Sunday, 18 October 2020
Mlango wa ufahamu
Habari za wakati huu rafiki yangu, bilashaka umeamshwa salama na uko tayari kwenda kuyakabili yale yote yaliyopo mbele yako, hongera na mungu akutangulie......
Leo tutakwenda kuangalia mlango mwingine utakao utumia kufanikiwa au kutofanikiwa kama hautoutumia mlango huo.
Sehemu iliyopita tuliweza kuona Kaka yetu ULOMI kupitia KITABU chake cha yajue Malango yanayoweza kukufikisha au kudidimiza maisha yako KIROHO, KIUCHUMI NA KIHISIA. Tuliweza kujifunza mlango wa msamaha Kwa kina na bila Shaka kama ulilielewa vizuri somo lile umejiponya, kwani kusamehe ni kujitibu mwenyewe.
Leo tunakwenda kuangalia mlango mwingine , MLANGO WA UFAHAMU, tunateseka na mambo mengi Kwa sababu hatuna ufahamu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yetu.
Neno la mungu linatuambia hivi;
Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, Kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka saying. *Daniel 9:2*
Kumbe kupitia neno hili tunaona umuhimu wa vitabu kwenye kutupatia ufahamu, Mwandishi anatumia neno UNDERSTAND Kwa kulinyambua na kupata neno Under lenye maana ya chini ya! Stand lenye maana ya simama na linapokua pamoja Lina maana KUJUA ULICHOSIMAMIA au sababu ya ulichosimamia.
Hivyo kama utajikuta umekwama na lolote Kwa kuchukua vitabu na kusoma utapata uelewa mpana Sana, usijiulize nianze na kitabu kipi? Uwe mkristo biblia ipo anza nayo ina kila kitu. Kama ni Muslim Quran ipo itakupa uelewa wa kutosha, kwenye vitabu Kuna siri nyingi Sana, ukiweza kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu nina hakika hutobaki kama ulivyo.
Mwandishi anaendelea Kwa kusema kwamba ukishajifunza kutoka kwenye vitabu na ukaunganisha na hekima ya kutenda yale uliyojifunza unapata ufahamu, hili linatupa tafsiri kwamba unaweza kusoma maelfu ya vitabu lakini kama huna hekima ya kutumia maarifa hayo basi hapo hakuna ulichofanya, kocha wangu anaita kuchafua akili.
Jiulize kabla watu hawajafahamu tiba Kwa magonjwa yaliyotukabili je ni watu wangapi walifariki?
Kwanini ufahamu ni lango?Ujinga na upumbavu ni ngome au vizuizi vinavyofanya watu wasifikie kiwango fulani cha maisha, wewe kuishi maisha ya dhiki na taabu siyo mpango wa mungu, kubaki vilevile kila siku siyo mpango wa mungu, hebu Anza kufungua vitabu na utoke huko.
Mwandishi ametumia mifano mingi ya kutufungua na kututoa kwenye giza la Ujinga na kutufanya waelewa, Kwenye injili ya Yohana mlango ule wa nane yesu anasema "mkikaa katika neno language, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli ;tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. *Yoh.8:31-32*
Rafiki Anza leo kujiwekea utaratibu wa kujifunza na utaona namna ulivyokuwa kifungoni Kwa Muda mrefu bila sababu wakati umezungukwa na maarifa ya kila aina.
Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na mungu akubariki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment