Thursday, 8 October 2020
Msingi muhimu wa biashara unaopaswa kulielewa.
Hongera Sana rafiki yangu Kwa kuchaguliwa tena kuifikia siku ya leo, wapo wengi walilala na mipango mizuri ya kuifanya leo lakini hawakuamka, wewe umefanikiwa kuifikia leo je ni yapi umepanga kufanya? Kama ni mipango Ile Ile ya kila siku je umejiandaa kupata matokeo tofauti? Nenda katekeleze zaidi ili uitendee haki siku hii.
Kila kitu ambacho tunakifanya kinaanzia na msingi, na ndio maana Mwandishi wa kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA ametuandalia masomo haya akiamini kwamba ukiyafuata utakua imara kwenye fedha pamoja na changamoto zake.
Ili nyumba isiweze kudondoshwa na tetemeko au upepo inahitaji msingi imara, vivyo hivyo na kwenye biashara unayofanya kama biashara haina misingi inayosimamia basi kudondoka ni hakika.
Je biashara imara inahitaji misingi gani?
Msingi wa kwanza wa biashara yoyote ni THAMANI, kwani tulishajifunza kwamba ili uweze kupata fedha lazima ubadilishane thamani na mwingine, hivyo kabla hujaanza biashara jiulize ni thamani gani nitawapa wengine Kisha wanipe fedha zao? Ni kipi nitatoa kwao wakaamua kunipa fedha zao walizozitafuta Kwa shida?
Siri nyingine ambayo ni msingi wa biashara yoyote ni KIPI NAFANYA NA WENGINE HAWAPO TAYARI KUKIFANYA kwenye biashara lazima uwe tofauti na wengine, lazima mteja apate kitu kwako ambacho kwingine siyo rahisi kukipata, kama unafungua biashara Kwa sababu umepata mtaji na unafanya kawaida kama wengi wanavyofanya basi utapata matokeo kama wengi wanavyopata Mwandishi anasema kama mteja anaweza kupata Kwa wengine kile anachokipata kwako, ukweli ni kwamba huna biashara, upo katikati ya kelele. Na kama umeamua kuingia kwenye biashara ambayo kila mtu anafanya basi ifanye Kwa namna tofauti na wengine wanavyoifanya.
Ipo Siri nyingine kubwa Sana kwenye biashara ambayo Mwandishi anasema huwezi isikia popote, biashara zote zenye mafanikio Zina sifa hiyo, Sifa hiyo ni KUHODHI biashara hizo au sehemu ya biashara hiyo, kama biashara unayofanya haitawali sehemu kubwa ya soko basi biashara hiyo ukuaji wake unakuwa mgumu Sana. KUHODHI huko isiwe ni Kwa kuwakandamiza wengine bali unapaswa kuwa bora zaidi ya wengine.
Rafiki kwenye biashara yako nenda the katoe thamani kubwa, jitofautishe na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama unayofanya wewe, na hodhi sehemu ya soko la biashara yako.
Asante Sana rafiki yangu nikutakie siku Njema na uwe na siku Njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0712161251 /0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment