Saturday, 25 July 2020

Maswali 12 ya kujiuliza kila siku na yatakwenda kubadilisha maisha yako......


Rafiki yangu kama unaishi na huna kipimo unachotumia kupima maisha yako kama unakua au hukui basi huna maisha,kwani maisha yasiyo pimwa hayafahi kuishi......

Kwanza kabisa nakusalimia rafiki wa ustawi wa fikra, ningekuwa nimeipoteza siku hii na kutoishi kama ingepita sijakuandikia, ninachokuandikia hapa ni kitu ambacho kimenitafakarisha sana leo, Kama ni msomaji wa falsafa na vitabu vingi huwezi niambia humfahamu RYAN HOLIDAY,Leo kupitia kurasa yake anatuletea Zawadi ya maswali kumi na mbili ambayo Kila binadamu anayetaka kufahamu kusudi la maisha yake anapaswa kujiuliza, karibu tuyasome pamoja, lengo ni kujipa majibu sahihi ya maswali haya, kaa chini na jipe majibu sahihi...

*1.Who do you spend time with?*
Hebu jiulize muda wako mwingi unatumia na nani? Goethe would say "Tell me who you spend time with and I Will tell you who you are".Msemo huu unatuambia kama ukitaka kumfahamu mtu alivyo basi angalia watu wanao mzunguka, rafiki yangu kama umezungukwa na watu walio kata tamaa basi tambuwa huwezi kuwa shujaa, kama muda mwingi unautumia na watu wanaolalamika basi huwezi acha kulalamika, kama wanaokuzunguka ni watu wa kushindwa basi na wewe utashindwa, hebu Leo amua kusikiliza na kujihusisha na washindi na kataa kabisa na watu wanao kuambia maisha ni magumu na hayawezekani, jiulize kama walio kuzunguka wanakuinua au kukushusha?

*2.Is this in my control?*
Jiulize kama unalohangaika nalo liko ndani ya uwezo wako au? Kutaka Kila mtu akupende ni jambo lililo nje ya uwezo wako, kumridhisha Kila mtu ni kupoteza muda wako, kufikiria wengine watanionaje nalo liko nje ya uwezo wako, kuishi kwa furaha ni jambo ambalo Kila binadamu ana uwezo nalo hivyo kabla hujakubali lolote likusumbuwe jiulize je lipo ndani ya uwezo Wangu? Acha kuangalia maoni ya wengine yanayokurudisha nyuma, we Fanya yako.

*3.What does your ideal day look like?*
Siku unayoishi Leo ndio itaamua kesho yako, acha kujidanganya kwamba miaka miwili, mitano au kumi nitakuwa nimefanya maendeleo makubwa wakati Leo yako hujuwi unakwenda kufanya nini? Ifahamu Leo yako na pambana nayo kwa Kila hali na Mali na hilo litaifanya kesho yako kuwa bora, hakika ni Leo yako na siyo kesho yako, kwani kesho yako itaamuliwa na Leo yako.

*4.To be or to do?*
Watu wengi tunaangalia matokeo ya nje kwa walio fanikiwa na kutamani kuwa kama wao, lakini mbaya zaidi hatupo tayari kuishi kwa vitendo yale wanayofanya, muda mwingi unatumia kujadili maisha ya wengine, kutizama tamthilia na kubishana siasa kisha kujiambia Kila siku unataka kuwa kama mtu fulani mwenye mafanikio, chaguwa kufanya na kuweka kazi na siyo kuendelea kuishi maisha ya kutamani bila ya kuweka kazi.

*5.If I am not for me,who is?If I am only for me,who am I?*
Rafiki siyo vibaya kufanya kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya familia yako na ndugu zako, lakini kama hicho ndio kitu pekee umekuja kufanya duniani basi maisha yako hayana maana yoyote, Kila unachojishughulisha nacho basi kifanye kwa ajili ya wengine na hapo utakuwa na maisha ya maana, ona una jukumu la kusaidia wengine na hapo utakuwa na maisha ya utoshelevu.

*6.What am I missing by choosing to worry or be afraid?*
Kila unapohisi hofu ikikujia jiulize ni kipi nimepanga kukikosa nikichaguwa hofu initawale? Gavin de Beycer writes "when you worry ask your self "what am I choosing to not see right now? Kauli hii inatuambia kwa kuishi maisha ya kuhofu ni Sawa na kuamua kufumba macho tusione wakati macho yetu ni mazima, fursa nyingi sana zinatupita kwakuchaguwa maisha ya kujiambia nikifanya biashara nitapata hasara, nikiacha kazi nitaishije? Na wakati tumeipa hofu itutawale ndipo fursa nyingi zinatupita na kubaki na maisha yetu yasiyo na tija yoyote.

*7.Am I doing my Job?*
Kila unapofanya jambo lolote jiulize kama hiyo ndio kazi yako, unaposengenya wengine jiulize hii ndio kazi yangu?fahamu kazi yako unayopaswa kuifanya na hakikisha unaikamilisha ipasavyo, kazi yako siyo umbeya lakini ndio muda mwingi unatumia kufanya umbeya, kazi yako siyo mpira lakini muda mwingi unautumia kubishania mpira, wewe siyo mwanasiasa lakini muda mwingi unazungumzia siasa.

*8.What is the most important thing?*
Kama hufahamu kitu gani muhimu sana kwako basi utajikuta unaishi maisha ya wengine na kuachana na yako, lazima ujiulize ni kipi muhimu zaidi kwenye maisha yako na hakiisha unakifanya na kukifikia na achana na vingine visivyo muhimu.

*9.Who is this for?*
Swali unalopaswa kujiuliza ni kwanini unafanya unachofanya? Kwanini naandika? Kwanini nawauzia watu? kwanini najifunza Kila siku? Watu wengi wanafanya kwasababu wameona na wengine wanafanya lakini hawana sababu za muhimu kwanini wafanye na ndio maana wakipitia magumu kidogo wanaachana na wanachofanya na kuanza kingine. Kwanini nafundisha? Kwanini naimba?

*10.Does this actually matter?*
Kila baada ya muda jiulize kama hicho unachofanya ni sahihi? Unachowaza, unachoongea, unachowatendea wengine ni sahihi? Ndio kitu muhimu wewe kukifanya?

*11.Will this be alive time or dead time?*
Muda wa kujiambia nitafanya, nitaanza, nitahakikisha, nitafurahia,nitanunua na mengine mengi yanayofanana na hayo tunayaita maisha mfu, maisha yaliyokufa, muda hai ni muda wa kujifunza na kuweka kwenye matendo na siyo kujiambia nitaanza au nitafanya wakati mwingine.

*12.Is this who I want to be?*
Unapenda uwe mtu wa hekima lakini unakasirika muda wote, unapenda uwe mtu wa mungu lakini huna uadirifu, unataka kuwa mama/baba bora lakini unafanya kinyume, ukidanganya jiulize ni hivi ndivyo ninavyotaka kuwa? Mwandishi anasema huwezi kuwa mtu wa kazi wakati unapenda njia za mkato,"How we do anything is how we do everything"Kama siyo mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa, huwezi jiambia umedanganya kidogo ila kesho utakuwa mkweli, huwezi kuwa mvivu kwenye kazi ulio ajiriwa halafu ukawa na bidii kwenye kazi ya kujiajiri kwasababu uvivu uko ndani mwako.

Rafiki mwandishi anakutaka umalizie na swali kutoka kwa Frakl Struggled-Kwako maisha yana maana gani? maswali haya utayajibu kwa vitendo na maamuzi utakayofanya na siyo kwa mdomo, nikutakie wakati mzuri na bora rafiki yangu.

Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga. Napatikana kwa amail yangu bna blog yangu ambayo nakuwekea hapa chini.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment