Wednesday, 7 October 2020

Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli sehemu ya pili....

Habari za wakati huu rafiki yangu, ikiwa ni siku nyingine tulivu na nzuri tumshukuru mungu wetu Kwa zawadi ya uhai, twende tukaitumie zawadi hii Kwa kuyatenda yampendezayo karibu..... Bilashaka Jana umejifunza kitu kwenye sehemu ya kwanza ya mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli na leo tutamalizia sehemu ya pili. Debasir aliendelea kuelezea maisha yake ya awali na watu waliendelea kuongezeka kumsikiliza, Debasir anasema baada ya kukimbia wadeni wake ilibidi auzwe kama mtumwa Kwa Tajiri mmoja na alikua akifanya kazi ya kuhudumia ngamia, pamoja na kwamba alifanya kazi hiyo kama mtumwa hakukubaliana na hali ya kwamba yeye ni mtumwa na pale mke wa Tajiri aliyemnunua alipotaka kufahamu kwanini Debasir hakukubaliana na hali ya utumwa ndipo Debasir anaelezea maisha yake ya awali, familia yenye uwezo na amemkimbia mke wake na ndugu zake Kwa sababu ya madeni hivyo hataki kukubali kwamba utumwa ndio mwisho wake, Nira anamuuliza kama anajiona ana roho ya utumwa au mtu huru? Debasir anajibu anajiona ni mtu huru, Nira mke wa tajiri anamwambia kama unaroho ya mtu huru tuthibitishie hilo nenda na uwakabili wadeni wako ili uwe huru. Siku moja Nira yule mke wa Tajiri alimwambia Debasir aandae ngamia kwani anataka kwenda kumtembelea mama yake, Debasir anaandaa ngamia na wanakwenda na ngamia wawili na wanapofika Kwa mama yake Nira anafukuza watumwa wengine na anampa nafasi Debasir ya kutoroka na ngamia wawili ili arudi akawakabili wadeni wake na awe huru Tena, Debasir anamshukuru Nira na anaanza safari na ngamia wawili huku Nira akijitetea Kwa mume wake kwamba Debasir ametoroka na ngamia wale. Safari ya kurudi nyumbani inakua safari ngumu na ya mateso kwani hakuifahamu njia vizuri na alipita kwenye jangwa na kiu ya maji pamoja na njaa vilimtesa Sana na baadae alianza kuona hakuna dalili ya kuishi kwani kifo kipo karibu. Lakini alipokumbuka swali kutoka Kwa Nira kama yeye ni mtu huru au mtumwa alijihisi kupata nguvu upya ya kusonga mbele kwani akifa atakufa kama mtumwa, baada ya siku kadhaa alifika sehemu yenye maji na matunda na hapo ndipo akaona ana uhakika wa kufika nyumbani. Ndipo anamgeukia Tarkadi mdeni wake na kumwambia je Kwa njaa hii uliyo nayo leo upo tayari kuwafuata wadeni wako wote na kulipa madeni yako ili uwe huru tena au utaendelea kukimbia?Tarkadi akasema simulizi hii imenipa mwanga na Sasa naona dunia Kwa uhalisia wake nitayakabili madeni yangu niwe huru tena. Mtu mmoja Kati ya waliokuwa wakimsikiliza Debasir walitaka kufahamu alipofika babeli nyumbani alifanikiwa kulipa madeni yake yote? Ndipo Debasir akasema aligundua walio mkopesha ni marafiki zake adui yake mkubwa ni madeni, hivyo aliwatafuta wadeni wake na kuwaeleza nia ya kuwalipa aliyonayo, wengi walifurahi lakini wengine walitaka kumpiga Kwa sababu walikasirika Sana. Debasir anasema Kati ya wanao mdai walipomuona ana nia ya kulipa madeni, mtu mmoja alimuunganisha na wafanyabiashara wa ngamia kwani walifahamu anao uzoefu kwenye ngamia na alifanikiwa kulipa madeni yote na Sasa ndio huyu mfanyabiashara mkubwa wa ngamia babeli. Rafiki kisa hiki kina mafunzo mengi Sana, wapo watu kila siku wanakimbia huku na huko ili kuwakwepa wanao wadai Kwa kuona ni maadui zao, kumbe maadui zao ni tibia zao za kukopa na madeni ndio maadui zao wakubwa ambao wapo nao na wanaenda nao kila sehemu hivyo kama unataka kuwa huru wakabili wadeni wako na walipe Kisha hali mikosi na bahati mbaya hazitaendelea kukuandama. Debasir alikataa hali ya utumwa na akajitenga nao hata wewe kataa utumwa wa madeni, tafuta uhuru wako leo. Asante Sana rafiki yangu, nimeona nikuletee somo hili leo badala ya wiki inayofuata kwani wengi wameona wiki ijayo ni mbali, nikutakie siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment