Monday, 26 October 2020
Zingatia Haya Ili Kuikuza Biashara Yako
Tunakila sababu kumshukuru mungu wetu kwa zawadi ya maisha, kila siku tujikumbushe kwamba lipo kusudi la sisi kuwepo duniani, tutumie nafasi hii kufanya yale yatakayoleta manufaa kwetu na kwa wengine, kataa mazoea badilika.
Leo tutamalizia sehemu ya mwisho ya biashara kama msingi wa mafanikio kwa kuangalia mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara yako.
Rafiki kitu ambacho unapaswa kukifahamu ni kwamba mafanikio ya biashara, hayaji kama ajali au bahati, bali yanatengenezwa. Lazima ujenge misingi imara ya kuwezesha biashara yako kukua.
*Msingi wa uaminifu na uadilifu*
Msingi mkuu wa biashara ni mahusiano, hakuna mahusiano yanayojengwa nje ya uaminifu na uadirifu. Fanya kitu kama ulivyo ahidi, udanganyifu kwenye biashara ni sumu.
*Maadili*
Lazima uwe na miiko yako kibiashara, lazima ujiambie ni mambo gani hutokuja kuyafanya kwenye biashara yako. Kwenye biashara kuna mambo mengi sana ya ushawishi kama hutajijengea miiko utajikuta kila ushauri unaufanyia kazi na hapo ndio unakua mwanzo wa angako kwenye biashara.
*Uvumilivu*
Mafanikio kwenye biashara ni kitu ambacho hakiji kama ajali, lazima uweke nguvu na muda kufanikiwa, kama huna uvumilivu huwezi kufanikiwa kwenye biashara, yapo mengi utakutana nayo na hutoambiwa popote na yatataka kukutoa kwenye mstari hivyo kama siyo imara utapotea.
*Shukrani*
Acha kulalamika na kuona mambo mabaya yanatokea kwako tu, uwe mtu wa shukrani. Unaposhukuru unafunguwa Milango kwako zaidi.
*Ushirikiano*
Huwezi kujenga biashara kubwa peke yako, unahitaji kushirikiana na wengine. Wasaidizi wako, wateja wako na kila mtu anayefahamu uwepo wa biashara yako lazima ushirikiane naye vizuri.
Ukiyasimamia haya ipasavyo nina hakika ngunzo ya biashara yako itakua imara sana na itakuwa vigumu kuvunjika.
Kitu cha kuondoka nacho kwenye somo hili ni kwamba tabia za mfanyabiashara ndio kikwazo kikubwa kwenye biashara na kwa asilimia chache ndio hutoka nje ya sababu hii.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Sunday, 25 October 2020
Na Hii Ndio Kanuni Ya Kuingia Kwenye Biashara
Hongera sana rafiki yangu, ni juma lingine tumelianza, sina shaka kwamba umeshapanga yale yote unayotaka kukamilisha kwenye juma hili na leo yapo ambayo umejipanga nayo kuyatekeleza, basi hakikisha hakuna lolote lisilo la msingi litakalokuwa sababu ya kuharibu mipango yako, lakini pia jiandae kwa changamoto zozote zinazoweza jitokeza na kazikabili.
Leo pia tunaendelea na mfululizo wa somo kuhusu biashara, kitabu chetu ni kile kile cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na Dereva wetu aliyetuandikia kitabu Dr. Makirita Amani. Karibu.....
Rafiki ni wachache sana kati ya wanaotamani kuingia kwenye biashara ndio wanafanikiwa kuanzisha biashara, yaani tuseme kati ya watu 100 wanaotamani kuanza biashara ni mmoja pekee ndio anafanikiwa kuanzisha biashara. Je kwanini watu wanaishia kutamani kuingia kwenye biashara na hawaingii?
Mwandishi anasema Kanuni ya kuanza biashara ni *just do it*. Acha kujipa maswali mengi yasiyo na tija kuhusu biashara gani ufanye na je ni changamoto zipi nitakutana nazo, wewe unachopaswa kufanya ni kuanza biashara na kisha ukishaanza ndio utaanza kufanyia kazi changamoto utakazokutana, anza na mteja mmoja kisha mtumie mteja huyo mmoja kuongeza wateja wengine.
Rafiki tafiti zinaonyesha biashara kubwa ambazo watu wengi wanamiliki siyo biashara walizo anza nazo, bali kwa kuboresha mawazo yao ya biashara ndio kumewafikisha kwenye kazi za juu za biashara.
Mwandishi wa kitabu anasema mafanikio kwenye biashara ni kitu cha kujaribu na kushindwa, mpaka pale unapoipata njia yako halisi, na kuitumia njia hiyo kukua zaidi na kufikia uhuru wako kifedha.
Kama una mpango wa kuanza biashara acha kujipa maswali na majibu bali nenda kaanze leo, anza na popote na chochote kisha weka nguvu na muda kuikuza biashara yako. Muhimu ni kujifunza na kuwa tayari kubadirika.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Saturday, 24 October 2020
Leo Nitakujibu Ni Swali Lako La Biashara Gani Ufanye Ili Uweze Kufanikiwa Haraka
Hongera sana rafiki yangu kwa kuweza kuifikia siku hii ya mwisho wa juma, siku ambayo nimekuwa nakusisitiza itumia kujitathimini na kujipa majibu sahihi, wapi umetoka, uko wapi? na wapi unataka kufika.......
Rafiki yangu karibu tuendelee na somo letu kuhusu biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kilichoandikwa na kocha Dr Makirita Amani.
Je ni biashara gani naweza kuanza kufanya na ikaniletea faida bila kuumiza kichwa?
Hili ni moja ya swali ambalo wengi hupenda kuliuliza sana na pengine hata wewe msomaji wangu umekuwa ukijiuliza sana na watu wamekupa majibu mengi na bado hujaridhika nayo, pengine hawakukupa jibu la moja kwa moja ambalo mimi nakwenda kukupa.
HAKUNA BIASHARA MOJA AMBAYO KILA MTU AKIIFANYA ATAFANIKIWA SANA, HAIPO.
swali hili limekuwa kikwazo kwa wengi kuingia kwenye biashara na siku zote uanza biashara fulani na wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo wanaacha na kuanza biashara nyingine na huo ndio unakuwa utaratibu wao na kujikuta hawafiki popote.
Kila mtu kuna biashara ambayo kwake yeye anaweza kuifanya vizuri na kufanikiwa. Hivyo swali muhimu ni biashara gani itakufaa wewe au mimi kuanza nayo?.
Hapa utaangalia vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na unavipendelea kufanya, ujuzi wako au uzoefu ambao tayari unao. Mazingira yanayokuzunguka na watu wanapitia changamoto zipi?.
Nenda kayafanyie kazi haya rafiki yangu na uwe na siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Friday, 23 October 2020
Vitu Viwili Vya Kuwekeza Wakati Biashara Yako Iko Hatua Za Mwanzo.
Maisha yetu sisi binadamu ni ya mchaka mchaka mpaka siku yetu ya mwisho kuishi hapa duniani itakapofika, acha kujidanganya na mapumziko ya mwisho wa wiki, tafuta kitu cha kufanya kuliko kukaa na kujidanganya kupumzika wakati kila siku unalalamika.
Leo tunaendelea kuangalia eneo la biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI NA FEDHA kutoka kwa mwandishi mzawa Amani Makirita karibu tuwe sote.
Watu wengi hufikiri wakishapata mtaji na kodi ya kulipia jengo la biashara basi wameshafanikiwa na pale mambo yanapoanza kuwa magumu ukimbilia kutoa sababu nyingi zisizo za kweli, lakini biashara yoyote ile kwenye hatua za chini au mwanzo inahitaji mambo mawili yafuatayo.
*Nguvu*
Hapa ni kwamba biashara inakuhitaji wewe kuweza kufanya kila kitu kwenye biashara yako, kufanya kwa ubora ambao wengine hawawezi kuufanya. Hapa ndio sehemu ambayo unajenga msingi wa biashara yako, na unafahamu kama msingi utakuwa mbovu nini kitatokea, acha kutumia muda mwingi kulalamikia mtu uliyemwajiri akusaidie, tumia nguvu zako kuhakikisha biashara inaijengea msingi imara.
*Muda*
Utahitaji muda ili kuweza kuikuza biashara yako kutoka chini kabisa mpaka ikawa biashara kubwa. Siyo kitu cha kulala masikini na kuamka tajiri, lazima ufahamu kwamba utahitaji kujenga wateja waaminifu wa biashara yako. Utahitaji muda wa kulielewa ki undani biashara yako kuliko mtu yeyote yule. Watu wengi kwenye biashara wanashindwa kwasababu wanaangalia matokeo ya haraka, unataka biashara ikue wakati wewe unaendelea na maisha ya kawaida na hukui. Kuamka muda ulizoea kuamka, kufuatilia mambo yasiyo muhimu kwako, kukaa na marafiki zako kupiga soga. Haya yote ni sumu kwa biashara yako inapokua kwenye hatua za mwanzo.
Lazima unapoanza biashara uwe tayari kuvuruga mahusiano na watu ambao ulikuwa nao kabla hujaanza biashara, hakikisha kila siku unaweka bidii ya kujifunza namna ya kuisimamia na kuikuza biashara yako.
Makala hii imeandikwa na mimi rafiki na Mwl. Kelvin Kinyaga
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Thursday, 22 October 2020
Kuanza Biashara Ukiwa Chini Kabisa.
Rafiki yangu hongera kwa kuendelea kujifunza pamoja na mimi kupitia mfululizo wa makala zangu, ni hitaji la kila aliye hai kujifunza kila siku namna ya kuishi vizuri na kufurahia maisha. Vyote vinavyokuletea msongo wa mawazo na kukuhuzunisha ni matokeo ya mtazamo tu mbovu ulio nao, karibu tuwe sote.....
Leo tunaendelea na somo letu kuhusu umuhimu wa biashara kwenye kuongeza kipato na yote tunayapata kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na mwandishi wetu mbobevu Dr. Amani Makirita.
_Kuanza biashara ukiwa chini kabisa_
Mwandishi wa kitabu ameanza kwa msisitizo kwamba, njia nzuri ya kuanza biashara, ni kuanzia chini kabisa. Hata kama unaweza kupata mtaji mkubwa, kupitia akiba zako mwenyewe au kuwa na uwezo wa kukopa. Siyo vyema kuanzia biashara juu, kama hujawahi kuwa kwenye biashara kabisa. Yapo mambo mengi sana unapaswa kujifunza Kwa matendo. Hata kama utakua umesoma vitabu, umehudhuria kozi nyingi, bado yapo mambo utajifunza pale unapoingia kwenye biashara.
Unapoanza biashara kuna makosa mengi sana madogo madogo utayafanya hivyo kwa sababu umeanzia chini hupati hasara kubwa yenye kukuondoa kwenye biashara yako. Kwa mfano kwenye kuajiri utapata watu wasio waaminifu na kuipa biashara yako uzito kama unavyoipa wewe na kukusababishia hasara, hivyo utajifunza hayo bila kupata hasara kubwa.
Hivyo rafiki yangu acha kufikiria ni pale utakapopata mamilioni ndio uingie kwenye biashara, kwani kwa kufanya hivyo utapata hasara kubwa na utakata tamaa kabisa ya kujirekebisha na kuanza upya.
Nakutakia siku njema rafiki yangu, nenda kaanze na kidogo na kikuze taratibu huku ukifanyia kazi kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye biashara yako.
Makala hii imeandikwa na mimi rafiki yako Mwl Kelvin Kinyaga
Asante sana na mwenyezi Mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Wednesday, 21 October 2020
KWA NINI KILA MTU ANAPASWA KUWA NA BIASHARA.
Rafiki kitu unachopaswa kukifahamu kwenye maisha ni kwamba hakuna kusimama, Kuna kwenda mbele au kurudi nyuma, kama ulichofanya Jana ndio unakwenda kufanya leo Kwa namna Ile Ile basi hapo umerudi nyuma, nenda kafanye zaidi ya Jana na utapata matokeo tofauti na uliyopata Jana.....
Leo tuendelee na somo letu kuhusu fedha na kwanini kila mtu anapaswa kuwa na biashara.
Kwanza ni ukweli usiopingika kwamba biashara ndiyo njia ya kuweza kuongeza kipato, ambayo haina kikomo. Hakuna mtu wa kukuzuia wewe kwenye Idadi ya biashara unazoweza kufungua, Pia hakuna atakayekupangia kikomo cha kipato chako unachotengeneza kupitia biashara.
Biashara ndio njia kubwa ya kuleta manufaa Kwa jamii zetu, taifa na hata dunia Kwa ujumla. Ni kupitia biashara ndio watu hutatuliwa matatizo yao makubwa. Pia biashara ndio sekta inayotoa ajira Kwa watu wengi zaidi. Na biashara ndio sehemu nzuri Sana ya kujifunza maisha. Mwandishi anasema biashara ndio chuo kikuu cha maisha, ni kweli kwani biashara haina maigizo yoyote, ukifanya kosa dogo adhabu yake ni hapo hapo.
Biashara itakufundisha kutoa thamani,kushindwa, kukataliwa, kukabiliana na changamoto, kupambana, uvumilivu na mengine mengi.Hivyo Mwandishi anasisitiza Kwa kila mtu anayetaka kujifunza maisha na kuyaelewa Kwa vitendo anapaswa kuingia kwenye biashara, kwani hakuna kitu ambacho biashara haitakufundisha.
Mwandishi anahitimisha sehemu hii Kwa kusema kila mtu anapaswa kuingia kwenye biashara kama moja ya kuongeza mifereji ya kipato. Hata kama unazo njia nyingine za kuongeza kipato kuwa na biashara kunaongeza mfereji mwingine. Watu wengi hupenda kupata njia za uhakika kama ajira ili kuingiza kipato lakini moja ya sheria za dunia ni kwamba hakuna jambo lolote ambalo ni uhakika wa asilimia 100. Wengi hujifunza hilo Kwa njia ngumu, pale kile walichokiwekea uhakika kinapowaangusha. Hivyo unapokuwa na biashara, tena zaidi ya moja, unazidi kupunguza hatari yako ya kutegemea sehemu moja au chache kwenye kutengeneza kipato chako.
Nenda kafanyie kazi haya uliyojifunza na anzisha biashara hata kama utaingiza mia mbili Kwa siku na Anza kuikuza polepole.
Uwe na siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki Sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Tuesday, 20 October 2020
MLANGO WA NDOTO
Ni kweli zipo changamoto nyingi ambazo unazipitia, je wafikiri hayo unayopitia ni mikosi? Unafikiri ni wewe peke yako unayapitia? Wacha kusikitika mshukuru mungu bado unayo nafasi ya kuyakabili yote na kusonga mbele.
Karibu rafiki yangu tuendelee kujifunza pamoja. Leo tunaangalia umuhimu wa Ndoto kwenye maisha yetu, tunaangalia ndoto kama lango.Binafsi kabla ya kusoma kitabu hiki sikua na elewa chochote kuhusu ndoto na ni moja ya sehemu ambayo sikuwahi kuipatia umuhimu wowote.
Kabla hatujajadili mlango huu wa ulimwengu wa kiroho ni vema tuangalie ni nini maana ya ndoto.
Ukiangalia kamusi ya kiingereza inatuambia:Ndoto ni mtiririko wa mawazo, picha na mhemuko unaotokea kwenye fikra za mtu akiwa usingizini.
Kwenye tovuti ya Wikipedia ;wao wanasema ndoto ni mrejesho wa sura, mashauri, hisia na msisimko ambavyo hutokea bila utawala wa akili wakati wa usiku kwenye vipindi mbalimbali vya usingizi.
Wanasayansi wanasema ndoto ni picha za fikra kwenye utu wa ndani zilizobeba sauti, sura na mhemuko wakati tumelala.
Tunaambiwa Kwa kawaida mtu mwenye Afya anaota mara 3 mpaka 7 Kwa usiku mmoja.
Kwenye Biblia ndoto zimetajwa mara 21 kutoka Kwa mfalme Yakobo. Kitabu cha mwanzo pekee ndoto zimeandikwa mara 33.Kitabu cha Nabii Daniel zimeandikwa mara 27.Agano jipya kama mara 8 pekee.
Kwa hali hii, ni vema tuone kuwa ndoto Zina umuhimu wake mkubwa kwenye maisha ya mtu.
Mungu aliongea na wanadamu Kwa njia ya ndoto, ukisoma kitabu cha mwanzo kwenye sura 41,Kwenye ndoto maarufu aliyoiota mfalme Farao ikitafsiriwa na Yusufu mwana wa Israel;utaona mungu akitumia ndoto kuongea na binadamu.
Ipo tofauti Kati ya Maono na ndoto. Maono hutokea wakati mtu hajalala na ndoto hutokea wakati mtu amelala.
Tunapokuwa tumelala, miili yetu ndio imelala lakini roho zetu hazilali. Hivyo Kuna mambo mengi Sana ya kiroho utendeka tukiwa tumelala.
Rafiki kama unahitaji kuelewa Kwa undani zaidi somo hili basi wasiliana moja Kwa moja na Mwandishi wa kitabu hiki mchungaji na Mwalimu Josephat Ulomi Kwa number 0763816739
Nenda ukasamehe wote waliokukosea, anza kupenda kujifunza na kuongeza ufahamu, anza kuamini kama ulikuwa huamini kwamba Yesu Kristo ni Lango hapa duniani kama ni mlengwa wa kristo, Anza kuheshimu ndoto Zina mengi ya kukufundisha na hapo utaanza kuona njia zako zinafunguka na unabarikiwa.
Asante Sana rafiki yangu nakutakia siku Njema na Mungu akubariki Sana Sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Monday, 19 October 2020
Yesu Kristof lango la ufalme wa mungu hapa duniani.
Rafiki yangu Habari za wakati huu, bilashaka ni mara nyingine zawadi ya pumzi inakaa ndani mwetu, huwezi amini ni maelfu ya watu Jana walikuwepo lakini leo ni wafu, tumshukuru mungu na tukaitumie zawadi hii Kwa kulitukuza Jina lake.
Rafiki yangu swala la Imani linaweza kutugawa lakini utakubaliana na mimi kwamba hilo siyo kusudi la mungu, leo nikiwa ninakwenda kuzungumzia yesu kristo kama lango Kwa wakristo, bilashaka na ndugu zetu waislam mtume Muhammad ndiye lango, Kwa wakristo hatuwezi fika mbinguni Kwa kupuuza Jina Yesu Kristo, vivyo hivyo Kwa wenzetu waislam hawawezi kupuuza Jina Muhammad Kwa safari ya kutafuta mbingu ya mwenyezi mungu, hivyo tunatumia Milango tofauti lakini safari yetu ni moja.
Kwa upande wetu wakristo Tunafahamu kwamba palikuwepo Adamu wa kwanza aliyemuasi mungu na hivyo Kwa sababu yeye alikuwa uzao wa kwanza, basi lilikua lango kwetu sisi wanadamu wote na ndio maana tunazaliwa na dhambi ya asili ambayo inaondolewa Kwa njia ya ubatizo kupitia Adamu wa pili ambaye ndie yesu kristo Masia mkombozi wa ulimwengu.
"Mimi ndimi mlango;mtu akiingia Kwa mimi, ataokoka;ataingia na kutoka, naye atapata malisho. You 10:9."
hapa yesu anatumia mfano huu kutuonyesha kwamba yeye njia ya wokovu Kwa watu wote wanaotamani kuingia kwenye ufalme wa mungu.
"Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima;mtu haji Kwa Baba, ila Kwa njia ya mimi ". Yoh 14:6"
Yesu mwenyewe anakiri kuwa yeye ndiye njia ya kweli na uzima. Dhambi ilitutenga na mungu lakini Kwa kumwamini yesu tunaingizwa tena kwenye ufalme wa mungu.
" Yohana 3:16,"Kwa maana jinsi hii mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele."
Kwa kunukuu vifungu hivi vya biblia hakuna namna tunaweza kuona nguvu ya yesu kristo inatutoa kwenye mateso na shida na mahangaiko na kutukomboa, siyo dhambini tu bali kwenye kila hitaji letu pale tunapomuhitaji.
Wapo wengi wanaoteseka Kwa kutafuta njia zisizo faha, Kwa waganga wa kienyeji kutafuta wabaya wao, Kwa mizimu ya mababu na hivyo kuteseka Kwa maisha yao yote, mfuate yesu kristo yeye atakuonyesha mambo makubwa ya ajabu usiyo yajua.
Nikutakie siku Njema na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Sunday, 18 October 2020
Mlango wa ufahamu
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka umeamshwa salama na uko tayari kwenda kuyakabili yale yote yaliyopo mbele yako, hongera na mungu akutangulie......
Leo tutakwenda kuangalia mlango mwingine utakao utumia kufanikiwa au kutofanikiwa kama hautoutumia mlango huo.
Sehemu iliyopita tuliweza kuona Kaka yetu ULOMI kupitia KITABU chake cha yajue Malango yanayoweza kukufikisha au kudidimiza maisha yako KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA. Tuliweza kujifunza mlango wa msamaha Kwa kina na bila Shaka kama ulilielewa vizuri somo lile umejiponya, kwani kusamehe ni kujitibu mwenyewe.
Leo tunakwenda kuangalia mlango mwingine , MLANGO WA UFAHAMU, tunateseka na mambo mengi Kwa sababu hatuna ufahamu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yetu.
Neno la mungu linatuambia hivi;
Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, Kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka saying. *Daniel 9:2*
Kumbe kupitia neno hili tunaona umuhimu wa vitabu kwenye kutupatia ufahamu, Mwandishi anatumia neno UNDERSTAND Kwa kulinyambua na kupata neno Under lenye maana ya chini ya! Stand lenye maana ya simama na linapokua pamoja Lina maana KUJUA ULICHOSIMAMIA au sababu ya ulichosimamia.
Hivyo kama utajikuta umekwama na lolote Kwa kuchukua vitabu na kusoma utapata uelewa mpana Sana, usijiulize nianze na kitabu kipi? Uwe mkristo biblia ipo anza nayo ina kila kitu. Kama ni Muslim Quran ipo itakupa uelewa wa kutosha, kwenye vitabu Kuna siri nyingi Sana, ukiweza kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu nina hakika hutobaki kama ulivyo.
Mwandishi anaendelea Kwa kusema kwamba ukishajifunza kutoka kwenye vitabu na ukaunganisha na hekima ya kutenda yale uliyojifunza unapata ufahamu, hili linatupa tafsiri kwamba unaweza kusoma maelfu ya vitabu lakini kama huna hekima ya kutumia maarifa hayo basi hapo hakuna ulichofanya, kocha wangu anaita kuchafua akili.
Jiulize kabla watu hawajafahamu tiba Kwa magonjwa yaliyotukabili je ni watu wangapi walifariki?
Kwanini ufahamu ni lango?Ujinga na upumbavu ni ngome au vizuizi vinavyofanya watu wasifikie kiwango fulani cha maisha, wewe kuishi maisha ya dhiki na taabu siyo mpango wa mungu, kubaki vilevile kila siku siyo mpango wa mungu, hebu Anza kufungua vitabu na utoke huko.
Mwandishi ametumia mifano mingi ya kutufungua na kututoa kwenye giza la Ujinga na kutufanya waelewa, Kwenye injili ya Yohana mlango ule wa nane yesu anasema "mkikaa katika neno language, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli ;tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. *Yoh.8:31-32*
Rafiki Anza leo kujiwekea utaratibu wa kujifunza na utaona namna ulivyokuwa kifungoni Kwa Muda mrefu bila sababu wakati umezungukwa na maarifa ya kila aina.
Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Thursday, 15 October 2020
Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 3
Rafiki yangu hongera Kwa kuweza kuifikia siku ya leo, nina amini changamoto unazozipitia ni daraja la kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine bora zaidi, usirudi nyuma songa mbele......
Leo tunaangalia sehemu ya tatu ya mtu huyu mwenye bahati kuliko wote babeli karibu tujifunze pamoja.
Rafiki yangu nina hakika tumekua pamoja tangu mwanzo mwa simulizi hii na umeweza kuona ni namna gani bidii inavyoweza kukufungulia njia za mafanikio.
Bidii ya kazi Kwa Sharru Nada inamvutia babu yake na kijana ambaye sharru anamuelezea alikua mshirika mwenzie kwenye biashara na hapo anataka kufahamu ni kipi kinamsukuma kijana huyu kufanya kazi Kwa bidii?
Rafiki wengi wetu makazini tunafanya kazi Kwa bidii tukitegemea kuongezeka Kwa mshahara au kufanya vyeo na ndio maana kila siku tumekua tukilalamikia waajiri, Kwa sharru Nada kazi ilimfanya atengeneze mahusiano mazuri na bwana wake na wateja wake huku akijiandaa na kununua uhuru wake.
Baada ya kumueleza babu yake na kijana huyo Nia yake mzee alimwambia kwamba hata yeye kazi anayofanya ya kutembeza vitu nyumba Kwa nyumba ni ushirika na bwana wake kwani na yeye alikua mtumwa kama yeye.
Kijana aliposikia babu yake alikua mtumwa alikataa kwani anafahamu babu yake alikuwa mtu mwenye fedha nyingi Sana, Lakini hakufahamu alizipataje.
Wapo wengi Sana ambao ni matajiri tunawafahamu lakini kama tungefahamu ni namna gani walianza pengine tungewapa heshima zao.
Kadri siku zilivyoenda ndivyo mfuko wa sharru ulivyotuna, Kwa kila kiasi cha fedha alichopata aliweka na hata bosi wake alimtegemea Sana, kwani kila sharru alipopata na yeye alipata zaidi, Lakini pesa alizopata huyo bosi wake ziliishia kwenye kamali.
Siku moja sharru akiendelea kukanda unga wake Kwa maandalizi ya bidhaa zake alikuja bwana mwingine na kumwambia Sharru kwamba huyo bwana wake ameshindwa kulipa deni lake hivyo inabidi achukuliwe yeye kama fidia.
Sharru ni mtumwa hana namna ya kukataa hivyo anakusanya fedha zake na kuambatana na bosi mpya, Kwa bahati mbaya Kwa bosi wake mpya maisha yanakua magumu zaidi, kazi zinakua ngumu na zisizo na maslahi yoyote,Sharru anaanza kukata tamaa ya maisha.
Lakini siku moja wanakuja watu kumchukua Kwa kumnunua kama mtumwa na anafukua fuko lake la fedha na kuambatana na watu wale, anafika sehemu aliyonunuliwa anakuta aliyemnunua ni yule rafiki yake, ambaye ni babu wa kijana yule, anafurahi na kujiona ni mtu mwenye bahati kubwa Sana.
Anamwambia alimtafuta bila mafanikio na aliposikia aliuzwa kama mtumwa alimfuatilia na kuamua kumnunua, hapo ndipo mwanzo wa ushirika kibiashara ulipoanzia Kati yake na babu yake.
Alipofika hapo kijana alifahamu kwamba watu hawazaliwi na kua matajiri bali ni Kwa kuweka kazi, alifurahi kufahamu kisa cha utajiri wa babu yake na kimemfungua kwamba kazi siyo Kwa watumwa pekee bali kiungo cha kununua uhuru wako.
Rafiki kazi uliyonayo Sasa ni utumwa wako, pamoja na kwamba inakusaidia lakini siku yoyote bwana wako akishindwa kulipa madeni au sababu nyingine utaondolewa kwenye kazi hiyo na maisha yatakua magumu Sana.
Anza leo maandalizi ya kununua uhuru wako Kwa kujifunza biashara, wafundishe watoto zako kutengeneza pesa kuliko kuajiriwa, ukifa leo wanao hawatakula mshahara wako, ila wanaweza simamia biashara ulizozianzisha na ikawa ukombozi kwao.
Mwisho wa simulizi ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, bilashaka umeondoka na vitu vya kufanyia kazi.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Wednesday, 14 October 2020
Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 2
Habari za wakati huu rafiki yangu, ni Ile Ile bahati ya kuweza kuifikia leo inaendelea kwetu, ni mimi na wewe wa kuchagua ni namna gani tunakwenda kuitumia, kulalamika, kubishania siasa na mpira au kuweka kazi na kuhakikisha maisha yetu yanakua bora zaidi.....
Sehemu ya pili ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, Tutaendelea na simulizi yetu, na Tutaendelea pale ambapo Hidan anataka kufahamu ni vipi Sharru Nada aliweza kutengeneza utajiri?
Sharru Nada anaendelea na simulizi yake kwamba yeye na babu yake huyo kijana walianza kama watumwa.
Yeye alichukuliwa baada ya Kaka yake kuuwa mtu, na mke wa yule mtu aliyeuwawa alimchukua Sharru kama fidia ya kifo cha mumewe.
Baadae mama yule aliamua kumuuza Sharru kama mtumwa, wakiwa njiani kwenda kuuzwa walisikia watu wakieleza namna watumwa babeli walivyofanyishwa kazi mpaka kufa. Hili lilimwogopesha Sana Sharru.
Lakini mtu mmoja alimwambia Sharru akifika babeli na mtu yeyote atakayejitokeza kununua mtumwa basi ajitokeze na kueleza kwamba yeye anapenda Sana kazi ili anunuliwe na kama asipopata mtu atapelekwa kujenga ukuta wa babeli na huko kulikuwa na kazi ngumu na mateso ya kila aina Kwa watumwa.
Magodi alimwambia Sharru kama ukinunuliwa nenda kaipende Sana kazi yako na ifanye Kwa bidii zote na kama mtu huyo hatoithamini kazi hiyo wewe ithamini, usiangalie kile unachozalisha kinakunufaishaje bali ona kitu hicho kinavyowanufaisha wengine.
Walipofika babeli Sharru alihakikisha anapata mtu atakayemnunua na kufanya kama alivyoshauriwa na Maggido. Kweli wanafika Babeli na Sharru anapata mtu wa kumnunua na hapo Sharru anajiona ni mtu mwenye bahati Sana Kwa kuweza kununuliwa kama mtumwa.
Basi Sharru alipofika Kwa bwana wake huyo aliyemnunua anapangiwa kazi ya kuwasha moto, kukanda unga na kufanya maandalizi mengine ili mikate na keki viandaliwe kwani bwana yule alifanya biashara ya kuuza keki na mikate.
Sharru aliweka bidii kubwa Sana na kuhakikisha siyo kwamba anashiriki kwenye maandalizi tu ya kutengeneza keki na mikate bali anafahamu mpaka zinavyotengenezwa, bwana yule alipendezwa Sana na bidii za Sharru kwenye kazi.
Siku moja Sharru ndipo alipopata wazo la kuhakikisha anaanza kutengeneza kipato ili aweze kununua uhuru wake na anapata wazo la kutumia Muda wa jioni wa mapumziko kufanya kazi ili apate fedha, anamfata bwana wake na kumueleza wazo hilo, kwamba angetengeneza keki zaidi na jioni kuuza na wangegawana fedha, bwana wake anakubali na Sharru anaanza zoezi hilo mara moja.
Mwanzo hali inakuwa ngumu kupata wateja lakini baadae mambo yanaanza kuwa mazuri na kwenye kuuza keki anakuja kukutana na babu yake na Hadan, ilikuwaje na nini kilitokea usikose sehemu inayofuata ili ufahamu Sharru alinunuaje uhuru wake?
Rafiki labda Kuna kitu umeanza kukiona kwenye simulizi hii, kwangu naona siku niliyopata ajira ni Sawa na siku Sharru aliyonunuliwa kama mtumwa, alifurahi na alikwenda kuifanya kazi yake Kwa mapenzi yote akifahamu kwamba yeye ni mtumwa, Vipi wewe unaipenda kazi unayofanya? Je unafahamu kwamba wewe ni mtumwa uliyenunuliwa na boss wako? Je mwisho wa utumwa huo ni lini?
Kabla hatujaendelea na kisa hiki nenda kayatafakari maswali hayo na Anza mipango ya kununua uhuru wako.
Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, tutaonana sehemu inayofuata.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Monday, 12 October 2020
Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli(The luckiest man in babylon)
Habari rafiki yangu, nakusalimu Kwa Jina la Mungu muumba wa ardhi na mbigu, tunakila sababu kufurahia pumzi yenye uhai wa kufanya mimi na wewe tukaweza kupata nafasi ya kuendelea kujifunza ili tusiwe miongoni mwa watakao angamia Kwa kukosa maarifa.
Leo tunaendele kuangalia kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu ambacho ukianza kukisoma hutamani kukiweka chini, nimejipa jukumu la kukisoma kila mwezi mpaka nihakikishe ninayaishi yote yaliyomo humu Kwa vitendo, kila ninapokisoma nakiona kipya.
*Mtu mwenye bahati kuliko watu wote babeli *
Sharu Nada mfanyabiashara ambaye alionekana nadhifu na mtanashati na alimiliki vitu vya thamani Sana, Mwandishi anatuambia huo ulikuwa muoekano wa nje ila ndani allikuwa na matatizo makubwa. Kabla hatujaendelea nimejiuliza Sana kwamba Kuna kumbe Kuna watu wengi Kwa nje tunawaona kama ni watu wenye maisha mazuri na tunatamani kuwa kama wao, Lakini kama tungefahamu undani wao Kwa namna wanavyopitia changamoto kubwa tusingeutamani utajiri huo.
Sharru Nada aliongoza msafara wake wa biashara kutoka Damascus kwenda Babeli, pamoja na kwamba njiani kulikuwa na watekaji lakini msafara wake ulikuwa na ulinzi wa kutosha hivyo kwake watekaji hawakumsumbua.
Kwenye msafara wake aliongozana na kijana aliyeitwa Hadan Gula, kijana huyu alikuwa mjukuu wa mshirika mwenzie kibiashara miaka ya nyuma, kijana huyu alifanana Sana na babu yake Kwa sura lakini siyo kwenye matendo, kwani hakupenda kazi na alipendelea kuvaa Vito vya thamani, urithi wote walioachiwa kutoka Kwa babu yake, yeye pamoja na baba yake waliuteketeza Kwa sababu hawakufahamu msingi wa fedha.
Wakiendelea na safari kuelekea Babeli Hadan Gula alimuuliza Sharru Nada, kila siku uko kwenye misafara ya kibiashara huna Muda wa kupumzika na kufurahia maisha? Ningekuwa wewe ningeishi kama mtoto wa mfalme.
Kijana akiwa kavalia heleni na bangiri aliamini kazi ni Kwa ajili ya watumwa lakini Tajiri kama Sharru hakupaswa kujitesa na chochote, wakati Hadan anaongea hayo Sharru aliwaza atawezaje kumsaidia kijana huyu kwani mtazamo alio nao kwenye fedha usingeweza mfikisha popote.
Wakiwa njiani aliona watu aliowaacha miaka 40 iliyopita wakifanya kazi zile zile, Kwa kipindi hicho aliziona ni kazi nzuri na alizozitamani lakini leo yeye ameweza kufikia utajiri mkubwa huku wale wanaofanya kazi alizozitamani Wakiwa na maisha ya kawaida.Aliamini kutoka Kwa watu wale ni kwamba wameshindwa kabadilisha mitazamo yao ndio maana maisha yao hayajabadilika.
Akiendelea kuwaza atamsaidiaje kijana yule aliyeongozana naye? Akamuuliza swali kama angependa kufahamu yeye na babu yake walikuwaje washirika kwenye biashara? Hidan anamwambia kwanini usiniambie umewezaje kutengeneza utajiri? Hicho ndio nataka kusikia.
Pengine na wewe unataka kusikia mwisho wa kisa hiki, basi usikose sehemu ya pili ya kisa cha mtu mwenye bahati kuliko wote babeli.
Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, endelea kujifunza kupitia kurasa hizi na nenda kafanyie kazi yote unayojifunza.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Saturday, 10 October 2020
Pain and sickness-opportunities for virtue
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na waendelea vizuri kabisa na Ile ndoto yako unaifanyia kazi kila siku, haijalishi unapiga hatua zipi kuifikia na changamoto zipi unazipitia hakikisha unakua kile unachotaka.
Leo tutaangalia mtazamo ambao unapaswa kuwa nao siku zote na utakufanya uwe na furaha Muda wote, mtazamo huu tutajifunza kutoka Kwa mwanafalsafa EPICTETUS
*Maumivu na magonjwa ni chachu ya kutufanya kuwa wema*
Tunapitia Maumivu ya kila aina kwenye maisha yetu, pengine ni magonjwa au changamoto mbalimbali za kimaisha, pengine unapitia Maumivu ya kichwa hicho ni kikwazo Kwa mwili lakini siyo kwenye fikra na maamuzi, ni Mara ngapi wakati Tunapitia changamoto ndogo ndipo tunaruhusu maisha yetu yote kuvurugika? ngoja nikupe kisa kifupi cha mwanafalsafa EPICTETUS.
Wakati wa Roma watu walikuwa wanamiliki watumwa na EPICTETUS alikuwa ni moja wa watumwa, kama tunavyofahamu mtumwa hana haki yoyote, pamoja na utumwa lakini aliumia mguu wake na kuwa mlemavu, Kwa usual aliishi maisha ambayo hakuwa na sababu yoyote ya kumfanya awe na furaha.
Pamoja na yote hayo falsafa ilimfanya awe na maisha bora Sana, yeye aliamini kwamba kitu ambacho hakuna mtu anaweza kutunyang'anya ni namna ya kufikiri kwetu.
Kuumwa, kuwa kwenye hatari hata kama kukikabili kifo tunapaswa kuwa na furaha na kushukuru Kwa nafasi ya maisha tuliyokuwa nayo mpaka Sasa, leo tunajifunza mengi kutoka Kwa mtumwa huyu. Yeye anaamini kukosa furaha ni matatizo binafsi na ni mtazamo wa fikra ndio unaotusumbua na siyo vitu vya nje.
Hebu chukulia mfano unaumwa homa, ukianza kulalamika kwamba umeshindwa kwenda kazini ni kuamua kujiumiza zaidi, Lakini ukiwaza kwamba ni Muda ambao utapata nafasi ya kuwa karibu na familia yako, pengine umekuwa Muda mwingi unautumia zaidi kwenye kazi kuliko familia, pengine Kwa Muda mrefu umekosa Muda wa kupumzisha mwili wako, EPICTETUS alifahamu Kuumwa mguu ni kikwazo Kwa mwili na siyo akili yake na ndio maana pamoja na yote Muda wote alikuwa mtu wa furaha pamoja na ulemavu na utumwa wake.
Je wewe rafiki yangu tatizo gani linalokunyima furaha? Amini hakuna jambo au mateso yoyote ya kuharibu namna ya kufikiri kwako labda uwe umeruhusu mwenyewe.
Nenda kaishi Kwa matumaini na jiandae na changamoto zozote zitakazojitokeza mbele yako, yapo mengi huwezi kuyabadili, jipe Muda na yote yatapita.Falsafa inatuambia hakuna watu wenye matatizo ya akili bali Kuna watu wanaojaribu kutoroka matatizo yao Kwa kuchagua kulalamika.
Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Thursday, 8 October 2020
Msingi muhimu wa biashara unaopaswa kulielewa.
Hongera Sana rafiki yangu Kwa kuchaguliwa tena kuifikia siku ya leo, wapo wengi walilala na mipango mizuri ya kuifanya leo lakini hawakuamka, wewe umefanikiwa kuifikia leo je ni yapi umepanga kufanya? Kama ni mipango Ile Ile ya kila siku je umejiandaa kupata matokeo tofauti? Nenda katekeleze zaidi ili uitendee haki siku hii.
Kila kitu ambacho tunakifanya kinaanzia na msingi, na ndio maana Mwandishi wa kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA ametuandalia masomo haya akiamini kwamba ukiyafuata utakua imara kwenye fedha pamoja na changamoto zake.
Ili nyumba isiweze kudondoshwa na tetemeko au upepo inahitaji msingi imara, vivyo hivyo na kwenye biashara unayofanya kama biashara haina misingi inayosimamia basi kudondoka ni hakika.
Je biashara imara inahitaji misingi gani?
Msingi wa kwanza wa biashara yoyote ni THAMANI, kwani tulishajifunza kwamba ili uweze kupata fedha lazima ubadilishane thamani na mwingine, hivyo kabla hujaanza biashara jiulize ni thamani gani nitawapa wengine Kisha wanipe fedha zao? Ni kipi nitatoa kwao wakaamua kunipa fedha zao walizozitafuta Kwa shida?
Siri nyingine ambayo ni msingi wa biashara yoyote ni KIPI NAFANYA NA WENGINE HAWAPO TAYARI KUKIFANYA kwenye biashara lazima uwe tofauti na wengine, lazima mteja apate kitu kwako ambacho kwingine siyo rahisi kukipata, kama unafungua biashara Kwa sababu umepata mtaji na unafanya kawaida kama wengi wanavyofanya basi utapata matokeo kama wengi wanavyopata Mwandishi anasema kama mteja anaweza kupata Kwa wengine kile anachokipata kwako, ukweli ni kwamba huna biashara, upo katikati ya kelele. Na kama umeamua kuingia kwenye biashara ambayo kila mtu anafanya basi ifanye Kwa namna tofauti na wengine wanavyoifanya.
Ipo Siri nyingine kubwa Sana kwenye biashara ambayo Mwandishi anasema huwezi isikia popote, biashara zote zenye mafanikio Zina sifa hiyo, Sifa hiyo ni KUHODHI biashara hizo au sehemu ya biashara hiyo, kama biashara unayofanya haitawali sehemu kubwa ya soko basi biashara hiyo ukuaji wake unakuwa mgumu Sana. KUHODHI huko isiwe ni Kwa kuwakandamiza wengine bali unapaswa kuwa bora zaidi ya wengine.
Rafiki kwenye biashara yako nenda the katoe thamani kubwa, jitofautishe na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama unayofanya wewe, na hodhi sehemu ya soko la biashara yako.
Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na uwe na siku Njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Wednesday, 7 October 2020
Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli sehemu ya pili....
Habari za wakati huu rafiki yangu, ikiwa ni siku nyingine tulivu na nzuri tumshukuru mungu wetu Kwa zawadi ya uhai, twende tukaitumie zawadi hii Kwa kuyatenda yampendezayo karibu.....
Bilashaka Jana umejifunza kitu kwenye sehemu ya kwanza ya mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli na leo tutamalizia sehemu ya pili.
Debasir aliendelea kuelezea maisha yake ya awali na watu waliendelea kuongezeka kumsikiliza, Debasir anasema baada ya kukimbia wadeni wake ilibidi auzwe kama mtumwa Kwa Tajiri mmoja na alikua akifanya kazi ya kuhudumia ngamia, pamoja na kwamba alifanya kazi hiyo kama mtumwa hakukubaliana na hali ya kwamba yeye ni mtumwa na pale mke wa Tajiri aliyemnunua alipotaka kufahamu kwanini Debasir hakukubaliana na hali ya utumwa ndipo Debasir anaelezea maisha yake ya awali, familia yenye uwezo na amemkimbia mke wake na ndugu zake Kwa sababu ya madeni hivyo hataki kukubali kwamba utumwa ndio mwisho wake, Nira anamuuliza kama anajiona ana roho ya utumwa au mtu huru? Debasir anajibu anajiona ni mtu huru, Nira mke wa tajiri anamwambia kama unaroho ya mtu huru tuthibitishie hilo nenda na uwakabili wadeni wako ili uwe huru.
Siku moja Nira yule mke wa Tajiri alimwambia Debasir aandae ngamia kwani anataka kwenda kumtembelea mama yake, Debasir anaandaa ngamia na wanakwenda na ngamia wawili na wanapofika Kwa mama yake Nira anafukuza watumwa wengine na anampa nafasi Debasir ya kutoroka na ngamia wawili ili arudi akawakabili wadeni wake na awe huru Tena, Debasir anamshukuru Nira na anaanza safari na ngamia wawili huku Nira akijitetea Kwa mume wake kwamba Debasir ametoroka na ngamia wale.
Safari ya kurudi nyumbani inakua safari ngumu na ya mateso kwani hakuifahamu njia vizuri na alipita kwenye jangwa na kiu ya maji pamoja na njaa vilimtesa Sana na baadae alianza kuona hakuna dalili ya kuishi kwani kifo kipo karibu.
Lakini alipokumbuka swali kutoka Kwa Nira kama yeye ni mtu huru au mtumwa alijihisi kupata nguvu upya ya kusonga mbele kwani akifa atakufa kama mtumwa, baada ya siku kadhaa alifika sehemu yenye maji na matunda na hapo ndipo akaona ana uhakika wa kufika nyumbani.
Ndipo anamgeukia Tarkadi mdeni wake na kumwambia je Kwa njaa hii uliyo nayo leo upo tayari kuwafuata wadeni wako wote na kulipa madeni yako ili uwe huru tena au utaendelea kukimbia?Tarkadi akasema simulizi hii imenipa mwanga na Sasa naona dunia Kwa uhalisia wake nitayakabili madeni yangu niwe huru tena.
Mtu mmoja Kati ya waliokuwa wakimsikiliza Debasir walitaka kufahamu alipofika babeli nyumbani alifanikiwa kulipa madeni yake yote? Ndipo Debasir akasema aligundua walio mkopesha ni marafiki zake adui yake mkubwa ni madeni, hivyo aliwatafuta wadeni wake na kuwaeleza nia ya kuwalipa aliyonayo, wengi walifurahi lakini wengine walitaka kumpiga Kwa sababu walikasirika Sana.
Debasir anasema Kati ya wanao mdai walipomuona ana nia ya kulipa madeni, mtu mmoja alimuunganisha na wafanyabiashara wa ngamia kwani walifahamu anao uzoefu kwenye ngamia na alifanikiwa kulipa madeni yote na Sasa ndio huyu mfanyabiashara mkubwa wa ngamia babeli.
Rafiki kisa hiki kina mafunzo mengi Sana, wapo watu kila siku wanakimbia huku na huko ili kuwakwepa wanao wadai Kwa kuona ni maadui zao, kumbe maadui zao ni tibia zao za kukopa na madeni ndio maadui zao wakubwa ambao wapo nao na wanaenda nao kila sehemu hivyo kama unataka kuwa huru wakabili wadeni wako na walipe Kisha hali mikosi na bahati mbaya hazitaendelea kukuandama.
Debasir alikataa hali ya utumwa na akajitenga nao hata wewe kataa utumwa wa madeni, tafuta uhuru wako leo.
Asante Sana rafiki yangu, nimeona nikuletee somo hili leo badala ya wiki inayofuata kwani wengi wameona wiki ijayo ni mbali, nikutakie siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Tuesday, 6 October 2020
Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli (The Camel trader of Babylon)
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na unaendelea salama na ratiba zako za kila siku, umejipangaje kua bora zaidi ya Jana, kufanya yaliyosahihi na kuachana na yale yasiyo na tija kwenye siku hii unayo iendea?....
Rafiki yangu karibu tuchambue kitabu pamoja, leo tutajifunza kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kupitia mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli, ni somo zuri Sana ambalo wakati nikipasoma sitamani kuweka kitabu chini bali kuendelea kusoma, karibu tuwe sote mpaka mwisho wa makala hii.
Tarkad mtoto wa Azure alikua akipita mtaaini akiangaza macho karibu na sehemu wanazouza chakula pengine angeweza kukutana na mtu ambaye anamfahamu ili amkopeshe fedha na kumnunulia chakula, anasema akili hufikiria Sana harufu ya chakula wakati una njaa kali.
Wakati anaendelea kuangaza hapa na pale ndipo anakutana na mtu ambae hakutaka kukutana naye, mtu huyo si mwingine bali Debasir mfanyabiashara wa ngamia aliyemkopesha fedha na kutomlipa kama walivyokubaliana Debasir anafurahi kukutana na mdeni wake na anapohitaji kulipwa deni lake Tarkad anajieleza kwamba hana pesa na amekua na bahati mbaya.Hilo linamshangaza Debasir kwamba watu wote wenye bahati mbaya ni wale wanaofikiria kukopa kuliko kulipa madeni yao.
Basi Debasir anamwambia Tarkad amfate na atampa hadithi moja itakayomfundisha. Na wanakwenda kukaa ndani ya sehemu inayouza chakula na Debasir anaagiza mguu wa mbuzi na mkate pamoja na mboga mboga na Juice Kwa sababu alikua na njaa Sana, Lakini anamwambia muhudumu asimsahau na rafiki yake Tarkad Kwa kumletea maji ya kunywa ya baridi kwani joto lilikua kali Sana, Tarkad alisikitika Sana kwani pamoja na njaa ya siku mbili anakweda kukaa akiangalia mtu akila mguu wa mbuzi huku yeye akiendelea kumkodolea macho, Kwa kua alidaiwa na amepewa ahadi ya kupewa hadithi itakayokwenda kumfundisha na kumuondoa kwenye utumwa wa madeni ilibidi akae na kusikiliza.
Debasir alianza kuelezea maisha yake ya huko nyuma ya kuishi Kwa kukopa na kujificha akikimbia wale waliomkopesha mpaka kuuzwa kama mtumwa lakini baadae anafanikiwa na kuwa mfanyabiashara mkubwa wa ngamia wa Babeli.
Nini kilitokea, tusubirie sehemu ya pili ya simulizi hii tutaona nini Debasir alifanya mpaka kuushinda umasikini na Kuja kua mfanyabiashara mkubwa.
Ondoka na somo hili kwamba bahati mbaya huwaendea wale wote ambao wanafurahia mkopo na kuchukizwa kulipa deni hilo, Lakini pia huangalia ni wapi kwingine ataweza kukopeshwa.
Ninakupenda Sana rafiki yangu, nikutakie siku Njema na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Sunday, 4 October 2020
Nifanye nini pale Malango ya kiroho, kiuchumi na kihisia yanapofungwa?
Habari za wakati huu mpendwa rafiki yangu, Tumefanikiwa kulifikia juma lingine, bilashaka Kuna mengi yako mbele yetu ya kuyafanikisha, nikutie nguvu kwamba haijarishi ni magumu yapi unayapitia basi tambua hupaswi kurudi nyuma......
Rafiki yangu kila mmoja anafahamu nini maana ya neno mlango na kazi zake, sehemu yoyote ambayo unatumia kuingia na kutokea ni lango.
Leo napenda kukuletea uchambuzi wa kitabu cha Kaka yangu Mwalimu na mchungaji JOSEPHAT ULOMI, kwenye kitabu chake cha YAJUE MALANGO YANAYOWEZA KUKUFANIKISHA AU KUDIDIMIZA MAISHA YAKO KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA ana mengi ya kutufundisha.
Lango la kwanza ambalo ndilo tutaliangalia leo ni LANGO LA MSAMAHA.
Mwandishi ameanza Kwa kuangalia lengo kuu la kila mwanadamu ni kuishi maisha ya furaha, Amani na uhuru na hivyo kuyapata haya ni lazima uwe tayari kuachana na na mawazo yoyote hasi na yatakayokuzuia kufikia adhima yako hiyo.
Mwandishi anaamini kanuni kubwa ya maisha ya furaha inapatikana kwenye kauli ifuatayo.
Wewe ni mzima wa akili Kwa kiwango kile unachoweza kusamehe bure, kusahau na kuachilia Kwa yale na vyote vilivyo kuumiza.
Hivyo kutokusamehe ni kujiweka kifungoni wewe mwenyewe na pale unapohitaji kutoka kwenye kifungo basi funguo ni kusamehee.
Mwandishi amegawa makundi manne ambayo unapaswa kusamehe na kujirudishia uhuru wako kua ni;
1.Wazazi wako
Wengi Sana wamejiweka kifungoni Kwa kushindwa kuwasamehe wazazi au walezi wao, pengine Kuna mengi kweli walipaswa kukufanyia kama kukupeleka shule na kukuonyesha upendo lakini hawakufanya hivyo, hivyo Kwa kila changamoto unayopitia unaona wao ndio sababu na kujikuta Muda mwingi hutumii kutatua changamoto zinazokukabili bali kulalamika na kubaki kifungoni.
2.Kundi la pili ni wale watu waliokuwa na uhusiano wa karibu Sana kwetu.
Pengine ulimkabidhi mtu akili na moyo wako wote na ulimwamini Sana lakini akaja kukufanyia kitu kibaya Sana.
Kama hatutofikia hali ya kusamehe tunajikuta kwenye hali ya kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo, namna ya kuondokana na hali ya chuki na ya kutosamehe watu hawa ni wakujiona wewe mwenyewe umechangia kuingia kwenye mahusiano usiyo yafahamu vizuri hivyo unapaswa kujisamehe na kumsamehe aliyekukosea pia.
3.Kundi la Tatu ni kumsamehe kila mtu.
Kila aliewahi kukukosea una kila sababu ya kumsamehe bure na kusahau.
4.Kundi la nne na la mwisho ni kujisamehe wewe mwenyewe.
Rafiki Kuna mengi Sana yalitokea kwenye maisha yako na unaona wewe ndio ulikua chanzo na unatamani ungefuta hali hiyo na kuibadili lakini haikuwezekana, hivyo Muda mwingi unautumia kujilaumu na kujiambia laiti ningelijua ningefanya moja, mbili, tatu.
Kujilaumu ni kujiweka kwenye kifungo kikubwa Sana.
Hivyo rafiki yangu msamaha ni lango la mafanikio yako, kama hutojisamehe na kusamehe wengine basi utakua huna faida duniani wala mbinguni, kote utakua umejiweka kwenye kifungo.
Tutaendelea kuona Malango mengine kwenye kila siku kama ya leo, Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Wednesday, 30 September 2020
Biashara, njia ya uhakika ya kutengeneza kipato kisicho na ukomo
Habari rafiki yangu, bilashaka mimi na wewe tunapaswa kuanza siku hii Kwa kumshukuru mungu, ukiangalia ni vitu vingi Sana tunavyo kama zawadi, ukiangalia wapendwa, ndugu na marafiki na Afya zetu ni zawadi kubwa Sana kwetu.....
Leo tunaangalia umuhimu wa biashara kwenye maisha yetu, na kwanini kama kweli unataka kufikia uhuru wa kifedha lazima ujihusishe na biashara.
mwandishi wa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA anatukumbusha kwamba tofauti ya mapato na matumizi ndio itakayo amua wewe uwe masikini au Tajiri, yaani kama unatumia zaidi ya kile unachopata basi unakua unajiondolea nafasi ya kufanikiwa, Lakini hata kama utabana namna gani kipato chako lazima matumizi ya msingi yafanyike, huwezi Sema sitakula Kwa sababu nikila matumizi yatazidi kipato au kusomesha watoto na matumizi mengine ya msingi.
Kwanini njia zingine kama Ajira haziwezi kukupa uhuru wa kifedha?
Kwa upande wa Ajira huwezi Pata uhuru wa kifedha Kwa sababu unalipwa Kwa kusubiria maamuzi ya mtu mwingine, hata kama utaongeza bidii na kuzalisha zaidi bado huna maamuzi ya kujilipa zaidi,Lakini pia hata unapoamua kujiajiri hakikisha kile ulichojiajiri nacho unakitengenezea mfumo mzuri wa kuhakikisha hakikutegemei wewe moja Kwa moja.
Biashara yenye mfumo mzuri ndio tiba tiba ya ukomo wa kifedha.
Haijalishi unaweka bidii namna gani kama kile unachojihusisha nacho kama kinakuhitaji moja Kwa moja basi utafika sehemu ya ukomo wa Muda, ukomo wa nguvu na hapo ndipo biashara yenye mfumo mzuri itakua mkombozi kwako, kwani ukilala kitandani fedha itaendelea kuingia, ukifikia uzee fedha itaendelea kuingia.
Hili halihitaji kwenda shule na kuchukua degree kulielewa kwani jamii inayokuzunguka itakuonyesha ukweli huu na utaona wale wenye mfumo mzuri walivyohuru kwenye fedha na fedha zinawafanyia kazi siku zote.
Tutaendelea kujifunza zaidi somo hili la biashara Kwa kuangalia namna ya kujenga misingi imara ya biashara yako.
Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu, nakupenda daima na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Monday, 28 September 2020
Nenda nyumbani mwambie mke wako ukuta wa babeli ni imara utawalinda nyie na Mali zenu
Habari za wakati huu rafiki yangu, ni bahati nyingine ya kipekee mimi na wewe tumeweza Kuiona siku hii, twende tukaitumie Kwa yale yaliyo muhimu na yasiyo na tija tuachane nayo.....
Kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON ipo hadithi moja inayoelezea uimara wa kuta zilizozunguka mji wa babeli.
Kama tulivyojifunza kwamba babeli ulikua ni mji wenye utajiri mkubwa Sana, hili lilitokana na maarifa waliyonayo kuhusu fedha na bidii ya watu wa mji huo, Lakini kama tujuavyo watu wakishafahamu sehemu Kuna Mali watapambana kuipata Mali hiyo.
Siku moja mfalme wa babeli alisafiri na jeshi lake kuu kuelekea nchi za mbali na mwanya huo ulitumiwa na maharamia walio kua na siraha wakitaka kuufanyia mateka na kupora Mali zote za mji huo.
Wananchi wa babeli waliingiwa na hofu kubwa kwani walifahamu kwamba kufanikiwa Kwa mateka hao kuingia babeli ingekua mwisho wa uhuru wao, Mali zao na hata utu wao.
Kutokana na mji huo kua na kuta imara haikua rahisi kuingia babeli lakini watekaji hawakukukata tamaa ya kutaka kuingia babeli, wakati yote hayo yakiendelea yupo askari mmoja aliyeitwa Banzar alikua akitoa taarifa Kwa Wananchi wa babeli hali ya uvamizi ule ilikua inaendeleaje ili kuwapa Wananchi taadhali endapo mambo yangewaendea vibaya.
Wamama na watoto Kwa wazee walikua wakihofu zaidi kwani wao ndio wangekua wahanga wakubwa kama babeli ikivamiwa, hivyo Muda wote walifika Kwa askari huyo kuulizia hali inakwendaje, Lakini Banzar alimjibu kila aliyemuuliza kwamba wewe watulivu kwani ukuta wa babeli ni imara na utawalinda.
Baada ya wiki Tatu na zaidi wavamizi walikata tamaa na kuondoka babeli na Wananchi walitoka ndani walikojificha Kwa hofu wakishangilia kwani ukuta wa babeli Kwa uimara wake waliokolewa dhidi ya mateka.
Rafiki yangu hata kwenye fedha na utajiri wako unahitaji kuwa na kuta imara kama za mji wa babeli ili kuulinda utajiri wako na mfano wa kuta hizo ni kama zifuatazo hapa chini.
1.Kuwa na bima ya vitu mbalimbali unavyomiliki ni ukuta dhidi ya Mali hizo.
2.Kuwa na akiba iliyo sehemu salama ni kuta imara dhidi ya utajiri wako.
3.Kuwekeza katika uwekezaji imara na unaoaminika ni kuta imara na itakulinda dhidi ya pesa zako na utajiri wako.
Nikutakie siku Njema rafiki yangu na kazi Njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944 /0712161251
Sunday, 27 September 2020
Jipe majibu sahihi ya maswali haya
Hongera Sana rafiki yangu Kwa kuweza kupata bahati ya kuifikia siku hii, bilashaka uko tayari kwenda kupambana na mikiki mikiki ya siku, karibu tuendelee kujifunza kupitia maswali.......
Kabla hatujaangalia maswali ya kujiuliza nikuambie kitu kimoja, maswali ni njia bora Sana ya kujifanyia tathimini kwani yanakuonyesha uko wapi na unataka kufika wapi.
Karibu uweze kutenga Muda wako na kujipa majibu sahihi.
1.Je unaipenda kazi yako? kama sivyo ni kwanini?
rafiki ni wengi Sana wanafanya kazi wasizo zipenda lakini ukiwauliza sababu za kutopenda wengi watasema haziwalipi vizuri, je na wewe sababu ni hiyo?Je umepanga kuondoka lini kwenye kazi hiyo usiyoipenda? Au utaendelea na utumwa huo maisha yako yote?
2.Vipi ukijiangalia kadri unavyokua uwezo wako wa kujiamini unaongezeka au unapungua?
Fahamu hili na lifanyie kazi mapema.
3.Je unajifunza kutokana na makosa yako au unarudia makosa yaleyale kila siku?
4.Ni nani shujaa wako na unajifunza kwake na kila siku anakupa msukumo zaidi wa kuzifikia ndoto zako?
5.Una ndoto gani kubwa inayoeleweka? Kama ipo ni ipi hiyo? Na je ni mipango gani uliyo nayo kuifikia Naoto hiyo?
Rafiki kama utaweza kukaa chini na kujipa majibu ya maswali haya Kwa usahihi? Nina hakika Kuna sehemu unakwenda ila kama utaona unakosa majibu naomba tuwasiliane kwani nina amini utakua mwanzo mzuri.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Unajifunza nini kwenye kisa hiki kifupi?
Habari za wakati huu rafiki, una maadui wengi Sana na adui yako mkuu ni yule unayemuona ukijitazama kwenye kioo, adui wengine ni mazoea na kutojifunza, hebu jiulize wiki hili la 39 tangu mwaka umeanza linakwisha umefanya nini? Je umejifunza nini?.......
Leo nataka tujifunze kitu kimoja ambacho kilinipa ujasili kwenye mambo mengine mengi Sana na yamenisaidia Sana.
Nimetoka nyumbani naelekea bank na nina uhitaji wa haraka na fedha ninazohitaji kutoa Kwa njia ya ATM kufika nakuta foleni ni ndefu na Kati ya ATM tatu ni moja tu ndio inafanya kazi bahati mbaya ilikua ni siku ya jumapili na bank zimefungwa siwezi tolea ndani na bahati mbaya habari ya mawakala haikuwepo Kwa wakati huo, wakati najiuliza nifanyaje nikajiuliza nani kasema hizo ATM mbili hazifanyi kazi? Nikagundua ni askari anayelinda hapo alikua akiwaelekeza watu kwamba hizo ATM mbili hazifanyi kazi Lakini Kwa wakati huo hayupo eneo la ATM bali yuko pembeni anaongea na mtu, Kwa sababu nilikua na haraka nilimuomba aliyekua nyuma yangu ngoja nikaangalie pengine mtandao umerudi na kama sivyo ningerudi kwenye foleni yangu, nilipofika nilikuta mtandao uko Safi na bahati nzuri na Ile ATM nyingine mambo yalikua hivyo hivyo,nikatoa fedha na kila mtu akashangazwa kwamba tumetumia ATM moja Kwa shida wakati ATM zote zilikua zinafanya kazi, rafiki pengine kwako tukio hili lisiwe na maana lakini kwangu lilinipa sheria.
KWANGU MWENYEWE
1.Nikiwa na shauku ya jambo lolote siangalii changamoto zilizopo mbele yangu bali kile ninachohitaji Kwa mbinu na gharama yoyote.
2.Asili itakuruhusu kukupatia unachotaka kama kweli kutoka moyoni unakihitaji.
3.Sikia lakini usiamini kirahisi thibitisha kile unachokisikia.
4.Acha kufuata wingi tumia njia zako.
ASKARI
Usiwaongoze watu kwenye jambo ambalo wewe mwenyewe hulifahamu ki undani na hujalisimamia ipasavyo.
Kama Kuna la Ziada umejifunza kwenye kisa hiki naomba unishirikishe Kwa njia yoyote Kati ya hizi hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Thursday, 24 September 2020
Fate leads the willing and drags along the reluctant - Seneca
Mungu watu ni mwema Sana kuweza kutufanya mimi na wewe kuifikia siku hii, siyo kitu rahisi kwani wapo wengi Sana walitamani na imeshindikana, Kwa kulitambua hilo basi tuanze siku yetu Kwa kufanya yale ya msingi na kuacha kuutumia Muda wetu Kwa mambo ya siyo na tija......
Leo tunaangalia kauli ya mwanafalsafa Seneca ambayo inatupa zoezi la kufanyia kazi kila siku Kwa wiki nzima.
Rafiki yangu pale unapoanza kushindana ndipo mwanzo wako wa kushindwa unapoanza kwani chochote unachoshindana nacho unakipa nguvu dhidi yako. Hata kama una nguvu kiasi gani lazima ukubaliane na matokeo kwamba huwezi lazimisha na kuwazuia watu namna wanavyokufikiria.
Wapo watu wengi wanaoteseka na historia za maisha yao, hutamani kubadilisha hali zilizojitokeza kwenye maisha yao, historia ya elimu yako siyo muhimu Kwa Sasa, hali yako mbaya ya kimahusiano iliyokutesa huko Nyuma usiipe nafasi leo.
Pale utakapoanza kuyakubali madhaifu yako na kuruhusu maisha yako yaendelee, huku ukiangalia ni wapi unataka kufika na kujitaidi kutimiza yanayokupeleka huko ndio unaanza kukua, kubali Kuna vingi hujui na Anza kujifunza Mara moja, wape watu nafasi ya kuishi wanavyotaka na wewe ishi maisha yako huku ukifahamu Kuna vingi huwezi vibadili na haviwezi kua vile unavyotaka wewe, kukataliwa, kusemwa na wengine,kukejeriwa na kudharaurauliwa ni vitu ambavyo havitakiwi kukuumiza kichwa, wewe jipe sababu ya kuendelea na maisha yako na kubali mengine yako nje ya uwezo wako vipokee na vikubali.
Makala hii imeandikwa na mimi rafiki yako Mwl Kelvin Kinyaga, unaweza nipata zaidi Kwa mawasiliano binafsi hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Monday, 21 September 2020
Maswali ya kujiuliza unapotaka kukopa Kwa ajili ya kuanza biashara.
Hangera Sana rafiki yangu Kwa kuendelea kujifunza kupitia kurasa zangu za Ustawi wa fire, Leo tutakwenda kuangalia mambo ya msingi unayopaswa kuangalia kabla hujachukua mkopo ili kuanzisha biashara.......
Kwanza kabida unakumbuka tulijifunza kutoka kwenye kitabu cha Elimu ya msingi kuhusu fedha kwamba kukopa ili kuanzisha biashara no mkopo Mbaya. Leo tutajifunza Kwa kina kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kama mkopeshaji fedha babeli anavyotufundisha.
Kwanza kabisa Kwa yeyote anayetaka kukopa au kukopeshwa lazima ajiulize maswali kadha ya msingi. Na zaidi kabla hujamkopesha mtu hakikisha unafahamu yafuatayo.
A. Fedha unazokopa/anazokopa kwako ni za nini?
B. Kama ni Kwa ajili ya kufanya biashara je unao uzoefu au ujuzi na biashara hiyo?
C. Je unafahamu ni wapi utanunua Kwa bei ndogo zaidi unachotaka kuuza?
D. Je unafahamu ni wapi unapoweza kuuza Kwa bei nzuri na na kupata faida?
Rafiki Kwa wakopeshaji na wakopaji huwa na matamanio ya kupata wanachotaka, mkopeshaji ana tamaa ya kupata riba na mkopwaji huwa na tamaa ya kupata fedha ili kukamilisha alichopanga kufanyia fedha anazokopa Lakini mwisho wa siku wote hujikuta kwenye matatizo makubwa ya kifedha.
Taasisi za kifedha wako makini Sana kwenye hili na ndio maana hutoa mkopo pale dhamana ya mkopaji inapokua kubwa kuliko mkopo uliochukua, hivyo nenda kalifanyie kazi somo hili,usimkopeshe wala kukopa na kujikuta badala ya kumsaidia unayemkopesha unamuingiza kwenye matatizo makubwa zaidi na wewe pia kupoteza fedha zako, Pima hatari za mkopo unaochukua au kukopesha ili kuleta usalama wako wa kifedha.
Asante na nikutakie siku Norma, ili kujifunza zaidi fungua
https://kinyagakelvin.blogsport.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0712161251/0763766944
Thursday, 20 August 2020
Ustawi wa fikra Thursday 20,August 2020 _Madeni ni utumwa_ Habari za wakati huu rafiki, Leo tuangalie elimu ya fedha kipengere cha madeni.... Kwanza kabisa mwandishi ameanza na kauli kwamba Madeni ni utumwa... Kauli hii inakera lakini ina ukweli ndani yake, watu wengi sana wana amini hawawezi kufanikiwa bila ya kukopa, pamoja na mikopo wanayochukua bado maisha yanakua magumu zaidi, wengi hawafahamu ni wapi wanakosea, Elimu ya fedha ndio suruhu ya tatizo hili, lazima ufahamu mkopo upi ni mbaya na upi ni mzuri kwako ndio uchukue. Madeni ni utumwa kwasababu anayekudai anakua na usimamizi mkubwa juu yako. Kile ulichowekea kama dhamana kinaweza chukuliwa muda wowote. Madeni ni utumwa kwasababu unawafanyia kazi wanaokudai, Kila unapofanya bidii kwenye kazi,malipo unayopata unatumia kulipa deni. Watu wengi wanajiambia isingekua mikopo wasingekuwa hapo walipo na mikopo imewasaidia, hili linakuja kwasababu wengi wanao chukua mkopo hawapigi hesabu za kiasi gani wanalipa kwa mkopo waliochukua. Pamoja na yote hayo mwandishi anatuambia madeni mengi ni utumwa wa kujitakia. Asante na siku njema.
Friday, 31 July 2020
*Ustawi wa fikra* Wednesday 30,July 2020. _Hivi ndivyo wajanja wanavyoishi baada ya ongezeko la kipato chao_ Habari za wakati huu rafiki yangu, hongera kwa siku nyingine na tuna Kila sababu ya kumshukuru mungu..... Leo kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA tutaangalia dhana ya vipi utaweza kuzuia matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka. Rafiki kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba tabia moja unayopaswa kuwa nayo itakayokufikisha kwenye utajiri ni kuhakikisha matumizi yako ni kidogo kuliko kipato chako, kama kiasi unachopata unakitumia chote sahau kuhusu mafanikio. Mwandishi wa kitabu anasema kitu ambacho anakishangaa kwenye fedha hasa kwa waajiriwa ni hiki, japokuwa watu wanatofautiana vipato na mishahara wanayolipwa lakini Kila inapokaribia mwisho wa mwezi aliyepokea milioni moja na aliyepokea laki moja wote wanakuwa wameishiwa na kinachosababisha hili ni watu kuongeza matumizi Kila fedha inapoongezeka na kusababisha wawe watumwa kwenye fedha maisha yao yote lakini wajanja kwenye fedha hawaishi hivyo. Mwandishi anatoa mfano,pale kipato chako kinapoongezeka, jipe muda kidogo wa kuendelea na maisha yale ya kipato cha chini,tumia ongezeko hilo la kipato kuzalisha kipato cha zaidi. Baada ya kipindi cha miezi sita tangu upate ongezeko la kipato ndipo unaweza kuongeza matumizi yako kufikia nusu ya ongezeko na nusu kuendelea kuzalisha. Rafiki uwe umeajiriwa au kujiajiri au biashara hakikisha unakuwa mjanja kwa kuhakikisha huongezi matumizi yako Mara tu baada ya kuongezeka kipato chako. Asante na Leo nimekupa ujanja huu, nenda kautumie,biashara yako haitakua kama hutumii ujanja huu. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0763766944/0712161251
Monday, 27 July 2020
Ustawi wa fikra Monday, 27 July 2020 *Na hivi ndivyo kodi ilivyoanza........* Habari za wakati huu rafiki, asubuhi ya wiki lingine na nina imani umejipanga kuiendea siku hii kwa kufanya zaidi ya pale ulipofanya kwenye wiki lililoisha, kwani kama utafanya vile vile na kutokwenda hatua ya zaidi usitegemee kupata matokeo ya tofauti na uliyopata wiki iliyopita. Leo rafiki tuangalie historia ya kodi, kama upo serikalini unakatwa kodi, kama una biashara zako unakatwa kodi, kama huna kazi maalumu bado utalipa Kodi wakati ukihitaji huduma, Je nini chanzo cha kodi? Kwanini unalipa kodi? Rich dad alikuwa akiendelea na darasa lake na Leo anatufundisha historia ya kodi, anasema wakati wapo shule kuna mwalimu aliwaelezea habari za Robin Hood,mtu ambaye mwalimu huyo alimuelezea Robin kuwa mtu shujaa aliyewaibia matajiri vitu na kuwapa masikini, rich dad anasema yeye kwa upande wake alimuona Robin kama kibaka tu kwa kitendo chake hicho, anasema ingawa sasa Robin hayupo lakini watu wenye mtazamo kama wa Robin wapo na wanapenda kuona matajiri wanastahili kulipa kodi kubwa lakini ni kinyume chake. Miaka ya 1799-1816 Uingereza walitoa pendekezo la wananchi wake kulipa kodi ili kuiwezesha nchi yao kushinda kwenye vita, Marekani nao kwenye miaka ya 1861-1865 walitumia mbinu hiyo ya uingereza kuweza kusaidia taifa lao kushinda vita, baadaye kwenye mwaka wa 1874 uingereza waliweka sheria ya ulipaji wa kodi kuwa ni sehemu ya waingereza matajiri, Marekani nao mwaka 1913 walipitisha sheria hiyo, mwanzo raia wa nchi hizi waliaminishwa kwamba kodi ni kwa watu matajiri pekee na wao halitawahusu lakini kadri serikali zilivyokuwa ndivyo kodi zilipanuliwa na kuwafikia mpaka watu wa chini na sasa hivi Tabaka la kati na masikini wanalipa kodi zaidi ya matajiri, kwani matajiri wamewazidi ujanja wasomi, kivipi? *The power of corporation* Ni kupitia nguvu ya mashirika na makampuni ndipo matajiri wameweza kuizidi serikali kwenye kulipa kodi, hivi unafahamu mtu anayemiliki kampuni analipa kodi ndogo kuliko mtu anayemiliki biashara binafsi? Je unafahamu Leo kama una kampuni ukiwa na madeni au kuhitajika kufilisiwa Mali zako binafsi haziguswi isipokuwa kampuni yako pekee? Na kampuni ni karatasi linalotambulika kisheria na kupitia makampuni ndipo serikali na wasomi wamezidiwa ujanja na matajiri. Robert anasema hulipa kodi zaidi kwa sababu wao wanachofahamu ni kuamka na kwenda kazini na kipato kinapoongezeka na kodi inaongezeka pia, Robert anasema poor dad alimshauri akiwa mkubwa ahakikishe anapata kazi kwenye shirika zuri na kisha apande kazi taratibu mpaka kufika ngazi za juu, alipomweleza swala hilo Rich dad akamwambia kwanini usubirie kupandishwa ngazi? Kwanini usitengeneze ngazi yako mwenyewe? Hapa ni Sawa na sasa kuweka bidii kazini ili upandishwe vyeo ni kwanini usijiajiri na kuwa na kampuni yako mwenyewe? Robert anatuambia akiwa bado kwenye ajira mwaka 1974 alifuata ushauri wa baba tajiri na kuanzisha kampuni yake ya kwanza.Kampuni ya kuuza na kupangisha nyumba, anasema mwanzo kodi zilikuwa kubwa zaidi lakini baadaye alianza kuona ushauri wa baba tajiri ukifanya kazi na ndipo kupitia faida kutoka kwenye kampuni yake hii aliweza kununua gari lake la kwanza la kutembelea. Rafiki unahitaji kufahamu hesabu za fedha, kufahamu fedha unayopata na kuitumia kama mbegu kwa kununua ASSET na kupitia hilo utaweza kuzalisha na kupata fedha zaidi, Pia unahitaji kufanya uwekezaji ili fedha ikufanyie kazi, Pia utahitaji kulifahamu soko vizuri ili uweze kuuza zaidi na mwisho utahitaji kufahamu sheria ili ujuwe ni vipi utaweza kupata unafuu kwenye kodi na maisha kwa ujumla ili uwe na maisha bora. Rafiki kwa Leo tuishie hapa, nikutakie siku njema; Makala hii imeandaliwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga,mwanafunzi wa jinsi fedha inaweza kunifanyia kazi kupitia kupitia chuo cha Kisima cha maarifa, tuko pamoja na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogsport.com 0712161251/0763766944
Sunday, 26 July 2020
Hivi ndivyo unavyoweza kunoa siraha yako....
Habari za wakati huu rafiki, hongera kwa jumapili nyingine, siku ambayo tunamalizia wiki iliyopita kwa kutathimini yale tuliyofanya na wapi tumefanya vizuri na yapi hatukufanya vizuri kwenye wiki lililopita ili wiki hii tuweke bidii na kuwa bora zaidi......
Leo tuangalie maneno ya mwana falsafa *EPICTETUS* akitaka tufahamu kipi tunaweza kufanya na tukawa bora zaidi.
_"Even if I lack the talent, I will not abondon the effort on that account...., we do not abondon any discipline for despair of over being the best in it."_
Kauli hii inatuaminisha kwamba vipo vitu vinavyoweza kuzidi vipaji na elimu,ukivitumiaukivitumia unaweza kufanya makubwa na hiyo ndio siraha inayoweza tumiwa na Kila mtu.
*Weka kazi*
Watu wanaweza kukuzidi Kila kitu lakini wasikuzidi kuweka kazi, hakikisha Kila siku unafanya zaidi ya Jana, mwanzo utaonekana kama umechanganyikiwa na matokeo hayataonekana lakini ukiweka kazi zaidi lazima utafikia ukuu na utawazidi walio kuzidi elimu, wenye vipaji vikubwa na utabobea zaidi yao kwenye hilo unalofanya, tafiti zote duniani zinaonyesha hivyo, angalia waliofanya makubwa wana elimu ya kawaida na hawana vipaji vya kutisha ila walihakikisha wanaweka kazi kweli kweli.
*Nidhamu*
Ukiwa na nidhamu kwenye kidogo unachofanya kwa kuhakikisha unakiheshimu lazima kitakupa zaidi ila usipoweka nidhamu na kudharau hutafika popote hata ungekuwa na kipaji kizuri namna gani, ukiona mtu anafika mbali ni kwasababu ameheshimu kile alichonacho, unapokuwa na kidogo ukakithamini na kuhakikisha unakuwa mtu wa kuthamini ulipo napo patakuonyesha njia ya juu zaidi, haijalisha unataka kufika wapi lazima uanze na hapo ulipo na kuweka nidhamu ya Hali ya juu.
Kwenye kisima cha maarifa msingi wetu Mkuu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na tunaishi kwa vitendo jambo hili,hatuangalii uko wapi lakini kwa kuweka kazi na kujituma huku nidhamu ikiwa juu ni hakika kile tunachokitafuta lazima upate kile unachokitaka, dunia haitakupa vitu kwa urahisi lazima ufuate kanuni za asili ndipo dunia ikupe zaidi, ardhi ukiipa mbegu inakupa zaidi, kadri unavyopaipa mbegu zaidi ndivyo inakupa mazao mengi zaidi, nidhamu ya palizi na kuondoa magugu ndivyo unavyopata mazao zaidi, uvivu ni magugu kwenye kazi,kiburi ni magugu,dharau ni magugu kwenye mafanikio.Ondokana na vitu hivyo na utakuwa vyovyote unavyotaka.
Asante na nikutakie siku njema katika kuliendea wiki linaloanza kesho, katumie haya tunayoambiwa na mwanafalsafa EPICTETUS na kisha utaona matokeo utakayopata.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Saturday, 25 July 2020
Maswali 12 ya kujiuliza kila siku na yatakwenda kubadilisha maisha yako......
Rafiki yangu kama unaishi na huna kipimo unachotumia kupima maisha yako kama unakua au hukui basi huna maisha,kwani maisha yasiyo pimwa hayafahi kuishi......
Kwanza kabisa nakusalimia rafiki wa ustawi wa fikra, ningekuwa nimeipoteza siku hii na kutoishi kama ingepita sijakuandikia, ninachokuandikia hapa ni kitu ambacho kimenitafakarisha sana leo, Kama ni msomaji wa falsafa na vitabu vingi huwezi niambia humfahamu RYAN HOLIDAY,Leo kupitia kurasa yake anatuletea Zawadi ya maswali kumi na mbili ambayo Kila binadamu anayetaka kufahamu kusudi la maisha yake anapaswa kujiuliza, karibu tuyasome pamoja, lengo ni kujipa majibu sahihi ya maswali haya, kaa chini na jipe majibu sahihi...
*1.Who do you spend time with?*
Hebu jiulize muda wako mwingi unatumia na nani? Goethe would say "Tell me who you spend time with and I Will tell you who you are".Msemo huu unatuambia kama ukitaka kumfahamu mtu alivyo basi angalia watu wanao mzunguka, rafiki yangu kama umezungukwa na watu walio kata tamaa basi tambuwa huwezi kuwa shujaa, kama muda mwingi unautumia na watu wanaolalamika basi huwezi acha kulalamika, kama wanaokuzunguka ni watu wa kushindwa basi na wewe utashindwa, hebu Leo amua kusikiliza na kujihusisha na washindi na kataa kabisa na watu wanao kuambia maisha ni magumu na hayawezekani, jiulize kama walio kuzunguka wanakuinua au kukushusha?
*2.Is this in my control?*
Jiulize kama unalohangaika nalo liko ndani ya uwezo wako au? Kutaka Kila mtu akupende ni jambo lililo nje ya uwezo wako, kumridhisha Kila mtu ni kupoteza muda wako, kufikiria wengine watanionaje nalo liko nje ya uwezo wako, kuishi kwa furaha ni jambo ambalo Kila binadamu ana uwezo nalo hivyo kabla hujakubali lolote likusumbuwe jiulize je lipo ndani ya uwezo Wangu? Acha kuangalia maoni ya wengine yanayokurudisha nyuma, we Fanya yako.
*3.What does your ideal day look like?*
Siku unayoishi Leo ndio itaamua kesho yako, acha kujidanganya kwamba miaka miwili, mitano au kumi nitakuwa nimefanya maendeleo makubwa wakati Leo yako hujuwi unakwenda kufanya nini? Ifahamu Leo yako na pambana nayo kwa Kila hali na Mali na hilo litaifanya kesho yako kuwa bora, hakika ni Leo yako na siyo kesho yako, kwani kesho yako itaamuliwa na Leo yako.
*4.To be or to do?*
Watu wengi tunaangalia matokeo ya nje kwa walio fanikiwa na kutamani kuwa kama wao, lakini mbaya zaidi hatupo tayari kuishi kwa vitendo yale wanayofanya, muda mwingi unatumia kujadili maisha ya wengine, kutizama tamthilia na kubishana siasa kisha kujiambia Kila siku unataka kuwa kama mtu fulani mwenye mafanikio, chaguwa kufanya na kuweka kazi na siyo kuendelea kuishi maisha ya kutamani bila ya kuweka kazi.
*5.If I am not for me,who is?If I am only for me,who am I?*
Rafiki siyo vibaya kufanya kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya familia yako na ndugu zako, lakini kama hicho ndio kitu pekee umekuja kufanya duniani basi maisha yako hayana maana yoyote, Kila unachojishughulisha nacho basi kifanye kwa ajili ya wengine na hapo utakuwa na maisha ya maana, ona una jukumu la kusaidia wengine na hapo utakuwa na maisha ya utoshelevu.
*6.What am I missing by choosing to worry or be afraid?*
Kila unapohisi hofu ikikujia jiulize ni kipi nimepanga kukikosa nikichaguwa hofu initawale? Gavin de Beycer writes "when you worry ask your self "what am I choosing to not see right now? Kauli hii inatuambia kwa kuishi maisha ya kuhofu ni Sawa na kuamua kufumba macho tusione wakati macho yetu ni mazima, fursa nyingi sana zinatupita kwakuchaguwa maisha ya kujiambia nikifanya biashara nitapata hasara, nikiacha kazi nitaishije? Na wakati tumeipa hofu itutawale ndipo fursa nyingi zinatupita na kubaki na maisha yetu yasiyo na tija yoyote.
*7.Am I doing my Job?*
Kila unapofanya jambo lolote jiulize kama hiyo ndio kazi yako, unaposengenya wengine jiulize hii ndio kazi yangu?fahamu kazi yako unayopaswa kuifanya na hakikisha unaikamilisha ipasavyo, kazi yako siyo umbeya lakini ndio muda mwingi unatumia kufanya umbeya, kazi yako siyo mpira lakini muda mwingi unautumia kubishania mpira, wewe siyo mwanasiasa lakini muda mwingi unazungumzia siasa.
*8.What is the most important thing?*
Kama hufahamu kitu gani muhimu sana kwako basi utajikuta unaishi maisha ya wengine na kuachana na yako, lazima ujiulize ni kipi muhimu zaidi kwenye maisha yako na hakiisha unakifanya na kukifikia na achana na vingine visivyo muhimu.
*9.Who is this for?*
Swali unalopaswa kujiuliza ni kwanini unafanya unachofanya? Kwanini naandika? Kwanini nawauzia watu? kwanini najifunza Kila siku? Watu wengi wanafanya kwasababu wameona na wengine wanafanya lakini hawana sababu za muhimu kwanini wafanye na ndio maana wakipitia magumu kidogo wanaachana na wanachofanya na kuanza kingine. Kwanini nafundisha? Kwanini naimba?
*10.Does this actually matter?*
Kila baada ya muda jiulize kama hicho unachofanya ni sahihi? Unachowaza, unachoongea, unachowatendea wengine ni sahihi? Ndio kitu muhimu wewe kukifanya?
*11.Will this be alive time or dead time?*
Muda wa kujiambia nitafanya, nitaanza, nitahakikisha, nitafurahia,nitanunua na mengine mengi yanayofanana na hayo tunayaita maisha mfu, maisha yaliyokufa, muda hai ni muda wa kujifunza na kuweka kwenye matendo na siyo kujiambia nitaanza au nitafanya wakati mwingine.
*12.Is this who I want to be?*
Unapenda uwe mtu wa hekima lakini unakasirika muda wote, unapenda uwe mtu wa mungu lakini huna uadirifu, unataka kuwa mama/baba bora lakini unafanya kinyume, ukidanganya jiulize ni hivi ndivyo ninavyotaka kuwa? Mwandishi anasema huwezi kuwa mtu wa kazi wakati unapenda njia za mkato,"How we do anything is how we do everything"Kama siyo mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa, huwezi jiambia umedanganya kidogo ila kesho utakuwa mkweli, huwezi kuwa mvivu kwenye kazi ulio ajiriwa halafu ukawa na bidii kwenye kazi ya kujiajiri kwasababu uvivu uko ndani mwako.
Rafiki mwandishi anakutaka umalizie na swali kutoka kwa Frakl Struggled-Kwako maisha yana maana gani? maswali haya utayajibu kwa vitendo na maamuzi utakayofanya na siyo kwa mdomo, nikutakie wakati mzuri na bora rafiki yangu.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga. Napatikana kwa amail yangu bna blog yangu ambayo nakuwekea hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Wednesday, 22 July 2020
Gharama zilizojificha ambazo zinaongeza matumizi yako......
Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nyingine, Nina imani hujambo na waendelea na mipango yako mizuri ya Kila siku, endelea kuweka kazi kwani huyo ndio rafiki wa kweli na hawezi kukutupa.......
Leo tutaangalia sehemu ya matumizi ambayo wengi tunapoteza fedha zetu pasipokufahamu,au kuona ni kiasi kidogo lakini baada ya muda kupita tunakuwa tumepoteza kiasi kikubwa sana. Mwandishi anasema ni muhimu kufahamu kitu kinachochukuwa fedha kwenye mfuko wako kwani kadri matumizi yanavyoongezeka na kuwa makubwa ndivyo unavyojiweka mbali na utajiri. Na pale tutakapo dhibiti matumizi haya basi hata kiasi cha kujilipa kinaweza kuongezeka.
*Kundi la kwanza ni gharama za miamala ya kifedha*
Maisha yamekuwa rahisi sana,unaweza kukaa tu nyumbani kwako na kupata mahitaji yako yote muhimu ya kifedha. Urahisi huu umefanya tunapoteza fedha nyingi sana kwani huduma hizi nzuri zina gharama na kadri tunavyozitumia bila mipango ndivyo tunavyoingia gharama kubwa.
Hebu chukulia mfano mfanyakazi analipwa mshahara kupitia benki kisha akahamisha salio kwenye simu yake, akitaka kutoa itabidi aende kwa Wakala,hapo anakuwa amekatwa wakati anahamisha salio, kisha atakatwa kutoa fedha kwa Wakala na anapoteza takribani 10000 mpaka amepokea hela yake kama kiasi anachochukuwa ni laki moja kuendelea.Mwandishi anasema watu wengi hupenda kuacha fedha benki ili wasizitumie kirahisi lakini Kila wanapopata tatizo huenda Benki na kutoa salio na hapo kuongeza gharama, wengine huacha kwenye simu zao na kutoa kidogo kidogo na hapo pia gharama zinaongezeka. Kama una tabia za hivi nenda kachukuwe benki statement na utaona kiasi unachopoteza.
_Hatua za kuchukuwa_
A.Acha kufurahia huduma piga hesabu zako vizuri
B.Toa fedha zako kwa Mara moja na jijengee nidhamu ya kutorudi tena benki baada ya kutoa kiasi chote ulichopangia bajeti bila kurudirudi benki.
C.Kama uko mbali na benki na hivyo kuokoa gharama ya usafiri basi toa kiwango kikubwa kwa Mara moja kuliko kutoa Mara kwa Mara.
D.Kama unalipwa kwa njia ya simu kwa kazi unazofanya basi usitoe Kila unapolipwa bali subiria mpaka zimekuwa nyingi uzitoe kwa pamoja.
E.Kabla hujatumia huduma za ATM na simu kwenye miamala jiulize kama hakuna uwezekano wa kutumia njia nyingine ili kupunguza gharama.
*Kundi la pili;gharama za mawasiliano*
Kwa sasa mitandao ya simu wamekuwa wakitumia Kila ujanja ili kuchukuwa fedha zako zaidi, zamani ulikuwa ukijiunga unapata kifurushi chenye Kila kitu lakini sasa hivi wanataka ukijiunga mb,basi itakubidi ujiunge na dakika peke yake na meseji pia peke yake, hili limechangia gharama kuongezeka, mwandishi anasema usipokuwa makini kwa mwezi utatumia zaidi ya 30,000 kwa vorcher pekee, gharama hizo siyo kubwa kama na wewe una nufaika na mawasiliano lakini kama hulipwi kwa mawasiliano kiasi ni kikubwa sana.
_Kitu cha kufanya kuepukana na gharama hizi_
A.Chagua mtandao mmoja Mkuu utakao tumia na ukakupatia huduma na vifurushi unavyotaka kuliko kuwa na mitandao mingi inayokuongezea gharama.
B.Tenga muda maalumu wa kuwasiliana na watu muhimu wote kwa Mara moja, kuliko kufanya mawasiliano ya Kila siku na kuongeza gharama.
C.Unapotumia mitandao ya kijamii kabla ya kufunguwa picha au video unazotaka kuangalia, vipo vitu Vingi vinavyokula mb za kutosha na havina msingi wowote kwako.
D.Kabla hujafanya mawasiliano jiulize kuna fedha nitapata, Je nita imarisha mahusiano? Ninatengeneza mtandao mzuri? Nje na hapo achana na mawasiliano hayo.
*Kundi la tatu; gharama ndogo ndogo za nyumbani*
A.Vifurushi vya TV;kama unalipa zaidi ya 10000 kwa king'amuzi basi umeamua kupoteza fedha zako kwa vitu vingi visivyo na tija.
B.Fuatilia kwa umakini gharama za Umeme na Maji.
C.Vyakula vinavyoharibika na kutupwa ni sehemu inayochukuwa fedha zako nyingine.
Wengi wanapuuzia maeneo hayo lakini umasikini wao unatokana na kupuuza kwao kwani fedha nyingi hupotelea hapa.
*Kundi la nne; Gharama ndogo ndogo za maeneo ya kazi na biashara*
Kuwa makini na vyakula au Vinywaji unavyotumia kwa kununua kwenye maeneo ya kazi, maeneo hayo yamekuwa yanachukuwa fedha nyingi pasipo kufahamu, kitu muhimu ni Maji ya kunywa ambayo unaweza chemsha nyumbani na kubeba kwenda nayo kazini. Hata chakula unaweza beba kama eneo la kazi halina utaratibu mzuri wa chakula na hili litakupunzia gharama.
Rafiki ukikaa chini na kufanyia kazi maeneo hayo, tayari unakuwa na kiasi ambacho unaweza kuongezea kwenye mafungu yako ya ki uwekezaji na kupiga hatua zaidi za ki maendeleo.
Asante sana na uwe na siku njema, makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga, mwanafunzi wa namna fedha itaweza kunifanyia kazi kupitia chuo cha Kisima cha maarifa.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Tuesday, 21 July 2020
Nguvu ya taswira sehemu ya pili......
"Truly, thoughts are things, and their scope of operation is the world, itself"
Nimeona nianze na maneno hayo ambayo mwandishi amemalizia hivyo kutoka sura ninayokwenda kukushirikisha leo, kwanza kabisa niendelee kukushukuru wewe rafiki unayeendelea kujifunza na Nina hakika ukiyafanyia kazi haya utafika mbali sana.....
Rafiki kutoka kwenye kitabu chetu cha THINK AND GROW RICH ,wiki iliyopita tuliangalia umuhimu na aina za taswira na jinsi gani taswira itakupa chochote unachotaka kama utaitumia vizuri, rafiki labda nikuambie kitu kwamba mambo yote mazuri unayoyaona sasa na tunayatumia miaka kadhaa iliyopita hayakuwa halisia hivi, bali ilikuwa taswira kichwani kwa mtu, ndege zinazoruka angani na kusafirisha watu ilikuwa taswira kwa Write brothers, magari ilikuwa taswira kwa Henry Ford na mengine mengi mazuri yalitokana na taswira ambayo mtu mmoja aliiweka kwenye akili yake, Leo mwandishi ametuandalia kisa kimoja.
Miaka 50 iliyopita daktari mmoja alitoka kijijini na kwenda mjini akiwa na birika linaloonekana kuu kuu, alipofika mjini alikwenda kwenye duka moja na alionekana akiongea naye kwa siri, baadaye alionekana akimkabidhi birika lile pamoja na kanuni zilizopo kwenye birika lile, mwandishi anatuambia karani yule aliamua kutoa akiba yake yote na kumkabidhi karani yule, Je birika lile lilikuwa na nini, na je ni kanuni gani hiyo ambayo ilimfanya karani atoe akiba yake yote na kumpa daktari?
Karani yule alitoa akiba yake yote ya dola 500 za kimarekani na kumkabidhi daktari yule, Daktari alifurahi sana kuweza kutengeneza pesa kwa kuuza wazo kwa karani pasipo hata na uhakika kama wazo lile likichanganywa na kanuni zile litaweza kuleta matokeo, upande wa karani wasiwasi na mashaka vilimshika kwamba kanuni zile na birika vitamletea pesa kweli zaidi ya akiba yake ile aliyokuwa nayo?
Kabla sijaendelea na kisa hiki ambacho ni cha kweli na siyo cha kutungwa kama anavyosema mwandishi kwa kumnukuu "It is not a story from Arabian Nights, a story of facts".
Kipo kitu nimejifunza hapa kabla sijaendelea na simulizi hii ya kweli, kuna mawazo mengi sana tunayapuuza ambayo tunaona hayawezekani na kupitia mawazo hayo ndio tungeweza kutengeneza utajiri mkubwa sana, lakini pia woga wa kupoteza fedha zetu ndio kunatufanya tushindwe kujaribu vitu vipya vyenye manufaa kwetu.
Basi kupitia kanuni na birika lile karani aliweza kufanya mabadiliko makubwa sana duniani, kwani mpaka sasa karani huyo kupitia wazo lile na kuchanganya na ubunifu wake ameweza kutengeneza ajira za watu wengi duniani, kaweza kutengeneza tilioni za pesa, Mimi na wewe tumeburudika kupitia wazo na taswira kutoka kwa daktari kwenda kwa karani, kupitia birika lile leo ukiwa popote ulimwenguni, kwenye majiji na vijiji a hata uchumi ushuke vipi bado bidhaa hii itaendelea kuwepo, Je unataka kufahamu ni bidhaa gani hiyo? Basi ni COCA-COLA.
Rafiki hata wewe unayo mawazo na taswira pana sana lakini jamii itakuambia huwezi na wewe utakubaliana nao, lakini hata wewe una mawazo ya ki coca -cola lakini unajiambia haiwezekani na unapuuza ila ukiamua kufanya kitu nina hakika siku moja utajishukuru, toa kile cha kwenye taswira yako kiwe halisia.
Nikutakie siku njema rafiki yangu,usikubali siku ikapita bila ya kujifunza chochote, nikupongeze kwa kuendelea kutembelea USTAWI WA FIKRA na yapo mengi sana utaondoka nayo.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki yako, Mwl Kelvin Kinyaga na Mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kupitia chuo cha KISIMA CHA MAARIFA.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Monday, 20 July 2020
Tiba ya tano;Fanya sehemu unayoishi kuwa uwekezaji wenye faida.......
Siku nyingine, Nina amini kumekucha salama na uko tayari kuendelea kujifunza,kwani hakuna siku utajiambia huoni umuhimu wa kula, vivyo hivyo nakujifunza,kwa kuwa unaendelea kuishi basi una Kila sababu ya kuendelea kujifunza namna ya kuishi bora zaidi....
Kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tunaendelea na tiba za kutunisha mifuko yetu, baada ya kujifunza tiba zilizopita na sasa tuangalie tuba namba tano ambayo ni _Make of thy dwelling a profitable investment_
Mwandishi anatuonyesha baada ya kufuata tiba nne zilizopita na kutenga sehemu ya kipato na kuwekeza basi lazima fedha zitaanza kuongezeka na hapo utahitaji kuwa na nyumba yako mwenyewe, anasema hakuna familia yenye furaha kama haimiliki nyumba yake,hivyo tiba ya tano ni kuhakikisha unamiliki nyumba yako na hapo utatumia fedha unayolipa kodi kuwekeza kwenye maeneo mengine na hapo watoto wako watakuwa huru na kufurahia maisha.
Rafiki ni ukweli usiopingika kwamba kuwa na kwako kunaleta Uhuru na furaha lakini kama utaanza na tamaa ya kujenga nyumba yako kabla ya kuwekeza sehemu zingine zinazozalisha kwa haraka basi utakuwa kwako katika namna ya mateso ya kulipa madeni kwa kipindi kirefu sana, mwandishi anashauri hata kwa kukopa na kulipa deni pole pole siyo vibaya kama uwekezaji wako unaendelea kukua na ukalipa taratibu mkopo wako.
Angalizo, lazima uwe na hakika wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba yako hakuta athiri maeneo yako ya uwekezaji, wengi sana imeonekana wanapoanza ujenzi wanachukuwa sehemu za mitaji yao na kujengea nyumba zao na kisha kujikuta wanaanza upya na wakati huo gharama za maisha zinakuwa zimeongezeka.
Hivyo rafiki tambuwa kwamba utahitaji kuwa na kwako ili uwe huru na tumia nyumba yako kama sehemu ya uwekezaji, panda miti ya matunda, fuga na kama eneo ni kubwa weka hata bwawa la samaki na hilo litaongeza thamani ya nyumba yako na kukuinua ki uchumi na hivyo kufurahia maisha, usikubali nyumba yako kubaki na mapambo na maua pekee itumie kuwekeza. Asante na nikutakie siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Sunday, 19 July 2020
Usisubirie ufukuzwe kazi ndipo ugundue nyumba yako unayoishi siyo mali inayozalisha (Assets).......
Hongera ndugu yangu, siku nyingine na tunakwenda kuanza juma lingine kwa nguvu ile ile, pamoja na matokeo kidogo unayopata kwenye kile unachojishughulisha nacho bado una jukumu la kwenda mbele, kuweka kazi bila kurudi nyuma.......
Leo tutakwenda kuangalia sehemu nyingine ya kutupeleka kwenye utajiri kwa kupata ushauri wa baba tajiri, kabla hatujafika huko tumalizie mjadala wetu wa nyumba yako ya kuishi siyo mali inayozalisha kwa kusema hivi, waza umefukuzwa kazi Leo na huna chanzo chochote cha fedha na una nyumba yako unaishi na familia yako je nyumba hiyo itakusaidia kuondokana na adha ya kulipa kodi lakini haitakulisha, haitalipia ada za watoto wako shule na kufanya maisha yako kuendelea kama yalivyo sasa, mwandishi anasema watu hawaoni na kukubaliana na hili mpaka pale wanapoamua kuacha kazi au wakiachishwa kazi ndipo hukimbilia kuuza nyumba zao kwa bei ya chini na kutafuta kuwekeza kwenye maeneo yanayozalisha na wakati mwingine huwekeza sehemu wasizo zijuwa vizuri kutokana na hali za kuchanganyikiwa wanazokuwa nazo. Hapa ndipo anakuja na funzo la kwamba FANYA BIASHARA UNAYOIFAHAMU VIZURI.
Robert anatuambia akiwa mdogo baba masikini alimshauri kutafuta kazi inayolipa vizuri na baba tajiri alimshauri kuanza kuwekeza mapema ili ajipatie Uhuru kifedha, Je wewe Wazazi wako walikushauri mini?Na Je wewe unawashauri nini watoto zako? Je ni ushauri wa mama au baba tajiri au masikini? Jipe mwenyewe majibu ya maswali haya.
Mwandishi anasema matatizo ya fedha hutokana na watu kuwafanyia kazi watu wengine kwa muda mrefu bila kufahamu hatima yao. Anasema yote haya hutokana na mfumo wa elimu kuandaa watu kwa namna hiyo na siyo kuwafanya wafikie Uhuru wa kifedha. Watu wengi hujifunza taaluma mbali mbali na wanapoajiriwa wanafanyia kazi taaluma zao na anashangaa pale anapomuuliza mtu unafanya kazi gani anamjibu "Banker",akimuuliza unamiliki benki? Anajibu hapana.
Mwandishi anasema pamoja na kwamba umeajiriwa bado unahitaji kufanya biashara, watu hawataki kufanya biashara kwasababu ya hatari ya kupoteza fedha zao na hilo linawafanya kukubali kuishi kwenye utumwa wa kuajiriwa na kulipwa kidogo maisha yao yote. Hivyo anza Leo kufikiria ni biashara gani unapenda kufanya na jitaidi ujifunze kwa kina na kuijua ndipo uingie kwenye biashara hiyo, Anasema yeye alipenda sana majengo ndio maana aliamua kununua nyumba na kuzipandisha thamani halafu kuziuza kwa bei ya juu na kuwekeza kwenye makampuni kwani ndio maeneo aliyopenda, Je wewe unapenda nini? Chugua Leo na anza kujifunza kuwekeza huko na pambana uweze kufikia maeneo yafuatayo ki uwekezaji.
1.Biashara ambayo haihitaji uwepo wako moja kwa moja, kwani wengi ni watumwa wa biashara zao, kwani wasipokuwepo na biashara zao zinakufa.
2.Anza kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa, vipande na aina nyingine za dhamana na fedha
3.Uwekezaji kwenye nyumba za kupangisha au kuuza, hapa naona mwandishi alitengeneza mfumo mzuri sana wa kutambuwa wapi anapangisha na wapi ananunua na kupandisha thamani na kuuza na hilo limemsaidia kufikia utajiri mkubwa.
Rafiki bilashaka umeendelea kujifunza na umeondoka na kitu, acha kununua vitu visivyo zalisha kwa pesa yako, nunua nyumba ya kuishi, gari la kutembelea na vitu vya kifahari kupitia faida uliyopata kutoka kwenye uwekezaji uliofanya na ukifanyia kazi hili,Mimi na wewe tutakutana sehemu nzuri ki uchumi na kupongezena, ufukara siyo kitu cha kujivunia.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kwenye chuo cha Kisima cha maarifa, endelea kutembelea blog yangu na tuwasiliane kwa ushauri wowote kwani nazungukwa na wengi, asante.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Ufalme wa mbinguni unaanzia duniani......
Habari za wakati huu rafiki yangu, tuna kila sababu ya kumshukuru mungu kwa afya na uzima kwa wiki nzima na changamoto tulizopitia ni sehemu ya kutuimalisha kwani hakuna jaribu utakalopitia likakuacha dhaifu,kama halijakuua Basi limekuimarisha ki roho au ki akili......
Leo tupate neno kutoka kwa Mwinjili Mathayo (Mt:13:24-43)
Kupitia mwinjili Mathayo kwenye somo tajwa hapo juu tunaweza kuona yesu akiongea na makutano kwa kutumia mifano,kabla hatujaangalia mifano hiyo utakubaliana na Mimi kwamba maisha ya mbinguni ambayo Mimi na wewe tunayatamani kuishi baada ya kukamilisha maisha ya duniani, ikiwa mungu mwenyewe kupitia mwanae yesu kristo aliyaishi maisha ya dunia na mwisho akayashinda mauti basi na sisi lazima tujiulize na kufahamu msingi utakao tufanya siku moja tuyaishi maisha hayo ya umilele.
Kupitia masomo hayo yesu alitumia mifano mitatu akiifananisha na namna ufalme wa mbinguni unavyofanana, kupitia mifano hiyo tutaangalia mifano miwili tukiifananisha na maisha yetu ya Kila siku.
*1.Mfano wa ngano*
Kwenye mfano wa ngano na magugu tunapata funzo kubwa sana, wakati ukipanga mambo yako kwa usahihi kabisa na mipango mizuri kama tulivyoona kwenye mfano wa Shamba la ngano, mbegu bora na Shamba safi kabisa basi kitu tunachotarajia ni kupata mavuno safi yasiyo na changamoto yoyote, lakini baada ya muda kupita na ngano inapoanza kutoka inaambatana na magugu, magugu ni mfano wa changamoto ambazo zinaibuka pamoja na mipango mizuri tuliyoipanga, pamoja na changamoto hizo je maamuzi ni yapi? Kupitia neno la mungu tunafundishwa kwamba pale tunapopitia changamoto basi tunapaswa kuvumilia kwani kupitia somo nililokushirikisha tunaona watumwa wakishauri magugu kung'olewa lakini yesu anawajibu tusifanye hivyo tuyaache yakuwe pamoja na ngano na wakati wa kuvuna ndipo tutachambuwa ngano na kufunga matita magugu na kuyachoma moto, hapa tunapata funzo la kwamba safari ya maisha, safari ya mbinguni ni safari ambazo huwezi kujitenga na changamoto, kupoteza watu tunao wapenda, kujaribu biashara na kushindwa ni magugu kwetu, lakini hayo yote yanavyojitokeza kwanza tunapaswa kuyakubali na kuona ni sehemu ya ubinadamu wetu lakini mwisho utafika na mungu atatutenganisha na magugu, shida na mateso, hapa ndipo tunaona kwamba uvumilivu ni njia ya kweli ya kutufanya tushinde duniani na mbinguni.
*2.Mfano wa punje ya haradani*
Inasemekana haradani ndio mbegu ndogo kuliko zote, wakati nasoma hapa nikajiuliza kama punje ya ulezi ni kubwa kwa punje ya haradani Je hiyo punje ya haradani inafananaje? Lakini biblia inatuambia pamoja na udogo wa punje hii lakini ikiota inakuwa kubwa kuliko mboga zote na kutengeneza matawi ambayo hata nyuni wa angani hutua katika matawi yake. Rafiki haijalishi udogo wako ulio nao sasa, ki uchumi,ki mamlaka, ki umri na ki mtazamo lakini ukijifananisha na mbegu ya haradani unapata tumaini ya kwamba unaweza kuwa vyovyote unavyotaka.
Nini nimejifunza kwa somo hili?
Ushindi huja mwishoni baada ya maangaiko namateso ya muda mrefu wa kuvumilia na kujitoa kutafuta unachotaka bila kuchoka, safari ya yesu kwetu wakristo ni ki elelezo tosha, alibezwa, aliteswa,alitemewa mate na mengine mengi lakini alivumilia yote kwasababu alifahamu nini alikitafuta na mwishoni tunaona anaibuka Mshindi zidi ya mauti na kutukomboa, Je wewe unataka nini? Ufalme wa mbinguni, maisha ya utajiri na kusaidia wahitaji? Upo tayari kukabiliana na mateso yapi? Kipi unavumilia ili ushinde mwisho? Ukisemwa na kukosolewa unakasilika au unafahamu ni njia ya kufika unakotaka kufika? Vipi ukitemewa mate utakubaliana? Utavumilia? Nenda kayaishi haya kwa vitendo na mwishoni tutakutana pamoja tukishelekea ushindi pamoja.
Makala hii imeandikwa na Kelvin Kinyaga, mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya fedha kupitia Chuo cha Kisima cha maarifa tutakutana kesho tukifanyika Baraka.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Saturday, 18 July 2020
Usiniombe pesa niombe wazo..........
Habari rafiki,nikupongeze kwa siku na jumamosi nyingine, kwa wanaothamini muda wanafahamu tofauti kati jumamosi iliyopita na hii na hujipanga ili kuitofautisha na jumamosi inayofuata, ila kwa tulio wengi ni wale tunao furahia siku hizi za mwisho wa wiki na kuona ni siku za kupumzika na kustarehe kumbe kwa kufanya hivyo ndivyo tunazidi kujididimiza bila kufahamu.....
Rafiki tangu nimeanza kufahamu nguvu ya maarifa nimekuwa natumia njia moja wapo kupata kiasi cha pesa ninachohitaji na njia hiyo imekuwa ikinisaidia sana, njia hiyo ni kuchukuwa kiasi cha pesa ninachohitaji na kukigawa kwa 1000,2000,3000,4000 na kuendelea,Kwa mfano nina hitaji 360,000 kwa mwaka nitajuwa natakiwa kubuni wazo litakalotengeneza 1000 kwa siku, 720,000 wazo litakalotengeneza 2000 kwa siku, Nahitaji 1,080,000 nitahitaji wazo litakalonipati 3000 kwa siku na hili limekuwa likinisaidia sana, unaweza kusema huo ni uongo tu hicho kitu hakiwezekani, uweke 1000 Kila siku?hupati matatizo yoyote na kutumia fedha hiyo? Wewe unatushauri ulishafanya?rafiki pengine nakuandikia makala Kila siku na hufahamu nina jishughulisha na nini nje ya maarifa ninayokupa.
Kabla sijakwenda kukuambia najishughulisha na nini napenda nikuambie jambo moja ambalo masikini tunalipenda sana, mtu akipata tatizo lolote anakimbilia kutaka pesa ili atatue tatizo lake, hilo halina ubaya wowote na siyo tatizo lakini kuendelea kusubiria upate tatizo tena na tena na kuomba fedha au kukopa hilo ni tatizo tena tatizo kubwa, ni Sawa na mtu ambaye Kila siku anakwenda kuomba samaki kwa jirani yake kwamba hana mboga lakini hata siku moja hataki kujifunza namna ya kuvua samaki ili kesho asiombe tena. Basi na Mimi nimejifunza namna ya kutengeneza pesa ni kufahamu nahitaji kiasi gani na kisha kutengeneza wazo litakalowezesha nipate kiasi hicho, hapa chini nitakupa mifano kwa kutumia biashara ninazojishughulisha nazo.
*1.AJIRA*
Kupitia kisima cha maarifa nimejifunza Ajira ni ngazi ya daraja 0 na siwezi acha kuitaja kwani siku zote napambana ili niweze kuondokana na daraja hili au kutolitegemea kuendesha maisha yangu kwani utumwa wa kuuza muda,nguvu na maarifa yangu kwa kiwango anachopanga mnunuzi na pamoja na yote anaweza nifukuza na kunifanya nitaabike, pamoja na kutambuwa changamoto za daraja hili bado kwa sasa nipo kwenye hatari hii ya kutegemea mshahara wa mwezi kwa kuajiliwa na serikali kama Mwalimu wa Secondary hapa mjini moshi.
*Biashara ya visheti*
Hii ni biashara ambayo Mimi na mke wangu tulianza kwa kutumia kanununi niliyokushirikisha pale juu, tunahitaji mtaji wa biashara fulani ya ndoto yetu kama familia, tukajiuliza ni kiasi gani tunahitaji ili kuweza kupata kiasi hicho? Mshahara hautoshi je tukope? Hapana kanuni ya fedha inakataa kuanza biashara kwa mkopo, je tufanyaje? Ndipo tukaanzisha biashara ya vitafunwa aina ya visheti ili kutengeneza 2000 kwa siku itakayowezesha kufikia lengo hilo, kupitia kisima cha maarifa tukaweza jifunza namna ya kuuza biashara hii na kwasasa hasa shule zinapokuwa zimefunguliwa tunaweza tengeneza zaidi ya 2000 kwa siku kama faida, kwani bidhaa hiyo inauzika zaidi kwenye mikusanyiko ya watoto kama shule na kwenye mini supermarket na hata maduka ya watu binafsi.
*Biashara ya vorcher*
Biashara hii tumeipa Jina la Asante Corona, wakati wa ugonjwa wa Corona mtakumbuka kwamba shule zote zilifungwa na Mimi miongoni Mwa walimu ilinibidi kukaa nyumbani ili kuweza kutii agizo la serikali ili kupunguza maambukizi, hapo ndipo wazo la kuuza vorcher za likatujia wakati tukifikiria ni kwa vipi miaka ya mbele tutaweza kupata mtaji wa kiasi fulani cha fedha ili tuweze kuendesha familia na kuwa huru na kipato, ndipo tukaja na wazo la vorcher ambalo tulilifanya kama sehemu ya huduma lakini sasa ni moja ya biashara nzuri sana kama unaelewa nidhamu ya fedha kwani tulianza na mtaji wa 40,000 na sasa tumeweza kutengeneza Mara mbili ya kiasi hicho ndani ya miezi mitatu,ni kiasi kidogo lakini si Sawa na bure na kwasasa tumebuni namna bora ambayo tumaianza wiki hii na inakwenda vizuri zaidi, Je unafahamu kwa mwezi unatumia vorcher kiasi gani? Basi karibu uwe mteja wetu tutakufahamisha matumizi yako na kukusaidia namna bora ya kupangilia vifurushi vyako ili uweze kutumia kiasi kidogo kuliko unachotumia sasa, na kama utahitaji kukupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na ukarudisha mwisho wa mwezi kiasi hicho hicho ulichotumia bila riba unakaribishwa, tumeanza na watu watano na sasa tuna wateja watatu wa huduma hii na bado wawili, hivyo kama unataka kupata huduma hii kwetu tuwasiliane kwa mawasiliano nitakayoweka hapo chini.Maombi yanaweza kubaliwa au kukataliwa kwani ni biashara kwa wale wenye uaminifu pekee wa kupatiwa huduma hiyo, Asante corona itakupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na utalipia kiasi Sawa na huduma uliyopewa bila riba yoyote ile.
*Biashara ya tuition*
Chochote unachofanya unaweza kutumia kama sehemu ya kipato zaidi, pamoja na kwamba sasa tunatoka kazini saa kumi na moja na nusu bado nikitoka nafika nyumbani na kwenda kwenye nyumba za watu na kufundisha watoto zao tukifanya home work pamoja, wateja ni wengi sana wa huduma hii tatizo ni eneo la kufanyia huduma hii na muda, kwani Kila Mzazi anataka watoto wake wafundishiwe majumbani mwao.
Hizo zote ni biashara binafsi ambazo nazifanya Mimi na familia yangu, zipo nyingine ambano Nina shirikiana na wengine sijaziweka hapa na niseme kitu kimoja kwamba bila maarifa ninayopata na naendelea kupata kupitia vitabu na KISIMA CHA MAARIFA na kocha wangu AMANI MAKIRITA nisingeweza yote haya na nisingefika hapa, mke wangu kipenzi unalala saa nane ili maisha yaende asante sana,wana kisima cha maarifa taifa na Kisima cha maarifa Kilimanjaro,nyie ndio nguzo kubwa kwangu, familia ndugu na wewe rafiki yangu nawashukuru sana kwa kuendelea kunitia moyo, tuwe pamoja na tufike pamoja, safari ni ndefu na ngumu lakini tutafika.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga, unaweza endelea kujifunza kupitia blog yangu hapo chini;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0712161251/0763766944
Thursday, 16 July 2020
Siyo kuwa wa kwanza bali kwa ubora upi?
Rafiki habari za wakati huu, hongera tena kwa kuweza kuchaguliwa kuifikia siku hii, nina imani umeamka na nguvu ya kwenda kuweka kazi zaidi ili upate matokeo zaidi.
Leo kwenye ukurasa wa Ijumaa kutoka kwenye mfululizo wa makala za ustawi wa fikra tutaendelea kuangalia maisha ya falsafa, labda nikuambie kitu rafiki kama huna falsafa unayoishi basi tambuwa uko kwenye hatari kubwa ya kutofika kwenye kile ulichopanga, kuna watu wanaishi misingi yao pasipofahamu kwamba hiyo ndio falsafa na wakivunja misingi waliyojiwekea lazima waazibiwe. Leo kwenye falsafa tunakumbushwa maneno yanayosomeka.
"Slow is smooth, smooth is fast"
Maneno haya yanatukumbusha kwamba chochote unachokitaka kiwe rahisi basi kitapatikana pole pole na urahisi huo ukiwepo ndio kitakufanya ufanikiwe haraka na kwa wepesi, Msemo huu unataka kutuaminisha kwamba maisha ya haraka hayana maana kwetu na kama unataka mafanikio ya kweli basi lazima uweke nguvu na bidii kwa muda mrefu, lakini kwa tulio wengi tunataka matokeo ya haraka,tunataka biashara zetu ziwe kubwa kwa muda mfupi na ndio maana tunashindwa haraka sana na kukata tamaa ya kuendelea na kuanza tena lingine na kushindwa tena na maisha yanaendelea hivyo.
Leo falsafa inatutaka kwanza kufahamu nini tunafanya, mbili kwanini tunafanya? kivipi tunafanya? Na hapo ndio kile tunachofanya kitafanikiwa kwa haraka zaidi, kama unafanya biashara na hufahamu biashara hiyo ki undani, na kwanini unafanya biashara hiyo? Labda ni msukumo wa kupata fedha pekee na huduma unayotoa ni mbovu na unaifanya kwa mazoea bila ubunifu lazima ife, hivyo anza kuwaza miaka kumi unataka uwe umefika wapi kwenye kile unachofanya.
Wanajeshi wana Msemo wao unasema hivi "More haste, less speed,better a safe commander than bold" hivi ni kipi bora? Kwenda kwa tahadhali na kuwa salama au kuwa na haraka na kuwa mateka? Hivyo kama unataka haraka basi utaipata kwa kuweka umakini kwa kwa kwenda polepole, kwani kadri unavyoitaka haraka ndivyo unavyochelewa na kadri unavyokuwa na kusudi na kulifanyia kazi taratibu ndipo tunapolifikia kwa haraka na wepesi.
Acha kuchanganyikiwa ukiona wengine wanafanikiwa haraka, muhimu ni kufahamu nini unataka kujenga na jifunze ni kwa namna gani utafika pale unapotaka kufika. Ubora ndio muhimu na siyo haraka, nenda kalifanyie kazi hili na acha kuwaza uharaka waza ubora.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.kelvin Kinyaga
Wiki hii nimepata kitabu kutoka kwa rafiki yangu Dr.Raymond Mgeni,kitabu hiki kinahusu mazoezi 20 ya falsafa ya Ustoa, hivyo Kila ijumaa nitakuletea zoezi moja la kufanyia kazi wiki nzima. Asanteni sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251/0163766944
Wednesday, 15 July 2020
Jinsi ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora......
Rafiki yangu habari za wakati huu?, hongera kwa Zawadi ya maisha na kuweza kuifikia siku hii nzuri kabisa, ninaposema siku nzuri sijakubaguwa wewe unayepitia changamoto kwani Nina amini kwamba hayo unayopitia ndio uzuri wenyewe, uimara wa Kingo ya mtu unapimwa wakati wa mafuriko, mti imara utauona wakati wa dhoruba, hivyo kupitia changamoto siyo laana bali ni kipimo cha uimara wako na hivyo endelea kufurahia kwa lolote lile unalolipitia.......
Leo kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA tutaangalia namna ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora.
SIRI YA UTAJIRI NI UBAHILI,mwandishi ameanza na kauli hii kwa kusema watu wengi hupenda kuitumia. Na kupitia kauli hii kumefanya zoezi la kutengeneza utajiri kupewa taswira hasi. Kwasababu ubahili ni kubana sana fedha na kujinyima,na wengi wanaona hayo siyo maisha ya kuishi. Kwamba ni kwanini ujitese kutengeneza utajiri wa baadaye badala ya kuitumia fedha hiyo sasa na ukawa na maisha bora? Mwandishi anasema hili ni swali ambalo wengi hujiuliza na lina mantiki kwani hupaswi kuteseka leo ili kesho uwe na maisha mazuri.
Mwandishi anasema pamoja na kwamba kujitesa leo ili uishi maisha mazuri kesho siyo maamuzi sahihi lakini bado ukweli ni ule ule, matumizi yanapaswa kuwa madogo kuliko mapato. Lakini unalifikiaje hili huku ukiwa na maisha bora kabisa kwako, yasiyo ya kujitesa?
Swali unalopaswa kujiuliza hapa ni hili,kwenye mchakato wa kupata fedha na kuzitumia ni kitu gani unakijali sana? Kitu gani kinakupatia furaha wewe? Kwa kulifahamu hilo utaweza kudhibiti matumizi yako na huku ukiwa na maisha bora. Mwandishi anaitumia kauli inayopendwa sana kutumiwa na watu kwamba fedha haiwezi kununua furaha, kauli hii inatokana na watu kuahirisha maisha, wakiamini siku wakishakuwa na fedha basi ndio watakuwa na furaha,kitu ambacho hakiwezi kutokea. Mwandishi anataka tufahamu kitu kimoja kwamba fedha na furaha ni maeneo mawili tofauti kwenye maisha na yanaweza yasiwe na uhusiano wa utegemezi. Kitu muhimu kufahamu ni wewe kuwa na furaha kabla hata ya kuwa na fedha.
Tatizo la wengi wetu hatujuwi tunataka nini na kipi tunajali zaidi, tumekuwa tunaishi kwa matamanio na kujilinganisha na wengine pasipo kufahamu ni kipi hasa unachojali?na hili limekuwa linafanya tuishi kwa kutamani Kila kitu kwasababu tumeona wengine wanavyo, hapa mwandishi anatutaka tujifamu na kujitambuwa ni kipi tunataka kwenye maisha yetu na kuhakikisha kwa namna yoyote tunakipata. Na yale yote yasiyo na maana kwako unaachana nayo na hapo utakuwa na maisha ya furaha. Wakati nasoma hapa nikakumbuka maisha ya mama Theresa kwake umaana ulikuwa kusaidia wengine na alipomsaidia mtu aliona amepata furaha kubwa sana, upande wa Donald Trump yeye kwake furaha ilitokana na kumiliki majengo makubwa na kuyaandika jina lake Donald Trump na furaha huzidi pale jengo hilo linapokuwa refu kuliko majengo yote, kupitia watu hawa wawili tunajifunza kwamba pale unapofahamu nini hasa hitaji lako basi hakikisha unalipata, lakini hili halina maana kuweka hitaji lako kwa kile kilicho nje ya uwezo wako, huwezi kuwa huna mkono halafu ukataka muujiza utokee upate mkono ndio ufurahie, hivyo jiulize sasa hitaji lako ni nini? Mimi ninajisikia furaha kuzungukwa na watu wenye furaha na ndio maana Kila siku najitahidi wewe mtu wangu upate mafunzo yaliyo sahihi Je wewe ni kipi chenye maana na kukijali zaidi kwako?
Moja ya matajiri sana ambao wanasemekana ni bahili ni Bilionea Warren Buffet,ambaye wakati kitabu hiki kinaandikwa alikuwa tajiri namba mbili duniani na sasa ni namba tatu kama sijakosea, wakati kitabu hiki kinatolewa Julai 2019 tajiri huyu alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani 77(kwa report za mwaka 2017) Sawa na zaidi ya Tsh trilioni zaidi ya 150,karibu Mara kumi ya bajeti ya nchi yetu ya Tanzania. Pamoja na utajiri wake huo bado anaishi kwenye nyumba yake aliyonunua mwaka 1958 huko Omaha, Nebraska nchini Marekani. Amekaa kwenye nyumba moja kwa zaidi ya miaka 62 sasa.Alipoulizwa kwanini pamoja na utajiri wake bado anaishi maisha ya kawaida? Akajibu mafanikio kwake ni kufanya kile kitu anachopenda na kwake ni kuwekeza.Hivyo hicho ndio kitu anafanya na vingine vyote havina nafasi, ingekuwa huku kwetu wangesema ni masharti ya mganga na Kila maneno.
Rafiki bilashaka unahitaji maisha yenye furaha, anza sasa kufahamu hitaji lako na pambana mpaka uweze kulipata na acha kukimbizana na Kila kitu.
Nikutakie siku njema, makala hii imeandikwa na Mimi rafiki yako Mwl.Kelvin Kinyaga; ninayo kushirikisha ni baadhi tu, mengi mazuri zaidi yapo kwenye kitabu hiki, tuwasiliane upate nakala yako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Umuhimu wa taswira katika kufikia utajiri....
Rafiki yangu hongera kwa siku nyingine tena, Nina imani u mzima wa afya na tunaendelea vyema kusukuma gurudumu la maendeleo, lengo ni kuendelea kuifanya kazi ya kuifanya dunia kuwa na mazingira bora kuishi kwetu na kwa wengine....
LeoLeo kutoka kitabu cha THINK AND GROW RICH tutajifunza hatua nyingine muhimu katika kutengeneza utajiri, Hatua muhimu kuifahamu katika kutengeneza utajiri ni kutengeneza taswira.
Mambo yote tunayoyafurahia sasa miaka ya hapo nyuma havikuwepo, kupitia watu ambao leo tunawaita wagunduzi ndio vimeweza kuwepo na kutunufaisha, mwandishi wa kitabu hiki anatuambia kwamba zipo aina mbili za taswira.
*1.Taswira awali*
Taswira awali inajengwa kwa kutumia mawazo na mipango ambayo tayari ipo, hapa mtu unatengeneza taswira kwa kuoanisha mawazo au mipango mbalimbali na kupata wazo moja ambalo unalifanyia kazi, watu wengi tunatumia taswira awali kuweza kuboresha maisha yetu.
*2.Taswira bunifu*
Hapa unajenga taswira baada ya kupata wazo jipya na kulitumia kupata kitu kipya ambacho hakijawahi kufanyika, hapa ndipo pamewawezesha wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa duniani kubaki na heshima muda wote, jiulize mtu aliyeweza kututengenezea simu ambayo Mimi na wewe leo tunatumia, jiulize mtu aliyetengeneza usafiri, yote hayo yalikuwa kama picha(taswira)kwenye akili yake ya ndani na Leo hii tunafurahia maisha mazuri kupitia matokeo ya taswira.
Sayansi inatuambia vitu vyote vimeundwa kutokana na maada na nguvu. Hivyo kama utaitumia nguvu ya taswira basi unaweza kufanya chochote unachotaka kitokee, utajiri pia ni matokeo ya taswira hivyo ukitumia nguvu ya taswira na kuhamisha taswira hiyo kwenye uhalisia na mambo yanatokea, watu wengi wanayao taswira lakini Kila wanapojaribu kuitengeneza lakini baadaye huzipuuza na kuendelea kuishi maisha ya mazoea. Asante rafiki na uwe na siku njema.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga;
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin162.blogspot.com
0763766944/0712161251
Monday, 13 July 2020
Tiba ya nne kwa mifuko iliyo sinyaa.....
Tumshukuru mungu wetu Kila tunapopata bahati kuianza siku tukiwa na afya tele, nikushukuru wewe rafiki yangu unayeanza kuona umuhimu wa kusoma makala hizi, hiyo ni hatua ya kwanza, nikupongeze wewe unayechukuwa hatua Mara moja na kufanyia kazi masomo haya, siwezi kuwa mjinga kukupatia masomo haya ikiwa sina uhakika kwamba yatakusaidia, karibu tuwe sote....
Leo kutoka kwenye chambuzi za kitabu chetu pendwa cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tutaendelea kuangalia tiba kwa mifuko iliyosinyaa, kati ya tiba saba tutakazo jifunza tatu tumeshazichambuwa, tumeshafahamu kutenga asilimia kumi ya Kila kipato chako na kujilipa wewe kwanza, tumeshafahamu umuhimu wa kudhibiti matumizi yako,tukaona namna ya kufanya akiba yako izae zaidi na sasa tunakwenda kuangalia tiba ya nne LINDA HAZINA YAKO ISIPOTEE.
Utakapoanza kufanikiwa basi ndio unapaswa kuwa makini zaidi, kwani wengi ndipo huanza kuona kama changamoto nyingi zinajitokeza lakini ukiangalia kwa makini changamoto hizo zinasababishwa na mafanikio kidogo uliyopata. Na Arkadi alianza somo la nne kwa kuwaeleza kama hutolinda fedha zako basi zitapotea.
Sehemu kubwa inayowaangusha wengi ni pale wanapoanza kuona mafanikio ndipo Kila mtu kuwafuata na kuwapa ushauri wa wapi awekeze kutamlipa, na Mara nyingi humshauri kuwekeza ili apate faida ya haraka.Mwandishi anasema kama hutofikiri kwa makini utapoteza fedha zako.
Arkadi aliwauliza, Je ni vizuri kushawishika na faida kubwa wakati mtaji wote unaweza kupotea? Nadhani jibu ni hapana. Msingi wa kwanza wa uwekezaji ni usalama wa mtaji wako unaowekeza. Utapaswa kuweka umakini mkubwa na kuchunguza sehemu unayotaka kuwekeza fedha zako. Acha kutamanishwa na kupata faida kubwa kwa haraka.
Arkadi akitoa somo hili aliwakumbusha uwekezaji wake wa kwanza alivyopoteza kwa kutoweka umakini sehemu anayowekeza na akapata hasara hivyo aliwaeleza kwamba wasifanye makosa aliyofanya yeye.
Omba ushauri kwa wazoefu wa fedha na Fanya busara ndio ikuongoze katika uwekezaji, Kocha wetu huwa anapenda kutushauri kwamba kabla hujapokea ushauri wa mtu jiulize hiki anachonishauri kimemsaidiaje yeye kufika hapo alipo? Au amejifunza kwenye kitabu gani ili na Mimi nijifunze niweze kufanikiwa kwenye hili? Ukishapata majibu ndipo fanyia kazi ushauri huo.
Rafiki huwa tunapenda kupokea ushauri kwa Kila mtu, hasa watu tunao waheshimu, hata kama wamefanikiwa kifedha, swali la kujiuliza ni je hiki anachonishauri ndicho ambacho yeye kafanya na kufanikiwa? Au ndio ushauri wa madini kutoka kwa mfyatua matofari?
Nina imani unakwenda kufanyia kazi masomo haya, asante na uwe na siku njema rafiki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Comments (Atom)