Sunday, 4 October 2020
Nifanye nini pale Malango ya kiroho, kiuchumi na kihisia yanapofungwa?
Habari za wakati huu mpendwa rafiki yangu, Tumefanikiwa kulifikia juma lingine, bilashaka Kuna mengi yako mbele yetu ya kuyafanikisha, nikutie nguvu kwamba haijarishi ni magumu yapi unayapitia basi tambua hupaswi kurudi nyuma......
Rafiki yangu kila mmoja anafahamu nini maana ya neno mlango na kazi zake, sehemu yoyote ambayo unatumia kuingia na kutokea ni lango.
Leo napenda kukuletea uchambuzi wa kitabu cha Kaka yangu Mwalimu na mchungaji JOSEPHAT ULOMI, kwenye kitabu chake cha YAJUE MALANGO YANAYOWEZA KUKUFANIKISHA AU KUDIDIMIZA MAISHA YAKO KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA ana mengi ya kutufundisha.
Lango la kwanza ambalo ndilo tutaliangalia leo ni LANGO LA MSAMAHA.
Mwandishi ameanza Kwa kuangalia lengo kuu la kila mwanadamu ni kuishi maisha ya furaha, Amani na uhuru na hivyo kuyapata haya ni lazima uwe tayari kuachana na na mawazo yoyote hasi na yatakayokuzuia kufikia adhima yako hiyo.
Mwandishi anaamini kanuni kubwa ya maisha ya furaha inapatikana kwenye kauli ifuatayo.
Wewe ni mzima wa akili Kwa kiwango kile unachoweza kusamehe bure, kusahau na kuachilia Kwa yale na vyote vilivyo kuumiza.
Hivyo kutokusamehe ni kujiweka kifungoni wewe mwenyewe na pale unapohitaji kutoka kwenye kifungo basi funguo ni kusamehee.
Mwandishi amegawa makundi manne ambayo unapaswa kusamehe na kujirudishia uhuru wako kua ni;
1.Wazazi wako
Wengi Sana wamejiweka kifungoni Kwa kushindwa kuwasamehe wazazi au walezi wao, pengine Kuna mengi kweli walipaswa kukufanyia kama kukupeleka shule na kukuonyesha upendo lakini hawakufanya hivyo, hivyo Kwa kila changamoto unayopitia unaona wao ndio sababu na kujikuta Muda mwingi hutumii kutatua changamoto zinazokukabili bali kulalamika na kubaki kifungoni.
2.Kundi la pili ni wale watu waliokuwa na uhusiano wa karibu Sana kwetu.
Pengine ulimkabidhi mtu akili na moyo wako wote na ulimwamini Sana lakini akaja kukufanyia kitu kibaya Sana.
Kama hatutofikia hali ya kusamehe tunajikuta kwenye hali ya kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo, namna ya kuondokana na hali ya chuki na ya kutosamehe watu hawa ni wakujiona wewe mwenyewe umechangia kuingia kwenye mahusiano usiyo yafahamu vizuri hivyo unapaswa kujisamehe na kumsamehe aliyekukosea pia.
3.Kundi la Tatu ni kumsamehe kila mtu.
Kila aliewahi kukukosea una kila sababu ya kumsamehe bure na kusahau.
4.Kundi la nne na la mwisho ni kujisamehe wewe mwenyewe.
Rafiki Kuna mengi Sana yalitokea kwenye maisha yako na unaona wewe ndio ulikua chanzo na unatamani ungefuta hali hiyo na kuibadili lakini haikuwezekana, hivyo Muda mwingi unautumia kujilaumu na kujiambia laiti ningelijua ningefanya moja, mbili, tatu.
Kujilaumu ni kujiweka kwenye kifungo kikubwa Sana.
Hivyo rafiki yangu msamaha ni lango la mafanikio yako, kama hutojisamehe na kusamehe wengine basi utakua huna faida duniani wala mbinguni, kote utakua umejiweka kwenye kifungo.
Tutaendelea kuona Malango mengine kwenye kila siku kama ya leo, Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment