Monday, 28 September 2020

Nenda nyumbani mwambie mke wako ukuta wa babeli ni imara utawalinda nyie na Mali zenu

Habari za wakati huu rafiki yangu, ni bahati nyingine ya kipekee mimi na wewe tumeweza Kuiona siku hii, twende tukaitumie Kwa yale yaliyo muhimu na yasiyo na tija tuachane nayo..... Kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON ipo hadithi moja inayoelezea uimara wa kuta zilizozunguka mji wa babeli. Kama tulivyojifunza kwamba babeli ulikua ni mji wenye utajiri mkubwa Sana, hili lilitokana na maarifa waliyonayo kuhusu fedha na bidii ya watu wa mji huo, Lakini kama tujuavyo watu wakishafahamu sehemu Kuna Mali watapambana kuipata Mali hiyo. Siku moja mfalme wa babeli alisafiri na jeshi lake kuu kuelekea nchi za mbali na mwanya huo ulitumiwa na maharamia walio kua na siraha wakitaka kuufanyia mateka na kupora Mali zote za mji huo. Wananchi wa babeli waliingiwa na hofu kubwa kwani walifahamu kwamba kufanikiwa Kwa mateka hao kuingia babeli ingekua mwisho wa uhuru wao, Mali zao na hata utu wao. Kutokana na mji huo kua na kuta imara haikua rahisi kuingia babeli lakini watekaji hawakukukata tamaa ya kutaka kuingia babeli, wakati yote hayo yakiendelea yupo askari mmoja aliyeitwa Banzar alikua akitoa taarifa Kwa Wananchi wa babeli hali ya uvamizi ule ilikua inaendeleaje ili kuwapa Wananchi taadhali endapo mambo yangewaendea vibaya. Wamama na watoto Kwa wazee walikua wakihofu zaidi kwani wao ndio wangekua wahanga wakubwa kama babeli ikivamiwa, hivyo Muda wote walifika Kwa askari huyo kuulizia hali inakwendaje, Lakini Banzar alimjibu kila aliyemuuliza kwamba wewe watulivu kwani ukuta wa babeli ni imara na utawalinda. Baada ya wiki Tatu na zaidi wavamizi walikata tamaa na kuondoka babeli na Wananchi walitoka ndani walikojificha Kwa hofu wakishangilia kwani ukuta wa babeli Kwa uimara wake waliokolewa dhidi ya mateka. Rafiki yangu hata kwenye fedha na utajiri wako unahitaji kuwa na kuta imara kama za mji wa babeli ili kuulinda utajiri wako na mfano wa kuta hizo ni kama zifuatazo hapa chini. 1.Kuwa na bima ya vitu mbalimbali unavyomiliki ni ukuta dhidi ya Mali hizo. 2.Kuwa na akiba iliyo sehemu salama ni kuta imara dhidi ya utajiri wako. 3.Kuwekeza katika uwekezaji imara na unaoaminika ni kuta imara na itakulinda dhidi ya pesa zako na utajiri wako. Nikutakie siku Njema rafiki yangu na kazi Njema. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0763766944 /0712161251

No comments:

Post a Comment