Sunday, 5 July 2020
Mafanikio unayapimaje?
Habari za wakati huu rafiki, wiki lingine limekatika, hii ina maanisha ule mwaka tuliojiambia ni mpya ndio unaelekea ukingoni je ni kipi ulipanga kufanya kwa mwaka huu?je ulishaanza kufanya? Umekutana na magumu gani ya kukufanya usiendelee? Je umejiambia huu ni mwaka mbaya hivyo mipango yako umehahirisha mpaka mwaka mwingine? Basi kufanya hivyo ni kujiandaa kushindwa.
Leo nataka tuone usahihi wa neno mafanikio, Kila mtu anaweza kuelezea kwa namna yake anavyoona ni sahihi, leo nitakuelezea kwa namna wastoa wanavyoweza kuelezea maana ya mafanikio, kwanini nimependa kukushirikisha hili? Tafsiri hii itakufanya ufurahie maisha yako muda wote na siyo zile tafsiri ambazo wao wanaziita tafsiri za kitoto,tafsiri ya kupima mafanikio kwa Mali au fedha si kwamba tafsiri hii siyo sahihi pekee bali ni tafsiri itakayokufanya uhahirishe Kila siku yako kuishi ukijiambia utafurahia siku ukiwa na nyumba yako, unapata nyumba bado unaona huyafurahi mafanikio hayo kama ulivyodhani, unajiambia ukimiliki gari utakuwa na maisha mazuri na kufurahia, unapambana unalipata lakini unagundua huna furaha kama ulivyodhani, hapa ndipo tafsiri hii ya kifalsafa inapokuwa bora muda wote na itakufanya utenganishe mambo ya nje na maisha yako ya Kila siku, vipimo visivyo sahihi ndivyo vinakufanya ukose furaha ya kweli kwenye maisha yako na kuacha kufurahia, uwe na fedha au usiwe nazo uweze kufurahiakufurahia na kuishi kwa kusudi.
Kwanza unapaswa kufahamu maisha ni mchakato, Mwanafalsafa Ryan Holiday anasema "The definition of success is Autonomy" vile unavyoweza kuitawala siku yako moja ambayo ni leo kwa kutambuwa lililopita huwezi kulibadili na kesho huwezi kuimiliki kwani hujuwi nini kinaweza kutokea kunakufanya uishi kikamilifu, anza kuweka nguvu zako zote kwenye siku yako na ichukulie siku hiyo kama ndio nafasi ya mwisho kwako kuishi, weka ubunifu wako kwenye siku yako, Kila unapopata wazo la kujiambia utafanya kesho jiambie kesho naweza nisiamke je kwanini nisifanye sasa hivi ambayo ndio siku yangu kuishi. Kama ni watu walio nizunguka ni upendo kiasi gani naweza kuwaonyesha sasa hivi kwa kutambuwa kesho naweza nisiwepo, huwa tunashindwa kuishi Leo vizuri kwa kujidanganya kwamba kesho nitakuwa na gari, mwakani nitakuwa na nyumba yangu ndio nitafurahia ni kuchaguwa kushindwa kwani kadri unavyofikia kile unachojiambia utakifurahia ukikifikia unagundua kipo kingine bora zaidi na hivyo ndivyo unavyohahirisha kuishi na unapishana na mafanikio.
Mwanafalsafa wa kistoa Marcus Aurelius anasema maneno haya "Today I escaped auxiety or no,I discarded it,because it was within me,in my own perceptions not outside" kauli hii inatutaka tutambuwe kwamba umiliki pekee wa kitu chochote ni wa sasa hivi, mali, fedha na watu tunao wapenda uhakika wa kuendelea kuwa nao ni wa muda ulio nao pekee, usijiambie nitafanya nikiwa na...... Au nitafurahia nikiwa na .......,hapo ni kuchaguwa kutokuishi.
Kila siku nenda kaishi kikamilifu na acha kuangalia matokeo yoyote kwani wastoa hufurahia chochote anachopitia, matatizo, changamoto mbali mbali siyo vitu vya kututenga na furaha na kutufanya tusiishi kwa upendo kwani kwa kuvipokea au kutovipokea hakubadilishi ukweli wa kwamba Kila mtu atavipitia, hivyo Kila siku ishi kwa usahihi, tenda wema na ona huna nafasi nyingine, pamoja na kuichukulia siku yako kama siku ya mwisho haina maana kwamba usiweke kazi, jitoe na kubaliana na matokeo yoyote utakayopata kwenye siku yako na unapopata siku nyingine ya ziada anza kushukuru na kujiambia nimepewa siku hii nyingine ili nikamilishe yale ambayo Jana sikuyakamilisha na sitoongezewa siku nyingine.
Kwa kuishi hivyo hutakuwa na muda wa kuwachukia wengine, hutakuwa na muda wa kuwatendea ubaya wengine, hutakuwa na muda wa kushindana na yeyote bali utaishi maisha yako na kuyafurahia kwa Kila hali unayopitia na utaweka bidii kwa kufahamu pengine watoto, Wazazi,mke au mume pamoja na ndugu zako Leo pekee ndio siku unaweza kuwa nao, kwa kutambuwa muda pekee tunao miliki ni sasa kunatufanya tufurahie maisha yetu.
Makala hii imeandikwa na Mimi mwalimu Kelvin Kinyaga
kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment