Monday, 26 October 2020

Zingatia Haya Ili Kuikuza Biashara Yako

Tunakila sababu kumshukuru mungu wetu kwa zawadi ya maisha, kila siku tujikumbushe kwamba lipo kusudi la sisi kuwepo duniani, tutumie nafasi hii kufanya yale yatakayoleta manufaa kwetu na kwa wengine, kataa mazoea badilika. Leo tutamalizia sehemu ya mwisho ya biashara kama msingi wa mafanikio kwa kuangalia mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara yako. Rafiki kitu ambacho unapaswa kukifahamu ni kwamba mafanikio ya biashara, hayaji kama ajali au bahati, bali yanatengenezwa. Lazima ujenge misingi imara ya kuwezesha biashara yako kukua. *Msingi wa uaminifu na uadilifu* Msingi mkuu wa biashara ni mahusiano, hakuna mahusiano yanayojengwa nje ya uaminifu na uadirifu. Fanya kitu kama ulivyo ahidi, udanganyifu kwenye biashara ni sumu. *Maadili* Lazima uwe na miiko yako kibiashara, lazima ujiambie ni mambo gani hutokuja kuyafanya kwenye biashara yako. Kwenye biashara kuna mambo mengi sana ya ushawishi kama hutajijengea miiko utajikuta kila ushauri unaufanyia kazi na hapo ndio unakua mwanzo wa angako kwenye biashara. *Uvumilivu* Mafanikio kwenye biashara ni kitu ambacho hakiji kama ajali, lazima uweke nguvu na muda kufanikiwa, kama huna uvumilivu huwezi kufanikiwa kwenye biashara, yapo mengi utakutana nayo na hutoambiwa popote na yatataka kukutoa kwenye mstari hivyo kama siyo imara utapotea. *Shukrani* Acha kulalamika na kuona mambo mabaya yanatokea kwako tu, uwe mtu wa shukrani. Unaposhukuru unafunguwa Milango kwako zaidi. *Ushirikiano* Huwezi kujenga biashara kubwa peke yako, unahitaji kushirikiana na wengine. Wasaidizi wako, wateja wako na kila mtu anayefahamu uwepo wa biashara yako lazima ushirikiane naye vizuri. Ukiyasimamia haya ipasavyo nina hakika ngunzo ya biashara yako itakua imara sana na itakuwa vigumu kuvunjika. Kitu cha kuondoka nacho kwenye somo hili ni kwamba tabia za mfanyabiashara ndio kikwazo kikubwa kwenye biashara na kwa asilimia chache ndio hutoka nje ya sababu hii. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0712161251 /0763766944

No comments:

Post a Comment