Tuesday, 21 July 2020
Nguvu ya taswira sehemu ya pili......
"Truly, thoughts are things, and their scope of operation is the world, itself"
Nimeona nianze na maneno hayo ambayo mwandishi amemalizia hivyo kutoka sura ninayokwenda kukushirikisha leo, kwanza kabisa niendelee kukushukuru wewe rafiki unayeendelea kujifunza na Nina hakika ukiyafanyia kazi haya utafika mbali sana.....
Rafiki kutoka kwenye kitabu chetu cha THINK AND GROW RICH ,wiki iliyopita tuliangalia umuhimu na aina za taswira na jinsi gani taswira itakupa chochote unachotaka kama utaitumia vizuri, rafiki labda nikuambie kitu kwamba mambo yote mazuri unayoyaona sasa na tunayatumia miaka kadhaa iliyopita hayakuwa halisia hivi, bali ilikuwa taswira kichwani kwa mtu, ndege zinazoruka angani na kusafirisha watu ilikuwa taswira kwa Write brothers, magari ilikuwa taswira kwa Henry Ford na mengine mengi mazuri yalitokana na taswira ambayo mtu mmoja aliiweka kwenye akili yake, Leo mwandishi ametuandalia kisa kimoja.
Miaka 50 iliyopita daktari mmoja alitoka kijijini na kwenda mjini akiwa na birika linaloonekana kuu kuu, alipofika mjini alikwenda kwenye duka moja na alionekana akiongea naye kwa siri, baadaye alionekana akimkabidhi birika lile pamoja na kanuni zilizopo kwenye birika lile, mwandishi anatuambia karani yule aliamua kutoa akiba yake yote na kumkabidhi karani yule, Je birika lile lilikuwa na nini, na je ni kanuni gani hiyo ambayo ilimfanya karani atoe akiba yake yote na kumpa daktari?
Karani yule alitoa akiba yake yote ya dola 500 za kimarekani na kumkabidhi daktari yule, Daktari alifurahi sana kuweza kutengeneza pesa kwa kuuza wazo kwa karani pasipo hata na uhakika kama wazo lile likichanganywa na kanuni zile litaweza kuleta matokeo, upande wa karani wasiwasi na mashaka vilimshika kwamba kanuni zile na birika vitamletea pesa kweli zaidi ya akiba yake ile aliyokuwa nayo?
Kabla sijaendelea na kisa hiki ambacho ni cha kweli na siyo cha kutungwa kama anavyosema mwandishi kwa kumnukuu "It is not a story from Arabian Nights, a story of facts".
Kipo kitu nimejifunza hapa kabla sijaendelea na simulizi hii ya kweli, kuna mawazo mengi sana tunayapuuza ambayo tunaona hayawezekani na kupitia mawazo hayo ndio tungeweza kutengeneza utajiri mkubwa sana, lakini pia woga wa kupoteza fedha zetu ndio kunatufanya tushindwe kujaribu vitu vipya vyenye manufaa kwetu.
Basi kupitia kanuni na birika lile karani aliweza kufanya mabadiliko makubwa sana duniani, kwani mpaka sasa karani huyo kupitia wazo lile na kuchanganya na ubunifu wake ameweza kutengeneza ajira za watu wengi duniani, kaweza kutengeneza tilioni za pesa, Mimi na wewe tumeburudika kupitia wazo na taswira kutoka kwa daktari kwenda kwa karani, kupitia birika lile leo ukiwa popote ulimwenguni, kwenye majiji na vijiji a hata uchumi ushuke vipi bado bidhaa hii itaendelea kuwepo, Je unataka kufahamu ni bidhaa gani hiyo? Basi ni COCA-COLA.
Rafiki hata wewe unayo mawazo na taswira pana sana lakini jamii itakuambia huwezi na wewe utakubaliana nao, lakini hata wewe una mawazo ya ki coca -cola lakini unajiambia haiwezekani na unapuuza ila ukiamua kufanya kitu nina hakika siku moja utajishukuru, toa kile cha kwenye taswira yako kiwe halisia.
Nikutakie siku njema rafiki yangu,usikubali siku ikapita bila ya kujifunza chochote, nikupongeze kwa kuendelea kutembelea USTAWI WA FIKRA na yapo mengi sana utaondoka nayo.
Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki yako, Mwl Kelvin Kinyaga na Mwanafunzi wa namna fedha itanifanyia kazi kupitia chuo cha KISIMA CHA MAARIFA.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment