Saturday, 11 April 2020
Njia ya kukufanya ukue hii hapa.........
Rafiki yangu habari za wakati huu, karibu tutafakari pamoja namna ya kufanya mazingira yanayotuzunguka yanakuwa bora kwetu na kwa jamii inayotuzunguka na Leo nataka nikuambie usihangaike na kujiuliza ufanye nini ili uweze kupiga hatua, kukua na kufikia juu unakotaka kufika, kwani kama hukui kwenye kile unachofanya,biashara iko vile vile, namna ya kufanya iko vile vile basi fahamu kosa lako liko hapa.......
Kabla hatujaangalia njia ya kukupeleka kwenye safari yako ya mafanikio kwanza nikuambie kitu kimoja, hakuna mtu yeyote atakayefanya wewe ufikie mafanikio unayoyataka na ndoto unayotaka kufikia, sisi waandishi na makocha pamoja na wahamasishaji hatuna uwezo wa kukufanya utimizi ndoto zako, kazi yetu kubwa ni kukuonyesha njia ya kupita ili safari yako iwe rahisi lakini wewe ndio mwenye mamlaka ya mwisho na haina maana kwamba kwenye njia hiyo utakayoonyeshwa haitakuwa na pingamizi hapana, inaweza kuwa na pingamizi nyingi sana lakini ni wewe ndio utakayeamua zikufanye urudi nyuma au uendelee mbele, wiki hii ninasoma kitabu cha Robert Kiyosaki kinachoitwa Be rich and Happy na kwenye kitabu hicho Kiyosaki anasema hivi.
"Understand that the only way to progress in life is to learn new things,and that new things can be learned only by making mistakes, through trial and error"
Rafiki yangu maneno hayo juu yanatupa picha kwamba kama hukuwi basi usitafute mchawi kwani tatizo hapo ni kwamba hujaribu vitu vipya na ukishajaribu vitu vipya basi tambuwa utakosea na kwenye kukosea utajifunza na ukijifunza utapiga hatua. Hapa tunapata fundisho kwamba kusoma vitabu siyo mwisho wa kujifunza bali kusoma vitabu na kujaribu vitu vipya Kila siku, kataa kuwa kawaida, kataa kufanya vitu rahisi maana siyo asili ya dunia, maisha hayana maana kama hayana changamoto, kwani hata mmea mpaka unazaa matunda unapitia changamoto nyingi sana, upepo uliozidi ni changamoto,kukosa Maji na mengine mengi lakini mwisho wa siku unakuwa na kutoa matunda.
Rafiki yangu ondoka na ujumbe huu Leo;
Acha kuelezea matatizo yako kwa wengine, kulalamika ni kukataa mafanikio,nenda kajaribu vitu vipya, mazoea ni Sawa na Maji yaliyotuwama hayafai kunywa, kuwa Maji yenye mwendo na kwa kujaribu na kushindwa unakuwa imara, piga hatua ndogo ndogo utafika lakini kataa kusimama kwani masaa, siku na miaka havijawahi simama, ng'ang'ana na dunia itakupa chochote unachotaka.
Endelea kutembelea ukurasa wangu kupitia kiungo hiki; http//kinyagakelvin.blogsport.com na utajifunza mengi yatakayokupa nguvu ya kusogea Kule unakotaka kufika.
Ni Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, mjasiliamali mdogo, ninayeamini na kuwa na hakika kupitia vitabu Mimi na wewe kuna siku tutakutana sehemu ya juu na hata tukifa kimwili bado tutaendelea kuishi, tusiache kujifunza na karibu tuwe sote.waweza nitafuta kwa email adress yangu;
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment