Monday, 12 October 2020
Mtu mwenye bahati kuliko wote babeli(The luckiest man in babylon)
Habari rafiki yangu, nakusalimu Kwa Jina la Mungu muumba wa ardhi na mbigu, tunakila sababu kufurahia pumzi yenye uhai wa kufanya mimi na wewe tukaweza kupata nafasi ya kuendelea kujifunza ili tusiwe miongoni mwa watakao angamia Kwa kukosa maarifa.
Leo tunaendele kuangalia kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON kitabu ambacho ukianza kukisoma hutamani kukiweka chini, nimejipa jukumu la kukisoma kila mwezi mpaka nihakikishe ninayaishi yote yaliyomo humu Kwa vitendo, kila ninapokisoma nakiona kipya.
*Mtu mwenye bahati kuliko watu wote babeli *
Sharu Nada mfanyabiashara ambaye alionekana nadhifu na mtanashati na alimiliki vitu vya thamani Sana, Mwandishi anatuambia huo ulikuwa muoekano wa nje ila ndani allikuwa na matatizo makubwa. Kabla hatujaendelea nimejiuliza Sana kwamba Kuna kumbe Kuna watu wengi Kwa nje tunawaona kama ni watu wenye maisha mazuri na tunatamani kuwa kama wao, Lakini kama tungefahamu undani wao Kwa namna wanavyopitia changamoto kubwa tusingeutamani utajiri huo.
Sharru Nada aliongoza msafara wake wa biashara kutoka Damascus kwenda Babeli, pamoja na kwamba njiani kulikuwa na watekaji lakini msafara wake ulikuwa na ulinzi wa kutosha hivyo kwake watekaji hawakumsumbua.
Kwenye msafara wake aliongozana na kijana aliyeitwa Hadan Gula, kijana huyu alikuwa mjukuu wa mshirika mwenzie kibiashara miaka ya nyuma, kijana huyu alifanana Sana na babu yake Kwa sura lakini siyo kwenye matendo, kwani hakupenda kazi na alipendelea kuvaa Vito vya thamani, urithi wote walioachiwa kutoka Kwa babu yake, yeye pamoja na baba yake waliuteketeza Kwa sababu hawakufahamu msingi wa fedha.
Wakiendelea na safari kuelekea Babeli Hadan Gula alimuuliza Sharru Nada, kila siku uko kwenye misafara ya kibiashara huna Muda wa kupumzika na kufurahia maisha? Ningekuwa wewe ningeishi kama mtoto wa mfalme.
Kijana akiwa kavalia heleni na bangiri aliamini kazi ni Kwa ajili ya watumwa lakini Tajiri kama Sharru hakupaswa kujitesa na chochote, wakati Hadan anaongea hayo Sharru aliwaza atawezaje kumsaidia kijana huyu kwani mtazamo alio nao kwenye fedha usingeweza mfikisha popote.
Wakiwa njiani aliona watu aliowaacha miaka 40 iliyopita wakifanya kazi zile zile, Kwa kipindi hicho aliziona ni kazi nzuri na alizozitamani lakini leo yeye ameweza kufikia utajiri mkubwa huku wale wanaofanya kazi alizozitamani Wakiwa na maisha ya kawaida.Aliamini kutoka Kwa watu wale ni kwamba wameshindwa kabadilisha mitazamo yao ndio maana maisha yao hayajabadilika.
Akiendelea kuwaza atamsaidiaje kijana yule aliyeongozana naye? Akamuuliza swali kama angependa kufahamu yeye na babu yake walikuwaje washirika kwenye biashara? Hidan anamwambia kwanini usiniambie umewezaje kutengeneza utajiri? Hicho ndio nataka kusikia.
Pengine na wewe unataka kusikia mwisho wa kisa hiki, basi usikose sehemu ya pili ya kisa cha mtu mwenye bahati kuliko wote babeli.
Nikutakie siku Njema na mungu akubariki, endelea kujifunza kupitia kurasa hizi na nenda kafanyie kazi yote unayojifunza.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment