Thursday, 22 October 2020

Kuanza Biashara Ukiwa Chini Kabisa.

Rafiki yangu hongera kwa kuendelea kujifunza pamoja na mimi kupitia mfululizo wa makala zangu, ni hitaji la kila aliye hai kujifunza kila siku namna ya kuishi vizuri na kufurahia maisha. Vyote vinavyokuletea msongo wa mawazo na kukuhuzunisha ni matokeo ya mtazamo tu mbovu ulio nao, karibu tuwe sote..... Leo tunaendelea na somo letu kuhusu umuhimu wa biashara kwenye kuongeza kipato na yote tunayapata kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na mwandishi wetu mbobevu Dr. Amani Makirita. _Kuanza biashara ukiwa chini kabisa_ Mwandishi wa kitabu ameanza kwa msisitizo kwamba, njia nzuri ya kuanza biashara, ni kuanzia chini kabisa. Hata kama unaweza kupata mtaji mkubwa, kupitia akiba zako mwenyewe au kuwa na uwezo wa kukopa. Siyo vyema kuanzia biashara juu, kama hujawahi kuwa kwenye biashara kabisa. Yapo mambo mengi sana unapaswa kujifunza Kwa matendo. Hata kama utakua umesoma vitabu, umehudhuria kozi nyingi, bado yapo mambo utajifunza pale unapoingia kwenye biashara. Unapoanza biashara kuna makosa mengi sana madogo madogo utayafanya hivyo kwa sababu umeanzia chini hupati hasara kubwa yenye kukuondoa kwenye biashara yako. Kwa mfano kwenye kuajiri utapata watu wasio waaminifu na kuipa biashara yako uzito kama unavyoipa wewe na kukusababishia hasara, hivyo utajifunza hayo bila kupata hasara kubwa. Hivyo rafiki yangu acha kufikiria ni pale utakapopata mamilioni ndio uingie kwenye biashara, kwani kwa kufanya hivyo utapata hasara kubwa na utakata tamaa kabisa ya kujirekebisha na kuanza upya. Nakutakia siku njema rafiki yangu, nenda kaanze na kidogo na kikuze taratibu huku ukifanyia kazi kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye biashara yako. Makala hii imeandikwa na mimi rafiki yako Mwl Kelvin Kinyaga Asante sana na mwenyezi Mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment