Tuesday, 9 June 2020
Sehemu ya kipato changu ni mali yangu (II)......
Kama hakuna mtu anayekuambia unakosea basi unafanya vitu vya kawaida sana, rafiki yangu usiache kufanya kitu kwa hofu ya kukosea kwani kwenye makosa yako ndipo palipo na mafanikio yako, kubali kokosolewa ili uwe imara.........
Rafiki yangu wiki iliyopita tuliweza kuona na kutambuwa kitu kikubwa sana kwenye maisha yetu,kitu kinachotupa mwanzo wa mafanikio, SEHEMU YA KIPATO CHANGU NI MALI YANGU kama umeanza kufanya hivyo basi umeanza kuelekea kwenye utajiri,usisubilie mpaka uwe na fedha nyingi ndio uanze kutenga sehemu ya kumi ya kipato chako, haijarishi una madeni au huna anza kutenga sehemu ya kumi ya kipato chako kwa ajili ya maisha yako baadaye, kama laki moja haitoshi basi ni Sawa na ukitoa elfu kumi ukaitenga na kubaki na elfu tisini, huwezi jiambia maisha yamekuwa magumu kwasababu umetoa elfu kumi, mwepesi kutumia hela ambayo hujapokea kwa kukopa ili ukipokea ulipe kwa riba lakini mgumu kutoa asilimia kumi ya kipato chako na kuweka kwa ajili ya baadaye.Hebu tuendelee na simulizi yetu.
Baada ya Arkad kufahamishwa na tajiri Algamish kwamba kwa kuamua kutenga sehemu ya kumi na kuiwekeza kwa ajili ya kuiwekeza ili baadaye iweze kumzalishia alianza kufanyia kazi swala hilo Mara moja, kipindi cha huko nyuma watu walitumia dhahabu kama fedha, hivyo namna ya kuhifadhi ilikuwa ni kuifukia ardhini lakini kwa sasa hivi tuna benki ambazo unaweza kufunguwa akaunti na kuanza kuweka asilimia kumi ya kipato chako, bank zote kubwa wana huduma hizo CRDB,NMB,NBC na zingine kubwa, unaweza fika na kukubaliana nao kisha ukaanza kuweka asilimia kumi ya kipato chako kwa muda utakao jipangia bila kuzitoa na baada ya muda uliopanga kuisha unakwenda kuchukuwa fedha zako na faida kidogo kisha kuziwekeza sehemu uliyokusudia.
Basi Arkad anasema baada ya miezi kumi na mbili kuisha tajiri yule alirudi na kumuuliza kama alifanyia ushauri ule aliompatia, Arkadi akamjibu nimefanya kama ulivyonishauri bila kuacha, tajiri yule akammwambia vizuri sana je umeifanyia nini akiba yako hiyo? Arkadi akamjibu nimempatia Azmur mtengeneza matofali, amesafiri kwenda nchi za mbali na amesema atanunua madini adimu na akirudi tutayauza na tutagawana faida.
Tajiri yule akamwambia Arkad wewe ni mjinga utaaminije ushauri wa mtengeneza matofali kuhusu madini?akamwambia tayari umeshapoteza fedha zako anza kuweka tena upya, na kweli baada ya mtengeneza matofali kuludi anakuja na madini bandia katapeliwa. Hapa tunapatiwa funzo moja, uwekezaji ni kitu kinachowekezwa kwa umakini mkubwa sana, usiwekeze fedha zako sehemu usiyo ifahamu, lazima ufahamu kwa kina ni namna gani hapo unapowekeza patakupa faida na omba ushauri kwa mtu ambaye anafahamu kwa kina kile unachotaka kuwekeza, watu wakifahamu kwamba una fedha hupenda sana kutoa ushauri hivyo kuwa makini kupokea ushauri.
Arkadi alianza upya kutenga asilimi kumi upya na baada ya miezi kumi na mbili mingine kupita yule tajiri alirudi na kumuuliza Arkadi fedha ulizotenga umewekeza wapi? Akasema nimempa mkopeshaji anakopesha watu halafu faida tunagawana, tajiri akamwambia vizuri sana, Je faida unayopata unaitumiaje? Arkad akamwambia huwa na sherehekea na ana mpango wa kununua farasi ya kutembelea, zamani farasi walitumiwa kama Leo tunavyotumia gari, Algamish mtu tajiri alicheka akamwambia unakulaje watoto wanao kufanyia kazi wewe? Endelea kutumia faida kuwekeza ili baadaye ikutumikie uishi vizuri zaidi.Basi Arkad akapokea ushauri ule.
Hapa tunajifunza kwamba watu huwekeza kweli na baada ya muda kuanza kuona faida hukimbilia kununua anasa na kisha kurudi kwenye maisha yaleyale ya kuifanyia kazi fedha, tunatakiwa kuwekeza na pale faida inapokuwa kubwa kiasi cha kuweza kufanya matumizi ambayo hayakuzalishii fedha.
Rafiki nadhani unaweza kuanza kupata picha ni kwa namna gani fedha inaweza kukufanyia kazi na siyo wewe kuifanyia kazi fedha.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment