Wednesday, 21 October 2020
KWA NINI KILA MTU ANAPASWA KUWA NA BIASHARA.
Rafiki kitu unachopaswa kukifahamu kwenye maisha ni kwamba hakuna kusimama, Kuna kwenda mbele au kurudi nyuma, kama ulichofanya Jana ndio unakwenda kufanya leo Kwa namna Ile Ile basi hapo umerudi nyuma, nenda kafanye zaidi ya Jana na utapata matokeo tofauti na uliyopata Jana.....
Leo tuendelee na somo letu kuhusu fedha na kwanini kila mtu anapaswa kuwa na biashara.
Kwanza ni ukweli usiopingika kwamba biashara ndiyo njia ya kuweza kuongeza kipato, ambayo haina kikomo. Hakuna mtu wa kukuzuia wewe kwenye Idadi ya biashara unazoweza kufungua, Pia hakuna atakayekupangia kikomo cha kipato chako unachotengeneza kupitia biashara.
Biashara ndio njia kubwa ya kuleta manufaa Kwa jamii zetu, taifa na hata dunia Kwa ujumla. Ni kupitia biashara ndio watu hutatuliwa matatizo yao makubwa. Pia biashara ndio sekta inayotoa ajira Kwa watu wengi zaidi. Na biashara ndio sehemu nzuri Sana ya kujifunza maisha. Mwandishi anasema biashara ndio chuo kikuu cha maisha, ni kweli kwani biashara haina maigizo yoyote, ukifanya kosa dogo adhabu yake ni hapo hapo.
Biashara itakufundisha kutoa thamani,kushindwa, kukataliwa, kukabiliana na changamoto, kupambana, uvumilivu na mengine mengi.Hivyo Mwandishi anasisitiza Kwa kila mtu anayetaka kujifunza maisha na kuyaelewa Kwa vitendo anapaswa kuingia kwenye biashara, kwani hakuna kitu ambacho biashara haitakufundisha.
Mwandishi anahitimisha sehemu hii Kwa kusema kila mtu anapaswa kuingia kwenye biashara kama moja ya kuongeza mifereji ya kipato. Hata kama unazo njia nyingine za kuongeza kipato kuwa na biashara kunaongeza mfereji mwingine. Watu wengi hupenda kupata njia za uhakika kama ajira ili kuingiza kipato lakini moja ya sheria za dunia ni kwamba hakuna jambo lolote ambalo ni uhakika wa asilimia 100. Wengi hujifunza hilo Kwa njia ngumu, pale kile walichokiwekea uhakika kinapowaangusha. Hivyo unapokuwa na biashara, tena zaidi ya moja, unazidi kupunguza hatari yako ya kutegemea sehemu moja au chache kwenye kutengeneza kipato chako.
Nenda kafanyie kazi haya uliyojifunza na anzisha biashara hata kama utaingiza mia mbili Kwa siku na Anza kuikuza polepole.
Uwe na siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki Sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment