Tuesday, 20 October 2020

MLANGO WA NDOTO

Ni kweli zipo changamoto nyingi ambazo unazipitia, je wafikiri hayo unayopitia ni mikosi? Unafikiri ni wewe peke yako unayapitia? Wacha kusikitika mshukuru mungu bado unayo nafasi ya kuyakabili yote na kusonga mbele. Karibu rafiki yangu tuendelee kujifunza pamoja. Leo tunaangalia umuhimu wa Ndoto kwenye maisha yetu, tunaangalia ndoto kama lango.Binafsi kabla ya kusoma kitabu hiki sikua na elewa chochote kuhusu ndoto na ni moja ya sehemu ambayo sikuwahi kuipatia umuhimu wowote. Kabla hatujajadili mlango huu wa ulimwengu wa kiroho ni vema tuangalie ni nini maana ya ndoto. Ukiangalia kamusi ya kiingereza inatuambia:Ndoto ni mtiririko wa mawazo, picha na mhemuko unaotokea kwenye fikra za mtu akiwa usingizini. Kwenye tovuti ya Wikipedia ;wao wanasema ndoto ni mrejesho wa sura, mashauri, hisia na msisimko ambavyo hutokea bila utawala wa akili wakati wa usiku kwenye vipindi mbalimbali vya usingizi. Wanasayansi wanasema ndoto ni picha za fikra kwenye utu wa ndani zilizobeba sauti, sura na mhemuko wakati tumelala. Tunaambiwa Kwa kawaida mtu mwenye Afya anaota mara 3 mpaka 7 Kwa usiku mmoja. Kwenye Biblia ndoto zimetajwa mara 21 kutoka Kwa mfalme Yakobo. Kitabu cha mwanzo pekee ndoto zimeandikwa mara 33.Kitabu cha Nabii Daniel zimeandikwa mara 27.Agano jipya kama mara 8 pekee. Kwa hali hii, ni vema tuone kuwa ndoto Zina umuhimu wake mkubwa kwenye maisha ya mtu. Mungu aliongea na wanadamu Kwa njia ya ndoto, ukisoma kitabu cha mwanzo kwenye sura 41,Kwenye ndoto maarufu aliyoiota mfalme Farao ikitafsiriwa na Yusufu mwana wa Israel;utaona mungu akitumia ndoto kuongea na binadamu. Ipo tofauti Kati ya Maono na ndoto. Maono hutokea wakati mtu hajalala na ndoto hutokea wakati mtu amelala. Tunapokuwa tumelala, miili yetu ndio imelala lakini roho zetu hazilali. Hivyo Kuna mambo mengi Sana ya kiroho utendeka tukiwa tumelala. Rafiki kama unahitaji kuelewa Kwa undani zaidi somo hili basi wasiliana moja Kwa moja na Mwandishi wa kitabu hiki mchungaji na Mwalimu Josephat Ulomi Kwa number 0763816739 Nenda ukasamehe wote waliokukosea, anza kupenda kujifunza na kuongeza ufahamu, anza kuamini kama ulikuwa huamini kwamba Yesu Kristo ni Lango hapa duniani kama ni mlengwa wa kristo, Anza kuheshimu ndoto Zina mengi ya kukufundisha na hapo utaanza kuona njia zako zinafunguka na unabarikiwa. Asante Sana rafiki yangu nakutakia siku Njema na Mungu akubariki Sana Sana. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment