Monday, 26 October 2020

Zingatia Haya Ili Kuikuza Biashara Yako

Tunakila sababu kumshukuru mungu wetu kwa zawadi ya maisha, kila siku tujikumbushe kwamba lipo kusudi la sisi kuwepo duniani, tutumie nafasi hii kufanya yale yatakayoleta manufaa kwetu na kwa wengine, kataa mazoea badilika. Leo tutamalizia sehemu ya mwisho ya biashara kama msingi wa mafanikio kwa kuangalia mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara yako. Rafiki kitu ambacho unapaswa kukifahamu ni kwamba mafanikio ya biashara, hayaji kama ajali au bahati, bali yanatengenezwa. Lazima ujenge misingi imara ya kuwezesha biashara yako kukua. *Msingi wa uaminifu na uadilifu* Msingi mkuu wa biashara ni mahusiano, hakuna mahusiano yanayojengwa nje ya uaminifu na uadirifu. Fanya kitu kama ulivyo ahidi, udanganyifu kwenye biashara ni sumu. *Maadili* Lazima uwe na miiko yako kibiashara, lazima ujiambie ni mambo gani hutokuja kuyafanya kwenye biashara yako. Kwenye biashara kuna mambo mengi sana ya ushawishi kama hutajijengea miiko utajikuta kila ushauri unaufanyia kazi na hapo ndio unakua mwanzo wa angako kwenye biashara. *Uvumilivu* Mafanikio kwenye biashara ni kitu ambacho hakiji kama ajali, lazima uweke nguvu na muda kufanikiwa, kama huna uvumilivu huwezi kufanikiwa kwenye biashara, yapo mengi utakutana nayo na hutoambiwa popote na yatataka kukutoa kwenye mstari hivyo kama siyo imara utapotea. *Shukrani* Acha kulalamika na kuona mambo mabaya yanatokea kwako tu, uwe mtu wa shukrani. Unaposhukuru unafunguwa Milango kwako zaidi. *Ushirikiano* Huwezi kujenga biashara kubwa peke yako, unahitaji kushirikiana na wengine. Wasaidizi wako, wateja wako na kila mtu anayefahamu uwepo wa biashara yako lazima ushirikiane naye vizuri. Ukiyasimamia haya ipasavyo nina hakika ngunzo ya biashara yako itakua imara sana na itakuwa vigumu kuvunjika. Kitu cha kuondoka nacho kwenye somo hili ni kwamba tabia za mfanyabiashara ndio kikwazo kikubwa kwenye biashara na kwa asilimia chache ndio hutoka nje ya sababu hii. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Sunday, 25 October 2020

Na Hii Ndio Kanuni Ya Kuingia Kwenye Biashara

Hongera sana rafiki yangu, ni juma lingine tumelianza, sina shaka kwamba umeshapanga yale yote unayotaka kukamilisha kwenye juma hili na leo yapo ambayo umejipanga nayo kuyatekeleza, basi hakikisha hakuna lolote lisilo la msingi litakalokuwa sababu ya kuharibu mipango yako, lakini pia jiandae kwa changamoto zozote zinazoweza jitokeza na kazikabili. Leo pia tunaendelea na mfululizo wa somo kuhusu biashara, kitabu chetu ni kile kile cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na Dereva wetu aliyetuandikia kitabu Dr. Makirita Amani. Karibu..... Rafiki ni wachache sana kati ya wanaotamani kuingia kwenye biashara ndio wanafanikiwa kuanzisha biashara, yaani tuseme kati ya watu 100 wanaotamani kuanza biashara ni mmoja pekee ndio anafanikiwa kuanzisha biashara. Je kwanini watu wanaishia kutamani kuingia kwenye biashara na hawaingii? Mwandishi anasema Kanuni ya kuanza biashara ni *just do it*. Acha kujipa maswali mengi yasiyo na tija kuhusu biashara gani ufanye na je ni changamoto zipi nitakutana nazo, wewe unachopaswa kufanya ni kuanza biashara na kisha ukishaanza ndio utaanza kufanyia kazi changamoto utakazokutana, anza na mteja mmoja kisha mtumie mteja huyo mmoja kuongeza wateja wengine. Rafiki tafiti zinaonyesha biashara kubwa ambazo watu wengi wanamiliki siyo biashara walizo anza nazo, bali kwa kuboresha mawazo yao ya biashara ndio kumewafikisha kwenye kazi za juu za biashara. Mwandishi wa kitabu anasema mafanikio kwenye biashara ni kitu cha kujaribu na kushindwa, mpaka pale unapoipata njia yako halisi, na kuitumia njia hiyo kukua zaidi na kufikia uhuru wako kifedha. Kama una mpango wa kuanza biashara acha kujipa maswali na majibu bali nenda kaanze leo, anza na popote na chochote kisha weka nguvu na muda kuikuza biashara yako. Muhimu ni kujifunza na kuwa tayari kubadirika. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Saturday, 24 October 2020

Leo Nitakujibu Ni Swali Lako La Biashara Gani Ufanye Ili Uweze Kufanikiwa Haraka

Hongera sana rafiki yangu kwa kuweza kuifikia siku hii ya mwisho wa juma, siku ambayo nimekuwa nakusisitiza itumia kujitathimini na kujipa majibu sahihi, wapi umetoka, uko wapi? na wapi unataka kufika....... Rafiki yangu karibu tuendelee na somo letu kuhusu biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kilichoandikwa na kocha Dr Makirita Amani. Je ni biashara gani naweza kuanza kufanya na ikaniletea faida bila kuumiza kichwa? Hili ni moja ya swali ambalo wengi hupenda kuliuliza sana na pengine hata wewe msomaji wangu umekuwa ukijiuliza sana na watu wamekupa majibu mengi na bado hujaridhika nayo, pengine hawakukupa jibu la moja kwa moja ambalo mimi nakwenda kukupa. HAKUNA BIASHARA MOJA AMBAYO KILA MTU AKIIFANYA ATAFANIKIWA SANA, HAIPO. swali hili limekuwa kikwazo kwa wengi kuingia kwenye biashara na siku zote uanza biashara fulani na wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo wanaacha na kuanza biashara nyingine na huo ndio unakuwa utaratibu wao na kujikuta hawafiki popote. Kila mtu kuna biashara ambayo kwake yeye anaweza kuifanya vizuri na kufanikiwa. Hivyo swali muhimu ni biashara gani itakufaa wewe au mimi kuanza nayo?. Hapa utaangalia vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na unavipendelea kufanya, ujuzi wako au uzoefu ambao tayari unao. Mazingira yanayokuzunguka na watu wanapitia changamoto zipi?. Nenda kayafanyie kazi haya rafiki yangu na uwe na siku njema. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Friday, 23 October 2020

Vitu Viwili Vya Kuwekeza Wakati Biashara Yako Iko Hatua Za Mwanzo.

Maisha yetu sisi binadamu ni ya mchaka mchaka mpaka siku yetu ya mwisho kuishi hapa duniani itakapofika, acha kujidanganya na mapumziko ya mwisho wa wiki, tafuta kitu cha kufanya kuliko kukaa na kujidanganya kupumzika wakati kila siku unalalamika. Leo tunaendelea kuangalia eneo la biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI NA FEDHA kutoka kwa mwandishi mzawa Amani Makirita karibu tuwe sote. Watu wengi hufikiri wakishapata mtaji na kodi ya kulipia jengo la biashara basi wameshafanikiwa na pale mambo yanapoanza kuwa magumu ukimbilia kutoa sababu nyingi zisizo za kweli, lakini biashara yoyote ile kwenye hatua za chini au mwanzo inahitaji mambo mawili yafuatayo. *Nguvu* Hapa ni kwamba biashara inakuhitaji wewe kuweza kufanya kila kitu kwenye biashara yako, kufanya kwa ubora ambao wengine hawawezi kuufanya. Hapa ndio sehemu ambayo unajenga msingi wa biashara yako, na unafahamu kama msingi utakuwa mbovu nini kitatokea, acha kutumia muda mwingi kulalamikia mtu uliyemwajiri akusaidie, tumia nguvu zako kuhakikisha biashara inaijengea msingi imara. *Muda* Utahitaji muda ili kuweza kuikuza biashara yako kutoka chini kabisa mpaka ikawa biashara kubwa. Siyo kitu cha kulala masikini na kuamka tajiri, lazima ufahamu kwamba utahitaji kujenga wateja waaminifu wa biashara yako. Utahitaji muda wa kulielewa ki undani biashara yako kuliko mtu yeyote yule. Watu wengi kwenye biashara wanashindwa kwasababu wanaangalia matokeo ya haraka, unataka biashara ikue wakati wewe unaendelea na maisha ya kawaida na hukui. Kuamka muda ulizoea kuamka, kufuatilia mambo yasiyo muhimu kwako, kukaa na marafiki zako kupiga soga. Haya yote ni sumu kwa biashara yako inapokua kwenye hatua za mwanzo. Lazima unapoanza biashara uwe tayari kuvuruga mahusiano na watu ambao ulikuwa nao kabla hujaanza biashara, hakikisha kila siku unaweka bidii ya kujifunza namna ya kuisimamia na kuikuza biashara yako. Makala hii imeandikwa na mimi rafiki na Mwl. Kelvin Kinyaga Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Thursday, 22 October 2020

Kuanza Biashara Ukiwa Chini Kabisa.

Rafiki yangu hongera kwa kuendelea kujifunza pamoja na mimi kupitia mfululizo wa makala zangu, ni hitaji la kila aliye hai kujifunza kila siku namna ya kuishi vizuri na kufurahia maisha. Vyote vinavyokuletea msongo wa mawazo na kukuhuzunisha ni matokeo ya mtazamo tu mbovu ulio nao, karibu tuwe sote..... Leo tunaendelea na somo letu kuhusu umuhimu wa biashara kwenye kuongeza kipato na yote tunayapata kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na mwandishi wetu mbobevu Dr. Amani Makirita. _Kuanza biashara ukiwa chini kabisa_ Mwandishi wa kitabu ameanza kwa msisitizo kwamba, njia nzuri ya kuanza biashara, ni kuanzia chini kabisa. Hata kama unaweza kupata mtaji mkubwa, kupitia akiba zako mwenyewe au kuwa na uwezo wa kukopa. Siyo vyema kuanzia biashara juu, kama hujawahi kuwa kwenye biashara kabisa. Yapo mambo mengi sana unapaswa kujifunza Kwa matendo. Hata kama utakua umesoma vitabu, umehudhuria kozi nyingi, bado yapo mambo utajifunza pale unapoingia kwenye biashara. Unapoanza biashara kuna makosa mengi sana madogo madogo utayafanya hivyo kwa sababu umeanzia chini hupati hasara kubwa yenye kukuondoa kwenye biashara yako. Kwa mfano kwenye kuajiri utapata watu wasio waaminifu na kuipa biashara yako uzito kama unavyoipa wewe na kukusababishia hasara, hivyo utajifunza hayo bila kupata hasara kubwa. Hivyo rafiki yangu acha kufikiria ni pale utakapopata mamilioni ndio uingie kwenye biashara, kwani kwa kufanya hivyo utapata hasara kubwa na utakata tamaa kabisa ya kujirekebisha na kuanza upya. Nakutakia siku njema rafiki yangu, nenda kaanze na kidogo na kikuze taratibu huku ukifanyia kazi kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye biashara yako. Makala hii imeandikwa na mimi rafiki yako Mwl Kelvin Kinyaga Asante sana na mwenyezi Mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Wednesday, 21 October 2020

KWA NINI KILA MTU ANAPASWA KUWA NA BIASHARA.

Rafiki kitu unachopaswa kukifahamu kwenye maisha ni kwamba hakuna kusimama, Kuna kwenda mbele au kurudi nyuma, kama ulichofanya Jana ndio unakwenda kufanya leo Kwa namna Ile Ile basi hapo umerudi nyuma, nenda kafanye zaidi ya Jana na utapata matokeo tofauti na uliyopata Jana..... Leo tuendelee na somo letu kuhusu fedha na kwanini kila mtu anapaswa kuwa na biashara. Kwanza ni ukweli usiopingika kwamba biashara ndiyo njia ya kuweza kuongeza kipato, ambayo haina kikomo. Hakuna mtu wa kukuzuia wewe kwenye Idadi ya biashara unazoweza kufungua, Pia hakuna atakayekupangia kikomo cha kipato chako unachotengeneza kupitia biashara. Biashara ndio njia kubwa ya kuleta manufaa Kwa jamii zetu, taifa na hata dunia Kwa ujumla. Ni kupitia biashara ndio watu hutatuliwa matatizo yao makubwa. Pia biashara ndio sekta inayotoa ajira Kwa watu wengi zaidi. Na biashara ndio sehemu nzuri Sana ya kujifunza maisha. Mwandishi anasema biashara ndio chuo kikuu cha maisha, ni kweli kwani biashara haina maigizo yoyote, ukifanya kosa dogo adhabu yake ni hapo hapo. Biashara itakufundisha kutoa thamani,kushindwa, kukataliwa, kukabiliana na changamoto, kupambana, uvumilivu na mengine mengi.Hivyo Mwandishi anasisitiza Kwa kila mtu anayetaka kujifunza maisha na kuyaelewa Kwa vitendo anapaswa kuingia kwenye biashara, kwani hakuna kitu ambacho biashara haitakufundisha. Mwandishi anahitimisha sehemu hii Kwa kusema kila mtu anapaswa kuingia kwenye biashara kama moja ya kuongeza mifereji ya kipato. Hata kama unazo njia nyingine za kuongeza kipato kuwa na biashara kunaongeza mfereji mwingine. Watu wengi hupenda kupata njia za uhakika kama ajira ili kuingiza kipato lakini moja ya sheria za dunia ni kwamba hakuna jambo lolote ambalo ni uhakika wa asilimia 100. Wengi hujifunza hilo Kwa njia ngumu, pale kile walichokiwekea uhakika kinapowaangusha. Hivyo unapokuwa na biashara, tena zaidi ya moja, unazidi kupunguza hatari yako ya kutegemea sehemu moja au chache kwenye kutengeneza kipato chako. Nenda kafanyie kazi haya uliyojifunza na anzisha biashara hata kama utaingiza mia mbili Kwa siku na Anza kuikuza polepole. Uwe na siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki Sana. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Tuesday, 20 October 2020

MLANGO WA NDOTO

Ni kweli zipo changamoto nyingi ambazo unazipitia, je wafikiri hayo unayopitia ni mikosi? Unafikiri ni wewe peke yako unayapitia? Wacha kusikitika mshukuru mungu bado unayo nafasi ya kuyakabili yote na kusonga mbele. Karibu rafiki yangu tuendelee kujifunza pamoja. Leo tunaangalia umuhimu wa Ndoto kwenye maisha yetu, tunaangalia ndoto kama lango.Binafsi kabla ya kusoma kitabu hiki sikua na elewa chochote kuhusu ndoto na ni moja ya sehemu ambayo sikuwahi kuipatia umuhimu wowote. Kabla hatujajadili mlango huu wa ulimwengu wa kiroho ni vema tuangalie ni nini maana ya ndoto. Ukiangalia kamusi ya kiingereza inatuambia:Ndoto ni mtiririko wa mawazo, picha na mhemuko unaotokea kwenye fikra za mtu akiwa usingizini. Kwenye tovuti ya Wikipedia ;wao wanasema ndoto ni mrejesho wa sura, mashauri, hisia na msisimko ambavyo hutokea bila utawala wa akili wakati wa usiku kwenye vipindi mbalimbali vya usingizi. Wanasayansi wanasema ndoto ni picha za fikra kwenye utu wa ndani zilizobeba sauti, sura na mhemuko wakati tumelala. Tunaambiwa Kwa kawaida mtu mwenye Afya anaota mara 3 mpaka 7 Kwa usiku mmoja. Kwenye Biblia ndoto zimetajwa mara 21 kutoka Kwa mfalme Yakobo. Kitabu cha mwanzo pekee ndoto zimeandikwa mara 33.Kitabu cha Nabii Daniel zimeandikwa mara 27.Agano jipya kama mara 8 pekee. Kwa hali hii, ni vema tuone kuwa ndoto Zina umuhimu wake mkubwa kwenye maisha ya mtu. Mungu aliongea na wanadamu Kwa njia ya ndoto, ukisoma kitabu cha mwanzo kwenye sura 41,Kwenye ndoto maarufu aliyoiota mfalme Farao ikitafsiriwa na Yusufu mwana wa Israel;utaona mungu akitumia ndoto kuongea na binadamu. Ipo tofauti Kati ya Maono na ndoto. Maono hutokea wakati mtu hajalala na ndoto hutokea wakati mtu amelala. Tunapokuwa tumelala, miili yetu ndio imelala lakini roho zetu hazilali. Hivyo Kuna mambo mengi Sana ya kiroho utendeka tukiwa tumelala. Rafiki kama unahitaji kuelewa Kwa undani zaidi somo hili basi wasiliana moja Kwa moja na Mwandishi wa kitabu hiki mchungaji na Mwalimu Josephat Ulomi Kwa number 0763816739 Nenda ukasamehe wote waliokukosea, anza kupenda kujifunza na kuongeza ufahamu, anza kuamini kama ulikuwa huamini kwamba Yesu Kristo ni Lango hapa duniani kama ni mlengwa wa kristo, Anza kuheshimu ndoto Zina mengi ya kukufundisha na hapo utaanza kuona njia zako zinafunguka na unabarikiwa. Asante Sana rafiki yangu nakutakia siku Njema na Mungu akubariki Sana Sana. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Monday, 19 October 2020

Yesu Kristof lango la ufalme wa mungu hapa duniani.

Rafiki yangu Habari za wakati huu, bilashaka ni mara nyingine zawadi ya pumzi inakaa ndani mwetu, huwezi amini ni maelfu ya watu Jana walikuwepo lakini leo ni wafu, tumshukuru mungu na tukaitumie zawadi hii Kwa kulitukuza Jina lake. Rafiki yangu swala la Imani linaweza kutugawa lakini utakubaliana na mimi kwamba hilo siyo kusudi la mungu, leo nikiwa ninakwenda kuzungumzia yesu kristo kama lango Kwa wakristo, bilashaka na ndugu zetu waislam mtume Muhammad ndiye lango, Kwa wakristo hatuwezi fika mbinguni Kwa kupuuza Jina Yesu Kristo, vivyo hivyo Kwa wenzetu waislam hawawezi kupuuza Jina Muhammad Kwa safari ya kutafuta mbingu ya mwenyezi mungu, hivyo tunatumia Milango tofauti lakini safari yetu ni moja. Kwa upande wetu wakristo Tunafahamu kwamba palikuwepo Adamu wa kwanza aliyemuasi mungu na hivyo Kwa sababu yeye alikuwa uzao wa kwanza, basi lilikua lango kwetu sisi wanadamu wote na ndio maana tunazaliwa na dhambi ya asili ambayo inaondolewa Kwa njia ya ubatizo kupitia Adamu wa pili ambaye ndie yesu kristo Masia mkombozi wa ulimwengu. "Mimi ndimi mlango;mtu akiingia Kwa mimi, ataokoka;ataingia na kutoka, naye atapata malisho. You 10:9." hapa yesu anatumia mfano huu kutuonyesha kwamba yeye njia ya wokovu Kwa watu wote wanaotamani kuingia kwenye ufalme wa mungu. "Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima;mtu haji Kwa Baba, ila Kwa njia ya mimi ". Yoh 14:6" Yesu mwenyewe anakiri kuwa yeye ndiye njia ya kweli na uzima. Dhambi ilitutenga na mungu lakini Kwa kumwamini yesu tunaingizwa tena kwenye ufalme wa mungu. " Yohana 3:16,"Kwa maana jinsi hii mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele." Kwa kunukuu vifungu hivi vya biblia hakuna namna tunaweza kuona nguvu ya yesu kristo inatutoa kwenye mateso na shida na mahangaiko na kutukomboa, siyo dhambini tu bali kwenye kila hitaji letu pale tunapomuhitaji. Wapo wengi wanaoteseka Kwa kutafuta njia zisizo faha, Kwa waganga wa kienyeji kutafuta wabaya wao, Kwa mizimu ya mababu na hivyo kuteseka Kwa maisha yao yote, mfuate yesu kristo yeye atakuonyesha mambo makubwa ya ajabu usiyo yajua. Nikutakie siku Njema na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Sunday, 18 October 2020

Mlango wa ufahamu

Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka umeamshwa salama na uko tayari kwenda kuyakabili yale yote yaliyopo mbele yako, hongera na mungu akutangulie...... Leo tutakwenda kuangalia mlango mwingine utakao utumia kufanikiwa au kutofanikiwa kama hautoutumia mlango huo. Sehemu iliyopita tuliweza kuona Kaka yetu ULOMI kupitia KITABU chake cha yajue Malango yanayoweza kukufikisha au kudidimiza maisha yako KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA. Tuliweza kujifunza mlango wa msamaha Kwa kina na bila Shaka kama ulilielewa vizuri somo lile umejiponya, kwani kusamehe ni kujitibu mwenyewe. Leo tunakwenda kuangalia mlango mwingine , MLANGO WA UFAHAMU, tunateseka na mambo mengi Kwa sababu hatuna ufahamu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yetu. Neno la mungu linatuambia hivi; Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, Kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka saying. *Daniel 9:2* Kumbe kupitia neno hili tunaona umuhimu wa vitabu kwenye kutupatia ufahamu, Mwandishi anatumia neno UNDERSTAND Kwa kulinyambua na kupata neno Under lenye maana ya chini ya! Stand lenye maana ya simama na linapokua pamoja Lina maana KUJUA ULICHOSIMAMIA au sababu ya ulichosimamia. Hivyo kama utajikuta umekwama na lolote Kwa kuchukua vitabu na kusoma utapata uelewa mpana Sana, usijiulize nianze na kitabu kipi? Uwe mkristo biblia ipo anza nayo ina kila kitu. Kama ni Muslim Quran ipo itakupa uelewa wa kutosha, kwenye vitabu Kuna siri nyingi Sana, ukiweza kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu nina hakika hutobaki kama ulivyo. Mwandishi anaendelea Kwa kusema kwamba ukishajifunza kutoka kwenye vitabu na ukaunganisha na hekima ya kutenda yale uliyojifunza unapata ufahamu, hili linatupa tafsiri kwamba unaweza kusoma maelfu ya vitabu lakini kama huna hekima ya kutumia maarifa hayo basi hapo hakuna ulichofanya, kocha wangu anaita kuchafua akili. Jiulize kabla watu hawajafahamu tiba Kwa magonjwa yaliyotukabili je ni watu wangapi walifariki? Kwanini ufahamu ni lango?Ujinga na upumbavu ni ngome au vizuizi vinavyofanya watu wasifikie kiwango fulani cha maisha, wewe kuishi maisha ya dhiki na taabu siyo mpango wa mungu, kubaki vilevile kila siku siyo mpango wa mungu, hebu Anza kufungua vitabu na utoke huko. Mwandishi ametumia mifano mingi ya kutufungua na kututoa kwenye giza la Ujinga na kutufanya waelewa, Kwenye injili ya Yohana mlango ule wa nane yesu anasema "mkikaa katika neno language, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli ;tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. *Yoh.8:31-32* Rafiki Anza leo kujiwekea utaratibu wa kujifunza na utaona namna ulivyokuwa kifungoni Kwa Muda mrefu bila sababu wakati umezungukwa na maarifa ya kila aina. Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Thursday, 15 October 2020

Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 3

Rafiki yangu hongera Kwa kuweza kuifikia siku ya leo, nina amini changamoto unazozipitia ni daraja la kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine bora zaidi, usirudi nyuma songa mbele...... Leo tunaangalia sehemu ya tatu ya mtu huyu mwenye bahati kuliko wote babeli karibu tujifunze pamoja. Rafiki yangu nina hakika tumekua pamoja tangu mwanzo mwa simulizi hii na umeweza kuona ni namna gani bidii inavyoweza kukufungulia njia za mafanikio. Bidii ya kazi Kwa Sharru Nada inamvutia babu yake na kijana ambaye sharru anamuelezea alikua mshirika mwenzie kwenye biashara na hapo anataka kufahamu ni kipi kinamsukuma kijana huyu kufanya kazi Kwa bidii? Rafiki wengi wetu makazini tunafanya kazi Kwa bidii tukitegemea kuongezeka Kwa mshahara au kufanya vyeo na ndio maana kila siku tumekua tukilalamikia waajiri, Kwa sharru Nada kazi ilimfanya atengeneze mahusiano mazuri na bwana wake na wateja wake huku akijiandaa na kununua uhuru wake. Baada ya kumueleza babu yake na kijana huyo Nia yake mzee alimwambia kwamba hata yeye kazi anayofanya ya kutembeza vitu nyumba Kwa nyumba ni ushirika na bwana wake kwani na yeye alikua mtumwa kama yeye. Kijana aliposikia babu yake alikua mtumwa alikataa kwani anafahamu babu yake alikuwa mtu mwenye fedha nyingi Sana, Lakini hakufahamu alizipataje. Wapo wengi Sana ambao ni matajiri tunawafahamu lakini kama tungefahamu ni namna gani walianza pengine tungewapa heshima zao. Kadri siku zilivyoenda ndivyo mfuko wa sharru ulivyotuna, Kwa kila kiasi cha fedha alichopata aliweka na hata bosi wake alimtegemea Sana, kwani kila sharru alipopata na yeye alipata zaidi, Lakini pesa alizopata huyo bosi wake ziliishia kwenye kamali. Siku moja sharru akiendelea kukanda unga wake Kwa maandalizi ya bidhaa zake alikuja bwana mwingine na kumwambia Sharru kwamba huyo bwana wake ameshindwa kulipa deni lake hivyo inabidi achukuliwe yeye kama fidia. Sharru ni mtumwa hana namna ya kukataa hivyo anakusanya fedha zake na kuambatana na bosi mpya, Kwa bahati mbaya Kwa bosi wake mpya maisha yanakua magumu zaidi, kazi zinakua ngumu na zisizo na maslahi yoyote,Sharru anaanza kukata tamaa ya maisha. Lakini siku moja wanakuja watu kumchukua Kwa kumnunua kama mtumwa na anafukua fuko lake la fedha na kuambatana na watu wale, anafika sehemu aliyonunuliwa anakuta aliyemnunua ni yule rafiki yake, ambaye ni babu wa kijana yule, anafurahi na kujiona ni mtu mwenye bahati kubwa Sana. Anamwambia alimtafuta bila mafanikio na aliposikia aliuzwa kama mtumwa alimfuatilia na kuamua kumnunua, hapo ndipo mwanzo wa ushirika kibiashara ulipoanzia Kati yake na babu yake. Alipofika hapo kijana alifahamu kwamba watu hawazaliwi na kua matajiri bali ni Kwa kuweka kazi, alifurahi kufahamu kisa cha utajiri wa babu yake na kimemfungua kwamba kazi siyo Kwa watumwa pekee bali kiungo cha kununua uhuru wako. Rafiki kazi uliyonayo Sasa ni utumwa wako, pamoja na kwamba inakusaidia lakini siku yoyote bwana wako akishindwa kulipa madeni au sababu nyingine utaondolewa kwenye kazi hiyo na maisha yatakua magumu Sana. Anza leo maandalizi ya kununua uhuru wako Kwa kujifunza biashara, wafundishe watoto zako kutengeneza pesa kuliko kuajiriwa, ukifa leo wanao hawatakula mshahara wako, ila wanaweza simamia biashara ulizozianzisha na ikawa ukombozi kwao. Mwisho wa simulizi ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, bilashaka umeondoka na vitu vya kufanyia kazi. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Wednesday, 14 October 2020

Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli (The luckiest man in babylon) 2

Habari za wakati huu rafiki yangu, ni Ile Ile bahati ya kuweza kuifikia leo inaendelea kwetu, ni mimi na wewe wa kuchagua ni namna gani tunakwenda kuitumia, kulalamika, kubishania siasa na mpira au kuweka kazi na kuhakikisha maisha yetu yanakua bora zaidi..... Sehemu ya pili ya mtu mwenye bahati kuliko wote babeli, Tutaendelea na simulizi yetu, na Tutaendelea pale ambapo Hidan anataka kufahamu ni vipi Sharru Nada aliweza kutengeneza utajiri? Sharru Nada anaendelea na simulizi yake kwamba yeye na babu yake huyo kijana walianza kama watumwa. Yeye alichukuliwa baada ya Kaka yake kuuwa mtu, na mke wa yule mtu aliyeuwawa alimchukua Sharru kama fidia ya kifo cha mumewe. Baadae mama yule aliamua kumuuza Sharru kama mtumwa, wakiwa njiani kwenda kuuzwa walisikia watu wakieleza namna watumwa babeli walivyofanyishwa kazi mpaka kufa. Hili lilimwogopesha Sana Sharru. Lakini mtu mmoja alimwambia Sharru akifika babeli na mtu yeyote atakayejitokeza kununua mtumwa basi ajitokeze na kueleza kwamba yeye anapenda Sana kazi ili anunuliwe na kama asipopata mtu atapelekwa kujenga ukuta wa babeli na huko kulikuwa na kazi ngumu na mateso ya kila aina Kwa watumwa. Magodi alimwambia Sharru kama ukinunuliwa nenda kaipende Sana kazi yako na ifanye Kwa bidii zote na kama mtu huyo hatoithamini kazi hiyo wewe ithamini, usiangalie kile unachozalisha kinakunufaishaje bali ona kitu hicho kinavyowanufaisha wengine. Walipofika babeli Sharru alihakikisha anapata mtu atakayemnunua na kufanya kama alivyoshauriwa na Maggido. Kweli wanafika Babeli na Sharru anapata mtu wa kumnunua na hapo Sharru anajiona ni mtu mwenye bahati Sana Kwa kuweza kununuliwa kama mtumwa. Basi Sharru alipofika Kwa bwana wake huyo aliyemnunua anapangiwa kazi ya kuwasha moto, kukanda unga na kufanya maandalizi mengine ili mikate na keki viandaliwe kwani bwana yule alifanya biashara ya kuuza keki na mikate. Sharru aliweka bidii kubwa Sana na kuhakikisha siyo kwamba anashiriki kwenye maandalizi tu ya kutengeneza keki na mikate bali anafahamu mpaka zinavyotengenezwa, bwana yule alipendezwa Sana na bidii za Sharru kwenye kazi. Siku moja Sharru ndipo alipopata wazo la kuhakikisha anaanza kutengeneza kipato ili aweze kununua uhuru wake na anapata wazo la kutumia Muda wa jioni wa mapumziko kufanya kazi ili apate fedha, anamfata bwana wake na kumueleza wazo hilo, kwamba angetengeneza keki zaidi na jioni kuuza na wangegawana fedha, bwana wake anakubali na Sharru anaanza zoezi hilo mara moja. Mwanzo hali inakuwa ngumu kupata wateja lakini baadae mambo yanaanza kuwa mazuri na kwenye kuuza keki anakuja kukutana na babu yake na Hadan, ilikuwaje na nini kilitokea usikose sehemu inayofuata ili ufahamu Sharru alinunuaje uhuru wake? Rafiki labda Kuna kitu umeanza kukiona kwenye simulizi hii, kwangu naona siku niliyopata ajira ni Sawa na siku Sharru aliyonunuliwa kama mtumwa, alifurahi na alikwenda kuifanya kazi yake Kwa mapenzi yote akifahamu kwamba yeye ni mtumwa, Vipi wewe unaipenda kazi unayofanya? Je unafahamu kwamba wewe ni mtumwa uliyenunuliwa na boss wako? Je mwisho wa utumwa huo ni lini? Kabla hatujaendelea na kisa hiki nenda kayatafakari maswali hayo na Anza mipango ya kununua uhuru wako. Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, tutaonana sehemu inayofuata. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Monday, 12 October 2020

Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli(The luckiest man in babylon)

Habari rafiki yangu, nakusalimu Kwa Jina la Mungu muumba wa ardhi na mbigu, tunakila sababu kufurahia pumzi yenye uhai wa kufanya mimi na wewe tukaweza kupata nafasi ya kuendelea kujifunza ili tusiwe miongoni mwa watakao angamia Kwa kukosa maarifa. Leo tunaendele kuangalia kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu ambacho ukianza kukisoma hutamani kukiweka chini, nimejipa jukumu la kukisoma kila mwezi mpaka nihakikishe ninayaishi yote yaliyomo humu Kwa vitendo, kila ninapokisoma nakiona kipya. *Mtu mwenye bahati kuliko watu wote babeli * Sharu Nada mfanyabiashara ambaye alionekana nadhifu na mtanashati na alimiliki vitu vya thamani Sana, Mwandishi anatuambia huo ulikuwa muoekano wa nje ila ndani allikuwa na matatizo makubwa. Kabla hatujaendelea nimejiuliza Sana kwamba Kuna kumbe Kuna watu wengi Kwa nje tunawaona kama ni watu wenye maisha mazuri na tunatamani kuwa kama wao, Lakini kama tungefahamu undani wao Kwa namna wanavyopitia changamoto kubwa tusingeutamani utajiri huo. Sharru Nada aliongoza msafara wake wa biashara kutoka Damascus kwenda Babeli, pamoja na kwamba njiani kulikuwa na watekaji lakini msafara wake ulikuwa na ulinzi wa kutosha hivyo kwake watekaji hawakumsumbua. Kwenye msafara wake aliongozana na kijana aliyeitwa Hadan Gula, kijana huyu alikuwa mjukuu wa mshirika mwenzie kibiashara miaka ya nyuma, kijana huyu alifanana Sana na babu yake Kwa sura lakini siyo kwenye matendo, kwani hakupenda kazi na alipendelea kuvaa Vito vya thamani, urithi wote walioachiwa kutoka Kwa babu yake, yeye pamoja na baba yake waliuteketeza Kwa sababu hawakufahamu msingi wa fedha. Wakiendelea na safari kuelekea Babeli Hadan Gula alimuuliza Sharru Nada, kila siku uko kwenye misafara ya kibiashara huna Muda wa kupumzika na kufurahia maisha? Ningekuwa wewe ningeishi kama mtoto wa mfalme. Kijana akiwa kavalia heleni na bangiri aliamini kazi ni Kwa ajili ya watumwa lakini Tajiri kama Sharru hakupaswa kujitesa na chochote, wakati Hadan anaongea hayo Sharru aliwaza atawezaje kumsaidia kijana huyu kwani mtazamo alio nao kwenye fedha usingeweza mfikisha popote. Wakiwa njiani aliona watu aliowaacha miaka 40 iliyopita wakifanya kazi zile zile, Kwa kipindi hicho aliziona ni kazi nzuri na alizozitamani lakini leo yeye ameweza kufikia utajiri mkubwa huku wale wanaofanya kazi alizozitamani Wakiwa na maisha ya kawaida.Aliamini kutoka Kwa watu wale ni kwamba wameshindwa kabadilisha mitazamo yao ndio maana maisha yao hayajabadilika. Akiendelea kuwaza atamsaidiaje kijana yule aliyeongozana naye? Akamuuliza swali kama angependa kufahamu yeye na babu yake walikuwaje washirika kwenye biashara? Hidan anamwambia kwanini usiniambie umewezaje kutengeneza utajiri? Hicho ndio nataka kusikia. Pengine na wewe unataka kusikia mwisho wa kisa hiki, basi usikose sehemu ya pili ya kisa cha mtu mwenye bahati kuliko wote babeli. Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, endelea kujifunza kupitia kurasa hizi na nenda kafanyie kazi yote unayojifunza. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Saturday, 10 October 2020

Pain and sickness-opportunities for virtue

Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na waendelea vizuri kabisa na Ile ndoto yako unaifanyia kazi kila siku, haijalishi unapiga hatua zipi kuifikia na changamoto zipi unazipitia hakikisha unakua kile unachotaka. Leo tutaangalia mtazamo ambao unapaswa kuwa nao siku zote na utakufanya uwe na furaha Muda wote, mtazamo huu tutajifunza kutoka Kwa mwanafalsafa EPICTETUS *Maumivu na magonjwa ni chachu ya kutufanya kuwa wema* Tunapitia Maumivu ya kila aina kwenye maisha yetu, pengine ni magonjwa au changamoto mbalimbali za kimaisha, pengine unapitia Maumivu ya kichwa hicho ni kikwazo Kwa mwili lakini siyo kwenye fikra na maamuzi, ni Mara ngapi wakati Tunapitia changamoto ndogo ndipo tunaruhusu maisha yetu yote kuvurugika? ngoja nikupe kisa kifupi cha mwanafalsafa EPICTETUS. Wakati wa Roma watu walikuwa wanamiliki watumwa na EPICTETUS alikuwa ni moja wa watumwa, kama tunavyofahamu mtumwa hana haki yoyote, pamoja na utumwa lakini aliumia mguu wake na kuwa mlemavu, Kwa usual aliishi maisha ambayo hakuwa na sababu yoyote ya kumfanya awe na furaha. Pamoja na yote hayo falsafa ilimfanya awe na maisha bora Sana, yeye aliamini kwamba kitu ambacho hakuna mtu anaweza kutunyang'anya ni namna ya kufikiri kwetu. Kuumwa, kuwa kwenye hatari hata kama kukikabili kifo tunapaswa kuwa na furaha na kushukuru Kwa nafasi ya maisha tuliyokuwa nayo mpaka Sasa, leo tunajifunza mengi kutoka Kwa mtumwa huyu. Yeye anaamini kukosa furaha ni matatizo binafsi na ni mtazamo wa fikra ndio unaotusumbua na siyo vitu vya nje. Hebu chukulia mfano unaumwa homa, ukianza kulalamika kwamba umeshindwa kwenda kazini ni kuamua kujiumiza zaidi, Lakini ukiwaza kwamba ni Muda ambao utapata nafasi ya kuwa karibu na familia yako, pengine umekuwa Muda mwingi unautumia zaidi kwenye kazi kuliko familia, pengine Kwa Muda mrefu umekosa Muda wa kupumzisha mwili wako, EPICTETUS alifahamu Kuumwa mguu ni kikwazo Kwa mwili na siyo akili yake na ndio maana pamoja na yote Muda wote alikuwa mtu wa furaha pamoja na ulemavu na utumwa wake. Je wewe rafiki yangu tatizo gani linalokunyima furaha? Amini hakuna jambo au mateso yoyote ya kuharibu namna ya kufikiri kwako labda uwe umeruhusu mwenyewe. Nenda kaishi Kwa matumaini na jiandae na changamoto zozote zitakazojitokeza mbele yako, yapo mengi huwezi kuyabadili, jipe Muda na yote yatapita.Falsafa inatuambia hakuna watu wenye matatizo ya akili bali Kuna watu wanaojaribu kutoroka matatizo yao Kwa kuchagua kulalamika. Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Thursday, 8 October 2020

Msingi muhimu wa biashara unaopaswa kulielewa.

Hongera Sana rafiki yangu Kwa kuchaguliwa tena kuifikia siku ya leo, wapo wengi walilala na mipango mizuri ya kuifanya leo lakini hawakuamka, wewe umefanikiwa kuifikia leo je ni yapi umepanga kufanya? Kama ni mipango Ile Ile ya kila siku je umejiandaa kupata matokeo tofauti? Nenda katekeleze zaidi ili uitendee haki siku hii. Kila kitu ambacho tunakifanya kinaanzia na msingi, na ndio maana Mwandishi wa kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA ametuandalia masomo haya akiamini kwamba ukiyafuata utakua imara kwenye fedha pamoja na changamoto zake. Ili nyumba isiweze kudondoshwa na tetemeko au upepo inahitaji msingi imara, vivyo hivyo na kwenye biashara unayofanya kama biashara haina misingi inayosimamia basi kudondoka ni hakika. Je biashara imara inahitaji misingi gani? Msingi wa kwanza wa biashara yoyote ni THAMANI, kwani tulishajifunza kwamba ili uweze kupata fedha lazima ubadilishane thamani na mwingine, hivyo kabla hujaanza biashara jiulize ni thamani gani nitawapa wengine Kisha wanipe fedha zao? Ni kipi nitatoa kwao wakaamua kunipa fedha zao walizozitafuta Kwa shida? Siri nyingine ambayo ni msingi wa biashara yoyote ni KIPI NAFANYA NA WENGINE HAWAPO TAYARI KUKIFANYA kwenye biashara lazima uwe tofauti na wengine, lazima mteja apate kitu kwako ambacho kwingine siyo rahisi kukipata, kama unafungua biashara Kwa sababu umepata mtaji na unafanya kawaida kama wengi wanavyofanya basi utapata matokeo kama wengi wanavyopata Mwandishi anasema kama mteja anaweza kupata Kwa wengine kile anachokipata kwako, ukweli ni kwamba huna biashara, upo katikati ya kelele. Na kama umeamua kuingia kwenye biashara ambayo kila mtu anafanya basi ifanye Kwa namna tofauti na wengine wanavyoifanya. Ipo Siri nyingine kubwa Sana kwenye biashara ambayo Mwandishi anasema huwezi isikia popote, biashara zote zenye mafanikio Zina sifa hiyo, Sifa hiyo ni KUHODHI biashara hizo au sehemu ya biashara hiyo, kama biashara unayofanya haitawali sehemu kubwa ya soko basi biashara hiyo ukuaji wake unakuwa mgumu Sana. KUHODHI huko isiwe ni Kwa kuwakandamiza wengine bali unapaswa kuwa bora zaidi ya wengine. Rafiki kwenye biashara yako nenda the katoe thamani kubwa, jitofautishe na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama unayofanya wewe, na hodhi sehemu ya soko la biashara yako. Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na uwe na siku Njema. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Wednesday, 7 October 2020

Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli sehemu ya pili....

Habari za wakati huu rafiki yangu, ikiwa ni siku nyingine tulivu na nzuri tumshukuru mungu wetu Kwa zawadi ya uhai, twende tukaitumie zawadi hii Kwa kuyatenda yampendezayo karibu..... Bilashaka Jana umejifunza kitu kwenye sehemu ya kwanza ya mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli na leo tutamalizia sehemu ya pili. Debasir aliendelea kuelezea maisha yake ya awali na watu waliendelea kuongezeka kumsikiliza, Debasir anasema baada ya kukimbia wadeni wake ilibidi auzwe kama mtumwa Kwa Tajiri mmoja na alikua akifanya kazi ya kuhudumia ngamia, pamoja na kwamba alifanya kazi hiyo kama mtumwa hakukubaliana na hali ya kwamba yeye ni mtumwa na pale mke wa Tajiri aliyemnunua alipotaka kufahamu kwanini Debasir hakukubaliana na hali ya utumwa ndipo Debasir anaelezea maisha yake ya awali, familia yenye uwezo na amemkimbia mke wake na ndugu zake Kwa sababu ya madeni hivyo hataki kukubali kwamba utumwa ndio mwisho wake, Nira anamuuliza kama anajiona ana roho ya utumwa au mtu huru? Debasir anajibu anajiona ni mtu huru, Nira mke wa tajiri anamwambia kama unaroho ya mtu huru tuthibitishie hilo nenda na uwakabili wadeni wako ili uwe huru. Siku moja Nira yule mke wa Tajiri alimwambia Debasir aandae ngamia kwani anataka kwenda kumtembelea mama yake, Debasir anaandaa ngamia na wanakwenda na ngamia wawili na wanapofika Kwa mama yake Nira anafukuza watumwa wengine na anampa nafasi Debasir ya kutoroka na ngamia wawili ili arudi akawakabili wadeni wake na awe huru Tena, Debasir anamshukuru Nira na anaanza safari na ngamia wawili huku Nira akijitetea Kwa mume wake kwamba Debasir ametoroka na ngamia wale. Safari ya kurudi nyumbani inakua safari ngumu na ya mateso kwani hakuifahamu njia vizuri na alipita kwenye jangwa na kiu ya maji pamoja na njaa vilimtesa Sana na baadae alianza kuona hakuna dalili ya kuishi kwani kifo kipo karibu. Lakini alipokumbuka swali kutoka Kwa Nira kama yeye ni mtu huru au mtumwa alijihisi kupata nguvu upya ya kusonga mbele kwani akifa atakufa kama mtumwa, baada ya siku kadhaa alifika sehemu yenye maji na matunda na hapo ndipo akaona ana uhakika wa kufika nyumbani. Ndipo anamgeukia Tarkadi mdeni wake na kumwambia je Kwa njaa hii uliyo nayo leo upo tayari kuwafuata wadeni wako wote na kulipa madeni yako ili uwe huru tena au utaendelea kukimbia?Tarkadi akasema simulizi hii imenipa mwanga na Sasa naona dunia Kwa uhalisia wake nitayakabili madeni yangu niwe huru tena. Mtu mmoja Kati ya waliokuwa wakimsikiliza Debasir walitaka kufahamu alipofika babeli nyumbani alifanikiwa kulipa madeni yake yote? Ndipo Debasir akasema aligundua walio mkopesha ni marafiki zake adui yake mkubwa ni madeni, hivyo aliwatafuta wadeni wake na kuwaeleza nia ya kuwalipa aliyonayo, wengi walifurahi lakini wengine walitaka kumpiga Kwa sababu walikasirika Sana. Debasir anasema Kati ya wanao mdai walipomuona ana nia ya kulipa madeni, mtu mmoja alimuunganisha na wafanyabiashara wa ngamia kwani walifahamu anao uzoefu kwenye ngamia na alifanikiwa kulipa madeni yote na Sasa ndio huyu mfanyabiashara mkubwa wa ngamia babeli. Rafiki kisa hiki kina mafunzo mengi Sana, wapo watu kila siku wanakimbia huku na huko ili kuwakwepa wanao wadai Kwa kuona ni maadui zao, kumbe maadui zao ni tibia zao za kukopa na madeni ndio maadui zao wakubwa ambao wapo nao na wanaenda nao kila sehemu hivyo kama unataka kuwa huru wakabili wadeni wako na walipe Kisha hali mikosi na bahati mbaya hazitaendelea kukuandama. Debasir alikataa hali ya utumwa na akajitenga nao hata wewe kataa utumwa wa madeni, tafuta uhuru wako leo. Asante Sana rafiki yangu, nimeona nikuletee somo hili leo badala ya wiki inayofuata kwani wengi wameona wiki ijayo ni mbali, nikutakie siku Njema rafiki yangu na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Tuesday, 6 October 2020

Mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli (The Camel trader of Babylon)

Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na unaendelea salama na ratiba zako za kila siku, umejipangaje kua bora zaidi ya Jana, kufanya yaliyosahihi na kuachana na yale yasiyo na tija kwenye siku hii unayo iendea?.... Rafiki yangu karibu tuchambue kitabu pamoja, leo tutajifunza kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kupitia mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli, ni somo zuri Sana ambalo wakati nikipasoma sitamani kuweka kitabu chini bali kuendelea kusoma, karibu tuwe sote mpaka mwisho wa makala hii. Tarkad mtoto wa Azure alikua akipita mtaaini akiangaza macho karibu na sehemu wanazouza chakula pengine angeweza kukutana na mtu ambaye anamfahamu ili amkopeshe fedha na kumnunulia chakula, anasema akili hufikiria Sana harufu ya chakula wakati una njaa kali. Wakati anaendelea kuangaza hapa na pale ndipo anakutana na mtu ambae hakutaka kukutana naye, mtu huyo si mwingine bali Debasir mfanyabiashara wa ngamia aliyemkopesha fedha na kutomlipa kama walivyokubaliana Debasir anafurahi kukutana na mdeni wake na anapohitaji kulipwa deni lake Tarkad anajieleza kwamba hana pesa na amekua na bahati mbaya.Hilo linamshangaza Debasir kwamba watu wote wenye bahati mbaya ni wale wanaofikiria kukopa kuliko kulipa madeni yao. Basi Debasir anamwambia Tarkad amfate na atampa hadithi moja itakayomfundisha. Na wanakwenda kukaa ndani ya sehemu inayouza chakula na Debasir anaagiza mguu wa mbuzi na mkate pamoja na mboga mboga na Juice Kwa sababu alikua na njaa Sana, Lakini anamwambia muhudumu asimsahau na rafiki yake Tarkad Kwa kumletea maji ya kunywa ya baridi kwani joto lilikua kali Sana, Tarkad alisikitika Sana kwani pamoja na njaa ya siku mbili anakweda kukaa akiangalia mtu akila mguu wa mbuzi huku yeye akiendelea kumkodolea macho, Kwa kua alidaiwa na amepewa ahadi ya kupewa hadithi itakayokwenda kumfundisha na kumuondoa kwenye utumwa wa madeni ilibidi akae na kusikiliza. Debasir alianza kuelezea maisha yake ya huko nyuma ya kuishi Kwa kukopa na kujificha akikimbia wale waliomkopesha mpaka kuuzwa kama mtumwa lakini baadae anafanikiwa na kuwa mfanyabiashara mkubwa wa ngamia wa Babeli. Nini kilitokea, tusubirie sehemu ya pili ya simulizi hii tutaona nini Debasir alifanya mpaka kuushinda umasikini na Kuja kua mfanyabiashara mkubwa. Ondoka na somo hili kwamba bahati mbaya huwaendea wale wote ambao wanafurahia mkopo na kuchukizwa kulipa deni hilo, Lakini pia huangalia ni wapi kwingine ataweza kukopeshwa. Ninakupenda Sana rafiki yangu, nikutakie siku Njema na mungu akubariki. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

Sunday, 4 October 2020

Nifanye nini pale Malango ya kiroho, kiuchumi na kihisia yanapofungwa?

Habari za wakati huu mpendwa rafiki yangu, Tumefanikiwa kulifikia juma lingine, bilashaka Kuna mengi yako mbele yetu ya kuyafanikisha, nikutie nguvu kwamba haijarishi ni magumu yapi unayapitia basi tambua hupaswi kurudi nyuma...... Rafiki yangu kila mmoja anafahamu nini maana ya neno mlango na kazi zake, sehemu yoyote ambayo unatumia kuingia na kutokea ni lango. Leo napenda kukuletea uchambuzi wa kitabu cha Kaka yangu Mwalimu na mchungaji JOSEPHAT ULOMI, kwenye kitabu chake cha YAJUE MALANGO YANAYOWEZA KUKUFANIKISHA AU KUDIDIMIZA MAISHA YAKO KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA ana mengi ya kutufundisha. Lango la kwanza ambalo ndilo tutaliangalia leo ni LANGO LA MSAMAHA. Mwandishi ameanza Kwa kuangalia lengo kuu la kila mwanadamu ni kuishi maisha ya furaha, Amani na uhuru na hivyo kuyapata haya ni lazima uwe tayari kuachana na na mawazo yoyote hasi na yatakayokuzuia kufikia adhima yako hiyo. Mwandishi anaamini kanuni kubwa ya maisha ya furaha inapatikana kwenye kauli ifuatayo. Wewe ni mzima wa akili Kwa kiwango kile unachoweza kusamehe bure, kusahau na kuachilia Kwa yale na vyote vilivyo kuumiza. Hivyo kutokusamehe ni kujiweka kifungoni wewe mwenyewe na pale unapohitaji kutoka kwenye kifungo basi funguo ni kusamehee. Mwandishi amegawa makundi manne ambayo unapaswa kusamehe na kujirudishia uhuru wako kua ni; 1.Wazazi wako Wengi Sana wamejiweka kifungoni Kwa kushindwa kuwasamehe wazazi au walezi wao, pengine Kuna mengi kweli walipaswa kukufanyia kama kukupeleka shule na kukuonyesha upendo lakini hawakufanya hivyo, hivyo Kwa kila changamoto unayopitia unaona wao ndio sababu na kujikuta Muda mwingi hutumii kutatua changamoto zinazokukabili bali kulalamika na kubaki kifungoni. 2.Kundi la pili ni wale watu waliokuwa na uhusiano wa karibu Sana kwetu. Pengine ulimkabidhi mtu akili na moyo wako wote na ulimwamini Sana lakini akaja kukufanyia kitu kibaya Sana. Kama hatutofikia hali ya kusamehe tunajikuta kwenye hali ya kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo, namna ya kuondokana na hali ya chuki na ya kutosamehe watu hawa ni wakujiona wewe mwenyewe umechangia kuingia kwenye mahusiano usiyo yafahamu vizuri hivyo unapaswa kujisamehe na kumsamehe aliyekukosea pia. 3.Kundi la Tatu ni kumsamehe kila mtu. Kila aliewahi kukukosea una kila sababu ya kumsamehe bure na kusahau. 4.Kundi la nne na la mwisho ni kujisamehe wewe mwenyewe. Rafiki Kuna mengi Sana yalitokea kwenye maisha yako na unaona wewe ndio ulikua chanzo na unatamani ungefuta hali hiyo na kuibadili lakini haikuwezekana, hivyo Muda mwingi unautumia kujilaumu na kujiambia laiti ningelijua ningefanya moja, mbili, tatu. Kujilaumu ni kujiweka kwenye kifungo kikubwa Sana. Hivyo rafiki yangu msamaha ni lango la mafanikio yako, kama hutojisamehe na kusamehe wengine basi utakua huna faida duniani wala mbinguni, kote utakua umejiweka kwenye kifungo. Tutaendelea kuona Malango mengine kwenye kila siku kama ya leo, Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944