Monday, 20 July 2020
Tiba ya tano;Fanya sehemu unayoishi kuwa uwekezaji wenye faida.......
Siku nyingine, Nina amini kumekucha salama na uko tayari kuendelea kujifunza,kwani hakuna siku utajiambia huoni umuhimu wa kula, vivyo hivyo nakujifunza,kwa kuwa unaendelea kuishi basi una Kila sababu ya kuendelea kujifunza namna ya kuishi bora zaidi....
Kutoka kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tunaendelea na tiba za kutunisha mifuko yetu, baada ya kujifunza tiba zilizopita na sasa tuangalie tuba namba tano ambayo ni _Make of thy dwelling a profitable investment_
Mwandishi anatuonyesha baada ya kufuata tiba nne zilizopita na kutenga sehemu ya kipato na kuwekeza basi lazima fedha zitaanza kuongezeka na hapo utahitaji kuwa na nyumba yako mwenyewe, anasema hakuna familia yenye furaha kama haimiliki nyumba yake,hivyo tiba ya tano ni kuhakikisha unamiliki nyumba yako na hapo utatumia fedha unayolipa kodi kuwekeza kwenye maeneo mengine na hapo watoto wako watakuwa huru na kufurahia maisha.
Rafiki ni ukweli usiopingika kwamba kuwa na kwako kunaleta Uhuru na furaha lakini kama utaanza na tamaa ya kujenga nyumba yako kabla ya kuwekeza sehemu zingine zinazozalisha kwa haraka basi utakuwa kwako katika namna ya mateso ya kulipa madeni kwa kipindi kirefu sana, mwandishi anashauri hata kwa kukopa na kulipa deni pole pole siyo vibaya kama uwekezaji wako unaendelea kukua na ukalipa taratibu mkopo wako.
Angalizo, lazima uwe na hakika wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba yako hakuta athiri maeneo yako ya uwekezaji, wengi sana imeonekana wanapoanza ujenzi wanachukuwa sehemu za mitaji yao na kujengea nyumba zao na kisha kujikuta wanaanza upya na wakati huo gharama za maisha zinakuwa zimeongezeka.
Hivyo rafiki tambuwa kwamba utahitaji kuwa na kwako ili uwe huru na tumia nyumba yako kama sehemu ya uwekezaji, panda miti ya matunda, fuga na kama eneo ni kubwa weka hata bwawa la samaki na hilo litaongeza thamani ya nyumba yako na kukuinua ki uchumi na hivyo kufurahia maisha, usikubali nyumba yako kubaki na mapambo na maua pekee itumie kuwekeza. Asante na nikutakie siku njema.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment