Wednesday, 15 July 2020

Umuhimu wa taswira katika kufikia utajiri....


Rafiki yangu hongera kwa siku nyingine tena, Nina imani u mzima wa afya na tunaendelea vyema kusukuma gurudumu la maendeleo, lengo ni kuendelea kuifanya kazi ya kuifanya dunia kuwa na mazingira bora kuishi kwetu na kwa wengine....

LeoLeo kutoka kitabu cha THINK AND GROW RICH tutajifunza hatua nyingine muhimu katika kutengeneza utajiri, Hatua muhimu kuifahamu katika kutengeneza utajiri ni kutengeneza taswira.

Mambo yote tunayoyafurahia sasa miaka ya hapo nyuma havikuwepo, kupitia watu ambao leo tunawaita wagunduzi  ndio vimeweza kuwepo na kutunufaisha, mwandishi wa kitabu hiki anatuambia kwamba zipo aina mbili za taswira.

*1.Taswira awali*
Taswira awali inajengwa kwa kutumia mawazo na mipango ambayo tayari ipo, hapa mtu unatengeneza taswira kwa kuoanisha mawazo au mipango mbalimbali na kupata wazo moja ambalo unalifanyia kazi, watu wengi tunatumia taswira awali kuweza kuboresha maisha yetu.

*2.Taswira bunifu*
Hapa unajenga taswira baada ya kupata wazo jipya na kulitumia kupata kitu kipya ambacho hakijawahi kufanyika, hapa ndipo pamewawezesha wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa duniani kubaki na heshima muda wote, jiulize mtu aliyeweza kututengenezea simu ambayo Mimi na wewe leo tunatumia, jiulize mtu aliyetengeneza usafiri, yote hayo yalikuwa kama picha(taswira)kwenye akili yake ya ndani na Leo hii tunafurahia maisha mazuri kupitia matokeo ya taswira.

Sayansi inatuambia vitu vyote vimeundwa kutokana na maada na nguvu. Hivyo kama utaitumia nguvu ya taswira basi unaweza kufanya chochote unachotaka kitokee, utajiri pia ni matokeo ya taswira hivyo ukitumia nguvu ya taswira na kuhamisha taswira hiyo kwenye uhalisia na mambo yanatokea, watu wengi wanayao taswira lakini Kila wanapojaribu kuitengeneza lakini baadaye huzipuuza na kuendelea kuishi maisha ya mazoea. Asante rafiki na uwe na siku njema.

Makala hii imeandikwa na Mimi rafiki na Mwl.Kelvin Kinyaga;

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin162.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment