Sunday, 25 October 2020
Na Hii Ndio Kanuni Ya Kuingia Kwenye Biashara
Hongera sana rafiki yangu, ni juma lingine tumelianza, sina shaka kwamba umeshapanga yale yote unayotaka kukamilisha kwenye juma hili na leo yapo ambayo umejipanga nayo kuyatekeleza, basi hakikisha hakuna lolote lisilo la msingi litakalokuwa sababu ya kuharibu mipango yako, lakini pia jiandae kwa changamoto zozote zinazoweza jitokeza na kazikabili.
Leo pia tunaendelea na mfululizo wa somo kuhusu biashara, kitabu chetu ni kile kile cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na Dereva wetu aliyetuandikia kitabu Dr. Makirita Amani. Karibu.....
Rafiki ni wachache sana kati ya wanaotamani kuingia kwenye biashara ndio wanafanikiwa kuanzisha biashara, yaani tuseme kati ya watu 100 wanaotamani kuanza biashara ni mmoja pekee ndio anafanikiwa kuanzisha biashara. Je kwanini watu wanaishia kutamani kuingia kwenye biashara na hawaingii?
Mwandishi anasema Kanuni ya kuanza biashara ni *just do it*. Acha kujipa maswali mengi yasiyo na tija kuhusu biashara gani ufanye na je ni changamoto zipi nitakutana nazo, wewe unachopaswa kufanya ni kuanza biashara na kisha ukishaanza ndio utaanza kufanyia kazi changamoto utakazokutana, anza na mteja mmoja kisha mtumie mteja huyo mmoja kuongeza wateja wengine.
Rafiki tafiti zinaonyesha biashara kubwa ambazo watu wengi wanamiliki siyo biashara walizo anza nazo, bali kwa kuboresha mawazo yao ya biashara ndio kumewafikisha kwenye kazi za juu za biashara.
Mwandishi wa kitabu anasema mafanikio kwenye biashara ni kitu cha kujaribu na kushindwa, mpaka pale unapoipata njia yako halisi, na kuitumia njia hiyo kukua zaidi na kufikia uhuru wako kifedha.
Kama una mpango wa kuanza biashara acha kujipa maswali na majibu bali nenda kaanze leo, anza na popote na chochote kisha weka nguvu na muda kuikuza biashara yako. Muhimu ni kujifunza na kuwa tayari kubadirika.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment