Sunday, 5 July 2020

Hizi hapa sababu za kwanini nyumba yako ya kuishi siyo Asset.....


Rafiki yangu Mimi na wewe tuna Kila sababu kuanza juma hili kwa kumshukuru mungu, kwanza kwa afya na uzima, kwa kutupa nafasi ya kuzungukwa na familia pamoja na marafiki wazuri kama wewe,kwa kutupatia matajiri wanaolipa kodi zinazotumika kutupatia huduma muhimu, lakini tunamshukuru mungu hata kwa maadui zetu pamoja na watu wanao tuchukia, kupitia wao kunatukumbusha kwamba sisi ni wa bahati sana kutojengwa kwa misingi ya chuki kwani tumependelewa kwa kumpenda Kila mtu na tunaishi kwa furaha, tunaowaita maadui zetu wakati mwingine wanatuonyesha makosa yetu huku tunaowaita marafiki wakijaribu kufunika makosa yetu kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kama waswahili wanavyosema, hayo ni machache ya kupongeza lakini yapo mengi sana ya kushukuru......

Rafiki yangu tunaendelea na uchambuzi wa kitabu chetu cha Rich dad,poor dad.Wiki iliyopita tofauti kati ya Assets(mali inayozalisha)na Liabilities(Mali isiyo zalisha)mwandishi alielezea kwa mapana sana dhana hizo mbili kwa kumtumia baba tajiri, aliweza kutumia mchoro wa kwanza ukionyesha mzunguko wake wa fedha ni husubiria kipato na akikipata kinakwenda moja kwa moja kwenye matumizi, hivyo kinakwisha na kubaki hana kitu na kuishi kusubiria kipato kingine tena, wakati mzunguko wa fedha wa matajiri fedha ikitoka kwenye mapato inakwenda moja kwa moja kununua Mali inayozalisha na baada ya faida anayopata ndipo hugawa kiasi kwenda kwenye matumizi na kingine kubaki kikizalisha zaidi.

Leo tutaangalia nyumba zetu za kuishi ziko upande upi? Ni Mali inayozalisha au haizalishi? Mwandishi hakubaliani na namna ya neno "assets" na "liability" ilivyoelezewa kwenye dictionary na anasema ukitaka kuchanganyikiwa basi fuata maana ya kwenye dictionary, anasema maana iliyotolewa ni nzuri kwa kufundishia na imewalenga tabaka la juu ila siyo kwa watu wenye kipato cha wastani na cha chini. Mwandishi anajaribu kutuonyesha namna watu wanavyo amua kununua au kujenga nyumba kwa fedha za mkopo na kujikuta wakiishi mbio za panya za kupata kipato na kulipa madeni maisha yao yote.

Anasema rafiki yake hupenda kusema Msemo huu,na mnukuu "If you find you have dug your self into a hole...... Stop digging" akimaanisha unapojikuta umetumbukia kwenye shimo hatua ya kwanza ni kuacha kuchimba zaidi, hivyo ukijikuta kwenye shimo la madeni hatua ya kwanza kuchukuwa ni kuacha kukopa, lakini kwa watu wengi kwa kuamini nyumba ni Assets hujikuta wakiishi maisha ya mateso kwa maisha yao yote. Anasema siku moja alibishana na baba yake (poor dad) kwamba nyumba yao ni assets au liability, anasema akiwa na miaka 16 lakini baba huyu masikini na elimu yake kubwa Darasani ila elimu ya fedha yeye alimzidi. Kadri nyumba inavyokuwa kubwa na gharama za Maji, Umeme,samani na hata kodi ya jengo inakuwa kubwa, Robert anasema mpaka sasa bado watu wengi wanampinga akiwaambia nyumba siyo assets.

Haya hapa ni makosa makubwa matatatu ya kuwekeza kwenye nyumba ambayo haizalishi;

1.Unaishi maisha yako yote kulipa deni la nyumba.

2.Nyumba haiongezeki thamani kwa kasi.

3.Unakosa fursa zingine ambazo ungezitumia kuwekeza na kuzalishia badala yake unachimbia fedha zako kwenye nyumba.

Rafiki wajapani wanafahamu nguvu ya dunia sasa hutokana na sehemu tatu ambazo ni Siraha, fedha na akili na Kila taifa linapambana kuwa na vitu hivyo, hakikisha siku haipiti bila ya kujifunza, uwe na siku njema.

Makala hii imeandikwa na Mwl Kelvin Kinyaga

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment