakika kwamba kitakusaidia,nina hakika ukifanyia kazi masomo haya tutafika pamoja kule tunakotaka kufika......

Leo tunaendelea na uchambuzi wa kitabu chetu cha THINK AND GROW RICH,baada ya wiki iliyopita kuona namna akili yetu ilivyogawanyika na kufanya kazi,wiki hii tutaona hatua tatu za kufuata ili lengo lako ulilojiwekea liweze kutimia, watu wanafanya kazi na kulipwa au biashara lakini miaka yote mipango yao kifedha hahifikiwi kwasababu wanaishi kutamani pasipo na mpango madhubuti wa kuyafikia yale unayotamani na ndio maana wengi wanaingia kwenye mtego wa madeni kwa kufikiri hiyo ndio njia pekee ya kukamilisha mipango yao. Hapa chini nakuandikia hatua tatu unazopaswa kuzifuata ili mpango ulio nao uweze kukamilika.

HATUA YA KWANZA
Taja kiasi cha fedha unachohitaji,taja tarehe ya mwisho ya wewe kupata kiasi hicho na bidhaa au huduma unayotakiwa kutoa ili kupata kiasi hicho. Wakati unasema hivyo na kuweka mpango huo jione tayari unamiliki kiasi hicho.Hapa chini nakuwekea mfano wa hatua hii.

Mpaka kufikia June 1,mwaka 2021 nitakuwa nimepata Tsh 1095000 ambazo zitatokana na biashara ya Visheti.Nitahakikisha natoa huduma nzuri kwa wateja ili niweze kupata zaidi ya Tsh 3000 kwa siku kama faida. Nina amini nitakuwa nazimiliki fedha hizi. Imani yangu ina niambia tayari nimeshazipata fedha hizi, kwani tayari ninao mpango ninao ufuata na nina uhakika wa kupata fedha hizo muda huo utakapofika. Kama unavyanzo Vingi vya mapato basi Kila chanzo unakiwekea mpango wake na baadaye unaweka mpango wa majumuisho.Hili linategemeana na uwezo wa chanzo chako cha mapato kama ni cha siku, mwezi, miezi sita au mwaka.

HATUA YA PILI
Rudia Maelezo hayo asubuhi na jioni mpaka ile sehemu ya ubongo wa ndani (subconscious mind)iweze kuona kama ndio kitu kinachotokea kwenye maisha yako.

HATUA YA TATU
Weka nakala ya Maelezo yako haya sehemu ambayo unaweza kuyaona asubuhi na usiku na isome kabla ya kulala na pale unapoamka, Kila siku mpaka tarehe uliyojiwekea inapofika bila kuacha hata siku moja.

Mwanzo akili yako itaanza kupingana na hatua hizi na utaanza kuhisi kuzipuuzia lakini ukiweka ung'ang'anizi wa kuto kubali kurudi nyuma nina hakika wa zaidi ya asilimia tisini unakwenda kutimiza lengo lako ulilo jiwekea, lakini kama unajiambia unahitaji kiasi fulani cha fedha bila ya kufuata hatua hizo basi utakuwa unaishi kutamani na huwezi kutimiza malengo yako.

Unaweza ona Kila mwanzo Mwa mwaka watu wakifurahia mwaka mpya na kuweka mipango mizuri ila kabla ya kufika mwezi march zaidi ya asilimia 80 wanakuwa wamesharudi kwenye maisha yale yale ya Kila siku.

Rafiki yangu nenda kaweke mipango yako kifedha kwa namna hii na kama utafanya hivyo utaona nguvu itakayokusukuma na utapiga hatua Kila siku, haitakuwa rahisi lakini ukijiwekea ung'ang'anizi sina shaka utapata matokeo mazuri sana.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Mfalme akauliza inawezekanaje watu wachache sana kuwa matajiri kuliko wengine?



Habari rafiki na ndugu yangu, bilashaka uzima ni Zawadi ambayo imetufanya Mimi na wewe tuendelee kuwasiliana na kupeana maarifa ili kustawisha fikra zetu, karibu tuwe sote....

Kama ilivyokawaida yetu siku ya jumanne tunachambuwa kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON na mpaka sasa tumeshajifunza mengi na kuna mengi bado hatujajifunza hivyo karibu tuweze kuona nini tunaondoka nacho na kwenda kufanyia kazi.

Jina Babeli siyo geni masikioni pako, wasomaji wa vitabu vya dini wameshasikia sana habari za babeli, babeli ulikuwa ni mji uliokuwa na utajiri mkubwa sana na hilo liliwezekana kutokana na hekima ya watu walio ishi kwenye nchi hiyo, kutoka kuwa mji wenye Kila changamoto mpaka kufikia utajiri.Hilo liliwezekana kutokana na utayari wa wananchi wa mji huo kukubali kujifunza namna ya kuupata utajiri, je na wewe upo tayari kujifunza kama watu wa babeli? Basi usiishie njiani endelea kufuatilia makala hii mpaka mwisho.

Hapo zamani alikuwepo mfalme aliyeitwa Sargon, alikuwa mfalme wa babeli na baada ya kutoka vitani anarudi na kukuta watu wake wakiteseka, kazi hakuna, wafanyabiashara hawana wateja, wakulima hawawezi kuuza mazao yao kwani watu hawana dhahabu(fedha)za kununua chakula na hali ya maisha imekuwa ngumu. Akiwa anaendelea kuongea na kansela wake wanaulizana kwamba pamoja na hali hiyo kwani dhahabu (fedha) zilizokuwepo zimekwenda wapi? Ndipo kansela wake anamjibu zimefuata mkondo wake. Jibu hili linatupa funzo kwamba kuna watu wanavutia fedha kwao,tena wakati wengine wapo kwenye matatizo makubwa wengine ndio fedha zinaelekea kwao.

Baada ya kansela kumwambia mfalme dhahabu zote zimefuata mkondo wake ndipo mfalme anauliza inawezekanaje watu wachache sana kuwa matajiri kuliko wengine? Kansela akamjibu ni kwasababu wanajua jinsi ya kupata utajiri. Ndugu pengine na wewe ulishawahi kujiuliza swali hilo la kwamba inawezekanaje wengine wawe na fedha nyingi halafu wewe huna? Sasa pengine hukujipa jibu sahihi, pengine ulijiambia ni wachawi, wana roho mbaya na kujidanganya kwamba fedha hazinunui furaha, hayo yote siyo sahihi.

Mfalme Sargon na kansela wake wanatumia hekima ya kutowaza kama wewe unavyowawazia matajiri, wakakubaliana kwamba hawa watu wachache matajiri kuna kitu wanafahamu ambacho wengi hawakifahamu hivyo ikiwezekana watafute mtu atakayewafundisha na mtu huyo hakuwa mwingine bali Arkadi, mtu aliyekuwa na utajiri mkubwa sana na uliongezeka Kila siku, basi walikubaliana aitwe na awafundishe watu wachache na hao watu wakawafundishe wengine na wengine na baadaye taifa zima litakuwa na utajiri, basi Arkad aliitwa na kuulizwa kama angeweza kufanya hivyo na alikubaliana na siku iliyofuata alianza kuwafundisha watu 100.

Kweli siku iliyofuata Arkad alikuwa mbele ya watu 100 na alianza kuwaeleza kwamba hata yeye alianzia chini kabisa mpaka alipojifunza namna ya kutunisha mifuko yake iliyo sinyaa na hapo ndipo akawaambia anakwenda kuwapa Tiba saba zitakazo kwenda kutunisha mifuko yao na atawafundisha Kila siku tiba moja mpaka siku saba watakuwa wamejifunza tiba zote.

TIBA YA KWANZA-ANZA KUTUNISHA MFUKO WAKO
Arkad alianza kwa kuwauliza Kila mmoja anajishughulisha na anayo kazi inayomuingizia kipato? Wote walikuwa na kazi zinazowaingizia kipato, Arkadi akawaambia vizuri sana kwani kama unayo kazi yoyote inayo kuingizia kipato basi unayo nafasi kubwa sana ya kuufikia utajiri.

Akamgeukia mmoja aliyesema anauza mayai na kumuuliza je kama Kila asubuhi anapokea mayai 10 na jioni unatoa tisa na moja unaacha kwenye kikapu je baada ya muda nini kitatokea?muuza mayai akajibu kikapu kitajaa mayai, Arkad akamwambia ni kweli kwasababu unachukua mayai kidogo kuliko uliyopokea.

Hivyo akawaambia tiba ya kwanza ya mfuko ulio sinyaa ni kuhakikisha Kila fedha kumi unazopokea unatumia tisa na moja uunaweka kwenye mfuko wako na baada ya muda mfuko wako utatuna na kukua zaidi. Siyo kazi rahisi ila inawezekana.

Rafiki yangu leo tuishie hapa, bilashaka dhana hii unakwenda kuianza Mara moja, Mimi rafiki yako nilijifunza tiba hii 2018 kwa mara ya kwanza na nilianza Mara moja kuifanyia kazi, mwanzo ilikuwa ngumu lakini sasa ni sehemu ya maisha yangu, kwa Kila kipato ninachopokea asilimia kumi naiweka gerezani Kama tunavyoita kisima cha maarifa kwani ukiweka ndani hazitakosa matumizi, kujua gereza la asilimia kumi tuwasiliane, Asante na siku njema tukutane wiki ijayo tuone tiba zingine zilizobaki.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251
.

Sunday, 21 June 2020

Hivi ndivyo ujinga wa fedha unavyoathiri jamii....



Rafiki yangu hongera kwa kuwezi kuianza wiki hii nyingine, ni matumaini yangu hutokwenda kujipa sababu yoyote bali kutekeleza yale yote yaliyo kwenye mipango yako kama unavyoweza kukamilisha ratiba yako ya chakula na mipango yako ikapate kutimia.....

Kwanza kabisa nikushukuru kwa kuendelea kufuatilia mfululizo wa makala zangu kutoka katika kurasa zangu za Ustawi wa fikra, Nina hakika mabadiliko yoyote yanaanzia na fikra zetu.Hivyo sina shaka na nguvu ya maarifa kwenye mafanikio.

Kama ilivyokawaida yetu kwenye siku ya jumatatu tunachambuwa kitabu cha Rich dad,poor dad na mpaka kufikia Leo tumeshajifunza mambo mengi na hupaswi kusubiria chochote nenda kayaweke kwenye vitendo.Leo tutajifunza ni kwa namna gani utaweza kuzitawala fedha zako na siyo zenyewe kukutawala.

Leo mwandishi anatutaka kwanza tuweze kufahamu kwamba fedha haimalizi matatizo bali inayazidisha na kuyaongeza, mwanzo unapokuwa huna fedha unakuwa na matatizo kidogo, pengine ni makazi duni,mlo kamili hupati na shida ndogo ndogo, lakini kadri fedha zinapoongezeka na changamoto zake zinaongezeka na ndio maana wengi hurudi kwenye maisha yao ya mazoea, kwani wanapoanza kufanyia kazi fedha na kuziongeza na changamoto zinaongezeka na hii hutokana na watu kupenda kupata raha na furaha zaidi na vitu hivi huchangia matumizi kuongezeka.

NGUVU YA KUTAWALA FEDHA NA SIYO KUIGOPA
Wiki iliyopita tuliona namna hisia mbili zinavyotuendesha kwenye fedha, hisia za hofu ya kutokuwa na fedha na tamaa ya kuzitumia zimekuwa kikwazo kwetu kufanikiwa, sasa mwandishi anasema ukiweza kutawala hisia hizi mbili basi utakuwa pia umeweza kutawala fedha zako kwani fedha zinakuendesha kwasababu umeshindwa kutawala hisia zako.

Mwandishi anasema ujinga wa kutotaka kujifunza ndio sababu inayowafanya watu kuendelea kuteseka na fedha, watu wengi wakishahitimu masomo na hapo ndio inakuwa mwisho wa kujifunza na hapo ndipo wanapokubali kuendelea kuishi na ujinga wao, anasema watu hupenda kununua vitu vya kujionyesha na siyo kwasababu wana vihitaji na ni muhimu kwao kwa wakati huo,hayo yote ni matokeo ya ujinga wa kuto hitaji kujifunza.

Chukulia mfano Daktari anaongeza gharama za matibabu ili aweze kuongeza kipato chake, mwanasheria naye hivyo hivyo anataka kulipwa zaidi, mwalimu naye hivyo hivyo na mwisho wa siku mfanyabiashara naye anaongeza bei ya bidhaa na baada ya hapo serikali nayo inaongeza kodi na hivyo ndivyo ujinga wa fedha unavyo athiri jamii. Na pale tofauti ya wenye nacho na wasio nacho inapoongezeka na kuwa kubwa ndipo anguko la hilo taifa linapotokea.

Baada ya baba tajiri kuwaeleza Robert na Mike haya yote Robert akamuuliza kwa hiyo gharama hazitakiwi kuongezeka? Baba tajiri anawajibu kwa jamii inayoongozwa na serikali bei hazitakiwi kupanda bali kushuka.Akawaambia waendelee kufanya kazi bure huku vichwa vyao vikiendelea kufikiri ni kwa vipi wataondokana na mtego huo wa panya.

Robert na Mike Kila siku waliendelea kuwaza swali la wao kufanya kazi bila kulipwa, siku moja jumamosi wakiwa kazini walimuona yule anayewasimamia akichukuwa vitabu na kutaka kuondoka navyo ndipo wakamuuliza unavipeleka wapi? Akawajibu kuna sehemu anavirudisha ili kupewa vingine, basi walikwenda hiyo sehemu ya vitabu na kuuliza kama wanaweza kupatiwa vitabu vile na wakajibiwa inawezekana ila kwa sharti la kutoviuza.

Basi walivichukuwa vitabu vile na kwenda kuviweka nyumbani kwa kina Mike na walitumia sehemu ile kama maktaba na mkutubi akiwa ni msaidizi wa kazi wa kina Mike na watoto walikuja kusoma vitabu vile huku wakilipia, maktaba hiyo ilifunguliwa masaa mawili kwa siku na waliweza kupata dola 9 kwa wiki na walimlipa yule mkutubi dola 1,baadaye walianza kuwaza kufunguwa tawi lingine baada ya wateja kuongezeka, kwa bahati mbaya siku moja vurugu zilizuka pale maktaba na maktaba hiyo ikaamuliwa kufungwa.

Baba tajiri aliwapongeza kwa uthubutu wao na kuwaambia wasikate tamaa.

Rafiki yangu kwa Leo tuishie hapa tukutane tena wiki ijayo kuweza kuona kwa kina mafunzo yaliyo kwenye kitabu hiki, Asante na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Anza kujitawala kwanza ........



Habari za wakati huu rafiki yangu, ni jumapili nyingine inayotupa tafsiri kwamba wiki nyingine imeondoka, amini kwenye wiki hii wapo wengi ambao wamepitia changamoto kubwa kuliko unazopitia na hawajakata tamaa na wameendelea kusonga mbele je kwanini wewe ujiambie haiwezekani?Hebu Leo badilisha mbinu na jiandae kupeleka mashambulizi upya kwenye changamoto unazopitia, ukimshirikisha mungu na kuweka bidii hakutakuwa na wa kukuzuia........

Leo tunaendelea kubaki na falsafa, na Leo tutaangalia nukuu kutoka kwa mwanafalsafa ZENO anayetuambia "Man conquers the world by conquering himself" Hapa tunapata funzo kubwa kwamba huwezi kuitawala dunia kama umeshindwa kujitawala mwenyewe.

Huwa tunapenda kuwa viongozi bora tuweze kuongoza wengine, lakini huwezi kuongoza yoyote kama huwezi kujiongoza mwenyewe, kama unashindwa kujisimamia kwenye yale uliyopanga kuyakamilisha na Kila siku unajiambia nitaanza kesho je utaweza kumuongoza nani? Lazima wewe uanze kuwa mfano kisha dunia nzima itakufahamu na hata baada ya maisha ya hapa duniani bado utabaki kwenye mawazo ya watu.

Marekani wanafahamu karne ya 18 ilikuwa karne ya Marcus,karne ya 19 ilikuwa karne ya Jefferson na karne ya 20 ilikuwa karne ya Martin Luther king,hawa watu pamoja na kwamba walikuwa marekani lakini dunia nzima inatambuwa uwepo wao na vizazi  vingi vitapita na wataendelea kukumbukwa. Watu hawa waliweza kujisimamia na wakajiongoza na kisha watu wakaweka imani kwao na kuweza kuwafuata na kukubaliana nao.

Hivyo acha kuwaza mambo makubwa ya kutawala chochote kama huwezi kutawala fikra, hisia zako na hofu inakutawala,anza na wewe mwenyewe,anza na familia yako, anza ni jamii inayokuzunguka, taifa lako kisha Alama zako zitabaki na kusikika duniani.Asante sana na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251




Saturday, 20 June 2020

Udhaifu wa kuepukana nao.......



Rafiki yangu habari za wakati huu, bilashaka unaendelea vizuri,nikupongeze kwa kuendelea kujifunza kupitia ukurasa Wangu wa Ustawi wa fikra, hakikisha ufurahii tu kupata masomo haya hakikisha unachukua hatua za kubadilika, nimeona faida za kusoma vitabu nikajiambia sitokuwa Sawa nikipiga hatua peke yangu nikaamua kushiriki na wewe hivyo fanyia kazi mafundisho haya...........

Leo tutaangalia somo kutoka kwa wana falsafa wa kistoa, imeanza kuwa utamaduni kwangu Kila jumamosi kupitia mafunzo haya na hakika kama unahitaji utulivu hii ndio falsafa bora sana ya kutupatia utulivu mkubwa sana,falsafa hii haitaki kujielezea kwa watu kwamba wewe ni mstoa, wala kuandika masomo ya kistoa bali kwenda kuishi kwa vitendo yale utakayojifunza.

Leo kutoka kwenye falsafa hii tutajifunza jambo ambalo wengi tuna udhaifu nalo mkubwa sana, Kila mtu hapendi kuitwa dhaifu, tunapenda kuonekana ni jasiri,pamoja na matamanio hayo kuna mambo mengi tunayafanya tukiamini yanatufanya tuonekane jasiri kumbe ndio tunazidi kuwa dhaifu.

Hatuko tayari kuambiwa wazi wazi makosa yetu, hapa wana falsafa hii wanasema huu ni udhaifu mkubwa sana kwetu binadamu tulio wengi, tunapoambiwa makosa yetu lazima tutaanza kuangalia namna ya kujitetea na wakati mwingine kuwa tayari kuingia kwenye ugomvi na yeyote ambaye atatuonyesha makosa yetu wazi wazi.

Unaweza kuona wewe huna udhaifu huu lakini jiulize ni lini na nani alikukosoa na kukuonyesha makosa yako? Kama hakuna anayekukosoa je ni kwamba Kila unachofanya ni sahihi? Kama siyo sahihi basi inawezekana watu wamekuacha au umezungukwa na watu wasio sahihi, watu wa chini sana na ndio maana hawako tayari kukueleza ukweli pale unapokosea.

Mstoa Marcus Aurelius yeye alikuwa anatenga muda wa wa kuwashukuru watu walio mkosoa waziwazi na hilo lilimfanya awe jasiri zaidi na kuwa imara zaidi, hivyo rafiki kama unakasirika na huna mtu wa kujaribu kubeba ujasiri wa kukueleza makosa yako basi tambuwa una udhaifu mkubwa sana na hilo ndilo linalokufanya usipige hatua kwenye maisha yako, kwani watu wanaona makosa yako wazi wazi na hawapo tayari kukukosoa kwasababu wanafahamu hutokubaliana nao na wewe unaendelea kuamini akili yako iko sahihi kumbe wakati mwingine akili yako inakudanganya na kukufanya kuendelea kurudia makosa.

Asante sana rafiki yangu,nakupenda sana na sitoacha kushare upendo Wangu kwa kukuletea kile ninachojifunza,fanyia kazi haya na Nina hakika hutabaki kama ulivyo Leo.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Thursday, 18 June 2020

Kama mahitaji muhimu kwetu ni rahisi na yapo tele kwanini tunateseka?.......


Rafiki mungu alipoumba ulimwengu huu kabla ya kutuumba sisi binadamu alihakikisha mahitaji yote muhimu na ya msingi tunayapata kirahisi kabisa, na hapa ndio maana tuna amini kwamba dunia haijapungukiwa na chochote, Kila kitu kipo tele na kinapatikana kwa wingi, pamoja na yote hayo na dunia kua na utele bado binadamu tunateseka je kwanini? Hebu tuone mahitaji ya binadamu ya msingi ni yapi na utakubaliana na Mimi kwamba dunia inao utele.....

1.Hewa
Kupumua ni hitaji la binadamu, na ili tuweze kupumua vizuri tunahitaji hewa safi,je mungu alipo umba ulimwengu hukuweka hewa ya kutosha? Bilashaka ni hapana hewa ipo ya kutosha lakini watu kwa kuharibu mazingira na kukata miti, kuchoma misitu na kukua kwa sayansi na tekinolojia pamoja na viwanda tumeharibu mazingira yetu na magonjwa mengi kuibuka, na takwimu zinaonyesha vifo vingi hutokana na uharibifu wa mazingira. Pamoja na hatari hizo bado tunayo nafasi ya kurekebisha hilo kwa kuendelea kuyatunza mazingira yetu.

2.Chakula
Rafiki kwa asili sote tunakumbuka kwamba hapo kale binadamu hakua na nyenzo bora kama sasa, tunaweza kuona alitembea na kuokoteza matunda, baadaye aligundua moto na uwindaji ukafanyika,akaanza kula nyama ambayo ilibanikwa kwenye moto, baadaye akagundua kilimo,nakumbuka kijijini kwetu matunda yalitapakaa Kila eneo, lakini kwasababu ya uharibifu wetu tumepoteza vitu vyetu vya asili, Leo ukienda kijijini miti ya matunda imeharibiwa, ardhi yetu ilikua nzuri na yenye rutuba lakini Leo ugunduzi unatuambia tutumie mbolea, pamoja na kwamba tumeharibu ardhi zetu kwa kemikali lakini uharibifu ni mkubwa na vyakula vinaenda vikipungua, watu tumeacha kufuga wote tunataka kununua,je tutashindwa kuteseka?

3.Maji
Asilimia kubwa kwenye dunia tunayoishi tumezungukwa na Maji, Maji yapo ya kutosha lakini kwasababu ya uharibifu wetu tumeharibu na kuchafua vyanzo hivyo vya Maji na hivyo karne ya sasa huwezi enda mtoni na kunywa Maji kisha ukabaki salama, hata hivyo kutokana na akili na utashi wa binadamu bado tunaweza kupata Maji safi na salama.

Hayo ndio tunayoambiwa kwamba ni mahitaji muhimu, swali la kujiuliza ni kipi hapo ambacho hakihitaji fedha? Ukiondoa Hewa vingine vyote vinahitaji fedha ili uweze kuvipata na hata hewa kwa uharibifu wetu umefanya tuvute hewa chafu na kupata maradhi ambayo yatafanya twende hospitali ambapo bila fedha hatuwezi tibiwa, hivyo fedha ni hitaji kubwa ambalo kwa karne ya sasa tunalihitaji baada ya hewa ni fedha? Je fedha zina upungufu?

Kama fedha imekua muhimu kwetu basi amini hakuna upungufu wa kitu hicho, Leo tumeacha kufuga, nyumba zetu zimepambwa maua badala ya kulimwa mboga, miti ya matunda ni ya kutafuta, hakuna anayetaka kujishughulisha na kilimo, fedha zetu tunazozitafuta kwa shida zinapotelea huku na inafika sehemu tunamlaumu mungu kwamba ametuacha hatuna kitu, hebu tujifanyie tathimini upya kuna mahali tunakosea na hatutaki kulikubali hilo.

Asante sana rafiki nikutakie kazi njema, kwani huyu ndie rafiki wetu wa kweli tusikubali kukaa tu, kama ni mfanya kazi tumie siku za mapumziko kujishughulisha na kama tutakuwa na chakula cha kutosha Nina hakika hata matumizi mengine ya ziada tutayapata kirahisi tumekuwa wavivu na tegemezi sana ndio maana tunateseka.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Wednesday, 17 June 2020

Thamani ya kitu hupimwa kwenye vitu hivi vitatu......



Habari za wakati huu rafiki, hongera kwa siku hii nzuri, siku ambayo unakwenda kufanya zaidi ya Jana, naomba tuungane pamoja tuweze kuona ni vitu gani vinafanya kitu kingine kiwe na thamani kubwa na kingine kiwe na thamani ndogo?kama ni mfanyakazi au mfanyabiashara hapa ndipo patafanya watu wakulipe zaidi......

Baada ya wiki iliyopita kuweza kuona aina za vipato na kutambuwa ni aina gani inaweza kukupa utajiri basi wiki hii tuangalie misingi mitatu inayoamua thamani ya kitu unachofanya. JE KWANINI WATU WAKULIPE ZAIDI?

1.Uhitaji wa kile unachokifanya.
Rafiki kama unafanya kitu ambacho Kila mtu anakihitaji kweli basi thamani ya kitu hicho inakuwa kubwa, unaweza kuona malimao yalivyopanda bei msimu huu wa korona ni kwasababu Kila mtu aliaminishwa kwamba yanaweza kupunguza madhara ya kusambaa mwilini kwa ugonjwa huo.Hivyo kama huduma unayotoa si watu wengi wanahitaji basi hapo thamani yake inakuwa ndogo pia.

2.Upatikanaji wa wanaoweza kukifanya.
Kama kile unachofanya wapo wengi waliopo tayari kukifanya kitu hicho basi thamani yake inakuwa ndogo, hapa ndipo watu huona vingine vikithaminiwa zaidi ya vingine, Leo wewe ukiwa na digrii ya elimu na mwingine akawa na digrii ya urubani huhitaji kufahamu nani atalipwa zaidi hivyo hapo si kwamba mwalimu hana umuhimu lakini ni wangapi wako tayari kusomea urubani na wangapi wapo tayari kusomea ualimu? Hivyo kama Kila mtu yupo tayari kufanya unachofanya basi tambuwa hapo thamani yake ni ya chini.

3.Namna unavyokifanya kitu hicho.
Hapa mwandishi ametolea mfano wa makazini mfano hospitalini, unakuta Kila mtu akienda hospitalini anasema anataka kutibiwa na daktari fulani, ina maana hapo daktari huyo anayafanya tofauti na wengine na siyo kitu kingine, hivyo kama kitu unakifanya kawaida basi tumbuwa thamani yake inakuwa ndogo.

Rafiki ifahamu misingi hii mitatu na itumie kutengeneza thamani zaidi itakayotengeneza kipato zaidi, jiambie kuanzia sasa nitafanya kitu chenye uhitaji kwa wengi, kitu ambacho wengine hawapo tayari kufanya na nitakifanya kwa viwango vya juu sana kiasi kwamba Kila mtu atavutiwa na kukiona kina thamani ya juu sana na kuwa tayari kulipa zaidi.

Hapo umeshaona ni wapi unakosea kwenye kazi, biashara na Kila kitu unachofanya na sasa anza kubadilika taratibu kwa kujiwekea thamani zaidi. Asante tuonane wiki ijayo siku kama hii tutaendelea kupata chambuzi kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA,kujipatia nakala yako naomba tuwasiliane ni kitabu ambacho hakipaswi kukosekana kwenye shelvu yako ya vitabu.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Tuesday, 16 June 2020

Akili ya ndani katika safari ya mafanikio.......



Leo kabla sijakuambia nilichokuandalia naomba nikukumbushe kwamba hakuna chochote unachomiliki kwenye ulimwengu huu, vyote ulivyonavyo umeazimwa kwa muda na kuna siku mwenye navyo anaweza kuvichukua.Afya,Mali na utajiri, watu unao wapenda sana na chochote kile ulichonacho hata uhai wako umepewa kwa muda hivyo vipe thamani sasa ili vinapochukuliwa na aliyekupa usijutie na uwe imara kupokea matokeo.........

Rafiki yangu siku ya jumatano ni siku ambayo nakuchambulia kitabu cha THINK AND GROW RICH na hapa tunaangalia namna kufikiri kwetu kunavyosababisha ama tufanikiwe au kuendelea kuwa na maisha ya ufukara. Wiki iliyopita tuliona hatua tano za kufuata ili kujijengea uwezo wa kujiamini, nina imani ulizisoma na sasa hali ya kujiamini imeanza kujengeka, Leo tutaangalia aina za akili tulizonazo na namna zinavyofanya kazi.

Akili ya mwanadamu imegawanyika katika sehemu kuu tatu, yaani AKILI INAYOFIKIRI NA KUFANYA MAAMUZI(CONSCIOUS MIND),lakini pia ipo AKILI ISIYOFIKIRI WALA KUFANYA MAAMUZI ILA HUPOKEA TAARIFA INAYOINGIZWA (SUBCONSCIOUS MIND) na mwisho ni AKILI YA JUU KABISA INAYOTAWALA AKILI HIZI (SUPERCONSCIOUS MIND), hizi ndizo aina tatu za akili ambazo Kila binadamu anazo lakini namna tunavyoweza kuzitumia ndio kunatuletea utofauti.

Katika aina hizi tatu,akili ya ndani ambayo haifanyi maamuzi ina nguvu kubwa sana ya kuweza kupokea taarifa inayoingia kwenye akili yako.Pale taarifa hizo zinapofanywa kwa kujirudia rudia inatengeneza mambo hayo kuwa kweli. Hii ndio maana pale unapopokea sana taarifa zinazokujengea hofu ya kushindwa basi hali hiyo ya kushindwa itakuwa ikiendelea kwako na kama utajijengea mazingira ya kushinda basi hali hizo za kushinda zitaendelea.

Wakati nasoma eneo hili nilipata picha kubwa sana, Mimi kama mwalimu sitakiwi kumjengea mwanafunzi hali yoyote ya kumuonyesha yeye ni wa kushindwa hata kama anafanya vibaya kwenye mitiani yake, kwani hali hiyo ikijengeka kwenye akili yake anajiona ni wa kushindwa kwenye Kila kitu, vipi watoto zako hapo nyumbani? Nadhani sasa umeanza kuelewa kwani kama mwalimu wa DIAMOND alimwonyesha kwamba yeye ni wa kushindwa kwa kigezo cha mtihani sijuwi leo akikutana naye wanaongea nini?

Hivyo rafiki ipo njia ya kuitumia akili hii ya ndani na ikakufanyia kitu unachotaka, ipe amri akili yako ya ndani ili kutengeneza mazingira yatakayowezesha kufikia utajiri.Mwandishi anaita njia hii AUTO-SUGGESTION au SELF SUGGESTION hapa unaweza kuandika kwenye karatasi hitaji lako kubwa kwenye maisha yako na kulisoma Kila siku na kama utafanya hivyo huku ukiweka kazi na juhudi ya kupata kile unachotaka basi hakuna kitakachoshindikana,nimalizie kwa kumnukuu mwandishi hapa chini.

"Recall what has been said about the subconscious mind resembling a fertile garden spot,in which weeds will grow in abundance, if the seeds of more desirable crops are not sown there in"

Hivyo akili zetu za ndani ni mfano wa Shamba, kama utaliacha liwe na magugu hakuna mbegu itakayozaa ila ukilifanyia palizi na kuliwekea mbolea lazima litazaa na kustawi vizuri, hivyo kataa kabisa kauli hasi, hata kama wote watakuambia utashindwa wewe mwambie akili yako ya ndani hakuna kushindwa utanipa ninachotaka.

Asante sana rafiki na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Sehemu ya kipato changu ni mali yangu (III)......



Rafiki yangu hongera kwa afya na siku hii nzuri,hakika mungu wetu ni Mkuu sana tuna Kila sababu ya kumtukuza.........

Leo tunaendelea na sehemu ya tatu ya SEHEMU YA KIPATO CHANGU NI MALI YANGU na bila wasiwasi sasa umefahamu huruhusiwi kugawa fedha zako kwa Kila mtu na kujisahau wewe mwenyewe na nikuambie kitu kimoja kuhusu fedha, KAMA HUWEZI KUISHI CHINI YA KIPATO CHAKO hata ukipewa fedha kiasi gani utazitawanya na kurudi maisha yako ya awali, anza sasa kujijengea nidhamu ya kutumia chini ya kipato chako kwanza,haijalishi kipato chako ni kidogo kiasi gani tumia chini ya hicho unachopokea.

Tuendelee na simulizi ya Arkadi anayesimulia utajiri wake kutokana na ushauri aliopata kutoka kwa mtu mwenye hekima Algamish,kilipita kipindi cha takribani miaka miwili na tajiri Algamish alirudi na kukutana na Arkad na kumuuliza umeshaupata utajiri? Arkadi akamjibu hapana bado ila Nina vyanzo Vingi vya mapato ambavyo vinaendelea kumzalishia. Algamish akamwambia vizuri sana je bado unapokea ushauri wa muuza matofali? Arkad akasema labda kuhusu matofali na siyo vitu vingine.

Baada ya mazungumzo hayo Algamish akamwambia Arkad nimeshakuwa mzee sasa na kwakuwa umeshajifunza namna fedha inavyotengenezwa, Jinsi ya kuzitunza fedha na kivipi fedha inaweza kukufanyia kazi, yeye ni mzee na Mtoto wake anawaza namna ya kutumia fedha na utajiri wa baba yake. Hivyo akamuomba Arkad akawe msimamizi wa vyanzo vyake vya mapato. Arkad alikubali na alisimamia vizuri sana Mali zile na wote wakapata faida.Alikua anawapa simulizi hii wakamwambia Arkadi una bahati sana,Arkadi akawajibu mnasema nina bahati mmesahau nilivyoanza na kupoteza fedha zangu na kuvumilia kuanza tena? Wakamwambia je na sisi tukifuata ushauri huu tutakuwa na utajiri kama wako? Akawajibu mkiweka nguvu na jitihada lazima mtafanikiwa na fedha zinapatikana kwa njia za ajabu sana.

Rafiki hapa kuna funzo tunalipata, fedha inaanza kutengenezwa kwa kuishi chini ya kipato unachopata, fedha unazopata utaweza kuzitunza kama utapokea ushauri kwa watu wenye uzoefu wa kitu unachotaka kufanya, na kama utaiwekeza sehemu unayoifahamu itakufanyia wewe kazi badala ya wewe kuendelea kuitumikia kwa maisha yako yote.

Hayo ndio machache kuhusu fedha kwa kuanzia, wiki ijayo siku kama hii ya jumanne tutaendelea na sehemu nyingine kwa kuanza kuangalia ni namna gani tunaweza kutunisha mifuko iliyo sinyaa, zipo njia saba ambazo tunazipata toka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON naomba usikose hata somo moja na endelea kupitia masomo yaliyopita kwa kubonyeza;

https://kinyagakelvin.blogspot.com

Kinyagakelvin162@gmail.com

0763766944/0712161251

Monday, 15 June 2020

Tatizo ni kwamba huna na uifahamu elimu unayopaswa kuijua maisha yako yote ya hapa duniani.



Rafiki yangu nakukumbusha kwamba thamani unayolipwa ndio thamani yako halisi, huwezi kubali kwenda sokoni kununua embe moja kwa Tsh Milioni moja hata kama una fedha kiasi gani, ndivyo anayekulipa anavyoona thamani yako na kukulipa kile unachostahili, na wewe umelizika na kiasi hicho kwasababu hakuna anayekuhitaji ili akulipe zaidi, ungekua na thamani kubwa Kila mtu angekung'ang'ania na kutaka akulipe zaidi ili anufaike na wewe, sina la kukuambia kama unaona hustahili kulipwa unacholipwa jiulize ni nani anaweza kunilipa zaidi? Kwa thamani gani niliyo nayo?


Kama unasoma hapa nina hakika mtazamo wako unaanza kubadilika na kama unahitaji kupata ufafanuzi zaidi tuwasiliane kwani nimezungukwa na maarifa mengi sahihi na pia nimezungukwa na wana kisima cha maarifa zaidi ya mia mbili waliobobea kwenye Kila eneo, kuanzia udaktari, ufugaji, sheria, kilimo na Kila aina ya changamoto kama si Mimi basi nitakuunganisha nao na changamoto zako zitapungua hivyo usijiwekee mipaka kupata ushauri zaidi.

Leo tunaendelea na chambuzi ya kitabu cha RICH DAD, POOR DAD wiki iliyopita tuliweza kuona tofauti ya masikini na matajiri,MATAJIRI HAWAIFANYII KAZI FEDHA na hapo tuliweza kuona Robert na Mike wanapatiwa somo hilo na kuanza kulielewa. Sasa Leo tutaona ni namna gani fedha inaweza kukufanyia kazi wewe na mwandishi anasema elimu hii ndio elimu uliyopaswa kuifahamu na kuisoma maisha yako yote, lakini pamoja na utitili wa vyeti ulivyo navyo bado hujawahi kufundishwa ni kwa namna gani fedha itakufanyia kazi wewe badala ya wewe kuifanyia kazi fedha.

Mike na Robert somo lilipoanza kuwaingia Rich dad anawauliza mko tayari kuendelea na somo? Wakajibu ndio, akawaambia kama mko tayari basi mtaendelea kufanya kazi na safari hii siwalipi chochote, kwa mshangao Robert akabaki kuwaza kwamba amekuja kudai aongezewe mshahara badala yake halipwi kabisa!!? Nadhani hata wewe ungeshangaa. Rich dad akawaambia wachague kama wanataka kuwa kama wafanya kazi wengine atawaongeza mshahara mpaka kufikia dola za kimarekani 5 kwa saa ,kutoka kuwalipa senti kumi.Hapa Robert anasema kwa umri wake mdogo alikua anatamani sana kulipwa kiasi hicho lakini kwasababu somo la kutoifanyia kazi fedha lilikua limeingia alikaa kimya na kuto kubali ofa hiyo ili afundishwe ni namna gani fedha itakwenda kumfanyia kazi, basi baada ya kukataa ofa hiyo kubwa Rich dad akawaambia waendelee na kazi.

Robert na Mike waliendelea kufanya kazi bure bila ya kulipwa chochote, na Robert hakumwambia baba yake masikini (poor dad)kwamba anafanya kazi bila kulipwa kwa baba yake na Mike(Rich dad) na baada ya hizo wiki tatu kufanya kazi bila malipo Rich dad anarudi na kuwaambia waende matembezi pamoja, wakiwa matembezini anawauliza mambo yanakwendaje? Je kuna mambo mapya wamejifunza zaidi kwa hizo wiki tatu? Kwasababu kama mnataka kua na utajiri lazima mjifunze mambo mengi.

HISIA HIZI MBILI ZINAWEZA KUKUFANYA UWE MTUMWA WA FEDHA MAISHA YAKO YOTE, ZIFAHAMU NA ONDOKANA NA UTUMWA HUO.
Baada ya Rich dad kuona vijana wanavutiwa na somo la kutaka kufahamu namna fedha inavyowafanyia kazi Rich dad anawaambia nukuu hii ambayo nataka na wewe uifahamu.

"Most people have a price.And they have a price because of human emotions named fear and greed.First,the fear of being without money motivates us to work hard, and then once we get that paycheck,greed or disire starts us thinking about all the wonderful things money can buy."

Hapa rich dad anasema ukweli mtupu,hisia za hofu na tamaa ni hisia zinazofanya waajiriwa tuendelee kuwa watumwa,kwanza inaanza hofu ya kuto kua na fedha, hofu  hii inatusukuma kufanya kazi kwa bidii ili tulipwe na tukishalipwa fedha tunaingiwa tamaa ya kuzitumia fedha hizo. Hapa mwandishi anasema hili linatufanya tutengeneze kanuni ya AMKA, NENDA KAZINI, PATA MSHAHARA, LIPA MADENI.na kanuni hii inaendelea kwa maisha yetu yote, hivyo tunakuwa watumwa wa fedha kwa maisha yetu yote. Hisia hizi zinafanya kazi Kila fedha inapoongezeka tamaa ya kuzitumia inakuwepo na kukufanya uendelee na utaratibu huu. Na hapa mwandishi anaita utaratibu huu MBIO ZA PANYA kwani haziwezi kutufikisha popote pale kwenye kujikomboa ki uchumi.

Baada ya kumsikiliza baba tajiri Robert akauliza Je kuna njia nyingine? Baba tajiri akamjibu ndio ipo njia nyingine ambayo matajiri wanaitumia.Akawaambia wafanyakazi wengi wanapata hisia za hofu ya kutokuwa na fedha ila badala ya kuikabili kwa kufikiri wanakimbilia kutaka walipwe zaidi na hapo wanakuwa watumwa wa fedha kwa maisha yao yote.

Kwa Leo tuishie hapa rafiki, Kila jumatatu uchambuzi wa kitabu cha Rich dad, poor dad utakujia kupitia page hii ya Ustawi wa fikra, kama ulipoteza masomo yaliyopita bonyeza  https://kinyagakelvin.blogspot.com  na hapo utayapata yote, endelea tuwe sote kuna mengi sana utajifunza.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251


Sunday, 14 June 2020

Tatizo lako unapenda kujifunza wakati wa machafuko........



Wiki nyingine imekatika, kipi umefanya cha maana kwenye wiki hili? Kipi cha tofauti na wiki zilizopita? Kama ni chakula hata wanyama wa mwituni wamekula na kushiba, jiulize ni lipi la maana umefanya ambalo wanyama wengine hawawezi kufanya? Umeingiza shilingi ngapi? Umetumia shilingi ngapi?kipi umepanga kufanya wiki hili linaloaanza?

Wakati napitia kitabu cha Steve chandler cha 100 ways to motivate your self,Hamasa namba 5 ilisomeka hivi "LEARN TO SWEAT IN PEACE" hapa pakanivutia kusoma zaidi ndani nikakutana na sentensi inayosomeka "As they say in the Navy seals,the more you sweat in peacetime, the less you bleed in war"

Hebu ona mfano huo, hebu vuta picha wewe ni mwanajeshi na siku ambazo hakuna vita wala tatizo lolote hufanyi mazoezi yoyote ya kivita, unasubiria mpaka wakati wa vita ndio uanze kujifunza je utakwenda kushinda vita hiyo? Kama ni mjenzi utasubiria wakati mvua inanyesha ndio uanze kujenga? Kama ni mwanafunzi utasubiria mpaka wakati wa mitihani ndio usome, kama ni mgonjwa utasubiria mpaka umezidiwa kabisa ndio uende hospitalini, Je hakuna namna ya kushindwa kwa hayo yote, kwani huwezi subiria wakati wa vita ndio ujifunze mbinu za kivita na ukashinda. Sasa jiulize kwanini wewe unapenda kuendelea kuendesha maisha yako kwa mfumo huo?

Unasubiria hela ya kustafia ndio uanze biashara?
Huo ni wakati wa machafuko na lazima utashindwa kwenye hiyo biashara na wakati huo ukipoteza ni umepoteza moja kwa moja, wangapi umewaona wameanza biashara za usafirishaji, duka na baada ya muda mfupi kufariki? Usisubirie wakati wa machafuko kuingia vitani anza sasa ili upate uzoefu.

Unasubiria ufukuzwe kazi ndio uanze biashara?
Kila siku nakupa masomo ya namna ya namna unavyotegemea chanzo kimoja cha kipato ilivyo hatari, hebu fikiria bwawa linalotegemea Maji kutoka kwenye chanzo kimoja si lazima likauke? Bahari haikauki kwasababu inapokea Maji kutoka kwenye vyanzo Vingi vya mito ndio maana inaitwa bahari, kumbuka kuna siku kazi hiyo unayoilalamikia kwamba inakulipa kidogo itakua haipo tena, hicho kiduka kimoja au biashara yako moja uliyo nayo kuna siku itakumbwa na dhoruba na isiwepo kabisa, je hapo ndio utaanza kuchukua hatua?

Unaendelea kukaa kwa Wazazi, ndugu na jamaa hutaki kuanza na biashara ndogo kwasababu mama au baba wapo wanaendelea kukulisha,je unafahamu ni lini watu hao hawatakuwepo? Elimu yako nenda kaionyeshe kwa kujitegemea huo mchezo unaocheza ni hatari sana amka rafiki.

Yapo mengi sana ambayo binadamu tunasubiria mpaka wa machafuko ndio tuanze, ila ujumbe wa Leo unasema kadri unavyotoa jasho Leo wakati mambo yako shwari ndivyo wakati wa vita utakapofika utakavyo mwaga damu kidogo, lakini kama sasa unafurahia biashara moja uliyo nayo, kazi uliyo nayo, ndugu uliye naye basi tambuwa kuna siku vitu na watu hao hawatakuwepo na unaweza jifunza kwa wengine bila kusubiria wakati huo ufike.

Sitoacha ku kukumbusha rafiki yangu wakati mzuri wa kujifunza ni wakati huu usisubirie wakati wa mitihani hapo utakuwa umejiandaa kushindwa.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Friday, 12 June 2020

Kabla hujalaumu kwa lolote jiulize maswali haya mawili........



Nafahamu swala la bajeti linaendelea hapo ulipo,sielewi mnajadili nini lakini hiyo ni bajeti ya nchi,vipi yako?je ipo tayari? Pamoja na yote mtakayojadili kumbukeni bajeti ya nchi ina gawanyika sehemu mbili matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo je wewe yako ina matumizi ya kawaida pekee au na bajeti ya maendeleo umeweka? Hayo ndio yatakua na umuhimu kwako mengine yote hapo ni kelele tu .........

Rafiki yangu sisi binadamu ni viumbe ambao ni wepesi sana kulalamika, vipo vitu vingi ambavyo tunaona tuna haki kulalamika, kabla sijafahamu hasara za kulalamika sikuwahi kufahamu ni kwa namna gani najichelewesha kwa kulalamika, kuna siku nilimuuliza rafiki yangu anitajie faida za kulalamika na aliponitajia ndipo nikagundua kuna sehemu kuna shida kwenye kulalamika kwetu,kwenye kitabu cha Be rich and happy mwandishi ametupa sababu mbili zinazofanya tulalamike na sababu hizi zimefanya niwe najiuliza maswali mawili kabla sijalaumu kwa kitu chochote, naomba na wewe ujifunze na kujiuliza maswali haya.

1.Ujinga Wangu uko wapi kwenye hili ninalolalamikia?
Mwandishi anasema sababu moja wapo inayofanya watu walalamike ni ujinga walio nao wa kushindwa kufahamu ufumbuzi sahihi wa matatizo yao, unalalamikia bosi wako, wateja wako kwenye biashara, serikali, ndugu na hata Wazazi kwasababu ya ujinga wako, mtu mmoja amewahi kusema mke wangu amebadilika sana na sielewi kwa nini?angejiuliza swali la ujinga Wake uko wapi asingelalamika kwetu,kwanza angefahamu ujinga wake ni kujaribu kulalamika kwetu kuhusu mke wake, mbili angefahamu kwamba watu hawabadiliki ila wanatoa makucha yao baada ya kujaribu kuficha kwa muda mrefu, tatu wakati anaoa alifanya maamuzi peke yake je anavyoshirikisha wengine huo si ujinga? Hivyo jiambie siku zote Mimi ni mjinga ndio maana na lalamika na si vinginevyo.

2.Nina danganya nini kwenye hili ninalotaka kulalamikia?
Sababu zote unazojipa kwamba ni za msingi na ni haki yako kulalamika basi tambua kwamba zote ni za uongo na sababu za kweli zitakazofanya uchukue hatua sahihi hutaki kuzisema kwasababu zina kugusa mwenyewe, unalalamika kwamba serikali haijakupa nafasi ya kazi na umesoma?basi huo ni uongo kwasababu zipo sababu zingine za kwamba hutaki kuonekana wa chini na kujishughulisha na chochote cha kukuingizia kipato, unalalamika kipato ni kidogo na bosi wako ndio tatizo kwani hakulipi vizuri, huo wote ni uongo na ukweli unaukwepa kwasababu unakuhusu wewe kwani umezoea kuishi kwa mazoea na hutaki kubadilika.

Hebu jiulize wale wa piga picha walio tupiga picha na kusubiria zikasafishwe mwanzo walisema nini sababu ya biashara zao kua mbaya? Ulishawahi jiuliza simu za motolora, Nokia, Philips na zingine nyingi zilizotoka kama matoleo ya mwanzo wangeendelea kukomaa na aina ile ya simu vipi wasingesema biashara ni mbaya kwa kisingizio cha uchumi?Hebu acha kuwaza mawazo yaleyale kwa kutegemea matokeo tofauti, usilaumu biashara zimekua ngumu kwasababu yoyote ile bali jiulize mwenyewe UJINGA WANGU UKO WAPI?NI LIPI NATAKA KUJIDANGANYA MWENYEWE? baada ya kujipa maswali hayo utagundua ujinga wako wote na uongo unaotaka kuaminisha wengine na kupata majibu sahihi ya kusonga mbele. Acha kulalamika chukua hatua.Ukichaa ni matokeo ya kujaribu kukwepa majukumu yako, tuendelee kuwa pamoja,nakupenda daima.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Thursday, 11 June 2020

Usipime utajiri wako kwa kiasi cha kipato unachotengeneza pekee bali pamoja na njia unazotumia kutengeneza kipato........,.


Nakusalimia ndugu yangu, mfanyakazi unaye subiria kwa umakini kuona bajeti ya mwaka huu inakwendaje kubadilisha maisha yako, nakupa pole kwasababu hicho unachokitarajia ni zaidi ya utumwa kwenye maisha yako hebu pata muda na waza kwa kina huko nyuma umeongezewa mishahara mingapi je kipi ulifanyia? Je matatizo ya kifedha yalikwisha? Hebu jaribu kuwaza nje ya box uondokane na utumwa huo......

Rafiki yangu Leo tuangalie maana ya neno KIPATO na  aina za vipato pamoja na kipato kitakacho amua Uhuru wako kifedha, wiki iliyopita niligusia eneo la fedha na sheria zake, pamoja na kwamba najitahidi kugusia maeneo mengi lakini yapo maeneo mengi naruka kwani siwezi kukuchambulia Kila kitu, nakushauri tuwasiliane nikuambie ni namna gani unaweza jipatia kitabu hicho cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA.

KIPATO maana yake nini? Kipato ni ile fedha unayolipwa kutokana na kufanya au kuwezesha kitu fulani kufanyika.Inaweza kuwa ni kazi ambayo umefanya wewe au bidhaa na huduma ulizotoa kwa wengine ambazo wanazihitaji ili maisha yao kuwa bora. Hapa unaweza kuona kwamba namna ya ukubwa wa huduma au matatizo ya wengine unavyoweza kuyatatua ndivyo na wingi wa fedha ulivyo. Ndio maana masomo yaliyopita tuliona kwamba fedha ni matokeo ya thamani unayotoa kwa wengine. Kila mmoja wetu anaingiza kipato kwa namna yake mwenyewe, wapo walio ajiriwa na walio jiajiri wenyewe.

Wengi tunatamani kupokea kipato kikubwa lakini hatufahamu kwamba kwa kuendelea kufanya kitu kile kile tutaendelea kupokea kitu kile kile, kama unataka kupata kipato kikubwa zaidi basi ongeza wigo wa kutatua matatizo ya wengine siyo kung'ang'ana na kitu kile kile. Pamoja na utofauti wa majukumu yetu tunayobeba na kutuingizia kipato zipo aina kuu mbili tu za kipato,ambazo unapaswa kuzifahamu kwa kina na umuhimu wake kwenye maisha yako.

1.KIPATO CHA MOJA KWA MOJA(ACTIVE INCOME)
Kipato chochote ambacho unakipata kwa kutegemea uwepo wako moja kwa moja ndio ulipwe hicho ni kipato cha moja kwa moja. Kama umeajiriwa basi lazima uende kazini ndio ulipwe, Kama ni mfanyabiashara lazima uwepo eneo la biashara ndio uingize kipato, changamoto za kipato hiki ni kwamba kina ukomo kwasababu huwezi kuwa sehemu nyingi kwa wakati mmoja, kipato hiki kinahitaji masaa yako ambayo hayawezi kuzidi 24,hivyo hata kama unalipwa kiasi kikubwa namna gani bado huwezi kuwa na Uhuru kifedha na ndio maana wengi tunao ingiza kipato kupitia njia hii pale tunapofariki kama ni familia Mara moja inaanza kuhangaika kwani na kipato kinaondoka Mara moja.

2.KIPATO KISICHO CHA MOJA KWA MOJA (PASSIVE INCOME)
Hiki ni kipato ambacho kinaingia hata pasipo uwepo wako wa moja kwa moja kwenye shughuli inayokuingizia kipato. Ukiwa umelala kipato kinaingia, uwe matembezini na familia kipato kinaingia.Hapa kipato kinaingia kwasababu ya uwekezaji ulio fanya.uwekezaji kwenye hisa au riba unayopata kutokana na fedha ulizowekeza.

Rafiki nafikiri sasa umeweza kuona ni kipato gani unakihitaji kati ya vipato hivyo viwili, baada kujijengea usomaji wa vitabu kwa muda mrefu nilipata kupenda kujifunza falsafa ya ustoa na katika mafunzo hayo lipo swali ambalo huwa napenda kujiuliza FAMILIA YANGU ITAISHI VIPI KAMA NITAKUFA SASA HIVI?sasa kama kipato changu kitaendelea kuwa cha moja kwa moja nadhani unafahamu hali itakuwaje.

Hivyo rafiki pambana siku zote ufahamu namna ya kuwekeza na tena anza kuwekeza sasa hivi, kabla sijawa member wa KISIMA CHA MAARIFA niliamini uwekezaji ni kwa watu wenye vipato vya ubilionea lakini baada ya kujifunza nimeweza kuanza kuwekeza taratibu na kwa kipato hiki hiki unachokiona ni kidogo, kutaka kufahamu ni kwa vipi unaweza kuwekeza karibu sana KISIMA CHA MAARIFA sehemu itakayo badili maisha yako.Rafiki wewe ni wa thamani kwangu ndio maana unapokea makala hii, nakupenda daima na mungu akubariki.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Wednesday, 10 June 2020

Hivi ndivyo unavyoweza kujifungua na vifungo ulivyojifungia kwenye maisha yako na kuwa huru tena.........



Rafiki wale wanao amini kwenye ushirikina na uchawi huwa wanayo imani kwamba kuna binadamu anaweza kufunga au kuchukua nyota zao, hivyo hutembea kwa waganga wa kienyeji ili waweze kuludishiwa nyota zao. Haya yote yanatokana na uelewa mdogo wa namna gani unaweza jifunga au kujiweka huru na kifungo kupitia imani ulizonazo mwenyewe.........

Wiki zilizo pita tuliweza kuona namna shauku na imani zilivyo na nguvu kuamua hatima za maisha yetu na mwandishi wa kitabu cha THINK AND GROW RICH anatuambia, pale tunapokosa imani tunakua na hali ya kutojiamini na kutojiamini kuna tujengea  hofu na hofu ndio kitu kinachotuangusha sana.Leo tutaangalia hatua tano za kutujengea kujiamini.

Kabla hatuja angalia hatua hizo tano tunapaswa kuelewa kwamba jamii inao mchango mkubwa sana wa kutujengea hali za kutojiamini, hebu jiulize kwenye familia yako Mtoto anakemewa Mara ngapi kwa siku pale anapojaribu kufanya vitu tofauti tofauti? Je kufokewa huko kunakwenda sambamba na pongezi? Shuleni je? Makazini nako? Sasa twende tuone namna ya kujijengea hali ya kujiamini kwenye maisha yetu.

Mwandishi anaita FIVE SELF CONFIDENCE FORMULA.
1.Jiambie "Ninafahamu ninao uwezo na nafsi yangu itaweza kuvumilia na nitaendelea kuchukua hatua mpaka nitakapo pata ninachotaka.

2.Mawazo ninayotengeneza yatakua kweli,na Kila siku nitaweka picha ya kile ninachotaka kwenye mawazo yangu mpaka kitimie.

3.Kujiamini kutaniwezesha kufikia kile ninachohitaji na Kila siku nitajijengea kujiamini.

4.Kwa kua nimeshajiwekea lengo na dhumuni sitoacha kujaribu Kila namna mpaka nilifikie.

5.Ukweli na haki ni msingi kwenye utajiri Wangu, hivyo kama biashara ninayofanya haiwafaidishi wengine sito ifanya, wivu, chuki, majungu na ubinafsi havitakua na nafasi kwenye maisha yangu na nitawapenda binadamu wote kwani mawazo hasi dhidi ya wengine havita niletea mafanikio.

Baada ya kuandika hatua hizo tano mwandishi anasema weka sahihi na Kila siku rudia kusoma hatua hizo na hali ya kujiamini itajengeka na hapo utakua umejitoa kwenye hofu na kutoogopa changamoto yoyote.

Your are "the master of your fate, the captain of your soul" because we have the power to control our thoughts.

Hakuna yeyote anayeweza kutawala uwezo wako wa kufikiri hivyo kwa kutambua hilo unaweza kua vyovyote vile unavyotaka, tambua hilo na litumie rafiki yangu.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Tuesday, 9 June 2020

Sehemu ya kipato changu ni mali yangu (II)......



Kama hakuna mtu anayekuambia unakosea basi unafanya vitu vya kawaida sana, rafiki yangu usiache kufanya kitu kwa hofu ya kukosea kwani kwenye makosa yako ndipo palipo na mafanikio yako, kubali kokosolewa ili uwe imara.........

Rafiki yangu wiki iliyopita tuliweza kuona na kutambuwa kitu kikubwa sana kwenye maisha yetu,kitu kinachotupa mwanzo wa mafanikio, SEHEMU YA KIPATO CHANGU NI MALI YANGU kama umeanza kufanya hivyo basi umeanza kuelekea kwenye utajiri,usisubilie mpaka uwe na fedha nyingi ndio uanze kutenga sehemu ya kumi ya kipato chako, haijarishi una madeni au huna anza kutenga sehemu ya kumi ya kipato chako kwa ajili ya maisha yako baadaye, kama laki moja haitoshi basi ni Sawa na ukitoa elfu kumi ukaitenga na kubaki na elfu tisini, huwezi jiambia maisha yamekuwa magumu kwasababu umetoa elfu kumi, mwepesi kutumia hela ambayo hujapokea kwa kukopa ili ukipokea ulipe kwa riba lakini mgumu kutoa asilimia kumi ya kipato chako na kuweka kwa ajili ya baadaye.Hebu tuendelee na simulizi yetu.

Baada ya Arkad kufahamishwa na tajiri Algamish kwamba kwa kuamua kutenga sehemu ya kumi na kuiwekeza kwa ajili ya kuiwekeza ili baadaye iweze kumzalishia alianza kufanyia kazi swala hilo Mara moja, kipindi cha huko nyuma watu walitumia dhahabu kama fedha, hivyo namna ya kuhifadhi ilikuwa ni kuifukia ardhini lakini kwa sasa hivi tuna benki ambazo unaweza kufunguwa akaunti na kuanza kuweka asilimia kumi ya kipato chako, bank zote kubwa wana huduma hizo CRDB,NMB,NBC na zingine kubwa, unaweza fika na kukubaliana nao kisha ukaanza kuweka asilimia kumi ya kipato chako kwa muda utakao jipangia bila kuzitoa na baada ya muda uliopanga kuisha unakwenda kuchukuwa fedha zako na faida kidogo kisha kuziwekeza sehemu uliyokusudia.

Basi Arkad anasema baada ya miezi kumi na mbili kuisha tajiri yule alirudi na kumuuliza kama alifanyia ushauri ule aliompatia, Arkadi akamjibu nimefanya kama ulivyonishauri bila kuacha, tajiri yule akammwambia vizuri sana je umeifanyia nini akiba yako hiyo? Arkadi akamjibu nimempatia Azmur mtengeneza matofali, amesafiri kwenda nchi za mbali na amesema atanunua madini  adimu na akirudi tutayauza na tutagawana faida.

Tajiri yule akamwambia Arkad wewe ni mjinga utaaminije ushauri wa mtengeneza matofali  kuhusu madini?akamwambia tayari umeshapoteza fedha zako anza kuweka tena upya, na kweli baada ya mtengeneza matofali kuludi anakuja na madini bandia katapeliwa. Hapa tunapatiwa funzo moja, uwekezaji ni kitu kinachowekezwa kwa umakini mkubwa sana, usiwekeze fedha zako sehemu usiyo ifahamu, lazima ufahamu kwa kina ni namna gani hapo unapowekeza patakupa faida na omba ushauri kwa mtu ambaye anafahamu kwa kina kile unachotaka kuwekeza, watu wakifahamu kwamba una fedha hupenda sana kutoa ushauri hivyo kuwa makini kupokea ushauri.

Arkadi alianza upya kutenga asilimi kumi upya na baada ya miezi kumi na mbili mingine kupita yule tajiri alirudi na kumuuliza Arkadi fedha ulizotenga umewekeza wapi? Akasema nimempa mkopeshaji anakopesha watu halafu faida tunagawana, tajiri akamwambia vizuri sana, Je faida unayopata unaitumiaje? Arkad akamwambia huwa na sherehekea na ana mpango wa kununua farasi ya kutembelea, zamani farasi walitumiwa kama Leo tunavyotumia gari, Algamish mtu tajiri alicheka akamwambia unakulaje watoto wanao kufanyia kazi wewe? Endelea kutumia faida kuwekeza ili baadaye ikutumikie uishi vizuri zaidi.Basi Arkad akapokea ushauri ule.

Hapa tunajifunza kwamba watu huwekeza kweli na baada ya muda kuanza kuona faida hukimbilia kununua anasa na kisha kurudi kwenye maisha yaleyale ya kuifanyia kazi fedha, tunatakiwa kuwekeza na pale faida inapokuwa kubwa kiasi cha kuweza kufanya matumizi ambayo hayakuzalishii fedha.

Rafiki nadhani unaweza kuanza kupata picha ni kwa namna gani fedha inaweza kukufanyia kazi na siyo wewe kuifanyia kazi fedha.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251


Monday, 8 June 2020

Hivi kazi nzuri ni ipi?....



Haijarishi unafanya kipi ilimradi kinakuingizia kipato una Kila sababu ya kumshukuru mungu kwa hilo, karibu rafiki yangu tujifunze pamoja......

Rafiki yangu zipo hadithi ambazo tumezizoea mashuleni, kwa familia zetu zikitutaka tusome kwabidii ili tuje kupata kazi nzuri yenye kutupatia maisha yenye furaha, Je ulishawahi kujiuliza kazi nzuri ni ipi?wakati ukitafakari jibu la swali hili hebu tuendelee na hadithi ya Mike na Robert.

Wiki iliyopita tuliona namna Robert alivyokasilishwa na namna baba yake Mike alivyowafanyisha kazi kwa malipo kidogo na ikafikia wakati Robert alihitaji kuacha kazi kwani alichokitegemea hakipati na analipwa ujira kidogo na hapo Baba tajiri ambaye ni baba wa Mike anampa somo la kwanza ambalo na wewe unapaswa kulifahamu ambalo matajiri wote wanaijuwa siri hiyo kwenye fedha.

MATAJIRI HAWAFANYII KAZI FEDHA.

Rafiki baba huyu tajiri aliwaambia Robert na Mike kwamba watu wengi hufanya kazi ili walipwe na siku zote hulaumu waajiri wao kwamba ni sababu ya maisha magumu kwani hawawalipi vizuri na kuwaza hivyo kunawanyima kuwapa fursa ya kuona makosa upande wao na wamekuwa wakizifanyia kazi fedha badala ya kuona ni namna gani fedha zinaweza kuwafanyia kazi wao.

Robert akamwambia kama ni hivyo basi sipo tayari kuendelea kulipwa kidogo ni bora niache kazi nikatafute kazi nyingine na baba yake Mike anamwambia na hivyo ndio wanavyofanya watu wengi pia huhangaika wakitafuta kazi nyingine kwa kudhani huku watatatua matatizo yao ya kifedha kumbe kadri wanavyolipwa zaidi ndivyo changamoto zinapngezeka, akampa mfano wa baba yake ambaye ni msomi wa PHD lakini bado ana matatizo kibao ya kifedha, akawapongeza kwa kutokubali kulipwa kidogo lakini kuondoka na kutafuta kazi nyingine siyo suruhu ya kumaliza matatizo yao.

Hapa rafiki tunapewa funzo kwamba watu wengi tunadharau kazi tulizonazo kwa kipimo cha malipo na kutamani kazi fulani za wengine na wakati mwingine kwa kuongeza elimu na jitiada mbali mbali tunafanikiwa kuzipata kazi hizo, pamoja na malipo mazuri bado changamoto za kifedha zinaendelea. Watu wengi hudhani kazi nzuri ni inayokulipa zaidi lakini matajiri wanafahamu kazi siyo tatizo tatizo ni elimu ya namna fedha inavyoweza kukufanyia kazi.

Baada kupewa somo hilo Robert na Mike walianza kuelewa lakini akauliza ni njia gani nitaitumia kutengeneza fedha zaidi? Rich dad akamwambia tumia kilichopo ndani ya kichwa chako, hicho ndio kitu pekee kitakachotatua matatizo yako ya kifedha.

Rafiki hapa tunapata funzo kwamba usilizike kulipwa kidogo maisha yako yote na wala usifikirie kwamba kazi inayokulipa kipato kikubwa itazimaliza changamoto zako za kifedha bali tumia ubongo wako kufikili namna fedha unayopata inaweza kukufanyia kazi wewe na hili litakuondolea matatizo yako yote ya kifedha. Asante sana rafiki na nikutakie siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944 /0712161251.

Sunday, 7 June 2020

Una mchango wako kwenye mambo kwenda vibaya.....



Habari za jumapili rafiki, ni kawaida yangu Kila mwisho Mwa wiki kujiuliza maswali kadhaa,wiki imekwisha nimejifunza nini? Nimefanya jambo gani litakalofanya nitimize ndoto zangu? Yapi nimefanya sahihi na yapi sitakiwi kuyarudia kufanya? Kama kuna changamoto ni namna gani naweza zikabili? Nakuomba na wewe upate muda huo ni muhimu sana.....

Rafiki huwa tunashindwa kwenye mambo mengi kwa kuamini kwamba wengine wametusababishia lakini hilo siyo sahihi na tafiti zinaonyesha mambo yanavyokwenda vibaya Kila mtu anao mchango wake, na ndio maana tunaambiwa mambo yakienda vibaya nenda kwenye kioo chako na yule unayemuona ndiye anapaswa kulalamikiwa.

Kocha wa mpira wa miguu Paul Bryant alikuwa akipenda kusema hivi "Jambo likiharibika jiambie ni Mimi nimelifanya, likienda vizuri kidogo sema ni sisi tumelifanya na likienda vizuri sana sema ni nyie mmefanya"

Hii ni kauli ya hekima sana, kauli inayokuondolea hali ya kulaumu wengine na kuona kasoro zako kirahisi na kwakufanya hivyo utapiga hatua kubwa sana rafiki yangu, nenda kaishi kauli hii siku zote na hakika utakuwa imara sana.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Saturday, 6 June 2020

Kazi yako ni kuwaongoza na kuwaelekeza na siyo kujaribu kuwatatulia matatizo yao yote yanayowakabiri.......



Hongera sana rafiki yangu, kama unajaribu kupunguza mateso kwa wengine ni kazi nzuri sana unafanya na endelea, watu wanateseka kwa kukosa upendo basi wasambazie upendo, watu wamekata tamaa ya kuendelea mbele wakumbushe jukumu lao, usimseme yoyote vibaya kama yeye hayupo hapo nenda kamfate mweleze atakuelewa kama amekosea na kurekebisha, je bado una kinyongo na mtu? Chuki haiwezi kukusaidia nenda kamwonyeshe upendo Leo anayekuchukia........

Leo tutaangalia sehemu ya malezi kwa watoto wetu, Kila Mzazi hapendi kuona Mtoto/watoto wake wakiteseka, hapendi waje kuhangaika na maisha ya baadaye,tunatamani kuona maisha yao yanakuwa mazuri.

Bahati mbaya sana pamoja na matamanio hayo hatuwaandai watoto wetu kuwa bora, kwani tunajaribu kuwaonyesha kwamba Kila kitu ni rahisi, Kila wanachotueleza tunapambana kuwapatia lakini je huo ni uhalisia wa maisha?Je maisha yatatupa Kila tunachohitaji?

Thomas Edison ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa sana na yeye ni miongoni Mwa mzazi ambaye alitamani sana watoto wake wawe na maisha mazuri lakini njia alizozitumia na ambazo wengi tunazitumia kulea na kuwaandaa watoto wetu hawawezi kuwa vile tunavyotaka na hilo lilimfanya mke wake amwandikie ujumbe ambao nitauweka hapa chini, ujumbe huo ulisomeka hivi;

 “You’ve made a success of your life,” she wrote, “built up tremendous industries successfully so you have nothing more to prove to the world that you are capable—All know it—Can’t you be happy in just letting the boys struggle along, with you to guide them… Forget a little bit that you are Charle’s manager and be a father—a big father!”

Sasa hili ndilo linatukumba Wazazi tulio wengi, hatuwezi wapa nafasi watoto wetu wakajisimamia, muda wote tunahitaji watutegemee sisi kwa Kila kitu, kama tunataka wakue,wajifunze na wawe na maisha mazuri basi waache wapambane wenyewe na kazi yako kubwa ni kuwaongoza tu, siyo Kila anachohitaji unampatia labda utaishi nae maisha yako yote.

Kazi yako ni kuwa baba na siyo boss kwa watoto wako, kama familia inakuchukulia wewe ndio boss wao basi fahamu kwamba kuna siku utalia machozi na hakutakuwa na wakukufuta machozi.

Asante na siku njema rafiki yangu.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Friday, 5 June 2020

Hizi ndizo zawadi za thamani unazopaswa kuzitumia ipasavyo na kuzitunza.........



Rafiki yangu ulishawahi kuwaza kwamba kuna siku unaweza pata ajari na ukavunjika mikono yote miwili,umeshawahi kuwaza kwamba kuna siku unaweza kuamka ukajikuta ni kipofu? Je vipi kama kuna kansa inaendelea kukutafuna taratibu lakini hujaitambuwa bado? Rafiki lengo langu siyo kukutisha kwani vitu hivi vinaweza mkuta yeyote, swali unalopaswa kulifikiria ni je mikono niliyopewa bure, macho na afya kwa ujumla navitumiaje?......

Leo rafiki nitakuambia Zawadi nne zenye thamani kubwa ambazo unapaswa kuzitambuwa na kuzitumia ipasavyo, Zawadi hizi zimeandikwa kwenye kitabu cha Robert kiyosaki cha BE RICH AND HAPPY na ukishazifahamu nenda kuziishi na kuzitumia ipasavyo.

1.Afya(Health);
Hii ni Zawadi kubwa unayopaswa kuitunza kweli kweli, afya ya roho, mwili na akili ni hitaji muhimu sana kwa maisha, hakikisha mwili wako unaufanyisha mazoezi kwani Maji yaliyotulia ni mfu na mwili usio na mazoezi ni mwili wenye magonjwa,hakikisha roho yako imeshiba kweli kweli amini kuna mungu na tenda yale yanayo mpendeza, mwili wako ndio nyumba ya akili na roho hivyo utunze sana, usiruhusu uchafu kuingia mwilini mwako na unakula vyakula na lishe bora, mwili wako unapaswa kupumzishwa, yote unayoyaangaikia sasa ni kazi bure kama Afya yako itatetereka, kuna watu hata ukiwapelekea mamilion ya fedha kwao ni kazi bure kwani afya zao zimetetereka hawajuwi wafanye nini.

2.Mahusiano
Unaweza ona  mahusiano yako na wengine ni kitu cha kawaida, ndoa yako kama umeoa au kuolewa, Wazazi, ndugu jamaa na marafiki zako wa kweli ni watu ambavyo ni wa thamani sana, kuna wengi walifika mbali sana lakini walipojaribu kupuuza watu wao wa karibu walipata mahangaiko makubwa sana, hivyo kuwa mwema kwao na usipuuze neno mahusiano ni Zawadi ya muhimu sana.

3.Kuheshimu watu wenye mafanikio
Hapa mwandishi anasema hivi

"I have found that what I hate in others I become and what I love in others I become"

Hakuna mtu asiyehitaji mafanikio na huwezi kupata mafanikio kwa kuwachukia waliofanikiwa, ninaweza kukuambia hili kwa namna pana sana lakini amini matajiri wanapenda sana watu waliofanikiwa na na kama unaona matajiri ni watu wabaya basi ninakuambia utakuwa masikini maisha yako yote kwani kile unachokichukia ndio ulichonacho, kama unamchukia mtu ina maana chuki ipo ndani mwako, basi kuanzia sasa tambuwa waliofanikiwa ni Zawadi kubwa sana kwako, huna gari lakini unasafiri, siyo daktari lakini ukiumwa unatibiwa, huna kiwanda cha nguo lakini unavaa nguo, hivyo heshimu waliofanikiwa na ona ni watu wanakufanya wewe uwe hivyo ulivyo na pambana ili uwe upande wa waliofanikiwa.

4.Kila siku yako moja ni Zawadi kubwa sana kwako.
Tatizo letu sisi binadamu kubwa ni mazoea, kwakuwa leo umeamka salama unajihakikishia kwamba na kesho utaamka salama lakini hilo siyo sahihi kabisa, Kila kunapokucha ona ni bahati ya pekee sana na itumie kwa kufanya yaliyo sahihi pekee, hivi unafahamu 80% ya mambo unayofanya hayana mchango wowote kwenye mafanikio yako? Ni asilimia 20% pekee ndio vitu vya maana, muda unaoangalia TV, kusema wengine na ushabiki usio na maana ni vitu visivyo na maana kabisa kwako.

Hizo ndizo Zawadi za kipekee kwenye maisha yako yote, zitunze sana kwani Kila siku yako moja mbele inapunguza siku zako za wewe kuwa hapa duniani, sambaza upendo kwa Kila mtu Kila siku, asante sana na nikutakie siku njema rafiki.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Wednesday, 3 June 2020

Kila unachopitia ni wewe ndio umekivuta........



Rafiki yangu acha kuwaza matatizo yako muda wote, kwani kwa kufanya hivyo unaendelea kuyavuta matatizo kwako, jukumu lako ni kuwaza namna sahihi ya kuondokana na matatizo hayo kwa mtazamo chanya......

Rafiki yangu matokeo uliyonayo sasa husababishwa na namna unavyofikiri, ipo nguvu kubwa inayoendesha maisha yetu, dhana hii inaitwa nguvu ya mvutano (LAW OF ATTRACTION) Sheria hii inasema kwamba Kila kitu ambacho tunacho kwenye maisha yetu,tumekivuta sisi wenyewe. Kuanzia kwenye fedha, mke uliyenaye au mume,huzuni au furaha, utajiri au umasikini,na mambo mengine mengi, mfano marafiki ulio nao ni Tabia zako na namna unavyofikiri ndio kumewavuta kwako.

Rafiki yangu nguvu hii inakufanyia maamuzi mengi sana, kama unafikiria fedha ni nzuri basi unaivutia kwako lakini kama unafikiria fedha ni mbaya na ni chanzo cha uovu basi fedha inakaa mbali na wewe, Jana tuliona nguvu ya Imani, hivyo anza kuona uzuri uliopo kwenye fedha huku ukiweka bidii hilo litakufanya uivutie pesa na ona changamoto kama fursa na siyo matatizo. Jiulize NAWEZAJE KUPATA FEDHA na siyo SIWEZI KUPATA FEDHA HIZO kama kitu ni muhimu jiambie unawezaje kukipata.

Rafiki kwa kuwa na mtazamo sahihi kwenye fedha kunakufanya uzivutie fedha zaidi, hebu tuangalie sheria tano za fedha unazopaswa kuzifahamu. Kutoka kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA mwandishi amezifafanua vizuri sana.Sheria hizi amezisoma kwenye kitabu cha The richest man in the Babylon ambacho nacho tunaendelea na uchambuzi wake.

1.Sheria ya kwanza ni KUJILIPA MWENYEWE;
Kanuni hii inasema kwamba fedha huenda kwa mtu ambaye anatenga siyo chini ya sehemu ya kumi ya kipato chake. Hii ni kwa ajili ya maisha ya baadaye, hapa ndipo ilipo dhana ya kujilipa wewe kwanza, unamlipa Kila mtu nqa kujisahau wewe mwenyewe, unamlipa muuza nguo, unamlipa fundi nyumba, unalipia Kila kitu na kujisahau wewe. Hivyo anza kutenga sehemu ya kumi ya kipato chako.

2.Sheria ya pili ni FEDHA KUKUFANYIA KAZI
Fedha hufanya kazi kwa juhudi kwa yule mtu ambaye anaweza kuiwekeza kwenye eneo ambalo linazalisha. Ile sehemu ya kumi unayojilipa iwekeze sehemu ambayo itazalisha zaidi. Iweke kwenye biashara au uwekezaji mwingine.

3.Sheria ya tatu ni UWEKEZAJI MAKINI.
Sheria hii inahitaji umakini mkubwa sana kwani fedha hung'ang'ana kwa yule ambaye anaiwekeza kwa ushauri wa watu wenye hekima.Ushauri ni kitu cha bure Mara nyingi na ndio maana Kila mtu akifahamu unayo fedha atahitaji kukushauri uzitumiaje, Wengi wamepoteza fedha kwa kukubali kupokea ushauri wa Kila mtu, kama unataka kufunguwa biashara ya kuuza nguo nenda kamfate mtu aliyeuza nguo kwa kuanzia chini na amekuwa anakua Kila siku, sehemu hii ni muhimu sana kwani ndio sehemu ambayo wengi wametapeliwa kwa kuambiwa kuna fursa wasizo zifahamu.

4.Sheria ya nne ya fedha ni HASARA KWENYE UWEKEZAJI.
Sheria hii kwa ufupi ni kwamba kama umeweka fedha zako sehemu usiyoifahamu basi fedha hiyo imepotea, kwenye kitabu cha The richest man in the Babylon tutaona kwa mifano swala hili.

5.Sheria  ya tano ya fedha ni UTAJIRI WA HARAKA
Kama una tabia ya kuwaza kwamba unaweza kutumia fedha kidogo kupata utajiri basi unajidanganya. Fedha ni matokeo ya bidii ya muda mrefu, kujituma na kushindwa kwingi lakini kamwe usitamani kupata kirahisi kwani matapeli wengi hutumia fursa hii kukuchukulia fedha zako. Kuwa na mkakati wa muda mfupi ili kukamilisha mpango wa muda mrefu.

Hizi ndio sheria tano za fedha, nenda kazifanyie kazi Nina hakika hutobaki hivyo ulivyo. Asante sana rafiki yangu.

Kinyagakelvin162@gmail.com

Kwa masomo mengine mengi yaliyopita bonyeza hapa chini;

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251



Maombi pasipo Imani ni kazi bure......


Habari za wakati huu ndugu yangu na rafiki yangu, baada ya salamu napenda kukuambia kwamba nina kupenda sana na ninakuombea Kila siku ufanikiwe lakini kama huna imani na mafanikio ninayokuombea maombi yangu kwako ni kazi bure.......

Rafiki tuendelee na chambuzi kutoka vitabuni, na Leo tuendelee kutoka kitabu chetu cha THINK AND GROW RICH,wiki iliyopita tulionao nguvu ya shauku kwenye mafanikio na mambo mengi ambayo yamefanyika hapa duniani ni kwasababu ya shauku kubwa ambazo zilikuwepo ndani Mwa watu, Henry Ford alipata shauku kubwa ya kuona watu wanaacha kutumia farasi kama njia kuu ya kusafiria na kugundua gari,Wright brothers walipata shauku ya kutengeneza kitu kitakachoruka kama njia ya usafiri na kugundua ndege, Thomas Edison alitamani tuwe na kitu kinachotoa Mwanga kutokana na Umeme na kugundua taa za umeme pamoja na majaribio zaidi ya elfu kumi yaliyoshindwa lakini hakukata tamaa, hivyo SHAUKU kubwa ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye mafanikio.

Leo tutaangalia hatua ya pili ambayo ni IMANI na namna inavyotengenezwa,Kwanza kabisa tuangalie Imani ni nini? Imani ni hali ya mawazo/akili ambayo inawezwa kutengenezwa au kuingizwa kwa mawazo yanayojirudia kwenye akili ya ndani ya binadamu(Subconscious mind) na kupitia  eneo hili ndio tunaweza kutengeneza utajiri mkubwa.

Eneo hili la akili ya ndani(Sub conscious mind) linaapokea kile kitu ambacho kinarudiwa sana na kukiona ndio sahihi, hata kama kitu hicho siyo sahihi kwakuwa umejiambia au kufanya kwa kurudia rudia basi sehemu hii inachukulia kitu hicho ni muhimu, hapa ndio maana mtu akitengeneza tabia hasa mbaya inakuwa ngumu kuivunja, tabia ya kukopa, wizi,uzinzi na tabia zingine kadha wa kadha,unapoanza kutengeneza tabia hizo kwa Mara ya kwanza kuna hali ya wasiwasi lakini unapozirudia Mara kwa Mara sehemu hii ya akili inachukulia ni kitu sahihi na kufanya uendelee kutekeleza.

Sasa unaweza kutumia eneo hili kutengeneza utajiri, unazikumbuka zile hatua sita za kufuata ili kufikia utajiri? Sasa kwa kuzisoma Kila siku unajitengenezea imani kwamba jambo lile ulilokusudia linawezekana, Kama una amini Kila jambo linalokutokea ni mkosi basi hali za namna hiyo zitaendelea kukutokea na kama una amini wewe ni mtu mwenye bahati nzuri, basi hali za uzuri zitaendelea kujitokeza dhidi yako.

Imani ni kitu ambacho kinalipa wazo lako maisha, ndio kinga pekee ya kushindwa.Imani inapochanganywa na maombi inafanya kitu kikubwa sana.

Rafiki nenda kaishi imani na tengeneza Imani chanya kwa kurudia vile ambavyo ni sahihi kwa kujiambia Kila siku nini unahitaji kwenye maisha yako, hakika hakutakuwa na chochote cha kukuzuia.

Kinyagakelvin162@gmail.com

Kupata masomo yaliyopita bonyeza kiungo hiki chini;

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/071216151

Tuesday, 2 June 2020

Sehemu ya kipato changu ni mali yangu.......



Rafiki hongera kwa siku hii nyingine, siku ambayo ni bahati sana kuiona na vyovyote unavyoichukulia siku hii lakini tambuwa upo wajibu wa kuifanya iwe bora zaidi kataa mazoea ishi kusudi la maisha yako.......

Rafiki yangu Leo tunaendelea na chambuzi kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu ambacho Kila siku ninavyoweka bidii kusoma vitabu vinavyohusiana na fedha waandishi hawaachi kuelezea umuhimu wa kitabu hicho kwenye maisha yao, ni kitabu ambacho kina nguvu sana kama utafanyia kazi kanuni za fedha utakazojifunza humo. Karibu tuendelee na uchambuzi......

Wiki iliyopita tuliona namna Arkad mtu tajiri kuwahi kuwepo kwenye mji wa Baberi akielezea ni kwa namna gani aliweza kutoka kwenye uandishi mpaka kuwa na utajiri mkubwa na namna alivyokutana na Algamish aliyemfundisha kanuni za fedha.

Algamish alipokwenda kuchukuwa kanuni yake aliyokuwa akiandikiwa na Arkad alikuta imekamilika ndipo akafurahi na kumwambia Arkad umetimiza ahadi yako sasa ni zamu yangu kutimiza ahadi yangu ya kukufundisha kanuni zitakazokufanya uwe na utajiri na alianza kwa kumwambia maneno haya chini ambayo nayanukuu kutoka kwa Algamish mwenyewe.

"I FOUND THE ROAD TO WEALTH WHEN I DECIDED THAT A PART OF ALL I EARNED WAS MINE TO KEEP."

Hii ndio kauli ya kwanza ambayo Algamish alimwambia Arkadi kama ushauri ambao mtu anapaswa kuanza nao pale anapotaka kuondokana na matatizo ya kifedha. Arkadi akauliza kwa mshangao Je ni hivyo tu ndio kutanifanya niwe tajiri?

Pengine hata wewe unaweza kushangaa, kwamba kwa kuamua kutenga pembeni sehemu ya kipato chako na kukifanya Mali yako kunakufanya uwe na utajiri?Je wewe unatenga sehemu ya kipato chako na kukifanya Mali yako?

Arkadi anamwambia Algamish kwamba lakini kwani kipato changu chote si ni Mali yangu? Pengine na wewe ungeuliza swali hilo kwani ndivyo unavyoamini,lakini ukweli siyo huo. Hebu jiulize swali moja,kipato chako kinakwenda wapi? Kama ni mwajiriwa kabla hujapata kipato chako kuna kodi, bima ya Afya,mifuko ya jamii na makato mengine yanakatwa moja kwa moja, halafu ukishachukuwa kiasi unachopata unaanza kulipa kodi ya nyumba, ada za watoto, hela ya chakula, bili za Umeme, king'amuzi na matumizi kadha wa kadha,kwahyo kipato unachopata unakitumia kwa kuwalipa wengine halafu wewe unajisahau kujilipa.

Rafiki yangu unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakikisha kabla hujawalipa wengine jilipe wewe kwanza, chukuwa si chini ya asilimia kumi ya kipato chako kiwekeze ili kije kukufanyia kazi baadaye na kama unatumia hela yote unayoipata basi hapo utazifanyia kazi fedha maisha yako yote lakini kama unatenga sehemu ya kipato chako na kuziwekeza basi itafikia wakati fedha zitakufanyia wewe kazi. Na hapa mwandishi anatushauri tulifanye hili mapema tusisubiri mpaka tunapokaribia uzeeni au kustafu ndio tuanze utamaduni huu kwani kadri utakavyopanda mti mapema ndivyo utakavyoota mapema.

Swali la kujiuliza je kama mwaka ulio anza kazi ungetenga asilimia 10 ya kipato chako Kila unapopokea fedha Leo ungekuwa na Tsh ngapi? Sasa kama hukufanya hivyo hebu jiulize asilimia 10 ya kipato chako Leo ukiizidisha Mara miezi 12 ya mwaka mmoja, halafu kiasi utakachopata ukakizidisha Mara miaka 10 unapata kiasi gani? Hujachelewa unaweza kuanza sasa.

Wiki inayofuata tutaona hatua inayofuata baada ya kuweka utaratibu wa kutenga sehemu hiyo ya kipato chako na ni kwa vipi utakiweka na namna ya kukiwekeza ili kikufanyie kazi wewe, asante sana rafiki pengine umejifunza kitu na unakwenda kukifanyia kazi Mara moja huna haja ya kuchelewa.

Makala hizi nzuri zimeandikwa na Mimi Mwalimu na mwandishi ambaye ninatamani tuvuke pamoja na ndio maana nakushirikisha na wewe.

Kinyagakelvin162@gmail.com

Blog yangu;
https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

Monday, 1 June 2020

Huyu ndiye mwalimu bora kuliko wote.......



Nakusalimu rafiki yangu, wanaweza kukuzurumu Kila kitu lakini siyo namna unavyoweza kufikiri, hivyo kama una ubongo hapo ulipo na afya basi huna sababu yeyote ya kuwa na hofu kwani kama aliyekuumba ameendelea kukupa vitu hivyo hakuna atakayekuny'ang'a bali ni jukumu lako kuvitumia ipasavyo.

Rafiki yangu kujifunza ni hitaji muhimu sana kwa binadamu na ndio maana kuna shule, wote tunafahamu jinsi ambavyo shuleni tunafundishwa,nadharia halafu tunafanya mtihani kisha tunapewa cheti halafu tunakwenda kazini.

Kuna namna zingine ambazo tunajifunza kwa makosa yetu wenyewe (ujinga) na kuna namna ambayo tunajifunza kupitia makosa ya wengine (uelevu).Pamoja na namna zote hizo za kujifunza yupo mwalimu bora sana ambaye tunapaswa kumfahamu ambaye unapaswa kumfahamu.

MAISHA
Huyu ndiye mwalimu sahihi sana, hebu jiulize maisha angekuwa anakusemesha au mnaweza kuongea naye si ungeweza kumgombeza sana pale mambo yako yanavyokwenda kinyume na matakwa yako? Wengine wangeweza kumshitaki maisha mahakamani kama angekuwa ni binadamu kwamba yamekuwa yakiwadhurumu na yanawapendelea wengine, lakini hilo haliwezekaniki.

Kwenye kitabu cha RICH DAD,POOR DAD tulianza kuona namna Robert na Mike walivyohitaji kuwa matajiri na wenye uwezo wa kutengeneza fedha, wanaamuwa kwenda kumuomba baba yake na Mike awafundishe jinsi ya kutengeneza fedha, wanapofika pale baba yake Mike anawakubalia lakini anawaambia hatowafundisha kwa namna wanavyofundishwa darasani, watakuwa wanakwenda kufanya kazi Kila jumamosi kwenye kampuni yake na atawalipa fedha kidogo kisha atawafundisha, walikubali na wakawa wanafanya kazi ya usafi na kupanga file za ofisi, siku zilizidi kwenda lakini baba yake na Mike hakuwafundisha, kitendo hicho kilimkasirisha sana Robert kwamba baba yake Mike ni mnyonyaji amekuwa hawajali kabisa wafanyakazi wake na kuwalipa kidogo, lakini alikubaliana nao kuwafundisha ila amekuwa hafanyi hivyo bali kuwatumikisha.

Baadaye baba yake Mike anakutana na Robert pamoja na Mike na Robert anaeleza kwamba anaomba waongezewe mshahara na atimize ahadi yake ya kuwafundisha kama sivyo anaacha kazi, ndipo baba yake Mike anamjibu mbona nimekuwa nawafundisha? Na je maana ya kufudisha ni kuwa nadharia kama mnavyofundishwa shuleni? Hivyo sivyo maisha yatakavyowafundisha, maisha hayana muda wa kuongea na nyie na kuwabembeleza yenyewe yanawasukuma tu,na hiyo ndio elimu halisia.

"Now I know I can choose a profession for the work I want to perform and not because of job security, benefit or how much I get paid"

Hili ni somo ambalo lipo kwenye kitabu hiki, tunafanya kazi ili tujuwe namna ya kazi hiyo inavyoendeshwa,siyo kwa ajiri ya usalama au kiasi gani unalipwa ila uzoefu utakaoupata na namna gani unakwenda kuutumia kwenye maisha yako.

Je wewe umeajiriwa kwenye biashara ya mtu? Unajifunza nini ili uende ukakitumie kwenye biashara yako baadaye ndio muhimu hapo na siyo unalipwa nini, wewe ni mwajiriwa kama mwalimu? Unajifunza namna zipi za kusimamia na kuendesha shule ili uje kufunguwa shule yako ndio muhimu na siyo unalipwa nini, bilashaka umeondoka na kitu hapa, asante na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com

My blog;
https://kinyagakelvin.blogspot.com

Hapo utajifunza masomo mengi zaidi.
0763766944/0712161251