Saturday, 24 October 2020

Leo Nitakujibu Ni Swali Lako La Biashara Gani Ufanye Ili Uweze Kufanikiwa Haraka

Hongera sana rafiki yangu kwa kuweza kuifikia siku hii ya mwisho wa juma, siku ambayo nimekuwa nakusisitiza itumia kujitathimini na kujipa majibu sahihi, wapi umetoka, uko wapi? na wapi unataka kufika....... Rafiki yangu karibu tuendelee na somo letu kuhusu biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kilichoandikwa na kocha Dr Makirita Amani. Je ni biashara gani naweza kuanza kufanya na ikaniletea faida bila kuumiza kichwa? Hili ni moja ya swali ambalo wengi hupenda kuliuliza sana na pengine hata wewe msomaji wangu umekuwa ukijiuliza sana na watu wamekupa majibu mengi na bado hujaridhika nayo, pengine hawakukupa jibu la moja kwa moja ambalo mimi nakwenda kukupa. HAKUNA BIASHARA MOJA AMBAYO KILA MTU AKIIFANYA ATAFANIKIWA SANA, HAIPO. swali hili limekuwa kikwazo kwa wengi kuingia kwenye biashara na siku zote uanza biashara fulani na wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo wanaacha na kuanza biashara nyingine na huo ndio unakuwa utaratibu wao na kujikuta hawafiki popote. Kila mtu kuna biashara ambayo kwake yeye anaweza kuifanya vizuri na kufanikiwa. Hivyo swali muhimu ni biashara gani itakufaa wewe au mimi kuanza nayo?. Hapa utaangalia vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na unavipendelea kufanya, ujuzi wako au uzoefu ambao tayari unao. Mazingira yanayokuzunguka na watu wanapitia changamoto zipi?. Nenda kayafanyie kazi haya rafiki yangu na uwe na siku njema. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment