Friday, 31 July 2020
*Ustawi wa fikra* Wednesday 30,July 2020. _Hivi ndivyo wajanja wanavyoishi baada ya ongezeko la kipato chao_ Habari za wakati huu rafiki yangu, hongera kwa siku nyingine na tuna Kila sababu ya kumshukuru mungu..... Leo kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA tutaangalia dhana ya vipi utaweza kuzuia matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka. Rafiki kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba tabia moja unayopaswa kuwa nayo itakayokufikisha kwenye utajiri ni kuhakikisha matumizi yako ni kidogo kuliko kipato chako, kama kiasi unachopata unakitumia chote sahau kuhusu mafanikio. Mwandishi wa kitabu anasema kitu ambacho anakishangaa kwenye fedha hasa kwa waajiriwa ni hiki, japokuwa watu wanatofautiana vipato na mishahara wanayolipwa lakini Kila inapokaribia mwisho wa mwezi aliyepokea milioni moja na aliyepokea laki moja wote wanakuwa wameishiwa na kinachosababisha hili ni watu kuongeza matumizi Kila fedha inapoongezeka na kusababisha wawe watumwa kwenye fedha maisha yao yote lakini wajanja kwenye fedha hawaishi hivyo. Mwandishi anatoa mfano,pale kipato chako kinapoongezeka, jipe muda kidogo wa kuendelea na maisha yale ya kipato cha chini,tumia ongezeko hilo la kipato kuzalisha kipato cha zaidi. Baada ya kipindi cha miezi sita tangu upate ongezeko la kipato ndipo unaweza kuongeza matumizi yako kufikia nusu ya ongezeko na nusu kuendelea kuzalisha. Rafiki uwe umeajiriwa au kujiajiri au biashara hakikisha unakuwa mjanja kwa kuhakikisha huongezi matumizi yako Mara tu baada ya kuongezeka kipato chako. Asante na Leo nimekupa ujanja huu, nenda kautumie,biashara yako haitakua kama hutumii ujanja huu. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0763766944/0712161251
Monday, 27 July 2020
Ustawi wa fikra Monday, 27 July 2020 *Na hivi ndivyo kodi ilivyoanza........* Habari za wakati huu rafiki, asubuhi ya wiki lingine na nina imani umejipanga kuiendea siku hii kwa kufanya zaidi ya pale ulipofanya kwenye wiki lililoisha, kwani kama utafanya vile vile na kutokwenda hatua ya zaidi usitegemee kupata matokeo ya tofauti na uliyopata wiki iliyopita. Leo rafiki tuangalie historia ya kodi, kama upo serikalini unakatwa kodi, kama una biashara zako unakatwa kodi, kama huna kazi maalumu bado utalipa Kodi wakati ukihitaji huduma, Je nini chanzo cha kodi? Kwanini unalipa kodi? Rich dad alikuwa akiendelea na darasa lake na Leo anatufundisha historia ya kodi, anasema wakati wapo shule kuna mwalimu aliwaelezea habari za Robin Hood,mtu ambaye mwalimu huyo alimuelezea Robin kuwa mtu shujaa aliyewaibia matajiri vitu na kuwapa masikini, rich dad anasema yeye kwa upande wake alimuona Robin kama kibaka tu kwa kitendo chake hicho, anasema ingawa sasa Robin hayupo lakini watu wenye mtazamo kama wa Robin wapo na wanapenda kuona matajiri wanastahili kulipa kodi kubwa lakini ni kinyume chake. Miaka ya 1799-1816 Uingereza walitoa pendekezo la wananchi wake kulipa kodi ili kuiwezesha nchi yao kushinda kwenye vita, Marekani nao kwenye miaka ya 1861-1865 walitumia mbinu hiyo ya uingereza kuweza kusaidia taifa lao kushinda vita, baadaye kwenye mwaka wa 1874 uingereza waliweka sheria ya ulipaji wa kodi kuwa ni sehemu ya waingereza matajiri, Marekani nao mwaka 1913 walipitisha sheria hiyo, mwanzo raia wa nchi hizi waliaminishwa kwamba kodi ni kwa watu matajiri pekee na wao halitawahusu lakini kadri serikali zilivyokuwa ndivyo kodi zilipanuliwa na kuwafikia mpaka watu wa chini na sasa hivi Tabaka la kati na masikini wanalipa kodi zaidi ya matajiri, kwani matajiri wamewazidi ujanja wasomi, kivipi? *The power of corporation* Ni kupitia nguvu ya mashirika na makampuni ndipo matajiri wameweza kuizidi serikali kwenye kulipa kodi, hivi unafahamu mtu anayemiliki kampuni analipa kodi ndogo kuliko mtu anayemiliki biashara binafsi? Je unafahamu Leo kama una kampuni ukiwa na madeni au kuhitajika kufilisiwa Mali zako binafsi haziguswi isipokuwa kampuni yako pekee? Na kampuni ni karatasi linalotambulika kisheria na kupitia makampuni ndipo serikali na wasomi wamezidiwa ujanja na matajiri. Robert anasema hulipa kodi zaidi kwa sababu wao wanachofahamu ni kuamka na kwenda kazini na kipato kinapoongezeka na kodi inaongezeka pia, Robert anasema poor dad alimshauri akiwa mkubwa ahakikishe anapata kazi kwenye shirika zuri na kisha apande kazi taratibu mpaka kufika ngazi za juu, alipomweleza swala hilo Rich dad akamwambia kwanini usubirie kupandishwa ngazi? Kwanini usitengeneze ngazi yako mwenyewe? Hapa ni Sawa na sasa kuweka bidii kazini ili upandishwe vyeo ni kwanini usijiajiri na kuwa na kampuni yako mwenyewe? Robert anatuambia akiwa bado kwenye ajira mwaka 1974 alifuata ushauri wa baba tajiri na kuanzisha kampuni yake ya kwanza.Kampuni ya kuuza na kupangisha nyumba, anasema mwanzo kodi zilikuwa kubwa zaidi lakini baadaye alianza kuona ushauri wa baba tajiri ukifanya kazi na ndipo kupitia faida kutoka kwenye kampuni yake hii aliweza kununua gari lake la kwanza la kutembelea. Rafiki unahitaji kufahamu hesabu za fedha, kufahamu fedha unayopata na kuitumia kama mbegu kwa kununua ASSET na kupitia hilo utaweza kuzalisha na kupata fedha zaidi, Pia unahitaji kufanya uwekezaji ili fedha ikufanyie kazi, Pia utahitaji kulifahamu soko vizuri ili uweze kuuza zaidi na mwisho utahitaji kufahamu sheria ili ujuwe ni vipi utaweza kupata unafuu kwenye kodi na maisha kwa ujumla ili uwe na maisha bora. Rafiki kwa Leo tuishie hapa, nikutakie siku njema; Makala hii imeandaliwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga,mwanafunzi wa jinsi fedha inaweza kunifanyia kazi kupitia kupitia chuo cha Kisima cha maarifa, tuko pamoja na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogsport.com 0712161251/0763766944
Sunday, 26 July 2020
Hivi ndivyo unavyoweza kunoa siraha yako....
Habari za wakati huu rafiki, hongera kwa jumapili nyingine, siku ambayo tunamalizia wiki iliyopita kwa kutathimini yale tuliyofanya na wapi tumefanya vizuri na yapi hatukufanya vizuri kwenye wiki lililopita ili wiki hii tuweke bidii na kuwa bora zaidi......
Leo tuangalie maneno ya mwana falsafa *EPICTETUS* akitaka tufahamu kipi tunaweza kufanya na tukawa bora zaidi.
_"Even if I lack the talent, I will not abondon the effort on that account...., we do not abondon any discipline for despair of over being the best in it."_
Kauli hii inatuaminisha kwamba vipo vitu vinavyoweza kuzidi vipaji na elimu,ukivitumiaukivitumia unaweza kufanya makubwa na hiyo ndio siraha inayoweza tumiwa na Kila mtu.
*Weka kazi*
Watu wanaweza kukuzidi Kila kitu lakini wasikuzidi kuweka kazi, hakikisha Kila siku unafanya zaidi ya Jana, mwanzo utaonekana kama umechanganyikiwa na matokeo hayataonekana lakini ukiweka kazi zaidi lazima utafikia ukuu na utawazidi walio kuzidi elimu, wenye vipaji vikubwa na utabobea zaidi yao kwenye hilo unalofanya, tafiti zote duniani zinaonyesha hivyo, angalia waliofanya makubwa wana elimu ya kawaida na hawana vipaji vya kutisha ila walihakikisha wanaweka kazi kweli kweli.
*Nidhamu*
Ukiwa na nidhamu kwenye kidogo unachofanya kwa kuhakikisha unakiheshimu lazima kitakupa zaidi ila usipoweka nidhamu na kudharau hutafika popote hata ungekuwa na kipaji kizuri namna gani, ukiona mtu anafika mbali ni kwasababu ameheshimu kile alichonacho, unapokuwa na kidogo ukakithamini na kuhakikisha unakuwa mtu wa kuthamini ulipo napo patakuonyesha njia ya juu zaidi, haijalisha unataka kufika wapi lazima uanze na hapo ulipo na kuweka nidhamu ya Hali ya juu.
Kwenye kisima cha maarifa msingi wetu Mkuu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na tunaishi kwa vitendo jambo hili,hatuangalii uko wapi lakini kwa kuweka kazi na kujituma huku nidhamu ikiwa juu ni hakika kile tunachokitafuta lazima upate kile unachokitaka, dunia haitakupa vitu kwa urahisi lazima ufuate kanuni za asili ndipo dunia ikupe zaidi, ardhi ukiipa mbegu inakupa zaidi, kadri unavyopaipa mbegu zaidi ndivyo inakupa mazao mengi zaidi, nidhamu ya palizi na kuondoa magugu ndivyo unavyopata mazao zaidi, uvivu ni magugu kwenye kazi,kiburi ni magugu,dharau ni magugu kwenye mafanikio.Ondokana na vitu hivyo na utakuwa vyovyote unavyotaka.
Asante na nikutakie siku njema katika kuliendea wiki linaloanza kesho, katumie haya tunayoambiwa na mwanafalsafa EPICTETUS na kisha utaona matokeo utakayopata.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Saturday, 25 July 2020
Maswali 12 ya kujiuliza kila siku na yatakwenda kubadilisha maisha yako......
Rafiki yangu kama unaishi na huna kipimo unachotumia kupima maisha yako kama unakua au hukui basi huna maisha,kwani maisha yasiyo pimwa hayafahi kuishi......
Kwanza kabisa nakusalimia rafiki wa ustawi wa fikra, ningekuwa nimeipoteza siku hii na kutoishi kama ingepita sijakuandikia, ninachokuandikia hapa ni kitu ambacho kimenitafakarisha sana leo, Kama ni msomaji wa falsafa na vitabu vingi huwezi niambia humfahamu RYAN HOLIDAY,Leo kupitia kurasa yake anatuletea Zawadi ya maswali kumi na mbili ambayo Kila binadamu anayetaka kufahamu kusudi la maisha yake anapaswa kujiuliza, karibu tuyasome pamoja, lengo ni kujipa majibu sahihi ya maswali haya, kaa chini na jipe majibu sahihi...
*1.Who do you spend time with?*
Hebu jiulize muda wako mwingi unatumia na nani? Goethe would say "Tell me who you spend time with and I Will tell you who you are".Msemo huu unatuambia kama ukitaka kumfahamu mtu alivyo basi angalia watu wanao mzunguka, rafiki yangu kama umezungukwa na watu walio kata tamaa basi tambuwa huwezi kuwa shujaa, kama muda mwingi unautumia na watu wanaolalamika basi huwezi acha kulalamika, kama wanaokuzunguka ni watu wa kushindwa basi na wewe utashindwa, hebu Leo amua kusikiliza na kujihusisha na washindi na kataa kabisa na watu wanao kuambia maisha ni magumu na hayawezekani, jiulize kama walio kuzunguka wanakuinua au kukushusha?
*2.Is this in my control?*
Jiulize kama unalohangaika nalo liko ndani ya uwezo wako au? Kutaka Kila mtu akupende ni jambo lililo nje ya uwezo wako, kumridhisha Kila mtu ni kupoteza muda wako, kufikiria wengine watanionaje nalo liko nje ya uwezo wako, kuishi kwa furaha ni jambo ambalo Kila binadamu ana uwezo nalo hivyo kabla hujakubali lolote likusumbuwe jiulize je lipo ndani ya uwezo Wangu? Acha kuangalia maoni ya wengine yanayokurudisha nyuma, we Fanya yako.
*3.What does your ideal day look like?*
Siku unayoishi Leo ndio itaamua kesho yako, acha kujidanganya kwamba miaka miwili, mitano au kumi nitakuwa nimefanya maendeleo makubwa wakati Leo yako hujuwi unakwenda kufanya nini? Ifahamu Leo yako na pambana nayo kwa Kila hali na Mali na hilo litaifanya kesho yako kuwa bora, hakika ni Leo yako na siyo kesho yako, kwani kesho yako itaamuliwa na Leo yako.
*4.To be or to do?*
Watu wengi tunaangalia matokeo ya nje kwa walio fanikiwa na kutamani kuwa kama wao, lakini mbaya zaidi hatupo tayari kuishi kwa vitendo yale wanayofanya, muda mwingi unatumia kujadili maisha ya wengine, kutizama tamthilia na kubishana siasa kisha kujiambia Kila siku unataka kuwa kama mtu fulani mwenye mafanikio, chaguwa kufanya na kuweka kazi na siyo kuendelea kuishi maisha ya kutamani bila ya kuweka kazi.
*5.If I am not for me,who is?If I am only for me,who am I?*
Rafiki siyo vibaya kufanya kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya familia yako na ndugu zako, lakini kama hicho ndio kitu pekee umekuja kufanya duniani basi maisha yako hayana maana yoyote, Kila unachojishughulisha nacho basi kifanye kwa ajili ya wengine na hapo utakuwa na maisha ya maana, ona una jukumu la kusaidia wengine na hapo utakuwa na maisha ya utoshelevu.
*6.What am I missing by choosing to worry or be afraid?*
Kila unapohisi hofu ikikujia jiulize ni kipi nimepanga kukikosa nikichaguwa hofu initawale? Gavin de Beycer writes "when you worry ask your self "what am I choosing to not see right now? Kauli hii inatuambia kwa kuishi maisha ya kuhofu ni Sawa na kuamua kufumba macho tusione wakati macho yetu ni mazima, fursa nyingi sana zinatupita kwakuchaguwa maisha ya kujiambia nikifanya biashara nitapata hasara, nikiacha kazi nitaishije? Na wakati tumeipa hofu itutawale ndipo fursa nyingi zinatupita na kubaki na maisha yetu yasiyo na tija yoyote.
*7.Am I doing my Job?*
Kila unapofanya jambo lolote jiulize kama hiyo ndio kazi yako, unaposengenya wengine jiulize hii ndio kazi yangu?fahamu kazi yako unayopaswa kuifanya na hakikisha unaikamilisha ipasavyo, kazi yako siyo umbeya lakini ndio muda mwingi unatumia kufanya umbeya, kazi yako siyo mpira lakini muda mwingi unautumia kubishania mpira, wewe siyo mwanasiasa lakini muda mwingi unazungumzia siasa.
*8.What is the most important thing?*
Kama hufahamu kitu gani muhimu sana kwako basi utajikuta unaishi maisha ya wengine na kuachana na yako, lazima ujiulize ni kipi muhimu zaidi kwenye maisha yako na hakiisha unakifanya na kukifikia na achana na vingine visivyo muhimu.
*9.Who is this for?*
Swali unalopaswa kujiuliza ni kwanini unafanya unachofanya? Kwanini naandika? Kwanini nawauzia watu? kwanini najifunza Kila siku? Watu wengi wanafanya kwasababu wameona na wengine wanafanya lakini hawana sababu za muhimu kwanini wafanye na ndio maana wakipitia magumu kidogo wanaachana na wanachofanya na kuanza kingine. Kwanini nafundisha? Kwanini naimba?
*10.Does this actually matter?*
Kila baada ya muda jiulize kama hicho unachofanya ni sahihi? Unachowaza, unachoongea, unachowatendea wengine ni sahihi? Ndio kitu muhimu wewe kukifanya?
*11.Will this be alive time or dead time?*
Muda wa kujiambia nitafanya, nitaanza, nitahakikisha, nitafurahia,nitanunua na mengine mengi yanayofanana na hayo tunayaita maisha mfu, maisha yaliyokufa, muda hai ni muda wa kujifunza na kuweka kwenye matendo na siyo kujiambia nitaanza au nitafanya wakati mwingine.
*12.Is this who I want to be?*
Unapenda uwe mtu wa hekima lakini unakasirika muda wote, unapenda uwe mtu wa mungu lakini huna uadirifu, unataka kuwa mama/baba bora lakini unafanya kinyume, ukidanganya jiulize ni hivi ndivyo ninavyotaka kuwa? Mwandishi anasema huwezi kuwa mtu wa kazi wakati unapenda njia za mkato,"How we do anything is how we do everything"Kama siyo mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa, huwezi jiambia umedanganya kidogo ila kesho utakuwa mkweli, huwezi kuwa mvivu kwenye kazi ulio ajiriwa halafu ukawa na bidii kwenye kazi ya kujiajiri kwasababu uvivu uko ndani mwako.
Rafiki mwandishi anakutaka umalizie na swali kutoka kwa Frakl Struggled-Kwako maisha yana maana gani? maswali haya utayajibu kwa vitendo na maamuzi utakayofanya na siyo kwa mdomo, nikutakie wakati mzuri na bora rafiki yangu.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga. Napatikana kwa amail yangu bna blog yangu ambayo nakuwekea hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Wednesday, 22 July 2020
Gharama zilizojificha ambazo zinaongeza matumizi yako......
Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nyingine, Nina imani hujambo na waendelea na mipango yako mizuri ya Kila siku, endelea kuweka kazi kwani huyo ndio rafiki wa kweli na hawezi kukutupa.......
Leo tutaangalia sehemu ya matumizi ambayo wengi tunapoteza fedha zetu pasipokufahamu,au kuona ni kiasi kidogo lakini baada ya muda kupita tunakuwa tumepoteza kiasi kikubwa sana. Mwandishi anasema ni muhimu kufahamu kitu kinachochukuwa fedha kwenye mfuko wako kwani kadri matumizi yanavyoongezeka na kuwa makubwa ndivyo unavyojiweka mbali na utajiri. Na pale tutakapo dhibiti matumizi haya basi hata kiasi cha kujilipa kinaweza kuongezeka.
*Kundi la kwanza ni gharama za miamala ya kifedha*
Maisha yamekuwa rahisi sana,unaweza kukaa tu nyumbani kwako na kupata mahitaji yako yote muhimu ya kifedha. Urahisi huu umefanya tunapoteza fedha nyingi sana kwani huduma hizi nzuri zina gharama na kadri tunavyozitumia bila mipango ndivyo tunavyoingia gharama kubwa.
Hebu chukulia mfano mfanyakazi analipwa mshahara kupitia benki kisha akahamisha salio kwenye simu yake, akitaka kutoa itabidi aende kwa Wakala,hapo anakuwa amekatwa wakati anahamisha salio, kisha atakatwa kutoa fedha kwa Wakala na anapoteza takribani 10000 mpaka amepokea hela yake kama kiasi anachochukuwa ni laki moja kuendelea.Mwandishi anasema watu wengi hupenda kuacha fedha benki ili wasizitumie kirahisi lakini Kila wanapopata tatizo huenda Benki na kutoa salio na hapo kuongeza gharama, wengine huacha kwenye simu zao na kutoa kidogo kidogo na hapo pia gharama zinaongezeka. Kama una tabia za hivi nenda kachukuwe benki statement na utaona kiasi unachopoteza.
_Hatua za kuchukuwa_
A.Acha kufurahia huduma piga hesabu zako vizuri
B.Toa fedha zako kwa Mara moja na jijengee nidhamu ya kutorudi tena benki baada ya kutoa kiasi chote ulichopangia bajeti bila kurudirudi benki.
C.Kama uko mbali na benki na hivyo kuokoa gharama ya usafiri basi toa kiwango kikubwa kwa Mara moja kuliko kutoa Mara kwa Mara.
D.Kama unalipwa kwa njia ya simu kwa kazi unazofanya basi usitoe Kila unapolipwa bali subiria mpaka zimekuwa nyingi uzitoe kwa pamoja.
E.Kabla hujatumia huduma za ATM na simu kwenye miamala jiulize kama hakuna uwezekano wa kutumia njia nyingine ili kupunguza gharama.
*Kundi la pili;gharama za mawasiliano*
Kwa sasa mitandao ya simu wamekuwa wakitumia Kila ujanja ili kuchukuwa fedha zako zaidi, zamani ulikuwa ukijiunga unapata kifurushi chenye Kila kitu lakini sasa hivi wanataka ukijiunga mb,basi itakubidi ujiunge na dakika peke yake na meseji pia peke yake, hili limechangia gharama kuongezeka, mwandishi anasema usipokuwa makini kwa mwezi utatumia zaidi ya 30,000 kwa vorcher pekee, gharama hizo siyo kubwa kama na wewe una nufaika na mawasiliano lakini kama hulipwi kwa mawasiliano kiasi ni kikubwa sana.
_Kitu cha kufanya kuepukana na gharama hizi_
A.Chagua mtandao mmoja Mkuu utakao tumia na ukakupatia huduma na vifurushi unavyotaka kuliko kuwa na mitandao mingi inayokuongezea gharama.
B.Tenga muda maalumu wa kuwasiliana na watu muhimu wote kwa Mara moja, kuliko kufanya mawasiliano ya Kila siku na kuongeza gharama.
C.Unapotumia mitandao ya kijamii kabla ya kufunguwa picha au video unazotaka kuangalia, vipo vitu Vingi vinavyokula mb za kutosha na havina msingi wowote kwako.
D.Kabla hujafanya mawasiliano jiulize kuna fedha nitapata, Je nita imarisha mahusiano? Ninatengeneza mtandao mzuri? Nje na hapo achana na mawasiliano hayo.
*Kundi la tatu; gharama ndogo ndogo za nyumbani*
A.Vifurushi vya TV;kama unalipa zaidi ya 10000 kwa king'amuzi basi umeamua kupoteza fedha zako kwa vitu vingi visivyo na tija.
B.Fuatilia kwa umakini gharama za Umeme na Maji.
C.Vyakula vinavyoharibika na kutupwa ni sehemu inayochukuwa fedha zako nyingine.
Wengi wanapuuzia maeneo hayo lakini umasikini wao unatokana na kupuuza kwao kwani fedha nyingi hupotelea hapa.
*Kundi la nne; Gharama ndogo ndogo za maeneo ya kazi na biashara*
Kuwa makini na vyakula au Vinywaji unavyotumia kwa kununua kwenye maeneo ya kazi, maeneo hayo yamekuwa yanachukuwa fedha nyingi pasipo kufahamu, kitu muhimu ni Maji ya kunywa ambayo unaweza chemsha nyumbani na kubeba kwenda nayo kazini. Hata chakula unaweza beba kama eneo la kazi halina utaratibu mzuri wa chakula na hili litakupunzia gharama.
Rafiki ukikaa chini na kufanyia kazi maeneo hayo, tayari unakuwa na kiasi ambacho unaweza kuongezea kwenye mafungu yako ya ki uwekezaji na kupiga hatua zaidi za ki maendeleo.
Asante sana na uwe na siku njema, makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga, mwanafunzi wa namna fedha itaweza kunifanyia kazi kupitia chuo cha Kisima cha maarifa.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Tuesday, 21 July 2020
Nguvu ya taswira sehemu ya pili......
"Truly, thoughts are things, and their scope of operation is the world, itself"
Nimeona nianze na maneno hayo ambayo mwandishi amemalizia hivyo kutoka sura ninayokwenda kukushirikisha leo, kwanza kabisa niendelee kukushukuru wewe rafiki unayeendelea kujifunza na Nina hakika ukiyafanyia kazi haya utafika mbali sana.....
Rafiki kutoka kwenye kitabu chetu cha THINK AND GROW RICH ,wiki iliyopita tuliangalia umuhimu na aina za taswira na jinsi gani taswira itakupa chochote unachotaka kama utaitumia vizuri, rafiki labda nikuambie kitu kwamba mambo yote mazuri unayoyaona sasa na tunayatumia miaka kadhaa iliyopita hayakuwa halisia hivi, bali ilikuwa taswira kichwani kwa mtu, ndege zinazoruka angani na kusafirisha watu ilikuwa taswira kwa Write brothers, magari ilikuwa taswira kwa Henry Ford na mengine mengi mazuri yalitokana na taswira ambayo mtu mmoja aliiweka kwenye akili yake, Leo mwandishi ametuandalia kisa kimoja.
Miaka 50 iliyopita daktari mmoja alitoka kijijini na kwenda mjini akiwa na birika linaloonekana kuu kuu, alipofika mjini alikwenda kwenye duka moja na alionekana akiongea naye kwa siri, baadaye alionekana akimkabidhi birika lile pamoja na kanuni zilizopo kwenye birika lile, mwandishi anatuambia karani yule aliamua kutoa akiba yake yote na kumkabidhi karani yule, Je birika lile lilikuwa na nini, na je ni kanuni gani hiyo ambayo ilimfanya karani atoe akiba yake yote na kumpa daktari?
Karani yule alitoa akiba yake yote ya dola 500 za kimarekani na kumkabidhi daktari yule, Daktari alifurahi sana kuweza kutengeneza pesa kwa kuuza wazo kwa karani pasipo hata na uhakika kama wazo lile likichanganywa na kanuni zile litaweza kuleta matokeo, upande wa karani wasiwasi na mashaka vilimshika kwamba kanuni zile na birika vitamletea pesa kweli zaidi ya akiba yake ile aliyokuwa nayo?
Kabla sijaendelea na kisa hiki ambacho ni cha kweli na siyo cha kutungwa kama anavyosema mwandishi kwa kumnukuu "It is not a story from Arabian Nights, a story of facts".
Kipo kitu nimejifunza hapa kabla sijaendelea na simulizi hii ya kweli, kuna mawazo mengi sana tunayapuuza ambayo tunaona hayawezekani na kupitia mawazo hayo ndio tungeweza kutengeneza utajiri mkubwa sana, lakini pia woga wa kupoteza fedha zetu ndio kunatufanya tushindwe kujaribu vitu vipya vyenye manufaa kwetu.
Basi kupitia kanuni na birika lile karani aliweza kufanya mabadiliko makubwa sana duniani, kwani mpaka sasa karani huyo kupitia wazo lile na kuchanganya na ubunifu wake ameweza kutengeneza ajira za watu wengi duniani, kaweza kutengeneza tilioni za pesa, Mimi na wewe tumeburudika kupitia wazo na taswira kutoka kwa daktari kwenda kwa karani, kupitia birika lile leo ukiwa popote ulimwenguni, kwenye majiji na vijiji a hata uchumi ushuke vipi bado bidhaa hii itaendelea kuwepo, Je unataka kufahamu ni bidhaa gani hiyo? Basi ni COCA-COLA.
Rafiki hata wewe unayo mawazo na taswira pana sana lakini jamii itakuambia huwezi na wewe utakubaliana nao, lakini hata wewe una mawazo ya ki coca -cola lakini unajiambia haiwezekani na unapuuza ila ukiamua kufanya kitu nina hakika siku moja utajishukuru, toa kile cha kwenye taswira yako kiwe halisia.
Nikutakie siku njema rafiki yangu,usikubali siku ikapita bila ya kujifunza chochote, nikupongeze kwa kuendelea kutembelea USTAWI WA FIKRA na yapo mengi sana utaondoka nayo.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki yako, Mwl Kelvin Kinyaga na Mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kupitia chuo cha KISIMA CHA MAARIFA.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Monday, 20 July 2020
Tiba ya tano;Fanya sehemu unayoishi kuwa uwekezaji wenye faida.......
Siku nyingine, Nina amini kumekucha salama na uko tayari kuendelea kujifunza,kwani hakuna siku utajiambia huoni umuhimu wa kula, vivyo hivyo nakujifunza,kwa kuwa unaendelea kuishi basi una Kila sababu ya kuendelea kujifunza namna ya kuishi bora zaidi....
Kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tunaendelea na tiba za kutunisha mifuko yetu, baada ya kujifunza tiba zilizopita na sasa tuangalie tuba namba tano ambayo ni _Make of thy dwelling a profitable investment_
Mwandishi anatuonyesha baada ya kufuata tiba nne zilizopita na kutenga sehemu ya kipato na kuwekeza basi lazima fedha zitaanza kuongezeka na hapo utahitaji kuwa na nyumba yako mwenyewe, anasema hakuna familia yenye furaha kama haimiliki nyumba yake,hivyo tiba ya tano ni kuhakikisha unamiliki nyumba yako na hapo utatumia fedha unayolipa kodi kuwekeza kwenye maeneo mengine na hapo watoto wako watakuwa huru na kufurahia maisha.
Rafiki ni ukweli usiopingika kwamba kuwa na kwako kunaleta Uhuru na furaha lakini kama utaanza na tamaa ya kujenga nyumba yako kabla ya kuwekeza sehemu zingine zinazozalisha kwa haraka basi utakuwa kwako katika namna ya mateso ya kulipa madeni kwa kipindi kirefu sana, mwandishi anashauri hata kwa kukopa na kulipa deni pole pole siyo vibaya kama uwekezaji wako unaendelea kukua na ukalipa taratibu mkopo wako.
Angalizo, lazima uwe na hakika wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba yako hakuta athiri maeneo yako ya uwekezaji, wengi sana imeonekana wanapoanza ujenzi wanachukuwa sehemu za mitaji yao na kujengea nyumba zao na kisha kujikuta wanaanza upya na wakati huo gharama za maisha zinakuwa zimeongezeka.
Hivyo rafiki tambuwa kwamba utahitaji kuwa na kwako ili uwe huru na tumia nyumba yako kama sehemu ya uwekezaji, panda miti ya matunda, fuga na kama eneo ni kubwa weka hata bwawa la samaki na hilo litaongeza thamani ya nyumba yako na kukuinua ki uchumi na hivyo kufurahia maisha, usikubali nyumba yako kubaki na mapambo na maua pekee itumie kuwekeza. Asante na nikutakie siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Sunday, 19 July 2020
Usisubirie ufukuzwe kazi ndipo ugundue nyumba yako unayoishi siyo mali inayozalisha (Assets).......
Hongera ndugu yangu, siku nyingine na tunakwenda kuanza juma lingine kwa nguvu ile ile, pamoja na matokeo kidogo unayopata kwenye kile unachojishughulisha nacho bado una jukumu la kwenda mbele, kuweka kazi bila kurudi nyuma.......
Leo tutakwenda kuangalia sehemu nyingine ya kutupeleka kwenye utajiri kwa kupata ushauri wa baba tajiri, kabla hatujafika huko tumalizie mjadala wetu wa nyumba yako ya kuishi siyo mali inayozalisha kwa kusema hivi, waza umefukuzwa kazi Leo na huna chanzo chochote cha fedha na una nyumba yako unaishi na familia yako je nyumba hiyo itakusaidia kuondokana na adha ya kulipa kodi lakini haitakulisha, haitalipia ada za watoto wako shule na kufanya maisha yako kuendelea kama yalivyo sasa, mwandishi anasema watu hawaoni na kukubaliana na hili mpaka pale wanapoamua kuacha kazi au wakiachishwa kazi ndipo hukimbilia kuuza nyumba zao kwa bei ya chini na kutafuta kuwekeza kwenye maeneo yanayozalisha na wakati mwingine huwekeza sehemu wasizo zijuwa vizuri kutokana na hali za kuchanganyikiwa wanazokuwa nazo. Hapa ndipo anakuja na funzo la kwamba FANYA BIASHARA UNAYOIFAHAMU VIZURI.
Robert anatuambia akiwa mdogo baba masikini alimshauri kutafuta kazi inayolipa vizuri na baba tajiri alimshauri kuanza kuwekeza mapema ili ajipatie Uhuru kifedha, Je wewe Wazazi wako walikushauri mini?Na Je wewe unawashauri nini watoto zako? Je ni ushauri wa mama au baba tajiri au masikini? Jipe mwenyewe majibu ya maswali haya.
Mwandishi anasema matatizo ya fedha hutokana na watu kuwafanyia kazi watu wengine kwa muda mrefu bila kufahamu hatima yao. Anasema yote haya hutokana na mfumo wa elimu kuandaa watu kwa namna hiyo na siyo kuwafanya wafikie Uhuru wa kifedha. Watu wengi hujifunza taaluma mbali mbali na wanapoajiriwa wanafanyia kazi taaluma zao na anashangaa pale anapomuuliza mtu unafanya kazi gani anamjibu "Banker",akimuuliza unamiliki benki? Anajibu hapana.
Mwandishi anasema pamoja na kwamba umeajiriwa bado unahitaji kufanya biashara, watu hawataki kufanya biashara kwasababu ya hatari ya kupoteza fedha zao na hilo linawafanya kukubali kuishi kwenye utumwa wa kuajiriwa na kulipwa kidogo maisha yao yote. Hivyo anza Leo kufikiria ni biashara gani unapenda kufanya na jitaidi ujifunze kwa kina na kuijua ndipo uingie kwenye biashara hiyo, Anasema yeye alipenda sana majengo ndio maana aliamua kununua nyumba na kuzipandisha thamani halafu kuziuza kwa bei ya juu na kuwekeza kwenye makampuni kwani ndio maeneo aliyopenda, Je wewe unapenda nini? Chugua Leo na anza kujifunza kuwekeza huko na pambana uweze kufikia maeneo yafuatayo ki uwekezaji.
1.Biashara ambayo haihitaji uwepo wako moja kwa moja, kwani wengi ni watumwa wa biashara zao, kwani wasipokuwepo na biashara zao zinakufa.
2.Anza kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa, vipande na aina nyingine za dhamana na fedha
3.Uwekezaji kwenye nyumba za kupangisha au kuuza, hapa naona mwandishi alitengeneza mfumo mzuri sana wa kutambuwa wapi anapangisha na wapi ananunua na kupandisha thamani na kuuza na hilo limemsaidia kufikia utajiri mkubwa.
Rafiki bilashaka umeendelea kujifunza na umeondoka na kitu, acha kununua vitu visivyo zalisha kwa pesa yako, nunua nyumba ya kuishi, gari la kutembelea na vitu vya kifahari kupitia faida uliyopata kutoka kwenye uwekezaji uliofanya na ukifanyia kazi hili,Mimi na wewe tutakutana sehemu nzuri ki uchumi na kupongezena, ufukara siyo kitu cha kujivunia.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kwenye chuo cha Kisima cha maarifa, endelea kutembelea blog yangu na tuwasiliane kwa ushauri wowote kwani nazungukwa na wengi, asante.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Ufalme wa mbinguni unaanzia duniani......
Habari za wakati huu rafiki yangu, tuna kila sababu ya kumshukuru mungu kwa afya na uzima kwa wiki nzima na changamoto tulizopitia ni sehemu ya kutuimalisha kwani hakuna jaribu utakalopitia likakuacha dhaifu,kama halijakuua Basi limekuimarisha ki roho au ki akili......
Leo tupate neno kutoka kwa Mwinjili Mathayo (Mt:13:24-43)
Kupitia mwinjili Mathayo kwenye somo tajwa hapo juu tunaweza kuona yesu akiongea na makutano kwa kutumia mifano,kabla hatujaangalia mifano hiyo utakubaliana na Mimi kwamba maisha ya mbinguni ambayo Mimi na wewe tunayatamani kuishi baada ya kukamilisha maisha ya duniani, ikiwa mungu mwenyewe kupitia mwanae yesu kristo aliyaishi maisha ya dunia na mwisho akayashinda mauti basi na sisi lazima tujiulize na kufahamu msingi utakao tufanya siku moja tuyaishi maisha hayo ya umilele.
Kupitia masomo hayo yesu alitumia mifano mitatu akiifananisha na namna ufalme wa mbinguni unavyofanana, kupitia mifano hiyo tutaangalia mifano miwili tukiifananisha na maisha yetu ya Kila siku.
*1.Mfano wa ngano*
Kwenye mfano wa ngano na magugu tunapata funzo kubwa sana, wakati ukipanga mambo yako kwa usahihi kabisa na mipango mizuri kama tulivyoona kwenye mfano wa Shamba la ngano, mbegu bora na Shamba safi kabisa basi kitu tunachotarajia ni kupata mavuno safi yasiyo na changamoto yoyote, lakini baada ya muda kupita na ngano inapoanza kutoka inaambatana na magugu, magugu ni mfano wa changamoto ambazo zinaibuka pamoja na mipango mizuri tuliyoipanga, pamoja na changamoto hizo je maamuzi ni yapi? Kupitia neno la mungu tunafundishwa kwamba pale tunapopitia changamoto basi tunapaswa kuvumilia kwani kupitia somo nililokushirikisha tunaona watumwa wakishauri magugu kung'olewa lakini yesu anawajibu tusifanye hivyo tuyaache yakuwe pamoja na ngano na wakati wa kuvuna ndipo tutachambuwa ngano na kufunga matita magugu na kuyachoma moto, hapa tunapata funzo la kwamba safari ya maisha, safari ya mbinguni ni safari ambazo huwezi kujitenga na changamoto, kupoteza watu tunao wapenda, kujaribu biashara na kushindwa ni magugu kwetu, lakini hayo yote yanavyojitokeza kwanza tunapaswa kuyakubali na kuona ni sehemu ya ubinadamu wetu lakini mwisho utafika na mungu atatutenganisha na magugu, shida na mateso, hapa ndipo tunaona kwamba uvumilivu ni njia ya kweli ya kutufanya tushinde duniani na mbinguni.
*2.Mfano wa punje ya haradani*
Inasemekana haradani ndio mbegu ndogo kuliko zote, wakati nasoma hapa nikajiuliza kama punje ya ulezi ni kubwa kwa punje ya haradani Je hiyo punje ya haradani inafananaje? Lakini biblia inatuambia pamoja na udogo wa punje hii lakini ikiota inakuwa kubwa kuliko mboga zote na kutengeneza matawi ambayo hata nyuni wa angani hutua katika matawi yake. Rafiki haijalishi udogo wako ulio nao sasa, ki uchumi,ki mamlaka, ki umri na ki mtazamo lakini ukijifananisha na mbegu ya haradani unapata tumaini ya kwamba unaweza kuwa vyovyote unavyotaka.
Nini nimejifunza kwa somo hili?
Ushindi huja mwishoni baada ya maangaiko namateso ya muda mrefu wa kuvumilia na kujitoa kutafuta unachotaka bila kuchoka, safari ya yesu kwetu wakristo ni ki elelezo tosha, alibezwa, aliteswa,alitemewa mate na mengine mengi lakini alivumilia yote kwasababu alifahamu nini alikitafuta na mwishoni tunaona anaibuka Mshindi zidi ya mauti na kutukomboa, Je wewe unataka nini? Ufalme wa mbinguni, maisha ya utajiri na kusaidia wahitaji? Upo tayari kukabiliana na mateso yapi? Kipi unavumilia ili ushinde mwisho? Ukisemwa na kukosolewa unakasilika au unafahamu ni njia ya kufika unakotaka kufika? Vipi ukitemewa mate utakubaliana? Utavumilia? Nenda kayaishi haya kwa vitendo na mwishoni tutakutana pamoja tukishelekea ushindi pamoja.
Makala hii imeandikwa na Kelvin Kinyaga, mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya fedha kupitia Chuo cha Kisima cha maarifa tutakutana kesho tukifanyika Baraka.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Saturday, 18 July 2020
Usiniombe pesa niombe wazo..........
Habari rafiki,nikupongeze kwa siku na jumamosi nyingine, kwa wanaothamini muda wanafahamu tofauti kati jumamosi iliyopita na hii na hujipanga ili kuitofautisha na jumamosi inayofuata, ila kwa tulio wengi ni wale tunao furahia siku hizi za mwisho wa wiki na kuona ni siku za kupumzika na kustarehe kumbe kwa kufanya hivyo ndivyo tunazidi kujididimiza bila kufahamu.....
Rafiki tangu nimeanza kufahamu nguvu ya maarifa nimekuwa natumia njia moja wapo kupata kiasi cha pesa ninachohitaji na njia hiyo imekuwa ikinisaidia sana, njia hiyo ni kuchukuwa kiasi cha pesa ninachohitaji na kukigawa kwa 1000,2000,3000,4000 na kuendelea,Kwa mfano nina hitaji 360,000 kwa mwaka nitajuwa natakiwa kubuni wazo litakalotengeneza 1000 kwa siku, 720,000 wazo litakalotengeneza 2000 kwa siku, Nahitaji 1,080,000 nitahitaji wazo litakalonipati 3000 kwa siku na hili limekuwa likinisaidia sana, unaweza kusema huo ni uongo tu hicho kitu hakiwezekani, uweke 1000 Kila siku?hupati matatizo yoyote na kutumia fedha hiyo? Wewe unatushauri ulishafanya?rafiki pengine nakuandikia makala Kila siku na hufahamu nina jishughulisha na nini nje ya maarifa ninayokupa.
Kabla sijakwenda kukuambia najishughulisha na nini napenda nikuambie jambo moja ambalo masikini tunalipenda sana, mtu akipata tatizo lolote anakimbilia kutaka pesa ili atatue tatizo lake, hilo halina ubaya wowote na siyo tatizo lakini kuendelea kusubiria upate tatizo tena na tena na kuomba fedha au kukopa hilo ni tatizo tena tatizo kubwa, ni Sawa na mtu ambaye Kila siku anakwenda kuomba samaki kwa jirani yake kwamba hana mboga lakini hata siku moja hataki kujifunza namna ya kuvua samaki ili kesho asiombe tena. Basi na Mimi nimejifunza namna ya kutengeneza pesa ni kufahamu nahitaji kiasi gani na kisha kutengeneza wazo litakalowezesha nipate kiasi hicho, hapa chini nitakupa mifano kwa kutumia biashara ninazojishughulisha nazo.
*1.AJIRA*
Kupitia kisima cha maarifa nimejifunza Ajira ni ngazi ya daraja 0 na siwezi acha kuitaja kwani siku zote napambana ili niweze kuondokana na daraja hili au kutolitegemea kuendesha maisha yangu kwani utumwa wa kuuza muda,nguvu na maarifa yangu kwa kiwango anachopanga mnunuzi na pamoja na yote anaweza nifukuza na kunifanya nitaabike, pamoja na kutambuwa changamoto za daraja hili bado kwa sasa nipo kwenye hatari hii ya kutegemea mshahara wa mwezi kwa kuajiliwa na serikali kama Mwalimu wa Secondary hapa mjini moshi.
*Biashara ya visheti*
Hii ni biashara ambayo Mimi na mke wangu tulianza kwa kutumia kanununi niliyokushirikisha pale juu, tunahitaji mtaji wa biashara fulani ya ndoto yetu kama familia, tukajiuliza ni kiasi gani tunahitaji ili kuweza kupata kiasi hicho? Mshahara hautoshi je tukope? Hapana kanuni ya fedha inakataa kuanza biashara kwa mkopo, je tufanyaje? Ndipo tukaanzisha biashara ya vitafunwa aina ya visheti ili kutengeneza 2000 kwa siku itakayowezesha kufikia lengo hilo, kupitia kisima cha maarifa tukaweza jifunza namna ya kuuza biashara hii na kwasasa hasa shule zinapokuwa zimefunguliwa tunaweza tengeneza zaidi ya 2000 kwa siku kama faida, kwani bidhaa hiyo inauzika zaidi kwenye mikusanyiko ya watoto kama shule na kwenye mini supermarket na hata maduka ya watu binafsi.
*Biashara ya vorcher*
Biashara hii tumeipa Jina la Asante Corona, wakati wa ugonjwa wa Corona mtakumbuka kwamba shule zote zilifungwa na Mimi miongoni Mwa walimu ilinibidi kukaa nyumbani ili kuweza kutii agizo la serikali ili kupunguza maambukizi, hapo ndipo wazo la kuuza vorcher za likatujia wakati tukifikiria ni kwa vipi miaka ya mbele tutaweza kupata mtaji wa kiasi fulani cha fedha ili tuweze kuendesha familia na kuwa huru na kipato, ndipo tukaja na wazo la vorcher ambalo tulilifanya kama sehemu ya huduma lakini sasa ni moja ya biashara nzuri sana kama unaelewa nidhamu ya fedha kwani tulianza na mtaji wa 40,000 na sasa tumeweza kutengeneza Mara mbili ya kiasi hicho ndani ya miezi mitatu,ni kiasi kidogo lakini si Sawa na bure na kwasasa tumebuni namna bora ambayo tumaianza wiki hii na inakwenda vizuri zaidi, Je unafahamu kwa mwezi unatumia vorcher kiasi gani? Basi karibu uwe mteja wetu tutakufahamisha matumizi yako na kukusaidia namna bora ya kupangilia vifurushi vyako ili uweze kutumia kiasi kidogo kuliko unachotumia sasa, na kama utahitaji kukupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na ukarudisha mwisho wa mwezi kiasi hicho hicho ulichotumia bila riba unakaribishwa, tumeanza na watu watano na sasa tuna wateja watatu wa huduma hii na bado wawili, hivyo kama unataka kupata huduma hii kwetu tuwasiliane kwa mawasiliano nitakayoweka hapo chini.Maombi yanaweza kubaliwa au kukataliwa kwani ni biashara kwa wale wenye uaminifu pekee wa kupatiwa huduma hiyo, Asante corona itakupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na utalipia kiasi Sawa na huduma uliyopewa bila riba yoyote ile.
*Biashara ya tuition*
Chochote unachofanya unaweza kutumia kama sehemu ya kipato zaidi, pamoja na kwamba sasa tunatoka kazini saa kumi na moja na nusu bado nikitoka nafika nyumbani na kwenda kwenye nyumba za watu na kufundisha watoto zao tukifanya home work pamoja, wateja ni wengi sana wa huduma hii tatizo ni eneo la kufanyia huduma hii na muda, kwani Kila Mzazi anataka watoto wake wafundishiwe majumbani mwao.
Hizo zote ni biashara binafsi ambazo nazifanya Mimi na familia yangu, zipo nyingine ambano Nina shirikiana na wengine sijaziweka hapa na niseme kitu kimoja kwamba bila maarifa ninayopata na naendelea kupata kupitia vitabu na KISIMA CHA MAARIFA na kocha wangu AMANI MAKIRITA nisingeweza yote haya na nisingefika hapa, mke wangu kipenzi unalala saa nane ili maisha yaende asante sana,wana kisima cha maarifa taifa na Kisima cha maarifa Kilimanjaro,nyie ndio nguzo kubwa kwangu, familia ndugu na wewe rafiki yangu nawashukuru sana kwa kuendelea kunitia moyo, tuwe pamoja na tufike pamoja, safari ni ndefu na ngumu lakini tutafika.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga, unaweza endelea kujifunza kupitia blog yangu hapo chini;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0712161251/0763766944
Thursday, 16 July 2020
Siyo kuwa wa kwanza bali kwa ubora upi?
Rafiki habari za wakati huu, hongera tena kwa kuweza kuchaguliwa kuifikia siku hii, nina imani umeamka na nguvu ya kwenda kuweka kazi zaidi ili upate matokeo zaidi.
Leo kwenye ukurasa wa Ijumaa kutoka kwenye mfululizo wa makala za ustawi wa fikra tutaendelea kuangalia maisha ya falsafa, labda nikuambie kitu rafiki kama huna falsafa unayoishi basi tambuwa uko kwenye hatari kubwa ya kutofika kwenye kile ulichopanga, kuna watu wanaishi misingi yao pasipofahamu kwamba hiyo ndio falsafa na wakivunja misingi waliyojiwekea lazima waazibiwe. Leo kwenye falsafa tunakumbushwa maneno yanayosomeka.
"Slow is smooth, smooth is fast"
Maneno haya yanatukumbusha kwamba chochote unachokitaka kiwe rahisi basi kitapatikana pole pole na urahisi huo ukiwepo ndio kitakufanya ufanikiwe haraka na kwa wepesi, Msemo huu unataka kutuaminisha kwamba maisha ya haraka hayana maana kwetu na kama unataka mafanikio ya kweli basi lazima uweke nguvu na bidii kwa muda mrefu, lakini kwa tulio wengi tunataka matokeo ya haraka,tunataka biashara zetu ziwe kubwa kwa muda mfupi na ndio maana tunashindwa haraka sana na kukata tamaa ya kuendelea na kuanza tena lingine na kushindwa tena na maisha yanaendelea hivyo.
Leo falsafa inatutaka kwanza kufahamu nini tunafanya, mbili kwanini tunafanya? kivipi tunafanya? Na hapo ndio kile tunachofanya kitafanikiwa kwa haraka zaidi, kama unafanya biashara na hufahamu biashara hiyo ki undani, na kwanini unafanya biashara hiyo? Labda ni msukumo wa kupata fedha pekee na huduma unayotoa ni mbovu na unaifanya kwa mazoea bila ubunifu lazima ife, hivyo anza kuwaza miaka kumi unataka uwe umefika wapi kwenye kile unachofanya.
Wanajeshi wana Msemo wao unasema hivi "More haste, less speed,better a safe commander than bold" hivi ni kipi bora? Kwenda kwa tahadhali na kuwa salama au kuwa na haraka na kuwa mateka? Hivyo kama unataka haraka basi utaipata kwa kuweka umakini kwa kwa kwenda polepole, kwani kadri unavyoitaka haraka ndivyo unavyochelewa na kadri unavyokuwa na kusudi na kulifanyia kazi taratibu ndipo tunapolifikia kwa haraka na wepesi.
Acha kuchanganyikiwa ukiona wengine wanafanikiwa haraka, muhimu ni kufahamu nini unataka kujenga na jifunze ni kwa namna gani utafika pale unapotaka kufika. Ubora ndio muhimu na siyo haraka, nenda kalifanyie kazi hili na acha kuwaza uharaka waza ubora.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.kelvin Kinyaga
Wiki hii nimepata kitabu kutoka kwa rafiki yangu Dr.Raymond Mgeni,kitabu hiki kinahusu mazoezi 20 ya falsafa ya Ustoa, hivyo Kila ijumaa nitakuletea zoezi moja la kufanyia kazi wiki nzima. Asanteni sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251/0163766944
Wednesday, 15 July 2020
Jinsi ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora......
Rafiki yangu habari za wakati huu?, hongera kwa Zawadi ya maisha na kuweza kuifikia siku hii nzuri kabisa, ninaposema siku nzuri sijakubaguwa wewe unayepitia changamoto kwani Nina amini kwamba hayo unayopitia ndio uzuri wenyewe, uimara wa Kingo ya mtu unapimwa wakati wa mafuriko, mti imara utauona wakati wa dhoruba, hivyo kupitia changamoto siyo laana bali ni kipimo cha uimara wako na hivyo endelea kufurahia kwa lolote lile unalolipitia.......
Leo kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA tutaangalia namna ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora.
SIRI YA UTAJIRI NI UBAHILI,mwandishi ameanza na kauli hii kwa kusema watu wengi hupenda kuitumia. Na kupitia kauli hii kumefanya zoezi la kutengeneza utajiri kupewa taswira hasi. Kwasababu ubahili ni kubana sana fedha na kujinyima,na wengi wanaona hayo siyo maisha ya kuishi. Kwamba ni kwanini ujitese kutengeneza utajiri wa baadaye badala ya kuitumia fedha hiyo sasa na ukawa na maisha bora? Mwandishi anasema hili ni swali ambalo wengi hujiuliza na lina mantiki kwani hupaswi kuteseka leo ili kesho uwe na maisha mazuri.
Mwandishi anasema pamoja na kwamba kujitesa leo ili uishi maisha mazuri kesho siyo maamuzi sahihi lakini bado ukweli ni ule ule, matumizi yanapaswa kuwa madogo kuliko mapato. Lakini unalifikiaje hili huku ukiwa na maisha bora kabisa kwako, yasiyo ya kujitesa?
Swali unalopaswa kujiuliza hapa ni hili,kwenye mchakato wa kupata fedha na kuzitumia ni kitu gani unakijali sana? Kitu gani kinakupatia furaha wewe? Kwa kulifahamu hilo utaweza kudhibiti matumizi yako na huku ukiwa na maisha bora. Mwandishi anaitumia kauli inayopendwa sana kutumiwa na watu kwamba fedha haiwezi kununua furaha, kauli hii inatokana na watu kuahirisha maisha, wakiamini siku wakishakuwa na fedha basi ndio watakuwa na furaha,kitu ambacho hakiwezi kutokea. Mwandishi anataka tufahamu kitu kimoja kwamba fedha na furaha ni maeneo mawili tofauti kwenye maisha na yanaweza yasiwe na uhusiano wa utegemezi. Kitu muhimu kufahamu ni wewe kuwa na furaha kabla hata ya kuwa na fedha.
Tatizo la wengi wetu hatujuwi tunataka nini na kipi tunajali zaidi, tumekuwa tunaishi kwa matamanio na kujilinganisha na wengine pasipo kufahamu ni kipi hasa unachojali?na hili limekuwa linafanya tuishi kwa kutamani Kila kitu kwasababu tumeona wengine wanavyo, hapa mwandishi anatutaka tujifamu na kujitambuwa ni kipi tunataka kwenye maisha yetu na kuhakikisha kwa namna yoyote tunakipata. Na yale yote yasiyo na maana kwako unaachana nayo na hapo utakuwa na maisha ya furaha. Wakati nasoma hapa nikakumbuka maisha ya mama Theresa kwake umaana ulikuwa kusaidia wengine na alipomsaidia mtu aliona amepata furaha kubwa sana, upande wa Donald Trump yeye kwake furaha ilitokana na kumiliki majengo makubwa na kuyaandika jina lake Donald Trump na furaha huzidi pale jengo hilo linapokuwa refu kuliko majengo yote, kupitia watu hawa wawili tunajifunza kwamba pale unapofahamu nini hasa hitaji lako basi hakikisha unalipata, lakini hili halina maana kuweka hitaji lako kwa kile kilicho nje ya uwezo wako, huwezi kuwa huna mkono halafu ukataka muujiza utokee upate mkono ndio ufurahie, hivyo jiulize sasa hitaji lako ni nini? Mimi ninajisikia furaha kuzungukwa na watu wenye furaha na ndio maana Kila siku najitahidi wewe mtu wangu upate mafunzo yaliyo sahihi Je wewe ni kipi chenye maana na kukijali zaidi kwako?
Moja ya matajiri sana ambao wanasemekana ni bahili ni Bilionea Warren Buffet,ambaye wakati kitabu hiki kinaandikwa alikuwa tajiri namba mbili duniani na sasa ni namba tatu kama sijakosea, wakati kitabu hiki kinatolewa Julai 2019 tajiri huyu alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani 77(kwa report za mwaka 2017) Sawa na zaidi ya Tsh trilioni zaidi ya 150,karibu Mara kumi ya bajeti ya nchi yetu ya Tanzania. Pamoja na utajiri wake huo bado anaishi kwenye nyumba yake aliyonunua mwaka 1958 huko Omaha, Nebraska nchini Marekani. Amekaa kwenye nyumba moja kwa zaidi ya miaka 62 sasa.Alipoulizwa kwanini pamoja na utajiri wake bado anaishi maisha ya kawaida? Akajibu mafanikio kwake ni kufanya kile kitu anachopenda na kwake ni kuwekeza.Hivyo hicho ndio kitu anafanya na vingine vyote havina nafasi, ingekuwa huku kwetu wangesema ni masharti ya mganga na Kila maneno.
Rafiki bilashaka unahitaji maisha yenye furaha, anza sasa kufahamu hitaji lako na pambana mpaka uweze kulipata na acha kukimbizana na Kila kitu.
Nikutakie siku njema, makala hii imeandikwa na Mimi rafiki yako Mwl.Kelvin Kinyaga; ninayo kushirikisha ni baadhi tu, mengi mazuri zaidi yapo kwenye kitabu hiki, tuwasiliane upate nakala yako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Umuhimu wa taswira katika kufikia utajiri....
Rafiki yangu hongera kwa siku nyingine tena, Nina imani u mzima wa afya na tunaendelea vyema kusukuma gurudumu la maendeleo, lengo ni kuendelea kuifanya kazi ya kuifanya dunia kuwa na mazingira bora kuishi kwetu na kwa wengine....
LeoLeo kutoka kitabu cha THINK AND GROW RICH tutajifunza hatua nyingine muhimu katika kutengeneza utajiri, Hatua muhimu kuifahamu katika kutengeneza utajiri ni kutengeneza taswira.
Mambo yote tunayoyafurahia sasa miaka ya hapo nyuma havikuwepo, kupitia watu ambao leo tunawaita wagunduzi ndio vimeweza kuwepo na kutunufaisha, mwandishi wa kitabu hiki anatuambia kwamba zipo aina mbili za taswira.
*1.Taswira awali*
Taswira awali inajengwa kwa kutumia mawazo na mipango ambayo tayari ipo, hapa mtu unatengeneza taswira kwa kuoanisha mawazo au mipango mbalimbali na kupata wazo moja ambalo unalifanyia kazi, watu wengi tunatumia taswira awali kuweza kuboresha maisha yetu.
*2.Taswira bunifu*
Hapa unajenga taswira baada ya kupata wazo jipya na kulitumia kupata kitu kipya ambacho hakijawahi kufanyika, hapa ndipo pamewawezesha wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa duniani kubaki na heshima muda wote, jiulize mtu aliyeweza kututengenezea simu ambayo Mimi na wewe leo tunatumia, jiulize mtu aliyetengeneza usafiri, yote hayo yalikuwa kama picha(taswira)kwenye akili yake ya ndani na Leo hii tunafurahia maisha mazuri kupitia matokeo ya taswira.
Sayansi inatuambia vitu vyote vimeundwa kutokana na maada na nguvu. Hivyo kama utaitumia nguvu ya taswira basi unaweza kufanya chochote unachotaka kitokee, utajiri pia ni matokeo ya taswira hivyo ukitumia nguvu ya taswira na kuhamisha taswira hiyo kwenye uhalisia na mambo yanatokea, watu wengi wanayao taswira lakini Kila wanapojaribu kuitengeneza lakini baadaye huzipuuza na kuendelea kuishi maisha ya mazoea. Asante rafiki na uwe na siku njema.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga;
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin162.blogspot.com
0763766944/0712161251
Monday, 13 July 2020
Tiba ya nne kwa mifuko iliyo sinyaa.....
Tumshukuru mungu wetu Kila tunapopata bahati kuianza siku tukiwa na afya tele, nikushukuru wewe rafiki yangu unayeanza kuona umuhimu wa kusoma makala hizi, hiyo ni hatua ya kwanza, nikupongeze wewe unayechukuwa hatua Mara moja na kufanyia kazi masomo haya, siwezi kuwa mjinga kukupatia masomo haya ikiwa sina uhakika kwamba yatakusaidia, karibu tuwe sote....
Leo kutoka kwenye chambuzi za kitabu chetu pendwa cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tutaendelea kuangalia tiba kwa mifuko iliyosinyaa, kati ya tiba saba tutakazo jifunza tatu tumeshazichambuwa, tumeshafahamu kutenga asilimia kumi ya Kila kipato chako na kujilipa wewe kwanza, tumeshafahamu umuhimu wa kudhibiti matumizi yako,tukaona namna ya kufanya akiba yako izae zaidi na sasa tunakwenda kuangalia tiba ya nne LINDA HAZINA YAKO ISIPOTEE.
Utakapoanza kufanikiwa basi ndio unapaswa kuwa makini zaidi, kwani wengi ndipo huanza kuona kama changamoto nyingi zinajitokeza lakini ukiangalia kwa makini changamoto hizo zinasababishwa na mafanikio kidogo uliyopata. Na Arkadi alianza somo la nne kwa kuwaeleza kama hutolinda fedha zako basi zitapotea.
Sehemu kubwa inayowaangusha wengi ni pale wanapoanza kuona mafanikio ndipo Kila mtu kuwafuata na kuwapa ushauri wa wapi awekeze kutamlipa, na Mara nyingi humshauri kuwekeza ili apate faida ya haraka.Mwandishi anasema kama hutofikiri kwa makini utapoteza fedha zako.
Arkadi aliwauliza, Je ni vizuri kushawishika na faida kubwa wakati mtaji wote unaweza kupotea? Nadhani jibu ni hapana. Msingi wa kwanza wa uwekezaji ni usalama wa mtaji wako unaowekeza. Utapaswa kuweka umakini mkubwa na kuchunguza sehemu unayotaka kuwekeza fedha zako. Acha kutamanishwa na kupata faida kubwa kwa haraka.
Arkadi akitoa somo hili aliwakumbusha uwekezaji wake wa kwanza alivyopoteza kwa kutoweka umakini sehemu anayowekeza na akapata hasara hivyo aliwaeleza kwamba wasifanye makosa aliyofanya yeye.
Omba ushauri kwa wazoefu wa fedha na Fanya busara ndio ikuongoze katika uwekezaji, Kocha wetu huwa anapenda kutushauri kwamba kabla hujapokea ushauri wa mtu jiulize hiki anachonishauri kimemsaidiaje yeye kufika hapo alipo? Au amejifunza kwenye kitabu gani ili na Mimi nijifunze niweze kufanikiwa kwenye hili? Ukishapata majibu ndipo fanyia kazi ushauri huo.
Rafiki huwa tunapenda kupokea ushauri kwa Kila mtu, hasa watu tunao waheshimu, hata kama wamefanikiwa kifedha, swali la kujiuliza ni je hiki anachonishauri ndicho ambacho yeye kafanya na kufanikiwa? Au ndio ushauri wa madini kutoka kwa mfyatua matofari?
Nina imani unakwenda kufanyia kazi masomo haya, asante na uwe na siku njema rafiki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Sunday, 12 July 2020
Nini utakosa kwa kufanya nyumba kuwa uwekezaji wako wa kwanza?
Hongera sana rafiki yangu kwa kuweza kuanza wiki yako kwa kujifunza, ukifanya kujifunza kuwe muhimu kama chakula Nina hakika hapo ndipo utafahamu kuishi ni nini na nikukaribishe kwenye ukurasa huu wa USTAWI WA FIKRA tujifunze pamoja.......
Wiki iliyopita tuliangalia ni kwanini nyumba yako ya kuishi siyo Mali inayozalisha (assets) na kwanini elimu ya matumizi ndio muhimu kuliko elimu ya kutafuta fedha, wengi tunaweka bidii kutafuta fedha lakini kadri tunavyozipata ndivyo tunavyojitenga nazo, ni kwasababu hatufahamu tuwekeze wapi ili fedha ziweze kutuzalishia zaidi.
Baada ya wiki iliyopita kujifunza kwamba nyumba ya kuishi siyo asset nilipata maswali mengi sana na wengi walionyesha kulishangaa hilo kwasababu ni imani ya wengi kwamba nyumba zao za kuishi ndio asset zao kumbe hakuna kitu kama hicho, Leo tutaendelea na chambuzi kutoka kwenye kitabu chetu cha Rich dad, poor dad.
Kwanza napenda ufahamu kwamba mwandishi wa kitabu hiki ni muwekezaji mkubwa wa real estate, kwa kununua na kujenga nyumba,pamoja na kuziuza hivyo anafahamu matatizo mengi yanayotokana na watu kukimbilia kujenga nyumba au kuwekeza kwenye nyumba kabla ya kufanya uwekezaji mwingine.
_Haya hapa ndio mambo matatu unayokosa kwa kuwekeza kwenye nyumba_
1.Kwanza unapoteza muda;kinachofanya tunapata shida tulio wengi kwenye fedha ni uhakika, hatutaki kufanya biashara kwasababu tunataka uhakika wa kulipwa mshahara, na hili ndilo linatufanya tuogope kufanya uwekezaji mwingine tukimbilie kuwekeza kwenye nyumba, hivi hao matajiri unaowatetemekea ulishawauliza walianzaje? Chukuwa gharama ya mitaji walio anza nayo kisha ipime na thamani uliyojengea nyumba yako na riba uliyolipa benki kisha ona kama ungechaguwa kuwekeza fedha hiyo kwenye uwekezaji mwingine ungekuwa wapi?
2.Kupoteza mtaji; Ungeweza kutumia fedha uliyojengea nyumba kama mtaji wa kuwekeza maeneo mengine lakini unajipa jukumu la kupeleka fedha zako ambazo umekopa kwa riba kubwa kwa kukopa, hapo unakuwa umeamua kufukia fedha zako.
3.Kukosa elimu; Ukianza kuwekeza kwenye nyumba ina maana utasubiria mpaka deni benki liishe ndio uanze kufikiria kuwekeza maeneo mengine, hapo utakuwa umechukuwa muda wako wa kupata elimu ya kuwekeza maeneo mengine kwasababu huna fedha za kuwekeza huko na ukajifunza, kwani biashara zina faida nyingi na thamani yake inakuwa haraka lakini hatua za mwanzo ni ngumu na zimewaangusha wengi na hilo ndilo linawapa wengi hofu ya kuwekeza huko, ni ukweli kama huna elimu ya biashara unayotaka kufanya lazima upoteze fedha zako.
Hilo ndilo mwandishi anasema watu huendelea kuishi kwa chanzo cha mshahala na kupoteza elimu ya kujifunza kwenye uwekezaji, kwani hakuna elimu inayoizidi elimu ya kufahamu namna fedha itakavyokufanyia kazi na siyo wewe kuifanyia kazi fedha. Madeni yanaongezeka kwa kuongeza matumizi na siyo kwa kupata kipato kidogo.
*Fahamu maeneo ambayo masikini anafanyia kazi*
1.Mwajiri-Masikini yeyote lazima amfanyie kazi mwajiri na kadri anavyoongeza bidii kwenye kazi ndivyo mwajiri wake anavyonufaika, tambuwa hakuna anayekuajiri ili utimize ndoto zako bali ndoto zake yeye mwajiri kupitia bidii na ujuzi wako.
2.Serikali-Kadri unavyoongezewa kipato na mwajiri ndivyo na serikali wanavyopokea Kodi kubwa kutoka kwako, hivyo muda wako umempa mwajiri na fedha zako unailipa serikali kupitia kodi, Fanya tafiti mwajiriwa namfanyabiashara nani analipa kodi kubwa.
3.Unaifanyia kazi benki-Masikini wengi hupenda kukopa na kuwekeza maeneo ambayo hayazalishi kama kujengea nyumba na kunua viwanja na hili linawafanya kufanyia kazi benki kwa maisha yao yote.
Pengine rafiki ni miongoni Mwa watu unaye fanyia kazi maeneo hayo na sasa umefahamu, hebu kumbuka ile kanuni ya mashimo, ukijikuta kwenye shimo acha kwanza kuchimba na angalia unatokaje, Je upo kwenye shimo la madeni basi nafasi ni hii ya kujifunza na kuondoka huko.
Majina niliyopewa na Wazazi Wangu ni Kelvin Kinyaga. Mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya fedha na namna fedha itakavyonifanyia kazi. Karibu twende pamoja.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
HITIMISHO
Somo letu limefika mwisho, hongera kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho nina amini litakusaidia kufuatilia kwa ukaribu zaidi taarifa zako za kifedha kwani unaweza kujaza ukiwa sehemu yoyote na muda wowote, kuna kitu nimejifunza kupitia somo hili, haijalishi unafahamu nini kwa udogo upi omba nafasi ya kushirikisha na utaongeza ufahamu kwenye jambo hilo kwani utajiandaa vya kutosha na kufahamu zaidi ya ulivyokua unafahamu mwanzo, nikushukuru kocha kwa nafasi hii uliyonipa kwani nina imani kwa kuweza kuwashirikisha haya nilipata nafasi ya kulifahamu somo hili kwa undani tofauti na mwanzo na sasa niwakaribishe kwa nyongeza kwa kile ambacho unakifahamu na sijakiweka hapa kwani application hii ina mambo mengi sana, lakini pia niwakaribishe kwa maswali na ufafanuzi zaidi,Hongereni kwa kuchaguwa kuwa humu kisimani kwani haita tokea mkafa kwa kiu ya maarifa, asanteni na uwe na siku njema.
Hapa chini ni mfano wa muonekano wa picha,maelezo ya jumla ya taarifa zako zote za kifedha, grafu zinazoonyesha asilimia kwa matumizi na kipato.
Picha ya kwanza itaonekana Kila unapogusa sehemu ya application hiyo kwa kuonyesha sehemu ya katikati (Balance over view) jumla ya kiasi kilichopo, sehemu ya juu ni sehemu inayoonyesha jumla ya matumizi yako(Total expenses) na sehemu ya chini ni sehemu ya matumizi (Recent outflow)na kipato kilichoingia (Recent inflow).
Picha ya pili inaonyesha matumizi na kipato kwa asilimia, sehemu nyekundu ni matumizi uliyofanya na kijani ni salio lililopo, chini ni grafu zinazoonyesha kiasi cha fedha kwa kipato na matumizi pia. Na kupata muonekano huu utapaswa kubonyeza sehemu ya juu inayoonyesha matumizi upande wa kishoto 223,000/475000 kipato chako upande wa kulia.
Jinsi ya kuweka taarifa zako za kifedha endapo kiwango cha kifedha kitaongezeka au kupungua kwa matumizi unayofanya.
Pichani chini unaona sehemu (+) bonyeza hapo na itakuletea muonekano mwingine kama unavyoosheshwa kwenye picha inayofuata, kama unataka kujaza taarifa kwa kipato kilichoongezeka bonyeza sehemu iliyoandikwa (Income),na kama unataka kujaza kwa matumizi uliyofanya basi bonyeza sehemu inayosomeka (Expense) na kama umehamisha salio kwenda kwenye akaunti zingine za kifedha kama malengo ambazo siyo matumizi bonyeza sehemu ya (Transfer) kisha jaza taarifa zinazohitajika kujazwa, sehemu ya Reminder na other ni taarifa za kifedha za ziada ambazo tutajifunza siku nyingine kwani siyo matumizi ambayo wengi tunatumia, hapa chini ni mfano wa picha inavyoonekana baada ya kubonyeza sehemu ya Expense ili kujaza matumizi uliyokwishafanya awali fuata Maelezo hapo chini.
1.From account-ukibonyeza hapo utajaza kiasi cha fedha kilichopo kwenye bajeti yako kabla hujaweka matumizi uliyofanya.
2.Category-Utajaza kwa kuchaguwa kwenye orodha aina ya matumizi uliyofanya, labda ni chakula, mavazi na matumizi mengine kama yanavyoonyeshwa kwenye picha nyingine chini, endapo matumizi uliyofanya hayapo kwenye orodha iliyopo bonyeza sehemu inayoonekana chini (+ add category) na kujaza aina ya matumizi hayo.
3.Merchant-Sehemu ulipofanyia matumizi hayo (sokoni(market) au sehemu nyinginezo.
4.Final amount-utajaza kiasi cha matumizi uliyofanya.
Hayo ndio maeneo muhimu kujaza na usipojaza mfumo utakugomea mpaka utakapoyajaza, sehemu zilizobaki,Discount/cash back na Tags siyo muhimu na hata usipoyajaza hayataleta athari yoyote.
*VITU MUHIMU KUFAHAMU HAPA*
Endapo aina ya matumizi unayotaka kujaza yalishafanyika ndani ya mwezi husika wa bajeti yako basi hutojaza kama taarifa mpya, utakwenda sehemu inayoonyesha matumizi(money outflow)na kwenda sehemu uliyojaza mwanzo kwa Ku edit taarifa zako kwa kubonyeza eneo la matumizi hayo na kwenda sehemu ya juu kulia yenye alama ya peni na kubofya kisha kujaza taarifa mpya za muda, tarehe, from account na sehemu ya final amount jaza taarifa ya fedha kwa kujumlisha salio la awali na jipya, kama ni mwezi mpya wa bajeti basi hutojumlisha salio la awali bali utalijaza kama salio jipya. Kisha utabofya sehemu ya (√) kisha kubonyeza sehemu ya save ili kuhifadhi taarifa zako. Hapa chini ni picha zote zinazoambata na somo hili.
Jinsi ya kuandaa bajeti yako na kuhifadhi kwenye application yako.
Kabla hujajaza taarifa yoyote sehemu ya bajeti itaonekana Tsh 0,hatua ya kwanza kufuata ni kupanga bajeti yako kulingana na kipato chako kisha kubonyeza sehemu yenye muonekano wa "v" kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini ili kuchaguwa muda ambao unataka bajeti yako iwe,kama ni wiki,mwezi au mwaka kama inavyoonekana hapo chini pichani, baada ya hapo utabonyeza sehemu iliyoandikwa budget started(tarehe unayotaka bajeti ianze) na budget ended(tarehe unayotaka bajeti yako iishie), baada ya hapo utabonyeza sehemu ambayo inasomeka Tsh 0 SET BUDGET na utaweka kiasi kulingana na budget yako na kisha kubonyeza sehemu iliyoandikwa DONE na bajeti yako itaifadhiwa.
Jinsi ya kuipakua app ya vmoney tracker, money manager and budget planer...
Utakwenda kwenye application ya play store na kuandika vmoney trucker na itatokea picha kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini na kisha download app iliyoonyeshwa na mshale na kisha utafuata maelekezo, bonyeza sehemu iliyoandikwa GOT IT mpaka itikapotokea picha ya pili chini.
UTANGULIZI
Karibuni kwenye darasa letu maalumu la Leo tarehe 12/07/2020,Kwenye darasa hili tutajifunza jinsi ya kupakua App yenye uwezo wa kutunza taarifa zako zote za fedha na namna ya kuitumia application hiyo.
Kwanza kabisa app hii alitushirikisha kocha terehe 03/02/2020 na kwa kuona ni kitu muhimu nilichukuwa ujumbe huo na kuuhifadhi kwenye stared messages na sikuhangaika nao kwa siku hiyo, huwa na kawaida wa kupitia message zilizohifadhiwa baada ya muda fulani kupita, kwenye mwezi wa tano mwishoni nilianza kufanyia kazi application hii na mpaka sasa nimeona faida zake na kwenye maswali mengi ya taarifa yangu ya mwezi sipati shida kuandaa kwani naweza zichukuwa taarifa zangu kutoka kwenye App hii na kuwasilisha kwenye taarifa yangu, hapa chini ni ujumbe huo Kila mmoja aupitie upya kama ulishaupoteza, karibuni tujifunze pamoja Nina imani kuna kitu mtaondoka nacho na mwishoni mtaweza kuongezea na kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi zaidi, unaweza kujifunza kwa vitendo kwa kufanya kile ninachokuelekeza, karibu sana rafiki yangu.
Huu hapa chini ujumbe wa kocha wa tarehe 03/02/2020.
Hii apa chini nayo ni Mobile App inaitwa inaitwa Vmoney tracker-Money manager and budget planner.
Nayo ni nzuri sana katika utunzaji wa taarifa zako zote kifedha kwa kadri zinavyoingia na zinavyotoka. Hii App is the best sababu imesheheni vitu vingi sana sana na unaweza kuingiza data zako mpka ikakupa balance sheet yako ya fedha.Ina categories nyingi sana na inakupa uwanja mpana wa kutunza hesabu zako kifedha.
Faida kubwa ni ile ile tu kwamba unaweza kurekodi taarifa zako muda wowote wakati wowote pale unapoingiza au kutoa fedha.
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.voutputs.vmoneytracker
Haya ndio majibu mawili ambayo unaweza kuwapa watoto wako wanapokuuliza maswali magumu...
Habari za wakati huu rafiki yangu, hongera kwa kuweza kuifikia jumapili nyingine tunakilatunakila sababu ya kumshukuru mungu, asante kwa kuzungukwa na watu wazuri pia na wanao tupenda, familia,Wazazi/walezi, ndugu jamaa na marafiki ni Zawadi tunazopaswa kuendelea kumshukuru mungu......
Rafiki utakubaliana na Mimi kwamba watoto ni watu wenye kupenda kudadisi vitu sana, hupenda kuuliza maswali magumu ili wapatiwe majibu sahihi lakini kwa bahati mbaya huwa hatuwapi majibu sahihi isipokuwa kuwadanganya ili kuondokana na usumbufu wa maswali hayo na pale wakiwa wakubwa tunaanza kushangaa ni wapi wamejifunzia uongo, pengine huwa hufahamu ni jibu gani unapaswa kuwapa ndio maana unadanganya, unakumbuka uongo tulio ambiwa watoto wanapatikana hospitalini kwa kununuliwa? Hili ni baadhi ya jibu la uongo tunalopenda kuwapa watoto lakini yapo mengi sana ambayo tunawadanganya na kuwapotosha kabisa, katika kupitia kwangu vitabu haya hapa ni majibu mawili sahihi kwao badala ya kuwkuwadaganya.
1.Mwambie akiwa mkubwa atafahamu;Badala ya kumdanganya kwa kumwambia mambo yasiyo sahihi mwambie awe na subira akiwa mkubwa atafahamu, hilo linaweza lisimtosheleze lakini litakuwa jibu sahihi, wengi watasema atakwenda kuuliza kwa mwingine na kupata jibu, lakini bado wewe utakuwa hujamfundisha uongo isipokuwa umemwambia siyo muda wake sahihi kulifahamu hilo.
2.Mwambie atumie akili yake; Vipo vitu vingi ambavyo hata sisi wenyewe hatuvifahamu na watoto wanapotuuliza tunaanza kuwapa majibu mepesi yasiyo na tija kwao, wewe huna pesa unamfundisha Mtoto kuhusu fedha, ni bora kumwambia atumie akili yake na kuja na mbinu tofauti kuliko kumdanganya, soma kwa bidii utapata fedha, huo bado ni uongo, ni bora ukamwambia swali hilo akamuulize mtu mwenye fedha alifanyaje akazipata fedha? Au atumie akili yake kwani wewe huna elimu hiyo kuliko kumpoteza kama ulivyopotea wewe.
Hayo ni baadhi ya majibu sahihi ya kumpa Mtoto wako, kuwa mkweli na Mtoto wako kufahamu kwamba kutofahamu Kila kitu ni hatua ya kufahamu mambo mengi zaidi.
Asante na nikutakie siku njema rafiki yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Saturday, 11 July 2020
"Hapana" na "Samahani",Sitaweza........
Habari za wakati huu rafiki, muda ni rasilimali muhimu sana kwenye maisha yetu na Kila mmoja wetu kapewa muda Sawa na mwingine lakini wengine wamechaguwa kujipa sababu ya kwamba muda ni mchache kwa kufanya vitu visivyo na maana.......
Kila nikikumbuka swala la muda siwezi kukumbuka kanuni ya PARETO ya 20/80 na hapo ndipo naacha kujificha kwenye kichaka cha kwamba muda hautoshi, kanuni hii inatuambia kwamba ni asilimia 20 pekee ya vitu tunavyofanya ndio vinaleta matokeo yenye manufaa kwetu na 80 ni mambo yasiyo na maana kabisa na yanapoteza nguvu na muda wetu.
Watu tunaishi kwa kujipa matumaini hewa kwa kufanya mambo Yale yale tuliyozoea kufanya,Kila siku unajiambia umekosa muda hata wa kusoma kurasa tano za kitabu na kujifunza, lakini haipiti siku hujaangalia taarifa ya habari kuanzia inaanza mpaka utabiri wa hali ya hewa, ukitoka hapo utahitaji kuangalia tamthilia fulani nzuri unayoifuatilia na siku ukiikosa unaona kama umekosa sehemu fulani ya maisha yako, lakini jiulize ni tamthilia ngapi zimepita tangu umeanza kuangalia? Ni ipi ilikupa funzo linalokuingizia fedha? Iliyokupa hamasa ya kuanza biashara? Ni taarifa gani ya habari umekupa manufaa? Habari zote muhimu kwako zitakufikia bila kuzitafuta, lakini mtu huyu akitoka kwenye TV anakwenda kitandani na anaamka saa moja na kukimbizana kuelekea ofisini, akifika ofisini busy na simu yake, hivi ndivyo tunavyoishi na kuendelea kujipa matumaini ya kwamba ipo siku mungu atajibu maombi, maombi yapi hayo? Ingekuwa maombi bila kazi unafanikiwa hakuna ambaye angeenda kazini.
Baada ya kutafakari namna tunavyooendesha maisha yetu ndipo nikakubaliana na mwanafalsafa Seneca kwamba "siyo kwamba hatuna muda au muda ni kidogo bali ni mwingi mpaka tumeamua kuupoteza" kumkuta mtu akisema napoteza poteza muda ni kawaida na ndio maana anakubali Kila kitu anachoambiwa, anaweka matumaini hewa kwenye Kila fursa inayojitokeza, ukiambiwa fuga kwale wanalipa unafuga, kesho biashara ya chakula upo, keshokutwa biashara ya nguo upo lakini Kila unachojaribu ukiona kina ugumu fulani unaacha na kukimbilia fursa nyingine na hapo ndipo wanafalsafa wanatuambia maneno haya chini.
"No" and "sorry",I can't", Neno hapana,samahani na siwezi kufanya yakatumike kwenye mambo mengi ambayo hayana tija kwako,ondoa mazoea na ishi kwa kusudi na Fanya yale yanayotoa msaada kwa wengine na kwako na achana na mambo yasiyo muhimu, chagueni siku za kuzima TV kama unaona huwezi kuachana nayo kabisa na tumia muda huo kukaa na familia yako kuzungumza hatima na ndoto zenu.
Rafiki nenda kayaishi haya Mara moja na utajishukuru siku moja, siyo rahisi kuondoa mazoea lakini nimeshakuambia vitu vinavyokurudisha nyuma nenda kaviweke kwenye matendo.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, unaweza kuendelea kujifunza kwa kubonyeza maandishi haya hapa chini.
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944/0712161251
Thursday, 9 July 2020
Acha kuwajaza hofu watoto wako.......
Siku nyingine ambayo Kila siku nimejifunza asili yake ni utulivu lakini pale tunapoianza kwa habari na mitandao ya kijamii ndipo tunapoanza kuziharibu asili hizo, habari hizo zinatufanya tuone maisha yetu hayana thamani na hali ya kukata tamaa inajengeka na hapo ndipo tunaposhindwa kwa Kila kitu kwenye siku zetu.
Rafiki yangu Leo wakati napitia meseji kwenye email yangu nikakutana na moja ya ujumbe ukielezea namna maisha ya John .F. Kennedy aliyekuwa Rais wa Marekani akijaribu kuelezea namna baba yake alivyomtenga na habari hasi, habari zozote za kumuonyesha kwamba mambo ni magumu na hayawezekani.
Wakati naendelea kusoma ndipo nokagundua kwamba Wazazi tulio wengi tunapenda kuyaongea mambo yetu yanayotuumiza mbele ya watoto pasipo kufahamu athari tunazowatengenezea hapo baadaye, hebu kumbuka ukiwa unapitia changamoto kubwa halafu Mtoto wako mdogo wa miaka miwili akiwa hafahamu lolote unalopitia, bado ataendelea na michezo yake na pengine akiona ndege ikipita angani atakuja kukuomba umnunulie na yeye ndege yake, unaweza kuona ni akili ya kitoto na ukaipuuza lakini hiyo ndio asili yetu, tunapozaliwa tunakuwa na hali ya kushinda lakini kwa kujaza mambo hasi kwenye akili yetu tunapoteza uwezo huo.
Kupitia kisa cha Kennedy tunaweza kuona akielezea mambo mengi mabaya yaliyotokea marekani amekuja kuyasoma akiwa shule lakini baba yake hakuwahi kumuonyesha kuna vitu vibaya vinaendelea, kama Mtoto anataka malezi bora hataki sababu, mjenge mwanao kwa kumuonyesha kwamba dunia ina Kila kitu ni yeye tu kuchaguwa ni kipi anataka kutumia,muweke mbali na mambo hasi na mfanye aone anapaswa kubeba majukumu yake yote hata pale mambo yanapokwenda vibaya, unapomuonyesha mwanao mambo ni magumu na hayawezekani atakuwa akiamini hivyo na hatasumbuwa akili yake.
Hivyo rafiki mwache mwanao aendelee na maisha yake ya kitoto kwa kumtimizia majukumu yake muhimu na kumuongoza huku na wewe ukibeba majukumu yako kama Mzazi, kama ni mwanafunzi mwambie ajira ziko nyingi sana na ni wavivu wa kufikiri ndio wanaamini kuna upungufu wa ajira, hili litamfanya asumbuwe akili yake kubuni vitu vipya, unapokubaliana naye kwamba hakuna ajira unamwambia akae asubirie kitu ambacho kwa dunia ya sasa mambo hayasubiriwi kutokea yanasababishwa.
Nenda leo kayaishi haya, kwa malezi yoyote unayotoa basi waonyeshe kwamba hakuna kitu wanaidai dunia na waonyeshe dunia ina Kila kitu bali uhaba ni msamiati wa wajinga, ndege hawana mikono na wanakula, wanyama hawana utashi na wanaishi kwa furaha je wewe mwenye utashi unaanzaje kuishi maisha ya kulalamika? Tafakari na chukua hatua.
Mwl.Kelvin Kinyaga ndie mwandishi wa makala hii na zingine kupitia blog hapa chini;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
Wednesday, 8 July 2020
Na hivi ndivyo unavyoweza kuyatumia mawazo yako mazuri uliyonayo kabla hujapata pesa........
Pale tunapogundua hakuna hongo wala sababu yoyote inayotufanya tuamke leo salama,haijalishi maumivu madogo madogo tuliyo nayo kutokana na mambo mbalimbalia ya nje lakini kitendo cha kutoa pumzi na kurudisha ndani ni kitendo cha kuanza siku hii kwa kumtukuza mungu wetu......
Karibu tena rafiki na ndugu yangu kwenye ukurasa huu ustawishe fikra zako, maana unahitaji ustawi wa fikra, ustawi wa kiroho pamoja na ustawi wa mwili ambao ndio hekalu linalobeba akili na roho zetu, ikiwa hata mwenyezi mungu mwenyewe alifahamu sisi watoto wake tunahangamia kwa kukosa maarifa je Mimi na wewe ni nani mpaka tuyapuuze?ili mwili na roho viwe salama vinahitaji akili timamu ambayo tunaipata kupitia maarifa.
Wiki iliyopita tuliangalia namna ya kugawa fedha zako kwenye mafungu yako na muhimu nikukumbushe tena, kama unahitaji kweli kufanikiwa basi lile fungu la tano ambalo ni matumizi yako,hakikisha haizidi asilimia sitini ya kipato chako. Leo tutajifunza namna ya kukaa na fedha zako hata pale unapozipokea kwa mkupuo tofauti na kiwango chako cha kimazoea unachokipokea siku zote.
Ni kawaida kwetu sisi binadamu kuwa na mipango mizuri kabla hatujapokea fedha, tukishapokea fedha mipango yote mizuri inapotea na kujikuta tukitumia fedha hizo kwa mambo mengine tofauti na mipango ya awali, hali hii imekuwa ikitesa watu wengi sana bila kufahamu sababu ni nini, kabla hatujaendelea na uchambuzi wa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA nikuambie vitu vitatu ambavyo vimenisaidia sana kwenye fedha,vitu hivi nilijifunza mwaka 2018 kwenye semina ya kisima cha maarifa ya kufungua mwaka huu, nimekuwa navisema na nitaendelea kuvisema.
Moja;Kujenga misingi ya kutokopa, mipango yako ya kifedha imekuwa inavurugika sana kwasababu umekuwa mwepesi kukopa, akili ya binadamu inatabia ya kutafuta urahisi na kutoroka ugumu hivyo kama kuna namna ya kupatikana urahisi basi ukipata tatizo kidogo unakimbilia kutafuta njia ya mkato kwa kukopa, mkopo maana yake natumia fedha zangu kabla sijazipokea na nikizipokea narudisha kwa mwenye nazo, kabla hujakopa jiulize nani utalipa? Na atalipa kutoka wapi? Ni kweli wapo wengi sana wanaofanikiwa kwa kukopa lakini hawalipi kwa fedha zao huko mbele tukifika kwenye mikopo mizuri na mikopo mibaya tutayaangalia kwa kina.
Mbili;Jijengee msingi wa kutokopesha;watu wengi sana wameingia kwenye matatizo na watu hasa wanao wapenda kwa kudhani kwamba wakiwakopesha basi mahusiano yao yataimalika lakini baada ya watu hao kutowalipa ndipo mahusiano hayo yanakuwa mabaya zaidi, hivyo kama unataka kumkopesha mtu ambaye ni ndugu au rafiki wa karibu jiambie kiasi ninachompa hakiwezi kuharibu undugu wetu na urafiki hata asiporudisha fedha hii, hivyo mpatie huku ukijiambia hata kisipo rudi sitoathirika wala urafiki wetu na undugu hautavunjika, Mara nyingi tunao wakopesha tunawaongezea matatizo kuliko kuwasaidia kwani Leo akikopa kwako siyo kwamba matatizo yake ya kifedha ndio yatakwisha bali atakopa na kwa mwingine na mwingine na mwisho wa siku anasema ana pepo la madeni, kumbe tatizo ni nyie rafiki zake.Sijasema usisaidie ndugu au rafiki bali toa msaada usio athiri uhusiano wenu mambo yakienda kinyume.
Tatu;Tengeneza bajeti yako kabla hujapokea kipato chako na ukikipokea usitumie nje ya bajeti hiyo hata kingetokea nini, kama kitu ni muhimu kipangie bajeti kwenye kipato kinachofuata.
Kama utayaishi mambo haya matatu nina uhakika kabisa changamoto za kifedha utaondokana nazo Mara moja, ni sehemu niliyoifanyia kazi kwa haraka sana na siku zote nitaendelea kuamini safari yangu ya mafanikio nguzo zake kuu ni hizo tatu na nimeanza na eneo hilo kwani linahusiana na somo letu la Leo.
Ninawezaje kudhibiti kipato kikubwa kinachoingia kwa Mara moja?
Mwandishi anasema wapo watu wengi kulingana na kazi zao au hali fulani wanayofikia hujikuta wakipokea hela nyingi kwa mkupuo, pensheni kwa wastafu, wachimba madini, biashara ya udalali, kupokea urithi, lakini wakati mwingine hata Mimi na wewe tunapata pesa nyingi tofauti na kawaida na zinakwisha bila kufahamu zimeishaje Je tatizo ni nini hapo? Watu wamekuwa na mawazo mazuri kifedha wakiwa hawana fedha na wakizipata mawazo hayo upotea mpaka watumie ziishe ndio mawazo mazuri hurudi tena.
Mwandishi anasema watu wakiwa na fedha nyingi hupenda kupokea ushauri kwa Kila mtu bila ya kuchunguza ushauri huo anaopewa, na kwa wastafu hali hii upelekea hadi kifo cha mapema pale anapokuja kustuka fedha hizo zimetumika na kwisha bila kufahamu amefanyia nini. Yafuatayo ni mambo muhimu kufanya pale unapopata fedha nyingi kwa mkupuo.
1.Usijioneshe kwa wengine kwamba una kipato kikubwa.
Hapa mwandishi anasema binadamu hatuna siri ,maisha yetu yapo wazi sana. Ukifunga mdomo wako usiseme, matendo yako yanakuwa yanaongea waziwazi. Hili limekuwa linawagharimu watu wengi sana kwenye fedha. Kama watu wanaweza kufahamu kwamba sasa hivi unayo fedha na sasa hivi huna fedha basi wewe ni muhanga na somo hili linakuhusu. Rafiki watu wengi sana hawapendi kutafuta fedha kwa njia ngumu bali njia za mkato mkato hivyo wakishafahamu unayofedha watatumia Kila mbinu kujifanya wakikushauri kumbe hukuchukulia fedha zako, hivyo hakikisha ukiwa na fedha au ukiwa huna usomeki na unaonekana kawaida.
2.Hatua ya pili ni kugawa mafungu ya kipato hicho.
Kosa kubwa ambalo wengi wanafanya ni kutogawa fedha hizo kwenye mafungu ya matumizi na uwekezaji na hapo mwandishi anasema mipango inakuja kukumbukwa fedha zinapobaki kidogo. Anasema wengi wamekuwa wanafanya maamuzi mabaya ya uwekezaji kwa kutolea mfano wa mstaafu kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha kama sehemu ya kutengeneza kipato. Anasema huo ni uwekezaji mbovu kwasababu nyumba ambayo itahitaji mtu kuweka mpaka milioni 50 mpaka ikamilike unakuta kwa mwaka haiwezi kukupa zaidi ya milioni mbili na hapo hujaweka gharama ya kuifanyia marekebisho, huu ni uwekezaji unaolipa kidogo kidogo,kitu ambacho siyo rafiki pale mtu anapokuwa amestafu ndio atumie kama njia kuu ya kumuingizia kipato.
3.Wekeza kwenye mambo unayoyajua kwa kina na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wenye uzoefu.
Mwandishi anasema watu wengi wakiwa na fedha nyingi wanaweza kuwekeza kwa ushauri ambao unatoka kwa Mtoto wa darasa la saba. Mara nunua Bajaji zitakulipa au Lima nyanya zitakutoa, anasema watu wengi wanaweka mtaji wao mkubwa kwa ushauri wa namna hiyo.
Mwandishi anamalizia sehemu hii kwa kusema unapopata kiasi kikubwa kwa mkupuo basi tulia kwanza mpaka mihemko itulie na upate ushauri wa kitaalamu ndipo uwekeze fedha zako.
Na Mimi nasema kwanini usubiri yote hayo? Anza kuwekeza sehemu unayotaka kabla hata hujapokea penshen yako au kupokea fedha nyingi ili ukizipata ziingie kwenye kitu unachokifahamu, kama kuna biashara unapanga kuifanya kwa fedha za kustafia basi ianze sasa baada ya kupokea ushauri wa kitaalamu na siyo usubirie mpaka ulipwe kiinua mgongo utakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza.
Nenda kayaweke kwenye vitendo rafiki yangu na nikuatakie siku njema. Asante nitaendelea kusamabaza upendo Wangu kwa kukupatia maarifa Kila siku.
kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
Bonyeza maandishi haya kupata makala zote zilizopo kwenye ustawi wa fikra.
0763766944/0712161251
Tuesday, 7 July 2020
Huwezi fika usiko kuona....
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka u buheri wa afya, hongera kwa siku nyingine ambayo umeipata tena,Zawadi kubwa sana kwetu kuweza kuifikia siku hii.
Leo kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH tutajifunza mambo matatu muhimu kuyatumia kama ngazi ili kufika kule unakotaka kufika.
Mwandishi anasema kitu kikubwa ambacho kinawakwamisha watu wengi ni kutokuwa na picha au mtazamo mpana wa kufanikiwa, wengi wanawaza maisha ya kawaida sana, nikiwa na watoto Wangu, wakasoma shule nzuri, tukajenga nyumba yetu na kununua gari hayo ndio mawazo ya kiwango cha juu kwa walio wengi, na kweli wanafikia ndoto hizo na kufa bila ya kuacha alama hapa duniani.
Rafiki unaweza kuona huhitaji tamaa zaidi ya kupata pesa, lakini huoni kwamba kujiwazia wewe peke yako ni ubinafsi mkubwa sana? Hebu waza mafanikio makubwa na ona kuna wengi wanahitaji msaada wako na kwa kuwaza hivyo hata mungu anakwenda kubariki kazi zako, zifuatazo ni njia tatu unazoweza kuzitumia ili kufikia kiwango cha juu ki mtazamo na kupiga hatua kwenye maisha yako.
1.Hatua ya kwanza ni KUPATA MAARIFA, rafiki kupitia maarifa utabadili mtazamo wako kwa kuwaza mambo ya viwango vya juu, Kila siku utakuwa na shauku ya kufikia mafanikio ya juu sana, kupitia maarifa utajifunza mbinu nyingi walizotumia wengine kufanikiwa, kupitia maarifa utaepukana na makosa mengi ambayo kwenye vitabu wengine waliyafanya na kuanguka hivyo wewe kutofanya walichofanya wao.
2.Hatua ya pili ni KUTUMIA UZOEFU WAKO,rafiki kwa kujaribu vitu vipya Kila siku tunapata uzoefu na kubuni mambo mapya, watu wengi hawafahamu kwamba ni kwa kupitia makosa waliyofanya kwa kujaribu na kushindwa basi wanapata uzoefu mkubwa sana na hilo linakuwa kama ngazi kwao kutumia kufanikiwa, hivyo kama ulijaribu kitu kipya na kushindwa basi kaa chini na jiulize nilikosea wapi na sasa nirekebishe ili kufika ninakotaka kufika? Lakini ukianza kuona mambo magumu na kuamua kuishi kwa mazoea basi utabakia hapo hapo.
3.Hatua ya tatu ni KUFANYA UCHUNGUZI WAKO MWENYEWE, watu wengi wanawaza makubwa sana lakini hupenda kusikiliza mawazo ya wengine bila ya kufanya uchunguzi, Leo utapokea maoni ya mtu alishindwa kwenye jambo fulani na kukubaliana naye kirahisi kwa sababu alizokupa, lakini ukichunguza ki undani utaona kuna makosa ya wazi mtu huyo alifanya yakamtenganisha na kile anachotaka, sikiliza sababu ila usikubaliane nazo kirahisi.
Rafiki anza kujijengea msingi wa kupata maarifa, tumia uzoefu kwa kujaribu vitu vipya na chunguza kile unachotaka kufanya na hilo litakuwa kama ngazi ya kupanda ili Mimi na wewe zitufikishe kule ambapo tunapaswa kuanza kupaona kuanzia sasa.
Kelvin Kinyaga ndio majina yangu niliyopewa na Wazazi Wangu, kufundisha ndio taaluma yangu na nitafanya hivyo siku zote za maisha yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Tiba ya tatu ya mifuko iliyo sinyaa....
Rafiki yangu karibu tena kwenye ukurasa huu wa ustawi wa fikra,tujifunze pamoja na kuweka kwenye matendo yale tutakayojifunza hapa, Nina hakika yatakusaidia ndio maana ukiwa kama ndugu na rafiki yangu Kila siku nimebeba jukumu la kukuandikia kwasababu nina uhakika wa nguvu iliyopo kwenye maarifa haya, siku nilipofahamu maarifa yana nguvu kuliko fedha ndio nilipoamua kutumia fedha kuyapata na baada ya kuyapata nimejipa jukumu la kukupatia wewe maarifa haya bure, bure hii usiitumie kuyapuuza kwani kuna siku utanitafuta kwa fedha na itakuwa ngumu kunipata....
Leo tunaendelea na uchambuzi wa kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu kinachokupa misingi sahihi ya kifedha, baada ya wiki kadhaa zilizopita kujifunza tiba ya kwanza ya kutenga Kila sehemu ya kumi ya kipato chako kinachoingia naTiba ya pili ya kudhibiti matumizi yako basi kitakacho jitokeza utaanza kuona mifuko yako iliyo sinyaa inaanza kutuna na kuongezeka na hapa ndipo tunaenda kujifunza tiba ya tatu.
Tiba ya tatu ya mifuko iliyo sinyaa ni KUIFANYA AKIBA YAKO IZAE ZAIDI.
Arkadi alianza kufundisha siku ya tatu kwa kuwaeleza namna alivyopoteza uwekezaji wake wa kwanza kwa mfyatua matofari lakini uwekezaji wa pili aliowekeza kwa mkopeshaji wa fedha na kisha kugawana faida ndio safari yake ya utajiri ilipoanzia na ndipo fedha ilipoanza kumfanyia kazi, aliweza kuitumia akiba yake kuwekeza maeneo mbali mbali yanayozalisha na akaupata utajiri.
Arkadi anasema utajiri wa mtu haupo kwenye fedha alizobeba kwenye mfuko wake bali kwenye uzalishaji unaofanyika na fedha zake.hapo ndipo kipato chake kitaweza kukua na kufikia utajiri. Akawaeleza kwamba kwa njia hiyo ndio kipato chake kimeweza kuwa mtumwa wake na kumfanyia kazi yeye.
Kwenye kitabu hiki kuna simulizi ya mkulima mmoja aliyepata Mtoto na kuamua kuwekeza kwa ajili ya Mtoto wake aliyezaliwa. Alichukuwa vipande kumi vya fedha na kumpatia mkopeshaji na kumwambia aviweke mpaka mwanae atakapokua na kuzihitaji. Na walikubaliana atapata robo ya kiwango kitakachokuwepo kwa Kila baada ya miaka minne kupita. Baada ya kupita miaka 25 mkulima alikwenda na kukuta vipande vimekuwa na kufikia vipande thelathini na moja na nusu, kwakuwa mwanae hakuviitaji vipande hivyo kwa wakati huo aliamua kuviacha viendelee kukua, baada ya kijana yule kufikisha miaka 50 alikuta vimekua na kufikia vipande 167,zaidi ya Mara 17 ya kiwango alichoweka cha vipande 10.Hivyo ndivyo Arkadi alipomalizia Tiba ya tatu kwa kuwaambia kama unataka utajiri basi Kila fedha unayopata tenga sehemu itakayokwenda kukuzalishia na kukufanyia kazi.
Rafiki kwa kupitia hayo tunajifunza kwamba uwekezaji ni kitu ambacho kinahitaji mtu asiye na papara ya fedha, kama unahitaji kunufaika na uwekezaji usiwe mtu wa kuangalia faida ya muda mfupi, lazima uweke muda wa miaka mingi na hapo utapata manufaa makubwa, hebu jiulize kama serikali wanachukuwa sehemu ya kipato chako na kukitumia kuwekeza na mwisho wa siku kukulipa pensheni nguvu zikikuishia na wakati mwingine kuona watu waakilalamika kwamba wameibiwa je kwanini usitumie uwekezaji kujitengenezea pensheni yako ya uhakika? Nenda kazifanyie kazi tiba hizi ulizojifunza Mara moja na Nina hakika utaanza kuona manufaa yake, tukutane wiki ijayo kwa ajili ya tiba zingine zilizobaki.
Kelvin Kinyaga ndio majina yangu, Mwl na mwandishi wa mfululizo wa makala hizi, nakupenda rafiki na nikutakie siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Sunday, 5 July 2020
Hizi hapa sababu za kwanini nyumba yako ya kuishi siyo Asset.....
Rafiki yangu Mimi na wewe tuna Kila sababu kuanza juma hili kwa kumshukuru mungu, kwanza kwa afya na uzima, kwa kutupa nafasi ya kuzungukwa na familia pamoja na marafiki wazuri kama wewe,kwa kutupatia matajiri wanaolipa kodi zinazotumika kutupatia huduma muhimu, lakini tunamshukuru mungu hata kwa maadui zetu pamoja na watu wanao tuchukia, kupitia wao kunatukumbusha kwamba sisi ni wa bahati sana kutojengwa kwa misingi ya chuki kwani tumependelewa kwa kumpenda Kila mtu na tunaishi kwa furaha, tunaowaita maadui zetu wakati mwingine wanatuonyesha makosa yetu huku tunaowaita marafiki wakijaribu kufunika makosa yetu kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kama waswahili wanavyosema, hayo ni machache ya kupongeza lakini yapo mengi sana ya kushukuru......
Rafiki yangu tunaendelea na uchambuzi wa kitabu chetu cha Rich dad,poor dad.Wiki iliyopita tofauti kati ya Assets(mali inayozalisha)na Liabilities(Mali isiyo zalisha)mwandishi alielezea kwa mapana sana dhana hizo mbili kwa kumtumia baba tajiri, aliweza kutumia mchoro wa kwanza ukionyesha mzunguko wake wa fedha ni husubiria kipato na akikipata kinakwenda moja kwa moja kwenye matumizi, hivyo kinakwisha na kubaki hana kitu na kuishi kusubiria kipato kingine tena, wakati mzunguko wa fedha wa matajiri fedha ikitoka kwenye mapato inakwenda moja kwa moja kununua Mali inayozalisha na baada ya faida anayopata ndipo hugawa kiasi kwenda kwenye matumizi na kingine kubaki kikizalisha zaidi.
Leo tutaangalia nyumba zetu za kuishi ziko upande upi? Ni Mali inayozalisha au haizalishi? Mwandishi hakubaliani na namna ya neno "assets" na "liability" ilivyoelezewa kwenye dictionary na anasema ukitaka kuchanganyikiwa basi fuata maana ya kwenye dictionary, anasema maana iliyotolewa ni nzuri kwa kufundishia na imewalenga tabaka la juu ila siyo kwa watu wenye kipato cha wastani na cha chini. Mwandishi anajaribu kutuonyesha namna watu wanavyo amua kununua au kujenga nyumba kwa fedha za mkopo na kujikuta wakiishi mbio za panya za kupata kipato na kulipa madeni maisha yao yote.
Anasema rafiki yake hupenda kusema Msemo huu,na mnukuu "If you find you have dug your self into a hole...... Stop digging" akimaanisha unapojikuta umetumbukia kwenye shimo hatua ya kwanza ni kuacha kuchimba zaidi, hivyo ukijikuta kwenye shimo la madeni hatua ya kwanza kuchukuwa ni kuacha kukopa, lakini kwa watu wengi kwa kuamini nyumba ni Assets hujikuta wakiishi maisha ya mateso kwa maisha yao yote. Anasema siku moja alibishana na baba yake (poor dad) kwamba nyumba yao ni assets au liability, anasema akiwa na miaka 16 lakini baba huyu masikini na elimu yake kubwa Darasani ila elimu ya fedha yeye alimzidi. Kadri nyumba inavyokuwa kubwa na gharama za Maji, Umeme,samani na hata kodi ya jengo inakuwa kubwa, Robert anasema mpaka sasa bado watu wengi wanampinga akiwaambia nyumba siyo assets.
Haya hapa ni makosa makubwa matatatu ya kuwekeza kwenye nyumba ambayo haizalishi;
1.Unaishi maisha yako yote kulipa deni la nyumba.
2.Nyumba haiongezeki thamani kwa kasi.
3.Unakosa fursa zingine ambazo ungezitumia kuwekeza na kuzalishia badala yake unachimbia fedha zako kwenye nyumba.
Rafiki wajapani wanafahamu nguvu ya dunia sasa hutokana na sehemu tatu ambazo ni Siraha, fedha na akili na Kila taifa linapambana kuwa na vitu hivyo, hakikisha siku haipiti bila ya kujifunza, uwe na siku njema.
Makala hii imeandikwa na Mwl Kelvin Kinyaga
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Mafanikio unayapimaje?
Habari za wakati huu rafiki, wiki lingine limekatika, hii ina maanisha ule mwaka tuliojiambia ni mpya ndio unaelekea ukingoni je ni kipi ulipanga kufanya kwa mwaka huu?je ulishaanza kufanya? Umekutana na magumu gani ya kukufanya usiendelee? Je umejiambia huu ni mwaka mbaya hivyo mipango yako umehahirisha mpaka mwaka mwingine? Basi kufanya hivyo ni kujiandaa kushindwa.
Leo nataka tuone usahihi wa neno mafanikio, Kila mtu anaweza kuelezea kwa namna yake anavyoona ni sahihi, leo nitakuelezea kwa namna wastoa wanavyoweza kuelezea maana ya mafanikio, kwanini nimependa kukushirikisha hili? Tafsiri hii itakufanya ufurahie maisha yako muda wote na siyo zile tafsiri ambazo wao wanaziita tafsiri za kitoto,tafsiri ya kupima mafanikio kwa Mali au fedha si kwamba tafsiri hii siyo sahihi pekee bali ni tafsiri itakayokufanya uhahirishe Kila siku yako kuishi ukijiambia utafurahia siku ukiwa na nyumba yako, unapata nyumba bado unaona huyafurahi mafanikio hayo kama ulivyodhani, unajiambia ukimiliki gari utakuwa na maisha mazuri na kufurahia, unapambana unalipata lakini unagundua huna furaha kama ulivyodhani, hapa ndipo tafsiri hii ya kifalsafa inapokuwa bora muda wote na itakufanya utenganishe mambo ya nje na maisha yako ya Kila siku, vipimo visivyo sahihi ndivyo vinakufanya ukose furaha ya kweli kwenye maisha yako na kuacha kufurahia, uwe na fedha au usiwe nazo uweze kufurahiakufurahia na kuishi kwa kusudi.
Kwanza unapaswa kufahamu maisha ni mchakato, Mwanafalsafa Ryan Holiday anasema "The definition of success is Autonomy" vile unavyoweza kuitawala siku yako moja ambayo ni leo kwa kutambuwa lililopita huwezi kulibadili na kesho huwezi kuimiliki kwani hujuwi nini kinaweza kutokea kunakufanya uishi kikamilifu, anza kuweka nguvu zako zote kwenye siku yako na ichukulie siku hiyo kama ndio nafasi ya mwisho kwako kuishi, weka ubunifu wako kwenye siku yako, Kila unapopata wazo la kujiambia utafanya kesho jiambie kesho naweza nisiamke je kwanini nisifanye sasa hivi ambayo ndio siku yangu kuishi. Kama ni watu walio nizunguka ni upendo kiasi gani naweza kuwaonyesha sasa hivi kwa kutambuwa kesho naweza nisiwepo, huwa tunashindwa kuishi Leo vizuri kwa kujidanganya kwamba kesho nitakuwa na gari, mwakani nitakuwa na nyumba yangu ndio nitafurahia ni kuchaguwa kushindwa kwani kadri unavyofikia kile unachojiambia utakifurahia ukikifikia unagundua kipo kingine bora zaidi na hivyo ndivyo unavyohahirisha kuishi na unapishana na mafanikio.
Mwanafalsafa wa kistoa Marcus Aurelius anasema maneno haya "Today I escaped auxiety or no,I discarded it,because it was within me,in my own perceptions not outside" kauli hii inatutaka tutambuwe kwamba umiliki pekee wa kitu chochote ni wa sasa hivi, mali, fedha na watu tunao wapenda uhakika wa kuendelea kuwa nao ni wa muda ulio nao pekee, usijiambie nitafanya nikiwa na...... Au nitafurahia nikiwa na .......,hapo ni kuchaguwa kutokuishi.
Kila siku nenda kaishi kikamilifu na acha kuangalia matokeo yoyote kwani wastoa hufurahia chochote anachopitia, matatizo, changamoto mbali mbali siyo vitu vya kututenga na furaha na kutufanya tusiishi kwa upendo kwani kwa kuvipokea au kutovipokea hakubadilishi ukweli wa kwamba Kila mtu atavipitia, hivyo Kila siku ishi kwa usahihi, tenda wema na ona huna nafasi nyingine, pamoja na kuichukulia siku yako kama siku ya mwisho haina maana kwamba usiweke kazi, jitoe na kubaliana na matokeo yoyote utakayopata kwenye siku yako na unapopata siku nyingine ya ziada anza kushukuru na kujiambia nimepewa siku hii nyingine ili nikamilishe yale ambayo Jana sikuyakamilisha na sitoongezewa siku nyingine.
Kwa kuishi hivyo hutakuwa na muda wa kuwachukia wengine, hutakuwa na muda wa kuwatendea ubaya wengine, hutakuwa na muda wa kushindana na yeyote bali utaishi maisha yako na kuyafurahia kwa Kila hali unayopitia na utaweka bidii kwa kufahamu pengine watoto, Wazazi,mke au mume pamoja na ndugu zako Leo pekee ndio siku unaweza kuwa nao, kwa kutambuwa muda pekee tunao miliki ni sasa kunatufanya tufurahie maisha yetu.
Makala hii imeandikwa na Mimi mwalimu Kelvin Kinyaga
kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Saturday, 4 July 2020
Hayatakuwa rahisi......
Rafiki hongera kwa siku hii nzuri, si kwamba tunaifurahia kwa sababu hatuna changamoto bali tunazo na zinatufanya tuwe imara zaidi, kubwa ni kumshukuru mungu wetu kwa Zawadi ya uhai na afya...
Rafiki yangu upo ukweli ambao unapaswa ku ufahamu kwamba pamoja na mafunzo unayoendelea kupokea na kufanyia kazi bado hutalala masikini na kuamka tajiri, mambo hayatakuwa rahisi, utahitaji kukubaliana na kutengwa,kutukanwa, kunyanyasika na kuendelea kuweka muda kwenye kile unachokipigania,anza kuwapa wengine wanachotaka bila ya kuaangalia watakupa nini kisha utapokea kile unachotaka. Safari ya mafanikio inahusisha Kila aina ya changamoto lakini pambana mpaka mwisho,kama unataka kuendelea kuwa imara zaidi basi tafuta falsafa ya kuishi nayo,kupitia falsafa ndio utaweza kuendeleza jamii.
Kama msingi ambao mwanafalsafa Seneca aliishi kwamba Kila kitu kinategemea maoni, vile ulivyo ni jinsi unavyojiona upon,acha kulalamikia wengine kwamba maoni yao kwako ndio yamekufikisha hapo bali kubali kwamba vile maisha yako yalivyo ni matokeo ya maoni uliyonayo juu yako. Hivyo anza kujipa maoni ya kwamba haijalishi utapitia kipi bado utapaswa kuwa imara Kila siku, hayo ndio maoni ya kujipa. Kile unachokihofia ndani mwake ndio kuna kitu chenye faida kwako.
Mambo hayatakuwa rahisi kwa kufanya hata kutokufanya, ila mambo yatakuwa magumu zaidi kwa kuikimbia hofu yako, je unataka kuanza biashara? Basi acha kujishauri na kujipa maoni ya kujikatisha tamaa, wewe anza na jiambie kabisa kwamba mambo hayatakuwa rahisi lakini nitakabiliana nayo yote. George Patton said "Fear kills more people than death" hofu inaua kuliko kifo chenyewe hivyo kukubali hofu ikutawale ni kukubali kufa na kusubiria siku ya kuzikwa.
Leo ni siku ya kuacha kupokea maoni ya wengine na kupuuzia maoni yako, nenda kaanze ulichopanga kufanya bila ya kuwa na hofu yoyote na kujiandaa na ugumu wowote utakaojitokeza,hilo litafanya upande ngazi ya juu zaidi kutoka hapo ulipo.
Makala hii imekufikia kupitia Mimi rafiki na mwalimu Kelvin Kinyaga.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Thursday, 2 July 2020
Unahitaji maandalizi.
Habari rafiki yangu, nikupongeze kwa siku nyingine ambayo ile bahati ya kuweza kuiona imetujia tena na hatufahamu bahati hii ni ya muda gani kutoka sasa, cha muhimu ni kujali muda na kutokubaliana upite bila kuishi kusudi ulilonalo.
Leo kwa ufupi kabisa nakukumbusha na nafahamu unafahamu hutoweza kushinda hata kama ndio hitaji lako bila ya maandalizi. Kocha mmoja aliyeitwa Bobby knight alipenda sana kuwaambia wachezaji wake "The will to win is not as important as the will to prepare to win".Kama unahitaji kushinda kweli basi tambuwa maandalizi ya kushinda ndio muhimu kuliko kitu chochote kwenye ushinda wako.
Rafiki kwa kuona umuhimu huo ndio maana napenda kukukaribisha ujiunge na kisima cha maarifa, kwani kuyasaka mafanikio ni kama kupigana vita na huwezi pigana vita peke yako unahitaji jeshi na jeshi unalopaswa kuungana nalo kwa mazoezi ya kushinda vita ya mafanikio ni Kisima cha maarifa.
Habari njema kwa wakazi wa moshi na Kilimanjaro ni kwamba kama ilivyo ratiba yetu kwa Kila Jumapili ya kwanza ya mwezi kwa wana kisima cha maarifa Tanzania tunakutana na kuweza kupeana mbinu za kushinda ikiwa na kupanga mipango yetu ya pamoja basi napenda kukuambia kwamba nina nafasi moja kwa Ajili ya wewe ambaye siyo mwana kisima cha maarifa na unaishi Kilimanjaro,karibu kwenye mkutano wetu utakaofanyika jumapili hii na utaweza kuona jinsi maandalizi ya kushinda yanavyohitaji kuwa na jeshi, nafasi ni moja pekee kama utahitaji tuwasiliane mapema.
Nikutakie siku njema na uwe wakati bora kwa maandalizi ya kufika kule unakotaka kufika.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Wednesday, 1 July 2020
Hivi ndivyo unavyoweza kukigawa kipato chako......
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na unaendelea vizuri, umeshapanga silaha zako kwa ajili ya kwenda kukamilisha yale uliyopanga kutekeleza, nami nakuongezea nyenzo maarifa ili ikusaidie kutimiza mipango yako karibu...
NINAWEZAJE KUGAWA KIPATO CHANGU?
Kila mtu anafahamu umuhimu wa bajeti, lakini pamoja na umuhimu huo changamoto zake huanzia kwenye namna ya kugawa kipato hicho kwenye mafungu, ninakumbuka miaka kadhaa iliyopita baada ya kufahamu mgawanyo wa fedha kwenye mafungu ndipo nilipogundua nilikuwa naishi kwa kuyapa umuhimu mambo yasiyo muhimu na kusahau mambo muhimu, mafungu haya matano yanakupa picha na uhalisia wa wapi umekuwa unapeleka fedha zako.
1.Fungu la kwanza ni kujilipa wewe mwenyewe kwanza.
Sehemu muhimu kabisa kupeleka fedha zako ni kutoa asilimia kumi kwa Kila kipato kinachoingia na kukitumia kukiwekeza ili kiweze kuzalisha zaidi, tumeshaona umuhimu wa fungu hili, usimlipe yeyote kabla ya kujilipa wewe kwanza.
2.Fungu la pili ni mfuko wa dharura
Fungu la pili muhimu unalopaswa kuwa nalo ni fungu la dharula, na hapa tunaposema dharura mwandishi anasisitiza iwe dharura ya kweli, michango ya sherehe siyo dharura, tunaposema dharura tuna maana kipato kikuu kinapotoweka labda kufukuzwa kazi au ugonjwa na unahitaji matibabu ndio fungu hili litatumika, chukuwa asilimia 60 ya kipato chako na dhidisha Mara sita,hicho ndio kiwango azia cha kuwa kwenye akaunti yako ya akiba kwa ajili ya dharura, ikiwa na maana utaweza kuishi kama unavyoishi sasa kwa miezi sita zaidi hata pale chanzo chako kikuu cha kipato kinapotoweka.Tenga asilimia kumi pia ya kipato chako kwa ajili ya fungu hili.
3.Fungu la tatu ni,Sadaka na utoaji mwingine.
Kulingana na imani yako Tenga asilimia kumi kwa ajili ya matoleo na Zaka na matoleo mengine kwa wenye uhitaji,kadri unavyotoa kwa ajili ya wengine ndivyo utakavyo Pokea zaidi hivyo ndivyo kanuni za asili zinavyosema.
4.Fungu la nne ni maendeleo binafsi.
Ninaposema maendeleo binafsi sina maana zile gharama za kununua vitu vya thamani unavyo vipenda, hapa unatenga sehemu ya kumi kwa ajili ya kununua vitabu vya mafunzo mbali mbali vitakavyo kupa Mwanga wa nini unapaswa kufanya, kama akili yako haijaendelea basi hakuna sehemu utakayo endelea, pia mwandishi anasema unaweza kutumia fungu hili kutembelea maeneo mazuri unayopenda, wewe pamoja na familia yako, hili litakufanya ufurahie maisha yako muda wote,hivyo fungu hili ni muhimu pia.
5.Fungu la tano ni matumizi yako.
Kama unataka kweli kujitoa kufanikiwa basi matumizi yako hayapaswi kuzidi 60 ya kipato chako, kama utatumia zaidi ya asilimia 60 basi sahau kuhusu utajiri, asilimia 60 ndio inapaswa kufanya Kila kitu, chakula, maradhi, ada za watoto, kodi ya nyumba, kununua gari,kununua samani za ndani, kulipia bili mbali mbali na matumizi mengine, utaanza kujiambia hili haliwezekani mbona kipato changu ni kidogo sana? Kitawezaje kukamilisha hayo yote? Hatua ya kwanza ni kuhakikisha matumizi yanakuwa ndani ya asilimia 60 kisha kutumia ile fedha unayojilipa mwenyewe kukiwekeza ili kukidhi mahitaji yako na siyo kujidanganya kuanza kutenga mafungu haya na kutumia chini ya asilimia 60 utakapokuwa na kipato kikubwa,huko ni kujidanganya.
Rafiki yangu nenda kaishi kwa mafungu hayo kama unahitaji kufanikiwa, mwanzo utaona hilo halitowezekana kwani mazoea yatakupa tabu, ila baada ya muda kupita utaona nguvu kubwa ya ushindi ikianza kujengeka ndani mwako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Posts (Atom)