Saturday, 4 July 2020
Hayatakuwa rahisi......
Rafiki hongera kwa siku hii nzuri, si kwamba tunaifurahia kwa sababu hatuna changamoto bali tunazo na zinatufanya tuwe imara zaidi, kubwa ni kumshukuru mungu wetu kwa Zawadi ya uhai na afya...
Rafiki yangu upo ukweli ambao unapaswa ku ufahamu kwamba pamoja na mafunzo unayoendelea kupokea na kufanyia kazi bado hutalala masikini na kuamka tajiri, mambo hayatakuwa rahisi, utahitaji kukubaliana na kutengwa,kutukanwa, kunyanyasika na kuendelea kuweka muda kwenye kile unachokipigania,anza kuwapa wengine wanachotaka bila ya kuaangalia watakupa nini kisha utapokea kile unachotaka. Safari ya mafanikio inahusisha Kila aina ya changamoto lakini pambana mpaka mwisho,kama unataka kuendelea kuwa imara zaidi basi tafuta falsafa ya kuishi nayo,kupitia falsafa ndio utaweza kuendeleza jamii.
Kama msingi ambao mwanafalsafa Seneca aliishi kwamba Kila kitu kinategemea maoni, vile ulivyo ni jinsi unavyojiona upon,acha kulalamikia wengine kwamba maoni yao kwako ndio yamekufikisha hapo bali kubali kwamba vile maisha yako yalivyo ni matokeo ya maoni uliyonayo juu yako. Hivyo anza kujipa maoni ya kwamba haijalishi utapitia kipi bado utapaswa kuwa imara Kila siku, hayo ndio maoni ya kujipa. Kile unachokihofia ndani mwake ndio kuna kitu chenye faida kwako.
Mambo hayatakuwa rahisi kwa kufanya hata kutokufanya, ila mambo yatakuwa magumu zaidi kwa kuikimbia hofu yako, je unataka kuanza biashara? Basi acha kujishauri na kujipa maoni ya kujikatisha tamaa, wewe anza na jiambie kabisa kwamba mambo hayatakuwa rahisi lakini nitakabiliana nayo yote. George Patton said "Fear kills more people than death" hofu inaua kuliko kifo chenyewe hivyo kukubali hofu ikutawale ni kukubali kufa na kusubiria siku ya kuzikwa.
Leo ni siku ya kuacha kupokea maoni ya wengine na kupuuzia maoni yako, nenda kaanze ulichopanga kufanya bila ya kuwa na hofu yoyote na kujiandaa na ugumu wowote utakaojitokeza,hilo litafanya upande ngazi ya juu zaidi kutoka hapo ulipo.
Makala hii imekufikia kupitia Mimi rafiki na mwalimu Kelvin Kinyaga.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment