Wednesday, 1 July 2020
Hivi ndivyo unavyoweza kukigawa kipato chako......
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na unaendelea vizuri, umeshapanga silaha zako kwa ajili ya kwenda kukamilisha yale uliyopanga kutekeleza, nami nakuongezea nyenzo maarifa ili ikusaidie kutimiza mipango yako karibu...
NINAWEZAJE KUGAWA KIPATO CHANGU?
Kila mtu anafahamu umuhimu wa bajeti, lakini pamoja na umuhimu huo changamoto zake huanzia kwenye namna ya kugawa kipato hicho kwenye mafungu, ninakumbuka miaka kadhaa iliyopita baada ya kufahamu mgawanyo wa fedha kwenye mafungu ndipo nilipogundua nilikuwa naishi kwa kuyapa umuhimu mambo yasiyo muhimu na kusahau mambo muhimu, mafungu haya matano yanakupa picha na uhalisia wa wapi umekuwa unapeleka fedha zako.
1.Fungu la kwanza ni kujilipa wewe mwenyewe kwanza.
Sehemu muhimu kabisa kupeleka fedha zako ni kutoa asilimia kumi kwa Kila kipato kinachoingia na kukitumia kukiwekeza ili kiweze kuzalisha zaidi, tumeshaona umuhimu wa fungu hili, usimlipe yeyote kabla ya kujilipa wewe kwanza.
2.Fungu la pili ni mfuko wa dharura
Fungu la pili muhimu unalopaswa kuwa nalo ni fungu la dharula, na hapa tunaposema dharura mwandishi anasisitiza iwe dharura ya kweli, michango ya sherehe siyo dharura, tunaposema dharura tuna maana kipato kikuu kinapotoweka labda kufukuzwa kazi au ugonjwa na unahitaji matibabu ndio fungu hili litatumika, chukuwa asilimia 60 ya kipato chako na dhidisha Mara sita,hicho ndio kiwango azia cha kuwa kwenye akaunti yako ya akiba kwa ajili ya dharura, ikiwa na maana utaweza kuishi kama unavyoishi sasa kwa miezi sita zaidi hata pale chanzo chako kikuu cha kipato kinapotoweka.Tenga asilimia kumi pia ya kipato chako kwa ajili ya fungu hili.
3.Fungu la tatu ni,Sadaka na utoaji mwingine.
Kulingana na imani yako Tenga asilimia kumi kwa ajili ya matoleo na Zaka na matoleo mengine kwa wenye uhitaji,kadri unavyotoa kwa ajili ya wengine ndivyo utakavyo Pokea zaidi hivyo ndivyo kanuni za asili zinavyosema.
4.Fungu la nne ni maendeleo binafsi.
Ninaposema maendeleo binafsi sina maana zile gharama za kununua vitu vya thamani unavyo vipenda, hapa unatenga sehemu ya kumi kwa ajili ya kununua vitabu vya mafunzo mbali mbali vitakavyo kupa Mwanga wa nini unapaswa kufanya, kama akili yako haijaendelea basi hakuna sehemu utakayo endelea, pia mwandishi anasema unaweza kutumia fungu hili kutembelea maeneo mazuri unayopenda, wewe pamoja na familia yako, hili litakufanya ufurahie maisha yako muda wote,hivyo fungu hili ni muhimu pia.
5.Fungu la tano ni matumizi yako.
Kama unataka kweli kujitoa kufanikiwa basi matumizi yako hayapaswi kuzidi 60 ya kipato chako, kama utatumia zaidi ya asilimia 60 basi sahau kuhusu utajiri, asilimia 60 ndio inapaswa kufanya Kila kitu, chakula, maradhi, ada za watoto, kodi ya nyumba, kununua gari,kununua samani za ndani, kulipia bili mbali mbali na matumizi mengine, utaanza kujiambia hili haliwezekani mbona kipato changu ni kidogo sana? Kitawezaje kukamilisha hayo yote? Hatua ya kwanza ni kuhakikisha matumizi yanakuwa ndani ya asilimia 60 kisha kutumia ile fedha unayojilipa mwenyewe kukiwekeza ili kukidhi mahitaji yako na siyo kujidanganya kuanza kutenga mafungu haya na kutumia chini ya asilimia 60 utakapokuwa na kipato kikubwa,huko ni kujidanganya.
Rafiki yangu nenda kaishi kwa mafungu hayo kama unahitaji kufanikiwa, mwanzo utaona hilo halitowezekana kwani mazoea yatakupa tabu, ila baada ya muda kupita utaona nguvu kubwa ya ushindi ikianza kujengeka ndani mwako.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment