Wednesday, 30 September 2020
Biashara, njia ya uhakika ya kutengeneza kipato kisicho na ukomo
Habari rafiki yangu, bilashaka mimi na wewe tunapaswa kuanza siku hii Kwa kumshukuru mungu, ukiangalia ni vitu vingi Sana tunavyo kama zawadi, ukiangalia wapendwa, ndugu na marafiki na Afya zetu ni zawadi kubwa Sana kwetu.....
Leo tunaangalia umuhimu wa biashara kwenye maisha yetu, na kwanini kama kweli unataka kufikia uhuru wa kifedha lazima ujihusishe na biashara.
mwandishi wa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA anatukumbusha kwamba tofauti ya mapato na matumizi ndio itakayo amua wewe uwe masikini au Tajiri, yaani kama unatumia zaidi ya kile unachopata basi unakua unajiondolea nafasi ya kufanikiwa, Lakini hata kama utabana namna gani kipato chako lazima matumizi ya msingi yafanyike, huwezi Sema sitakula Kwa sababu nikila matumizi yatazidi kipato au kusomesha watoto na matumizi mengine ya msingi.
Kwanini njia zingine kama Ajira haziwezi kukupa uhuru wa kifedha?
Kwa upande wa Ajira huwezi Pata uhuru wa kifedha Kwa sababu unalipwa Kwa kusubiria maamuzi ya mtu mwingine, hata kama utaongeza bidii na kuzalisha zaidi bado huna maamuzi ya kujilipa zaidi,Lakini pia hata unapoamua kujiajiri hakikisha kile ulichojiajiri nacho unakitengenezea mfumo mzuri wa kuhakikisha hakikutegemei wewe moja Kwa moja.
Biashara yenye mfumo mzuri ndio tiba tiba ya ukomo wa kifedha.
Haijalishi unaweka bidii namna gani kama kile unachojihusisha nacho kama kinakuhitaji moja Kwa moja basi utafika sehemu ya ukomo wa Muda, ukomo wa nguvu na hapo ndipo biashara yenye mfumo mzuri itakua mkombozi kwako, kwani ukilala kitandani fedha itaendelea kuingia, ukifikia uzee fedha itaendelea kuingia.
Hili halihitaji kwenda shule na kuchukua degree kulielewa kwani jamii inayokuzunguka itakuonyesha ukweli huu na utaona wale wenye mfumo mzuri walivyohuru kwenye fedha na fedha zinawafanyia kazi siku zote.
Tutaendelea kujifunza zaidi somo hili la biashara Kwa kuangalia namna ya kujenga misingi imara ya biashara yako.
Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu, nakupenda daima na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251/0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment