Saturday, 18 July 2020

Usiniombe pesa niombe wazo..........


Habari rafiki,nikupongeze kwa siku na jumamosi nyingine, kwa wanaothamini muda wanafahamu tofauti kati jumamosi iliyopita na hii na hujipanga ili kuitofautisha na jumamosi inayofuata, ila kwa tulio wengi ni wale tunao furahia siku hizi za mwisho wa wiki na kuona ni siku za kupumzika na kustarehe kumbe kwa kufanya hivyo ndivyo tunazidi kujididimiza bila kufahamu.....

Rafiki tangu nimeanza kufahamu nguvu ya maarifa nimekuwa natumia njia moja wapo kupata kiasi cha pesa ninachohitaji na njia hiyo imekuwa ikinisaidia sana, njia hiyo ni kuchukuwa kiasi cha pesa ninachohitaji na kukigawa kwa 1000,2000,3000,4000 na kuendelea,Kwa mfano nina hitaji 360,000 kwa mwaka nitajuwa natakiwa kubuni wazo litakalotengeneza 1000 kwa siku, 720,000 wazo litakalotengeneza 2000 kwa siku, Nahitaji 1,080,000 nitahitaji wazo litakalonipati 3000 kwa siku na hili limekuwa likinisaidia sana, unaweza kusema huo ni uongo tu hicho kitu hakiwezekani, uweke 1000 Kila siku?hupati matatizo yoyote na kutumia fedha hiyo? Wewe unatushauri ulishafanya?rafiki pengine nakuandikia makala Kila siku na hufahamu nina jishughulisha na nini nje ya maarifa ninayokupa.

Kabla sijakwenda kukuambia najishughulisha na nini napenda nikuambie jambo moja ambalo masikini tunalipenda sana, mtu akipata tatizo lolote anakimbilia kutaka pesa ili atatue tatizo lake, hilo halina ubaya wowote na siyo tatizo lakini kuendelea kusubiria upate tatizo tena na tena na kuomba fedha au kukopa hilo ni tatizo tena tatizo kubwa, ni Sawa na mtu ambaye Kila siku anakwenda kuomba samaki kwa jirani yake kwamba hana mboga lakini hata siku moja hataki kujifunza namna ya kuvua samaki ili kesho asiombe tena. Basi na Mimi nimejifunza namna ya kutengeneza pesa ni kufahamu nahitaji kiasi gani na kisha kutengeneza wazo litakalowezesha nipate kiasi hicho, hapa chini nitakupa mifano kwa kutumia biashara ninazojishughulisha nazo.

*1.AJIRA*
Kupitia kisima cha maarifa nimejifunza Ajira ni ngazi ya daraja 0 na siwezi acha kuitaja kwani siku zote napambana ili niweze kuondokana na daraja hili au kutolitegemea kuendesha maisha yangu kwani utumwa wa kuuza muda,nguvu na maarifa yangu kwa kiwango anachopanga mnunuzi na pamoja na yote anaweza nifukuza na kunifanya nitaabike, pamoja na kutambuwa changamoto za daraja hili bado kwa sasa nipo kwenye hatari hii ya kutegemea mshahara wa mwezi kwa kuajiliwa na serikali kama Mwalimu wa Secondary hapa mjini moshi.

*Biashara ya visheti*
Hii ni biashara ambayo Mimi na mke wangu tulianza kwa kutumia kanununi niliyokushirikisha pale juu, tunahitaji mtaji wa biashara fulani ya ndoto yetu kama familia, tukajiuliza ni kiasi gani tunahitaji ili kuweza kupata kiasi hicho? Mshahara hautoshi je tukope? Hapana kanuni ya fedha inakataa kuanza biashara kwa mkopo, je tufanyaje? Ndipo tukaanzisha biashara ya vitafunwa aina ya visheti ili kutengeneza 2000 kwa siku itakayowezesha kufikia lengo hilo, kupitia kisima cha maarifa tukaweza jifunza namna ya kuuza biashara hii na kwasasa hasa shule zinapokuwa zimefunguliwa tunaweza tengeneza zaidi ya 2000 kwa siku kama faida, kwani bidhaa hiyo inauzika zaidi kwenye mikusanyiko ya watoto kama shule na kwenye mini supermarket na hata maduka ya watu binafsi.

*Biashara ya vorcher*
Biashara hii tumeipa Jina la Asante Corona, wakati wa ugonjwa wa Corona mtakumbuka kwamba shule zote zilifungwa na Mimi miongoni Mwa walimu ilinibidi kukaa nyumbani ili kuweza kutii agizo la serikali ili kupunguza maambukizi, hapo ndipo wazo la kuuza vorcher za likatujia wakati tukifikiria ni kwa vipi miaka ya mbele tutaweza kupata mtaji wa kiasi fulani cha fedha ili tuweze kuendesha familia na kuwa huru na kipato, ndipo tukaja na wazo la vorcher ambalo tulilifanya kama sehemu ya huduma lakini sasa ni moja ya biashara nzuri sana kama unaelewa nidhamu ya fedha kwani tulianza na mtaji wa 40,000 na sasa tumeweza kutengeneza Mara mbili ya kiasi hicho ndani ya miezi mitatu,ni kiasi kidogo lakini si Sawa na bure na kwasasa tumebuni namna bora ambayo tumaianza wiki hii na inakwenda vizuri zaidi, Je unafahamu kwa mwezi unatumia vorcher kiasi gani? Basi karibu uwe mteja wetu tutakufahamisha matumizi yako na kukusaidia namna bora ya kupangilia vifurushi vyako ili uweze kutumia kiasi kidogo kuliko unachotumia sasa, na kama utahitaji kukupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na ukarudisha mwisho wa mwezi kiasi hicho hicho ulichotumia bila riba unakaribishwa, tumeanza na watu watano na sasa tuna wateja watatu wa huduma hii na bado wawili, hivyo kama unataka kupata huduma hii kwetu tuwasiliane kwa mawasiliano nitakayoweka hapo chini.Maombi yanaweza kubaliwa au kukataliwa kwani ni biashara kwa wale wenye uaminifu pekee wa kupatiwa huduma hiyo, Asante corona itakupa huduma ya vorcher kwa mwezi mzima na utalipia kiasi Sawa na huduma uliyopewa bila riba yoyote ile.

*Biashara ya tuition*
Chochote unachofanya unaweza kutumia kama sehemu ya kipato zaidi, pamoja na kwamba sasa tunatoka kazini saa kumi na moja na nusu bado nikitoka nafika nyumbani na kwenda kwenye nyumba za watu na kufundisha watoto zao tukifanya home work pamoja, wateja ni wengi sana wa huduma hii tatizo ni eneo la kufanyia huduma hii na muda, kwani Kila Mzazi anataka watoto wake wafundishiwe majumbani mwao.

Hizo zote ni biashara binafsi ambazo nazifanya Mimi na familia yangu, zipo nyingine ambano Nina shirikiana na wengine sijaziweka hapa na niseme kitu kimoja kwamba bila maarifa ninayopata na naendelea kupata kupitia vitabu na KISIMA CHA MAARIFA na kocha wangu AMANI MAKIRITA nisingeweza yote haya na nisingefika hapa,  mke wangu kipenzi unalala saa nane ili maisha yaende asante sana,wana kisima cha maarifa taifa na Kisima cha maarifa Kilimanjaro,nyie ndio nguzo kubwa kwangu, familia ndugu na wewe rafiki yangu nawashukuru sana kwa kuendelea kunitia moyo, tuwe pamoja na tufike pamoja, safari ni ndefu na ngumu lakini tutafika.

Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga, unaweza endelea kujifunza kupitia blog yangu hapo chini;

https://kinyagakelvin.blogspot.com

Kinyagakelvin162@gmail.com

0712161251/0763766944


No comments:

Post a Comment