Saturday, 10 October 2020
Pain and sickness-opportunities for virtue
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka hujambo na waendelea vizuri kabisa na Ile ndoto yako unaifanyia kazi kila siku, haijalishi unapiga hatua zipi kuifikia na changamoto zipi unazipitia hakikisha unakua kile unachotaka.
Leo tutaangalia mtazamo ambao unapaswa kuwa nao siku zote na utakufanya uwe na furaha Muda wote, mtazamo huu tutajifunza kutoka Kwa mwanafalsafa EPICTETUS
*Maumivu na magonjwa ni chachu ya kutufanya kuwa wema*
Tunapitia Maumivu ya kila aina kwenye maisha yetu, pengine ni magonjwa au changamoto mbalimbali za kimaisha, pengine unapitia Maumivu ya kichwa hicho ni kikwazo Kwa mwili lakini siyo kwenye fikra na maamuzi, ni Mara ngapi wakati Tunapitia changamoto ndogo ndipo tunaruhusu maisha yetu yote kuvurugika? ngoja nikupe kisa kifupi cha mwanafalsafa EPICTETUS.
Wakati wa Roma watu walikuwa wanamiliki watumwa na EPICTETUS alikuwa ni moja wa watumwa, kama tunavyofahamu mtumwa hana haki yoyote, pamoja na utumwa lakini aliumia mguu wake na kuwa mlemavu, Kwa usual aliishi maisha ambayo hakuwa na sababu yoyote ya kumfanya awe na furaha.
Pamoja na yote hayo falsafa ilimfanya awe na maisha bora Sana, yeye aliamini kwamba kitu ambacho hakuna mtu anaweza kutunyang'anya ni namna ya kufikiri kwetu.
Kuumwa, kuwa kwenye hatari hata kama kukikabili kifo tunapaswa kuwa na furaha na kushukuru Kwa nafasi ya maisha tuliyokuwa nayo mpaka Sasa, leo tunajifunza mengi kutoka Kwa mtumwa huyu. Yeye anaamini kukosa furaha ni matatizo binafsi na ni mtazamo wa fikra ndio unaotusumbua na siyo vitu vya nje.
Hebu chukulia mfano unaumwa homa, ukianza kulalamika kwamba umeshindwa kwenda kazini ni kuamua kujiumiza zaidi, Lakini ukiwaza kwamba ni Muda ambao utapata nafasi ya kuwa karibu na familia yako, pengine umekuwa Muda mwingi unautumia zaidi kwenye kazi kuliko familia, pengine Kwa Muda mrefu umekosa Muda wa kupumzisha mwili wako, EPICTETUS alifahamu Kuumwa mguu ni kikwazo Kwa mwili na siyo akili yake na ndio maana pamoja na yote Muda wote alikuwa mtu wa furaha pamoja na ulemavu na utumwa wake.
Je wewe rafiki yangu tatizo gani linalokunyima furaha? Amini hakuna jambo au mateso yoyote ya kuharibu namna ya kufikiri kwako labda uwe umeruhusu mwenyewe.
Nenda kaishi Kwa matumaini na jiandae na changamoto zozote zitakazojitokeza mbele yako, yapo mengi huwezi kuyabadili, jipe Muda na yote yatapita.Falsafa inatuambia hakuna watu wenye matatizo ya akili bali Kuna watu wanaojaribu kutoroka matatizo yao Kwa kuchagua kulalamika.
Asante na uwe na siku Njema rafiki yangu.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment