Sunday, 26 April 2020
Changamoto na matatizo yao siyo wanayokuambia, usikimbilie kutoa ushauri wako......
Rafiki yangu nakuita mwanamafanikio kwasababu Nina amini unalo kusudi ambalo unalifanyia kazi na Kila siku unapiga hatua kuliendea na ndio maana unasoma hapa, hivyo nikusihi usiishie hapa bali endelea kusoma mpaka mwisho na kuna kitu utaondoka nacho, karibu........
Rafiki yangu nina amini kwamba zipo changamoto nyingi unazipitia lakini Leo nataka tujadiliane kwa pamoja changamoto ya kuombwa kutoa ushauri, kuombwa msaada na watu wetu wa karibu ambao huna namna ya kuwakwepa kwa namna yeyote ile, na wakati mwingine umekuwa ukijaribu kuwasaidia lakini matatizo yao ni yale yale na inafika sehemu unahisi kuchoshwa nao, rafiki usichoshwe na hilo kwani rafiki yako nipo nitakuambia dawa ya tatizo hilo. Kabla hatujaenda kuangalia ki undani namna ya kutatua hili tuone shuhuda kutoka kwa rafiki yetu huyu.
"Nimechoshwa na tabia ya Mzazi wangu kuomba hela Mara kwa Mara na nikijaribu kumuanzishia biashara haidumu na anaendelea kuomba hela nashindwa nifanyaje ili nimsaidie"
Kama tunavyoona changamoto inayomkumba rafiki yetu, hapa ni Mzazi na huwezi sema unampotezea lazima umsaidie na shida ni vipi unamsaidia, kwanza kabisa kwa mtu huyu ni yeye mwenyewe alimtengenezea tabia Mzazi wake ya kumpa hela na chochote anachohitaji na inafika sehemu hawezi tena kumsaidia kwa kiwango cha kumridhisha Mzazi wake, hapa ni kwamba aliamini changamoto kwa Mzazi wake ni fedha kumbe si kweli, Msemo wa usimpe mtu samaki bali mfundishe namna ya kuvua samaki ndio unajidhihirisha hapa,kwa changamoto na matatizo yanayowakabiri wengi hasa watu wa karibu ufumbuzi wake siyo kuwatimizia wanachohitaji moja kwa moja kabla ya kupata suruhisho la kudumu.
Wiki hii nilikuwa napitia makala za ustoa ndio nikakutana na sababu nne zinazopelekea watu kupitia changamoto nyingi, pengine ulikuwa huzifahamu au unazifahamu na hukujuwa kama zina nguvu kubwa, zitumie kwako na kwa yeyote anayekuomba ushauri.
1.When we wake up
Rafiki kama hili ulikuwa unalichukulia pouwa basi unajidanganya,muda wa kuamka ni muhimu sana kwenye maisha yetu.
2.What we study and practice
Kujifunza na kusoma vitabu ni maisha, hivyo kama hakuna unapojifunza huna maisha.
3.Who we have in our lives as influences
Rafiki kama unamshauri mtu na hufahamu msukumo wake unatoka wapi ni kazi bure, unamshauri mtu afanye biashara na hana kusudi la kufanya hivyo unampotezea muda wake na wako pia.
4.Where we go and how we spend our time.
Muda ni Mali hivyo kama unampa mtu ushauri halafu yeye hafahamu thamani ya muda ni kazi bure.
Mambo haya manne ni muhimu sana na kabla hujamshauri mtu kitu chochote angalia mambo hayo manne na ona kama unaweza kuwapa ushauri na kuwatengenezea tabia mpya kwenye mambo hayo kisha changamoto zao zingine zitaondoka, na ukiona unajohusisha na mtu anayepuuza vitu hivi vinne basi jiandae kuumia.
Makala hii imeletwa nami rafiki yako, Mwl kelvin Kinyaga;
Msomaji na mwana kisima cha maarifa;
Unaweza nipata kwa No.0763766944;
Email adress Kinyagakelvin162@gmail.com
Blog yangu https://kinyagakelvin162.blogspot.com ukifunguwa kiungo hiki utapata makala na mafunzo mengi. Asante sana.
Friday, 17 April 2020
Tofauti ya kupenda na kuhitaji ndio itaamua ufike wapi......
Rafiki siyo Mara ya kwanza kukuambia siku hii umepewa kama Zawadi, Leo unaweza kuanza kunielewa nini nilikuwa ninamaanisha, hizo idadi za vifo unavyovisikia nisehemu ndogo sana, labda nikuulize kitu kimoja, tangu gonjwa hili la corona limeingia nchini vifo vingapi vimetangazwa? Je wangesema watangaze idadi ya wote waliokufa si utakubaliana na Mimi idadi hiyo ni ndogo sana, unafahamu kuna watu zaidi ya 20 wamekufa kwa Mara moja kwenye ajari? Pengine nao walikuwa wanawaza corona lakini hawajaondoka kwa corona, yote nayaandika lengo lisiwe kukutisha Bali kukufanya uishi kusudi na kuacha kujidanganya na kesho, kesho ni mbali kuliko siku zote, nenda kakamilishe yote uliyojipangia.
Rafiki na mwanamafanikio mwenzangu, sisi binadamu ni viumbe wa kupenda,Kila mmoja wetu vipo anavyovipenda,pengine ni kuangalia TV,pengine ni starehe,pengine ni kusoma vitabu, Pengine ni kuangalia mpira na vingine vingi, lakini wapo watu wanapenda vitu wanavyovihitaji pia,mfano mtu anapenda kufanya biashara na anahitaji biashara ili kuweza kufikia ndoto zake, hivyo mtu huyu kuyafikia mafanikio inakuwa rahisi sana kwani anapenda kile anachokihitaji,sasa tuchukulie mtu ambaye anaghairi kufanya kazi ili akatizame mpira, Je kupenda kwake kutizama mpira kuna mpa mahitaji yake?fedha na chakula anapata kwa kutizama mpira?
Hivyo nini unapaswa kufanya?
Usifanye kitu chochote kwasababu unakipenda bali jiulize ninakihitaji? Na siku zote anza na vile unavyohitaji kama kwa wakati mmoja hujuwi nini cha kufanya.
Jitaidi kujihusisha na vile unavyovihitaji na uvipende hivyo kwanza, nahitaji mafanikio na napenda kusoma vitabu na kujifunza na kubadilika, hapo hakuna wa kunizuia kufanikiwa.
Rafiki kwa Leo ni hayo machache,andika yote unayopenda na jiulize kama ndio unayohitaji halafu utaona ni nini unaweza kufanya.
Fungua kiungo https://Kinyagakelvin.blogspot.com na utajifunza zaidi, kuna masomo mengi yatakayo kuongoza kwenye safari yako ya mafanikio.
Imeandikwa na Mwl.Kelvin Kinyaga
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Saturday, 11 April 2020
Njia ya kukufanya ukue hii hapa.........
Rafiki yangu habari za wakati huu, karibu tutafakari pamoja namna ya kufanya mazingira yanayotuzunguka yanakuwa bora kwetu na kwa jamii inayotuzunguka na Leo nataka nikuambie usihangaike na kujiuliza ufanye nini ili uweze kupiga hatua, kukua na kufikia juu unakotaka kufika, kwani kama hukui kwenye kile unachofanya,biashara iko vile vile, namna ya kufanya iko vile vile basi fahamu kosa lako liko hapa.......
Kabla hatujaangalia njia ya kukupeleka kwenye safari yako ya mafanikio kwanza nikuambie kitu kimoja, hakuna mtu yeyote atakayefanya wewe ufikie mafanikio unayoyataka na ndoto unayotaka kufikia, sisi waandishi na makocha pamoja na wahamasishaji hatuna uwezo wa kukufanya utimizi ndoto zako, kazi yetu kubwa ni kukuonyesha njia ya kupita ili safari yako iwe rahisi lakini wewe ndio mwenye mamlaka ya mwisho na haina maana kwamba kwenye njia hiyo utakayoonyeshwa haitakuwa na pingamizi hapana, inaweza kuwa na pingamizi nyingi sana lakini ni wewe ndio utakayeamua zikufanye urudi nyuma au uendelee mbele, wiki hii ninasoma kitabu cha Robert Kiyosaki kinachoitwa Be rich and Happy na kwenye kitabu hicho Kiyosaki anasema hivi.
"Understand that the only way to progress in life is to learn new things,and that new things can be learned only by making mistakes, through trial and error"
Rafiki yangu maneno hayo juu yanatupa picha kwamba kama hukuwi basi usitafute mchawi kwani tatizo hapo ni kwamba hujaribu vitu vipya na ukishajaribu vitu vipya basi tambuwa utakosea na kwenye kukosea utajifunza na ukijifunza utapiga hatua. Hapa tunapata fundisho kwamba kusoma vitabu siyo mwisho wa kujifunza bali kusoma vitabu na kujaribu vitu vipya Kila siku, kataa kuwa kawaida, kataa kufanya vitu rahisi maana siyo asili ya dunia, maisha hayana maana kama hayana changamoto, kwani hata mmea mpaka unazaa matunda unapitia changamoto nyingi sana, upepo uliozidi ni changamoto,kukosa Maji na mengine mengi lakini mwisho wa siku unakuwa na kutoa matunda.
Rafiki yangu ondoka na ujumbe huu Leo;
Acha kuelezea matatizo yako kwa wengine, kulalamika ni kukataa mafanikio,nenda kajaribu vitu vipya, mazoea ni Sawa na Maji yaliyotuwama hayafai kunywa, kuwa Maji yenye mwendo na kwa kujaribu na kushindwa unakuwa imara, piga hatua ndogo ndogo utafika lakini kataa kusimama kwani masaa, siku na miaka havijawahi simama, ng'ang'ana na dunia itakupa chochote unachotaka.
Endelea kutembelea ukurasa wangu kupitia kiungo hiki; http//kinyagakelvin.blogsport.com na utajifunza mengi yatakayokupa nguvu ya kusogea Kule unakotaka kufika.
Ni Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mjasiliamali mdogo, ninayeamini na kuwa na hakika kupitia vitabu Mimi na wewe kuna siku tutakutana sehemu ya juu na hata tukifa kimwili bado tutaendelea kuishi, tusiache kujifunza na karibu tuwe sote.waweza nitafuta kwa email adress yangu;
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Sunday, 5 April 2020
Umri siyo kipimo cha ukubwa bali uwezo wa kufurahia matatizo na changamoto zako......
Rafiki yangu karibu tumalizie wiki pamoja,napenda tufunge juma pamoja ili tunapoanza wiki lingine tuwe na nguvu mpya za kukabiliana na magumu yaliyo mbele yetu.Kama unaweza kusoma hapa sina shaka ni miongoni Mwa watu wenye bahati sana....
Rafiki yangu miaka mitatu iliyopita kabla sijaanza kuishi maisha yangu nilikuwa miongoni Mwa watu ambao ni wengi lakini wanao ishi maisha ya maigizo, maisha ya majirani na maisha yasiyo eleweka, tabia ya mtu wa maisha haya ni mtu anayelalamika kwa jambo lolote lile, nilikuwa natamani maisha ya waigizaji wenzangu, maisha ya kutamani kuwa mbali na changamoto,maisha ya kutaka vitu vitokee bila jasho kwa kujiambia ukishasoma basi mengine yote ni akili yangu tu.
Mwanafalsafa Seneca aliwahi kusema hivi;
"
NO MAN IS MORE UNHAPPY THAN HE WHO NEVER FACE ADVERSITY.FOR HE IS NOT PERMITTED TO PROVE HIMSELF"
Kauli hii inatukumbusha umuhimu wa kuona changamoto na matatizo kama daraja la kutuvusha kutoka chini kwenda juu na kadri unavyopata matatizo na changamoto ndogo ndivyo unavyokosa furaha na ndivyo unavyojizuia kufika mafanikio ya juu. Na ndio maana unapoanza kufanyia mafunzo ya fedha unaona changamoto zinaongezeka, unalipwa fedha kidogo na unatakiwa uipunguze uiwekeze na usikope hivi ni vitu ambavyo siyo rahisi kama hujuwi umuhimu wa changamoto kwenye mafanikio.
Rafiki kauli ya kuondoka nayo Leo ni hii inayosema hivi;
"Kama sina changamoto,sina maisha na nimuigizaji wa maisha"
Ni Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mwandishi na muhamasishaji wa maarifa sahihi kupitia blog yangu ya http//kinyagakelvin.blogsports.com
0763766944
Asante na siku njema.
Subscribe to:
Comments (Atom)