Tuesday, 7 July 2020

Huwezi fika usiko kuona....



Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka u buheri wa afya, hongera kwa siku nyingine ambayo umeipata tena,Zawadi kubwa sana kwetu kuweza kuifikia siku hii.

Leo kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH tutajifunza mambo matatu muhimu kuyatumia kama ngazi ili kufika kule unakotaka kufika.

Mwandishi anasema kitu kikubwa ambacho kinawakwamisha watu wengi ni kutokuwa na picha au mtazamo mpana wa kufanikiwa, wengi wanawaza maisha ya kawaida sana, nikiwa na watoto Wangu, wakasoma shule nzuri, tukajenga nyumba yetu na kununua gari hayo ndio mawazo ya kiwango cha juu kwa walio wengi, na kweli wanafikia ndoto hizo na kufa bila ya kuacha alama hapa duniani.

Rafiki unaweza kuona huhitaji tamaa zaidi ya kupata pesa, lakini huoni kwamba kujiwazia wewe peke yako ni ubinafsi mkubwa sana? Hebu waza mafanikio makubwa na ona kuna wengi wanahitaji msaada wako na kwa kuwaza hivyo hata mungu anakwenda kubariki kazi zako, zifuatazo ni njia tatu unazoweza kuzitumia ili kufikia kiwango cha juu ki mtazamo na kupiga hatua kwenye maisha yako.

1.Hatua ya kwanza ni KUPATA MAARIFA, rafiki kupitia maarifa utabadili mtazamo wako kwa kuwaza mambo ya viwango vya juu, Kila siku utakuwa na shauku ya kufikia mafanikio ya juu sana, kupitia maarifa utajifunza mbinu nyingi walizotumia wengine kufanikiwa, kupitia maarifa utaepukana na makosa mengi ambayo kwenye vitabu wengine waliyafanya na kuanguka hivyo wewe kutofanya walichofanya wao.

2.Hatua ya pili ni KUTUMIA UZOEFU WAKO,rafiki kwa kujaribu vitu vipya Kila siku tunapata uzoefu na kubuni mambo mapya, watu wengi hawafahamu kwamba ni kwa kupitia makosa waliyofanya kwa kujaribu na kushindwa basi wanapata uzoefu mkubwa sana na hilo linakuwa kama ngazi kwao kutumia kufanikiwa, hivyo kama ulijaribu kitu kipya na kushindwa basi kaa chini na jiulize nilikosea wapi na sasa nirekebishe ili kufika ninakotaka kufika? Lakini ukianza kuona mambo magumu na kuamua kuishi kwa mazoea basi utabakia hapo hapo.

3.Hatua ya tatu ni KUFANYA UCHUNGUZI WAKO MWENYEWE, watu wengi wanawaza makubwa sana lakini hupenda kusikiliza mawazo ya wengine bila ya kufanya uchunguzi, Leo utapokea maoni ya mtu alishindwa kwenye jambo fulani na kukubaliana naye kirahisi kwa sababu alizokupa, lakini ukichunguza ki undani utaona kuna makosa ya wazi mtu huyo alifanya yakamtenganisha na kile anachotaka, sikiliza sababu ila usikubaliane nazo kirahisi.

Rafiki anza kujijengea msingi wa kupata maarifa, tumia uzoefu kwa kujaribu vitu vipya na chunguza kile unachotaka kufanya na hilo litakuwa kama ngazi ya kupanda ili Mimi na wewe zitufikishe kule ambapo tunapaswa kuanza kupaona kuanzia sasa.

Kelvin Kinyaga ndio majina yangu niliyopewa na Wazazi Wangu, kufundisha ndio taaluma yangu na nitafanya hivyo siku zote za maisha yangu.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment