Tuesday, 7 July 2020
Tiba ya tatu ya mifuko iliyo sinyaa....
Rafiki yangu karibu tena kwenye ukurasa huu wa ustawi wa fikra,tujifunze pamoja na kuweka kwenye matendo yale tutakayojifunza hapa, Nina hakika yatakusaidia ndio maana ukiwa kama ndugu na rafiki yangu Kila siku nimebeba jukumu la kukuandikia kwasababu nina uhakika wa nguvu iliyopo kwenye maarifa haya, siku nilipofahamu maarifa yana nguvu kuliko fedha ndio nilipoamua kutumia fedha kuyapata na baada ya kuyapata nimejipa jukumu la kukupatia wewe maarifa haya bure, bure hii usiitumie kuyapuuza kwani kuna siku utanitafuta kwa fedha na itakuwa ngumu kunipata....
Leo tunaendelea na uchambuzi wa kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu kinachokupa misingi sahihi ya kifedha, baada ya wiki kadhaa zilizopita kujifunza tiba ya kwanza ya kutenga Kila sehemu ya kumi ya kipato chako kinachoingia naTiba ya pili ya kudhibiti matumizi yako basi kitakacho jitokeza utaanza kuona mifuko yako iliyo sinyaa inaanza kutuna na kuongezeka na hapa ndipo tunaenda kujifunza tiba ya tatu.
Tiba ya tatu ya mifuko iliyo sinyaa ni KUIFANYA AKIBA YAKO IZAE ZAIDI.
Arkadi alianza kufundisha siku ya tatu kwa kuwaeleza namna alivyopoteza uwekezaji wake wa kwanza kwa mfyatua matofari lakini uwekezaji wa pili aliowekeza kwa mkopeshaji wa fedha na kisha kugawana faida ndio safari yake ya utajiri ilipoanzia na ndipo fedha ilipoanza kumfanyia kazi, aliweza kuitumia akiba yake kuwekeza maeneo mbali mbali yanayozalisha na akaupata utajiri.
Arkadi anasema utajiri wa mtu haupo kwenye fedha alizobeba kwenye mfuko wake bali kwenye uzalishaji unaofanyika na fedha zake.hapo ndipo kipato chake kitaweza kukua na kufikia utajiri. Akawaeleza kwamba kwa njia hiyo ndio kipato chake kimeweza kuwa mtumwa wake na kumfanyia kazi yeye.
Kwenye kitabu hiki kuna simulizi ya mkulima mmoja aliyepata Mtoto na kuamua kuwekeza kwa ajili ya Mtoto wake aliyezaliwa. Alichukuwa vipande kumi vya fedha na kumpatia mkopeshaji na kumwambia aviweke mpaka mwanae atakapokua na kuzihitaji. Na walikubaliana atapata robo ya kiwango kitakachokuwepo kwa Kila baada ya miaka minne kupita. Baada ya kupita miaka 25 mkulima alikwenda na kukuta vipande vimekuwa na kufikia vipande thelathini na moja na nusu, kwakuwa mwanae hakuviitaji vipande hivyo kwa wakati huo aliamua kuviacha viendelee kukua, baada ya kijana yule kufikisha miaka 50 alikuta vimekua na kufikia vipande 167,zaidi ya Mara 17 ya kiwango alichoweka cha vipande 10.Hivyo ndivyo Arkadi alipomalizia Tiba ya tatu kwa kuwaambia kama unataka utajiri basi Kila fedha unayopata tenga sehemu itakayokwenda kukuzalishia na kukufanyia kazi.
Rafiki kwa kupitia hayo tunajifunza kwamba uwekezaji ni kitu ambacho kinahitaji mtu asiye na papara ya fedha, kama unahitaji kunufaika na uwekezaji usiwe mtu wa kuangalia faida ya muda mfupi, lazima uweke muda wa miaka mingi na hapo utapata manufaa makubwa, hebu jiulize kama serikali wanachukuwa sehemu ya kipato chako na kukitumia kuwekeza na mwisho wa siku kukulipa pensheni nguvu zikikuishia na wakati mwingine kuona watu waakilalamika kwamba wameibiwa je kwanini usitumie uwekezaji kujitengenezea pensheni yako ya uhakika? Nenda kazifanyie kazi tiba hizi ulizojifunza Mara moja na Nina hakika utaanza kuona manufaa yake, tukutane wiki ijayo kwa ajili ya tiba zingine zilizobaki.
Kelvin Kinyaga ndio majina yangu, Mwl na mwandishi wa mfululizo wa makala hizi, nakupenda rafiki na nikutakie siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment