Wednesday, 14 October 2020

Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 2

Habari za wakati huu rafiki yangu, ni Ile Ile bahati ya kuweza kuifikia leo inaendelea kwetu, ni mimi na wewe wa kuchagua ni namna gani tunakwenda kuitumia, kulalamika, kubishania siasa na mpira au kuweka kazi na kuhakikisha maisha yetu yanakua bora zaidi..... Sehemu ya pili ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, Tutaendelea na simulizi yetu, na Tutaendelea pale ambapo Hidan anataka kufahamu ni vipi Sharru Nada aliweza kutengeneza utajiri? Sharru Nada anaendelea na simulizi yake kwamba yeye na babu yake huyo kijana walianza kama watumwa. Yeye alichukuliwa baada ya Kaka yake kuuwa mtu, na mke wa yule mtu aliyeuwawa alimchukua Sharru kama fidia ya kifo cha mumewe. Baadae mama yule aliamua kumuuza Sharru kama mtumwa, wakiwa njiani kwenda kuuzwa walisikia watu wakieleza namna watumwa babeli walivyofanyishwa kazi mpaka kufa. Hili lilimwogopesha Sana Sharru. Lakini mtu mmoja alimwambia Sharru akifika babeli na mtu yeyote atakayejitokeza kununua mtumwa basi ajitokeze na kueleza kwamba yeye anapenda Sana kazi ili anunuliwe na kama asipopata mtu atapelekwa kujenga ukuta wa babeli na huko kulikuwa na kazi ngumu na mateso ya kila aina Kwa watumwa. Magodi alimwambia Sharru kama ukinunuliwa nenda kaipende Sana kazi yako na ifanye Kwa bidii zote na kama mtu huyo hatoithamini kazi hiyo wewe ithamini, usiangalie kile unachozalisha kinakunufaishaje bali ona kitu hicho kinavyowanufaisha wengine. Walipofika babeli Sharru alihakikisha anapata mtu atakayemnunua na kufanya kama alivyoshauriwa na Maggido. Kweli wanafika Babeli na Sharru anapata mtu wa kumnunua na hapo Sharru anajiona ni mtu mwenye bahati Sana Kwa kuweza kununuliwa kama mtumwa. Basi Sharru alipofika Kwa bwana wake huyo aliyemnunua anapangiwa kazi ya kuwasha moto, kukanda unga na kufanya maandalizi mengine ili mikate na keki viandaliwe kwani bwana yule alifanya biashara ya kuuza keki na mikate. Sharru aliweka bidii kubwa Sana na kuhakikisha siyo kwamba anashiriki kwenye maandalizi tu ya kutengeneza keki na mikate bali anafahamu mpaka zinavyotengenezwa, bwana yule alipendezwa Sana na bidii za Sharru kwenye kazi. Siku moja Sharru ndipo alipopata wazo la kuhakikisha anaanza kutengeneza kipato ili aweze kununua uhuru wake na anapata wazo la kutumia Muda wa jioni wa mapumziko kufanya kazi ili apate fedha, anamfata bwana wake na kumueleza wazo hilo, kwamba angetengeneza keki zaidi na jioni kuuza na wangegawana fedha, bwana wake anakubali na Sharru anaanza zoezi hilo mara moja. Mwanzo hali inakuwa ngumu kupata wateja lakini baadae mambo yanaanza kuwa mazuri na kwenye kuuza keki anakuja kukutana na babu yake na Hadan, ilikuwaje na nini kilitokea usikose sehemu inayofuata ili ufahamu Sharru alinunuaje uhuru wake? Rafiki labda Kuna kitu umeanza kukiona kwenye simulizi hii, kwangu naona siku niliyopata ajira ni Sawa na siku Sharru aliyonunuliwa kama mtumwa, alifurahi na alikwenda kuifanya kazi yake Kwa mapenzi yote akifahamu kwamba yeye ni mtumwa, Vipi wewe unaipenda kazi unayofanya? Je unafahamu kwamba wewe ni mtumwa uliyenunuliwa na boss wako? Je mwisho wa utumwa huo ni lini? Kabla hatujaendelea na kisa hiki nenda kayatafakari maswali hayo na Anza mipango ya kununua uhuru wako. Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, tutaonana sehemu inayofuata. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment