Tuesday, 6 October 2020
Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli (The Camel trader of Babylon)
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na unaendelea salama na ratiba zako za kila siku, umejipangaje kua bora zaidi ya Jana, kufanya yaliyosahihi na kuachana na yale yasiyo na tija kwenye siku hii unayo iendea?....
Rafiki yangu karibu tuchambue kitabu pamoja, leo tutajifunza kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kupitia mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli, ni somo zuri Sana ambalo wakati nikipasoma sitamani kuweka kitabu chini bali kuendelea kusoma, karibu tuwe sote mpaka mwisho wa makala hii.
Tarkad mtoto wa Azure alikua akipita mtaaini akiangaza macho karibu na sehemu wanazouza chakula pengine angeweza kukutana na mtu ambaye anamfahamu ili amkopeshe fedha na kumnunulia chakula, anasema akili hufikiria Sana harufu ya chakula wakati una njaa kali.
Wakati anaendelea kuangaza hapa na pale ndipo anakutana na mtu ambae hakutaka kukutana naye, mtu huyo si mwingine bali Debasir mfanyabiashara wa ngamia aliyemkopesha fedha na kutomlipa kama walivyokubaliana Debasir anafurahi kukutana na mdeni wake na anapohitaji kulipwa deni lake Tarkad anajieleza kwamba hana pesa na amekua na bahati mbaya.Hilo linamshangaza Debasir kwamba watu wote wenye bahati mbaya ni wale wanaofikiria kukopa kuliko kulipa madeni yao.
Basi Debasir anamwambia Tarkad amfate na atampa hadithi moja itakayomfundisha. Na wanakwenda kukaa ndani ya sehemu inayouza chakula na Debasir anaagiza mguu wa mbuzi na mkate pamoja na mboga mboga na Juice Kwa sababu alikua na njaa Sana, Lakini anamwambia muhudumu asimsahau na rafiki yake Tarkad Kwa kumletea maji ya kunywa ya baridi kwani joto lilikua kali Sana, Tarkad alisikitika Sana kwani pamoja na njaa ya siku mbili anakweda kukaa akiangalia mtu akila mguu wa mbuzi huku yeye akiendelea kumkodolea macho, Kwa kua alidaiwa na amepewa ahadi ya kupewa hadithi itakayokwenda kumfundisha na kumuondoa kwenye utumwa wa madeni ilibidi akae na kusikiliza.
Debasir alianza kuelezea maisha yake ya huko nyuma ya kuishi Kwa kukopa na kujificha akikimbia wale waliomkopesha mpaka kuuzwa kama mtumwa lakini baadae anafanikiwa na kuwa mfanyabiashara mkubwa wa ngamia wa Babeli.
Nini kilitokea, tusubirie sehemu ya pili ya simulizi hii tutaona nini Debasir alifanya mpaka kuushinda umasikini na Kuja kua mfanyabiashara mkubwa.
Ondoka na somo hili kwamba bahati mbaya huwaendea wale wote ambao wanafurahia mkopo na kuchukizwa kulipa deni hilo, Lakini pia huangalia ni wapi kwingine ataweza kukopeshwa.
Ninakupenda Sana rafiki yangu, nikutakie siku Njema na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment