Sunday, 19 July 2020
Usisubirie ufukuzwe kazi ndipo ugundue nyumba yako unayoishi siyo mali inayozalisha (Assets).......
Hongera ndugu yangu, siku nyingine na tunakwenda kuanza juma lingine kwa nguvu ile ile, pamoja na matokeo kidogo unayopata kwenye kile unachojishughulisha nacho bado una jukumu la kwenda mbele, kuweka kazi bila kurudi nyuma.......
Leo tutakwenda kuangalia sehemu nyingine ya kutupeleka kwenye utajiri kwa kupata ushauri wa baba tajiri, kabla hatujafika huko tumalizie mjadala wetu wa nyumba yako ya kuishi siyo mali inayozalisha kwa kusema hivi, waza umefukuzwa kazi Leo na huna chanzo chochote cha fedha na una nyumba yako unaishi na familia yako je nyumba hiyo itakusaidia kuondokana na adha ya kulipa kodi lakini haitakulisha, haitalipia ada za watoto wako shule na kufanya maisha yako kuendelea kama yalivyo sasa, mwandishi anasema watu hawaoni na kukubaliana na hili mpaka pale wanapoamua kuacha kazi au wakiachishwa kazi ndipo hukimbilia kuuza nyumba zao kwa bei ya chini na kutafuta kuwekeza kwenye maeneo yanayozalisha na wakati mwingine huwekeza sehemu wasizo zijuwa vizuri kutokana na hali za kuchanganyikiwa wanazokuwa nazo. Hapa ndipo anakuja na funzo la kwamba FANYA BIASHARA UNAYOIFAHAMU VIZURI.
Robert anatuambia akiwa mdogo baba masikini alimshauri kutafuta kazi inayolipa vizuri na baba tajiri alimshauri kuanza kuwekeza mapema ili ajipatie Uhuru kifedha, Je wewe Wazazi wako walikushauri mini?Na Je wewe unawashauri nini watoto zako? Je ni ushauri wa mama au baba tajiri au masikini? Jipe mwenyewe majibu ya maswali haya.
Mwandishi anasema matatizo ya fedha hutokana na watu kuwafanyia kazi watu wengine kwa muda mrefu bila kufahamu hatima yao. Anasema yote haya hutokana na mfumo wa elimu kuandaa watu kwa namna hiyo na siyo kuwafanya wafikie Uhuru wa kifedha. Watu wengi hujifunza taaluma mbali mbali na wanapoajiriwa wanafanyia kazi taaluma zao na anashangaa pale anapomuuliza mtu unafanya kazi gani anamjibu "Banker",akimuuliza unamiliki benki? Anajibu hapana.
Mwandishi anasema pamoja na kwamba umeajiriwa bado unahitaji kufanya biashara, watu hawataki kufanya biashara kwasababu ya hatari ya kupoteza fedha zao na hilo linawafanya kukubali kuishi kwenye utumwa wa kuajiriwa na kulipwa kidogo maisha yao yote. Hivyo anza Leo kufikiria ni biashara gani unapenda kufanya na jitaidi ujifunze kwa kina na kuijua ndipo uingie kwenye biashara hiyo, Anasema yeye alipenda sana majengo ndio maana aliamua kununua nyumba na kuzipandisha thamani halafu kuziuza kwa bei ya juu na kuwekeza kwenye makampuni kwani ndio maeneo aliyopenda, Je wewe unapenda nini? Chugua Leo na anza kujifunza kuwekeza huko na pambana uweze kufikia maeneo yafuatayo ki uwekezaji.
1.Biashara ambayo haihitaji uwepo wako moja kwa moja, kwani wengi ni watumwa wa biashara zao, kwani wasipokuwepo na biashara zao zinakufa.
2.Anza kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa, vipande na aina nyingine za dhamana na fedha
3.Uwekezaji kwenye nyumba za kupangisha au kuuza, hapa naona mwandishi alitengeneza mfumo mzuri sana wa kutambuwa wapi anapangisha na wapi ananunua na kupandisha thamani na kuuza na hilo limemsaidia kufikia utajiri mkubwa.
Rafiki bilashaka umeendelea kujifunza na umeondoka na kitu, acha kununua vitu visivyo zalisha kwa pesa yako, nunua nyumba ya kuishi, gari la kutembelea na vitu vya kifahari kupitia faida uliyopata kutoka kwenye uwekezaji uliofanya na ukifanyia kazi hili,Mimi na wewe tutakutana sehemu nzuri ki uchumi na kupongezena, ufukara siyo kitu cha kujivunia.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kwenye chuo cha Kisima cha maarifa, endelea kutembelea blog yangu na tuwasiliane kwa ushauri wowote kwani nazungukwa na wengi, asante.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment