Thursday, 16 July 2020
Siyo kuwa wa kwanza bali kwa ubora upi?
Rafiki habari za wakati huu, hongera tena kwa kuweza kuchaguliwa kuifikia siku hii, nina imani umeamka na nguvu ya kwenda kuweka kazi zaidi ili upate matokeo zaidi.
Leo kwenye ukurasa wa Ijumaa kutoka kwenye mfululizo wa makala za ustawi wa fikra tutaendelea kuangalia maisha ya falsafa, labda nikuambie kitu rafiki kama huna falsafa unayoishi basi tambuwa uko kwenye hatari kubwa ya kutofika kwenye kile ulichopanga, kuna watu wanaishi misingi yao pasipofahamu kwamba hiyo ndio falsafa na wakivunja misingi waliyojiwekea lazima waazibiwe. Leo kwenye falsafa tunakumbushwa maneno yanayosomeka.
"Slow is smooth, smooth is fast"
Maneno haya yanatukumbusha kwamba chochote unachokitaka kiwe rahisi basi kitapatikana pole pole na urahisi huo ukiwepo ndio kitakufanya ufanikiwe haraka na kwa wepesi, Msemo huu unataka kutuaminisha kwamba maisha ya haraka hayana maana kwetu na kama unataka mafanikio ya kweli basi lazima uweke nguvu na bidii kwa muda mrefu, lakini kwa tulio wengi tunataka matokeo ya haraka,tunataka biashara zetu ziwe kubwa kwa muda mfupi na ndio maana tunashindwa haraka sana na kukata tamaa ya kuendelea na kuanza tena lingine na kushindwa tena na maisha yanaendelea hivyo.
Leo falsafa inatutaka kwanza kufahamu nini tunafanya, mbili kwanini tunafanya? kivipi tunafanya? Na hapo ndio kile tunachofanya kitafanikiwa kwa haraka zaidi, kama unafanya biashara na hufahamu biashara hiyo ki undani, na kwanini unafanya biashara hiyo? Labda ni msukumo wa kupata fedha pekee na huduma unayotoa ni mbovu na unaifanya kwa mazoea bila ubunifu lazima ife, hivyo anza kuwaza miaka kumi unataka uwe umefika wapi kwenye kile unachofanya.
Wanajeshi wana Msemo wao unasema hivi "More haste, less speed,better a safe commander than bold" hivi ni kipi bora? Kwenda kwa tahadhali na kuwa salama au kuwa na haraka na kuwa mateka? Hivyo kama unataka haraka basi utaipata kwa kuweka umakini kwa kwa kwenda polepole, kwani kadri unavyoitaka haraka ndivyo unavyochelewa na kadri unavyokuwa na kusudi na kulifanyia kazi taratibu ndipo tunapolifikia kwa haraka na wepesi.
Acha kuchanganyikiwa ukiona wengine wanafanikiwa haraka, muhimu ni kufahamu nini unataka kujenga na jifunze ni kwa namna gani utafika pale unapotaka kufika. Ubora ndio muhimu na siyo haraka, nenda kalifanyie kazi hili na acha kuwaza uharaka waza ubora.
Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.kelvin Kinyaga
Wiki hii nimepata kitabu kutoka kwa rafiki yangu Dr.Raymond Mgeni,kitabu hiki kinahusu mazoezi 20 ya falsafa ya Ustoa, hivyo Kila ijumaa nitakuletea zoezi moja la kufanyia kazi wiki nzima. Asanteni sana.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251/0163766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment