Wednesday, 30 September 2020
Biashara, njia ya uhakika ya kutengeneza kipato kisicho na ukomo
Habari rafiki yangu, bilashaka mimi na wewe tunapaswa kuanza siku hii Kwa kumshukuru mungu, ukiangalia ni vitu vingi Sana tunavyo kama zawadi, ukiangalia wapendwa, ndugu na marafiki na Afya zetu ni zawadi kubwa Sana kwetu.....
Leo tunaangalia umuhimu wa biashara kwenye maisha yetu, na kwanini kama kweli unataka kufikia uhuru wa kifedha lazima ujihusishe na biashara.
mwandishi wa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA anatukumbusha kwamba tofauti ya mapato na matumizi ndio itakayo amua wewe uwe masikini au Tajiri, yaani kama unatumia zaidi ya kile unachopata basi unakua unajiondolea nafasi ya kufanikiwa, Lakini hata kama utabana namna gani kipato chako lazima matumizi ya msingi yafanyike, huwezi Sema sitakula Kwa sababu nikila matumizi yatazidi kipato au kusomesha watoto na matumizi mengine ya msingi.
Kwanini njia zingine kama Ajira haziwezi kukupa uhuru wa kifedha?
Kwa upande wa Ajira huwezi Pata uhuru wa kifedha Kwa sababu unalipwa Kwa kusubiria maamuzi ya mtu mwingine, hata kama utaongeza bidii na kuzalisha zaidi bado huna maamuzi ya kujilipa zaidi,Lakini pia hata unapoamua kujiajiri hakikisha kile ulichojiajiri nacho unakitengenezea mfumo mzuri wa kuhakikisha hakikutegemei wewe moja Kwa moja.
Biashara yenye mfumo mzuri ndio tiba tiba ya ukomo wa kifedha.
Haijalishi unaweka bidii namna gani kama kile unachojihusisha nacho kama kinakuhitaji moja Kwa moja basi utafika sehemu ya ukomo wa Muda, ukomo wa nguvu na hapo ndipo biashara yenye mfumo mzuri itakua mkombozi kwako, kwani ukilala kitandani fedha itaendelea kuingia, ukifikia uzee fedha itaendelea kuingia.
Hili halihitaji kwenda shule na kuchukua degree kulielewa kwani jamii inayokuzunguka itakuonyesha ukweli huu na utaona wale wenye mfumo mzuri walivyohuru kwenye fedha na fedha zinawafanyia kazi siku zote.
Tutaendelea kujifunza zaidi somo hili la biashara Kwa kuangalia namna ya kujenga misingi imara ya biashara yako.
Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu, nakupenda daima na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Monday, 28 September 2020
Nenda nyumbani mwambie mke wako ukuta wa babeli ni imara utawalinda nyie na Mali zenu
Habari za wakati huu rafiki yangu, ni bahati nyingine ya kipekee mimi na wewe tumeweza Kuiona siku hii, twende tukaitumie Kwa yale yaliyo muhimu na yasiyo na tija tuachane nayo.....
Kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON ipo hadithi moja inayoelezea uimara wa kuta zilizozunguka mji wa babeli.
Kama tulivyojifunza kwamba babeli ulikua ni mji wenye utajiri mkubwa Sana, hili lilitokana na maarifa waliyonayo kuhusu fedha na bidii ya watu wa mji huo, Lakini kama tujuavyo watu wakishafahamu sehemu Kuna Mali watapambana kuipata Mali hiyo.
Siku moja mfalme wa babeli alisafiri na jeshi lake kuu kuelekea nchi za mbali na mwanya huo ulitumiwa na maharamia walio kua na siraha wakitaka kuufanyia mateka na kupora Mali zote za mji huo.
Wananchi wa babeli waliingiwa na hofu kubwa kwani walifahamu kwamba kufanikiwa Kwa mateka hao kuingia babeli ingekua mwisho wa uhuru wao, Mali zao na hata utu wao.
Kutokana na mji huo kua na kuta imara haikua rahisi kuingia babeli lakini watekaji hawakukukata tamaa ya kutaka kuingia babeli, wakati yote hayo yakiendelea yupo askari mmoja aliyeitwa Banzar alikua akitoa taarifa Kwa Wananchi wa babeli hali ya uvamizi ule ilikua inaendeleaje ili kuwapa Wananchi taadhali endapo mambo yangewaendea vibaya.
Wamama na watoto Kwa wazee walikua wakihofu zaidi kwani wao ndio wangekua wahanga wakubwa kama babeli ikivamiwa, hivyo Muda wote walifika Kwa askari huyo kuulizia hali inakwendaje, Lakini Banzar alimjibu kila aliyemuuliza kwamba wewe watulivu kwani ukuta wa babeli ni imara na utawalinda.
Baada ya wiki Tatu na zaidi wavamizi walikata tamaa na kuondoka babeli na Wananchi walitoka ndani walikojificha Kwa hofu wakishangilia kwani ukuta wa babeli Kwa uimara wake waliokolewa dhidi ya mateka.
Rafiki yangu hata kwenye fedha na utajiri wako unahitaji kuwa na kuta imara kama za mji wa babeli ili kuulinda utajiri wako na mfano wa kuta hizo ni kama zifuatazo hapa chini.
1.Kuwa na bima ya vitu mbalimbali unavyomiliki ni ukuta dhidi ya Mali hizo.
2.Kuwa na akiba iliyo sehemu salama ni kuta imara dhidi ya utajiri wako.
3.Kuwekeza katika uwekezaji imara na unaoaminika ni kuta imara na itakulinda dhidi ya pesa zako na utajiri wako.
Nikutakie siku Njema rafiki yangu na kazi Njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944 /0712161251
Sunday, 27 September 2020
Jipe majibu sahihi ya maswali haya
Hongera Sana rafiki yangu Kwa kuweza kupata bahati ya kuifikia siku hii, bilashaka uko tayari kwenda kupambana na mikiki mikiki ya siku, karibu tuendelee kujifunza kupitia maswali.......
Kabla hatujaangalia maswali ya kujiuliza nikuambie kitu kimoja, maswali ni njia bora Sana ya kujifanyia tathimini kwani yanakuonyesha uko wapi na unataka kufika wapi.
Karibu uweze kutenga Muda wako na kujipa majibu sahihi.
1.Je unaipenda kazi yako? kama sivyo ni kwanini?
rafiki ni wengi Sana wanafanya kazi wasizo zipenda lakini ukiwauliza sababu za kutopenda wengi watasema haziwalipi vizuri, je na wewe sababu ni hiyo?Je umepanga kuondoka lini kwenye kazi hiyo usiyoipenda? Au utaendelea na utumwa huo maisha yako yote?
2.Vipi ukijiangalia kadri unavyokua uwezo wako wa kujiamini unaongezeka au unapungua?
Fahamu hili na lifanyie kazi mapema.
3.Je unajifunza kutokana na makosa yako au unarudia makosa yaleyale kila siku?
4.Ni nani shujaa wako na unajifunza kwake na kila siku anakupa msukumo zaidi wa kuzifikia ndoto zako?
5.Una ndoto gani kubwa inayoeleweka? Kama ipo ni ipi hiyo? Na je ni mipango gani uliyo nayo kuifikia Naoto hiyo?
Rafiki kama utaweza kukaa chini na kujipa majibu ya maswali haya Kwa usahihi? Nina hakika Kuna sehemu unakwenda ila kama utaona unakosa majibu naomba tuwasiliane kwani nina amini utakua mwanzo mzuri.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Unajifunza nini kwenye kisa hiki kifupi?
Habari za wakati huu rafiki, una maadui wengi Sana na adui yako mkuu ni yule unayemuona ukijitazama kwenye kioo, adui wengine ni mazoea na kutojifunza, hebu jiulize wiki hili la 39 tangu mwaka umeanza linakwisha umefanya nini? Je umejifunza nini?.......
Leo nataka tujifunze kitu kimoja ambacho kilinipa ujasili kwenye mambo mengine mengi Sana na yamenisaidia Sana.
Nimetoka nyumbani naelekea bank na nina uhitaji wa haraka na fedha ninazohitaji kutoa Kwa njia ya ATM kufika nakuta foleni ni ndefu na Kati ya ATM tatu ni moja tu ndio inafanya kazi bahati mbaya ilikua ni siku ya jumapili na bank zimefungwa siwezi tolea ndani na bahati mbaya habari ya mawakala haikuwepo Kwa wakati huo, wakati najiuliza nifanyaje nikajiuliza nani kasema hizo ATM mbili hazifanyi kazi? Nikagundua ni askari anayelinda hapo alikua akiwaelekeza watu kwamba hizo ATM mbili hazifanyi kazi Lakini Kwa wakati huo hayupo eneo la ATM bali yuko pembeni anaongea na mtu, Kwa sababu nilikua na haraka nilimuomba aliyekua nyuma yangu ngoja nikaangalie pengine mtandao umerudi na kama sivyo ningerudi kwenye foleni yangu, nilipofika nilikuta mtandao uko Safi na bahati nzuri na Ile ATM nyingine mambo yalikua hivyo hivyo,nikatoa fedha na kila mtu akashangazwa kwamba tumetumia ATM moja Kwa shida wakati ATM zote zilikua zinafanya kazi, rafiki pengine kwako tukio hili lisiwe na maana lakini kwangu lilinipa sheria.
KWANGU MWENYEWE
1.Nikiwa na shauku ya jambo lolote siangalii changamoto zilizopo mbele yangu bali kile ninachohitaji Kwa mbinu na gharama yoyote.
2.Asili itakuruhusu kukupatia unachotaka kama kweli kutoka moyoni unakihitaji.
3.Sikia lakini usiamini kirahisi thibitisha kile unachokisikia.
4.Acha kufuata wingi tumia njia zako.
ASKARI
Usiwaongoze watu kwenye jambo ambalo wewe mwenyewe hulifahamu ki undani na hujalisimamia ipasavyo.
Kama Kuna la Ziada umejifunza kwenye kisa hiki naomba unishirikishe Kwa njia yoyote Kati ya hizi hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Thursday, 24 September 2020
Fate leads the willing and drags along the reluctant - Seneca
Mungu watu ni mwema Sana kuweza kutufanya mimi na wewe kuifikia siku hii, siyo kitu rahisi kwani wapo wengi Sana walitamani na imeshindikana, Kwa kulitambua hilo basi tuanze siku yetu Kwa kufanya yale ya msingi na kuacha kuutumia Muda wetu Kwa mambo ya siyo na tija......
Leo tunaangalia kauli ya mwanafalsafa Seneca ambayo inatupa zoezi la kufanyia kazi kila siku Kwa wiki nzima.
Rafiki yangu pale unapoanza kushindana ndipo mwanzo wako wa kushindwa unapoanza kwani chochote unachoshindana nacho unakipa nguvu dhidi yako. Hata kama una nguvu kiasi gani lazima ukubaliane na matokeo kwamba huwezi lazimisha na kuwazuia watu namna wanavyokufikiria.
Wapo watu wengi wanaoteseka na historia za maisha yao, hutamani kubadilisha hali zilizojitokeza kwenye maisha yao, historia ya elimu yako siyo muhimu Kwa Sasa, hali yako mbaya ya kimahusiano iliyokutesa huko Nyuma usiipe nafasi leo.
Pale utakapoanza kuyakubali madhaifu yako na kuruhusu maisha yako yaendelee, huku ukiangalia ni wapi unataka kufika na kujitaidi kutimiza yanayokupeleka huko ndio unaanza kukua, kubali Kuna vingi hujui na Anza kujifunza Mara moja, wape watu nafasi ya kuishi wanavyotaka na wewe ishi maisha yako huku ukifahamu Kuna vingi huwezi vibadili na haviwezi kua vile unavyotaka wewe, kukataliwa, kusemwa na wengine,kukejeriwa na kudharaurauliwa ni vitu ambavyo havitakiwi kukuumiza kichwa, wewe jipe sababu ya kuendelea na maisha yako na kubali mengine yako nje ya uwezo wako vipokee na vikubali.
Makala hii imeandikwa na mimi rafiki yako Mwl Kelvin Kinyaga, unaweza nipata zaidi Kwa mawasiliano binafsi hapa chini.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogsport.com
0712161251 /0763766944
Monday, 21 September 2020
Maswali ya kujiuliza unapotaka kukopa Kwa ajili ya kuanza biashara.
Hangera Sana rafiki yangu Kwa kuendelea kujifunza kupitia kurasa zangu za Ustawi wa fire, Leo tutakwenda kuangalia mambo ya msingi unayopaswa kuangalia kabla hujachukua mkopo ili kuanzisha biashara.......
Kwanza kabida unakumbuka tulijifunza kutoka kwenye kitabu cha Elimu ya msingi kuhusu fedha kwamba kukopa ili kuanzisha biashara no mkopo Mbaya. Leo tutajifunza Kwa kina kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kama mkopeshaji fedha babeli anavyotufundisha.
Kwanza kabisa Kwa yeyote anayetaka kukopa au kukopeshwa lazima ajiulize maswali kadha ya msingi. Na zaidi kabla hujamkopesha mtu hakikisha unafahamu yafuatayo.
A. Fedha unazokopa/anazokopa kwako ni za nini?
B. Kama ni Kwa ajili ya kufanya biashara je unao uzoefu au ujuzi na biashara hiyo?
C. Je unafahamu ni wapi utanunua Kwa bei ndogo zaidi unachotaka kuuza?
D. Je unafahamu ni wapi unapoweza kuuza Kwa bei nzuri na na kupata faida?
Rafiki Kwa wakopeshaji na wakopaji huwa na matamanio ya kupata wanachotaka, mkopeshaji ana tamaa ya kupata riba na mkopwaji huwa na tamaa ya kupata fedha ili kukamilisha alichopanga kufanyia fedha anazokopa Lakini mwisho wa siku wote hujikuta kwenye matatizo makubwa ya kifedha.
Taasisi za kifedha wako makini Sana kwenye hili na ndio maana hutoa mkopo pale dhamana ya mkopaji inapokua kubwa kuliko mkopo uliochukua, hivyo nenda kalifanyie kazi somo hili,usimkopeshe wala kukopa na kujikuta badala ya kumsaidia unayemkopesha unamuingiza kwenye matatizo makubwa zaidi na wewe pia kupoteza fedha zako, Pima hatari za mkopo unaochukua au kukopesha ili kuleta usalama wako wa kifedha.
Asante na nikutakie siku Norma, ili kujifunza zaidi fungua
https://kinyagakelvin.blogsport.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Posts (Atom)