Thursday, 9 July 2020
Acha kuwajaza hofu watoto wako.......
Siku nyingine ambayo Kila siku nimejifunza asili yake ni utulivu lakini pale tunapoianza kwa habari na mitandao ya kijamii ndipo tunapoanza kuziharibu asili hizo, habari hizo zinatufanya tuone maisha yetu hayana thamani na hali ya kukata tamaa inajengeka na hapo ndipo tunaposhindwa kwa Kila kitu kwenye siku zetu.
Rafiki yangu Leo wakati napitia meseji kwenye email yangu nikakutana na moja ya ujumbe ukielezea namna maisha ya John .F. Kennedy aliyekuwa Rais wa Marekani akijaribu kuelezea namna baba yake alivyomtenga na habari hasi, habari zozote za kumuonyesha kwamba mambo ni magumu na hayawezekani.
Wakati naendelea kusoma ndipo nokagundua kwamba Wazazi tulio wengi tunapenda kuyaongea mambo yetu yanayotuumiza mbele ya watoto pasipo kufahamu athari tunazowatengenezea hapo baadaye, hebu kumbuka ukiwa unapitia changamoto kubwa halafu Mtoto wako mdogo wa miaka miwili akiwa hafahamu lolote unalopitia, bado ataendelea na michezo yake na pengine akiona ndege ikipita angani atakuja kukuomba umnunulie na yeye ndege yake, unaweza kuona ni akili ya kitoto na ukaipuuza lakini hiyo ndio asili yetu, tunapozaliwa tunakuwa na hali ya kushinda lakini kwa kujaza mambo hasi kwenye akili yetu tunapoteza uwezo huo.
Kupitia kisa cha Kennedy tunaweza kuona akielezea mambo mengi mabaya yaliyotokea marekani amekuja kuyasoma akiwa shule lakini baba yake hakuwahi kumuonyesha kuna vitu vibaya vinaendelea, kama Mtoto anataka malezi bora hataki sababu, mjenge mwanao kwa kumuonyesha kwamba dunia ina Kila kitu ni yeye tu kuchaguwa ni kipi anataka kutumia,muweke mbali na mambo hasi na mfanye aone anapaswa kubeba majukumu yake yote hata pale mambo yanapokwenda vibaya, unapomuonyesha mwanao mambo ni magumu na hayawezekani atakuwa akiamini hivyo na hatasumbuwa akili yake.
Hivyo rafiki mwache mwanao aendelee na maisha yake ya kitoto kwa kumtimizia majukumu yake muhimu na kumuongoza huku na wewe ukibeba majukumu yako kama Mzazi, kama ni mwanafunzi mwambie ajira ziko nyingi sana na ni wavivu wa kufikiri ndio wanaamini kuna upungufu wa ajira, hili litamfanya asumbuwe akili yake kubuni vitu vipya, unapokubaliana naye kwamba hakuna ajira unamwambia akae asubirie kitu ambacho kwa dunia ya sasa mambo hayasubiriwi kutokea yanasababishwa.
Nenda leo kayaishi haya, kwa malezi yoyote unayotoa basi waonyeshe kwamba hakuna kitu wanaidai dunia na waonyeshe dunia ina Kila kitu bali uhaba ni msamiati wa wajinga, ndege hawana mikono na wanakula, wanyama hawana utashi na wanaishi kwa furaha je wewe mwenye utashi unaanzaje kuishi maisha ya kulalamika? Tafakari na chukua hatua.
Mwl.Kelvin Kinyaga ndie mwandishi wa makala hii na zingine kupitia blog hapa chini;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment