Monday, 27 July 2020

Ustawi wa fikra Monday, 27 July 2020 *Na hivi ndivyo kodi ilivyoanza........* Habari za wakati huu rafiki, asubuhi ya wiki lingine na nina imani umejipanga kuiendea siku hii kwa kufanya zaidi ya pale ulipofanya kwenye wiki lililoisha, kwani kama utafanya vile vile na kutokwenda hatua ya zaidi usitegemee kupata matokeo ya tofauti na uliyopata wiki iliyopita. Leo rafiki tuangalie historia ya kodi, kama upo serikalini unakatwa kodi, kama una biashara zako unakatwa kodi, kama huna kazi maalumu bado utalipa Kodi wakati ukihitaji huduma, Je nini chanzo cha kodi? Kwanini unalipa kodi? Rich dad alikuwa akiendelea na darasa lake na Leo anatufundisha historia ya kodi, anasema wakati wapo shule kuna mwalimu aliwaelezea habari za Robin Hood,mtu ambaye mwalimu huyo alimuelezea Robin kuwa mtu shujaa aliyewaibia matajiri vitu na kuwapa masikini, rich dad anasema yeye kwa upande wake alimuona Robin kama kibaka tu kwa kitendo chake hicho, anasema ingawa sasa Robin hayupo lakini watu wenye mtazamo kama wa Robin wapo na wanapenda kuona matajiri wanastahili kulipa kodi kubwa lakini ni kinyume chake. Miaka ya 1799-1816 Uingereza walitoa pendekezo la wananchi wake kulipa kodi ili kuiwezesha nchi yao kushinda kwenye vita, Marekani nao kwenye miaka ya 1861-1865 walitumia mbinu hiyo ya uingereza kuweza kusaidia taifa lao kushinda vita, baadaye kwenye mwaka wa 1874 uingereza waliweka sheria ya ulipaji wa kodi kuwa ni sehemu ya waingereza matajiri, Marekani nao mwaka 1913 walipitisha sheria hiyo, mwanzo raia wa nchi hizi waliaminishwa kwamba kodi ni kwa watu matajiri pekee na wao halitawahusu lakini kadri serikali zilivyokuwa ndivyo kodi zilipanuliwa na kuwafikia mpaka watu wa chini na sasa hivi Tabaka la kati na masikini wanalipa kodi zaidi ya matajiri, kwani matajiri wamewazidi ujanja wasomi, kivipi? *The power of corporation* Ni kupitia nguvu ya mashirika na makampuni ndipo matajiri wameweza kuizidi serikali kwenye kulipa kodi, hivi unafahamu mtu anayemiliki kampuni analipa kodi ndogo kuliko mtu anayemiliki biashara binafsi? Je unafahamu Leo kama una kampuni ukiwa na madeni au kuhitajika kufilisiwa Mali zako binafsi haziguswi isipokuwa kampuni yako pekee? Na kampuni ni karatasi linalotambulika kisheria na kupitia makampuni ndipo serikali na wasomi wamezidiwa ujanja na matajiri. Robert anasema hulipa kodi zaidi kwa sababu wao wanachofahamu ni kuamka na kwenda kazini na kipato kinapoongezeka na kodi inaongezeka pia, Robert anasema poor dad alimshauri akiwa mkubwa ahakikishe anapata kazi kwenye shirika zuri na kisha apande kazi taratibu mpaka kufika ngazi za juu, alipomweleza swala hilo Rich dad akamwambia kwanini usubirie kupandishwa ngazi? Kwanini usitengeneze ngazi yako mwenyewe? Hapa ni Sawa na sasa kuweka bidii kazini ili upandishwe vyeo ni kwanini usijiajiri na kuwa na kampuni yako mwenyewe? Robert anatuambia akiwa bado kwenye ajira mwaka 1974 alifuata ushauri wa baba tajiri na kuanzisha kampuni yake ya kwanza.Kampuni ya kuuza na kupangisha nyumba, anasema mwanzo kodi zilikuwa kubwa zaidi lakini baadaye alianza kuona ushauri wa baba tajiri ukifanya kazi na ndipo kupitia faida kutoka kwenye kampuni yake hii aliweza kununua gari lake la kwanza la kutembelea. Rafiki unahitaji kufahamu hesabu za fedha, kufahamu fedha unayopata na kuitumia kama mbegu kwa kununua ASSET na kupitia hilo utaweza kuzalisha na kupata fedha zaidi, Pia unahitaji kufanya uwekezaji ili fedha ikufanyie kazi, Pia utahitaji kulifahamu soko vizuri ili uweze kuuza zaidi na mwisho utahitaji kufahamu sheria ili ujuwe ni vipi utaweza kupata unafuu kwenye kodi na maisha kwa ujumla ili uwe na maisha bora. Rafiki kwa Leo tuishie hapa, nikutakie siku njema; Makala hii imeandaliwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga,mwanafunzi wa jinsi fedha inaweza kunifanyia kazi kupitia kupitia chuo cha Kisima cha maarifa, tuko pamoja na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogsport.com 0712161251/0763766944

No comments:

Post a Comment