Friday, 23 October 2020

Vitu Viwili Vya Kuwekeza Wakati Biashara Yako Iko Hatua Za Mwanzo.

Maisha yetu sisi binadamu ni ya mchaka mchaka mpaka siku yetu ya mwisho kuishi hapa duniani itakapofika, acha kujidanganya na mapumziko ya mwisho wa wiki, tafuta kitu cha kufanya kuliko kukaa na kujidanganya kupumzika wakati kila siku unalalamika. Leo tunaendelea kuangalia eneo la biashara kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI NA FEDHA kutoka kwa mwandishi mzawa Amani Makirita karibu tuwe sote. Watu wengi hufikiri wakishapata mtaji na kodi ya kulipia jengo la biashara basi wameshafanikiwa na pale mambo yanapoanza kuwa magumu ukimbilia kutoa sababu nyingi zisizo za kweli, lakini biashara yoyote ile kwenye hatua za chini au mwanzo inahitaji mambo mawili yafuatayo. *Nguvu* Hapa ni kwamba biashara inakuhitaji wewe kuweza kufanya kila kitu kwenye biashara yako, kufanya kwa ubora ambao wengine hawawezi kuufanya. Hapa ndio sehemu ambayo unajenga msingi wa biashara yako, na unafahamu kama msingi utakuwa mbovu nini kitatokea, acha kutumia muda mwingi kulalamikia mtu uliyemwajiri akusaidie, tumia nguvu zako kuhakikisha biashara inaijengea msingi imara. *Muda* Utahitaji muda ili kuweza kuikuza biashara yako kutoka chini kabisa mpaka ikawa biashara kubwa. Siyo kitu cha kulala masikini na kuamka tajiri, lazima ufahamu kwamba utahitaji kujenga wateja waaminifu wa biashara yako. Utahitaji muda wa kulielewa ki undani biashara yako kuliko mtu yeyote yule. Watu wengi kwenye biashara wanashindwa kwasababu wanaangalia matokeo ya haraka, unataka biashara ikue wakati wewe unaendelea na maisha ya kawaida na hukui. Kuamka muda ulizoea kuamka, kufuatilia mambo yasiyo muhimu kwako, kukaa na marafiki zako kupiga soga. Haya yote ni sumu kwa biashara yako inapokua kwenye hatua za mwanzo. Lazima unapoanza biashara uwe tayari kuvuruga mahusiano na watu ambao ulikuwa nao kabla hujaanza biashara, hakikisha kila siku unaweka bidii ya kujifunza namna ya kuisimamia na kuikuza biashara yako. Makala hii imeandikwa na mimi rafiki na Mwl. Kelvin Kinyaga Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment