Thursday, 15 October 2020

Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 3

Rafiki yangu hongera Kwa kuweza kuifikia siku ya leo, nina amini changamoto unazozipitia ni daraja la kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine bora zaidi, usirudi nyuma songa mbele...... Leo tunaangalia sehemu ya tatu ya mtu huyu mwenye bahati kuliko wote babeli karibu tujifunze pamoja. Rafiki yangu nina hakika tumekua pamoja tangu mwanzo mwa simulizi hii na umeweza kuona ni namna gani bidii inavyoweza kukufungulia njia za mafanikio. Bidii ya kazi Kwa Sharru Nada inamvutia babu yake na kijana ambaye sharru anamuelezea alikua mshirika mwenzie kwenye biashara na hapo anataka kufahamu ni kipi kinamsukuma kijana huyu kufanya kazi Kwa bidii? Rafiki wengi wetu makazini tunafanya kazi Kwa bidii tukitegemea kuongezeka Kwa mshahara au kufanya vyeo na ndio maana kila siku tumekua tukilalamikia waajiri, Kwa sharru Nada kazi ilimfanya atengeneze mahusiano mazuri na bwana wake na wateja wake huku akijiandaa na kununua uhuru wake. Baada ya kumueleza babu yake na kijana huyo Nia yake mzee alimwambia kwamba hata yeye kazi anayofanya ya kutembeza vitu nyumba Kwa nyumba ni ushirika na bwana wake kwani na yeye alikua mtumwa kama yeye. Kijana aliposikia babu yake alikua mtumwa alikataa kwani anafahamu babu yake alikuwa mtu mwenye fedha nyingi Sana, Lakini hakufahamu alizipataje. Wapo wengi Sana ambao ni matajiri tunawafahamu lakini kama tungefahamu ni namna gani walianza pengine tungewapa heshima zao. Kadri siku zilivyoenda ndivyo mfuko wa sharru ulivyotuna, Kwa kila kiasi cha fedha alichopata aliweka na hata bosi wake alimtegemea Sana, kwani kila sharru alipopata na yeye alipata zaidi, Lakini pesa alizopata huyo bosi wake ziliishia kwenye kamali. Siku moja sharru akiendelea kukanda unga wake Kwa maandalizi ya bidhaa zake alikuja bwana mwingine na kumwambia Sharru kwamba huyo bwana wake ameshindwa kulipa deni lake hivyo inabidi achukuliwe yeye kama fidia. Sharru ni mtumwa hana namna ya kukataa hivyo anakusanya fedha zake na kuambatana na bosi mpya, Kwa bahati mbaya Kwa bosi wake mpya maisha yanakua magumu zaidi, kazi zinakua ngumu na zisizo na maslahi yoyote,Sharru anaanza kukata tamaa ya maisha. Lakini siku moja wanakuja watu kumchukua Kwa kumnunua kama mtumwa na anafukua fuko lake la fedha na kuambatana na watu wale, anafika sehemu aliyonunuliwa anakuta aliyemnunua ni yule rafiki yake, ambaye ni babu wa kijana yule, anafurahi na kujiona ni mtu mwenye bahati kubwa Sana. Anamwambia alimtafuta bila mafanikio na aliposikia aliuzwa kama mtumwa alimfuatilia na kuamua kumnunua, hapo ndipo mwanzo wa ushirika kibiashara ulipoanzia Kati yake na babu yake. Alipofika hapo kijana alifahamu kwamba watu hawazaliwi na kua matajiri bali ni Kwa kuweka kazi, alifurahi kufahamu kisa cha utajiri wa babu yake na kimemfungua kwamba kazi siyo Kwa watumwa pekee bali kiungo cha kununua uhuru wako. Rafiki kazi uliyonayo Sasa ni utumwa wako, pamoja na kwamba inakusaidia lakini siku yoyote bwana wako akishindwa kulipa madeni au sababu nyingine utaondolewa kwenye kazi hiyo na maisha yatakua magumu Sana. Anza leo maandalizi ya kununua uhuru wako Kwa kujifunza biashara, wafundishe watoto zako kutengeneza pesa kuliko kuajiriwa, ukifa leo wanao hawatakula mshahara wako, ila wanaweza simamia biashara ulizozianzisha na ikawa ukombozi kwao. Mwisho wa simulizi ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, bilashaka umeondoka na vitu vya kufanyia kazi. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment