Sunday, 26 July 2020

Hivi ndivyo unavyoweza kunoa siraha yako....


Habari za wakati huu rafiki, hongera kwa jumapili nyingine, siku ambayo tunamalizia wiki iliyopita kwa kutathimini yale tuliyofanya na wapi tumefanya vizuri na yapi hatukufanya vizuri kwenye wiki lililopita ili wiki hii tuweke bidii na kuwa bora zaidi......

Leo tuangalie maneno ya mwana falsafa *EPICTETUS* akitaka tufahamu kipi tunaweza kufanya na tukawa bora zaidi.

_"Even if I lack the talent, I will not abondon the effort on that account...., we do not abondon any discipline for despair of over being the best in it."_

Kauli hii inatuaminisha kwamba vipo vitu vinavyoweza kuzidi vipaji na  elimu,ukivitumiaukivitumia unaweza kufanya makubwa na hiyo ndio siraha inayoweza tumiwa na Kila mtu.

*Weka kazi*
Watu wanaweza kukuzidi Kila kitu lakini wasikuzidi kuweka kazi, hakikisha Kila siku unafanya zaidi ya Jana, mwanzo utaonekana kama umechanganyikiwa na matokeo hayataonekana lakini ukiweka kazi zaidi lazima utafikia ukuu na utawazidi walio kuzidi elimu, wenye vipaji vikubwa na utabobea zaidi yao kwenye hilo unalofanya, tafiti zote duniani zinaonyesha hivyo, angalia waliofanya makubwa wana elimu ya kawaida na hawana vipaji vya kutisha ila walihakikisha wanaweka kazi kweli kweli.

*Nidhamu*
Ukiwa na nidhamu kwenye kidogo unachofanya  kwa kuhakikisha unakiheshimu lazima kitakupa zaidi ila usipoweka nidhamu na kudharau hutafika popote hata ungekuwa na kipaji kizuri namna gani, ukiona mtu anafika mbali ni kwasababu ameheshimu kile alichonacho, unapokuwa na kidogo ukakithamini na kuhakikisha unakuwa mtu wa kuthamini ulipo napo patakuonyesha njia ya juu zaidi, haijalisha unataka kufika wapi lazima uanze na hapo ulipo na kuweka nidhamu ya Hali ya juu.

Kwenye kisima cha maarifa msingi wetu Mkuu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na tunaishi kwa vitendo jambo hili,hatuangalii uko wapi lakini kwa kuweka kazi na kujituma huku nidhamu ikiwa juu ni hakika kile tunachokitafuta lazima upate kile unachokitaka, dunia haitakupa vitu kwa urahisi lazima ufuate kanuni za asili ndipo dunia ikupe zaidi, ardhi ukiipa mbegu inakupa zaidi, kadri unavyopaipa mbegu zaidi ndivyo inakupa mazao mengi zaidi, nidhamu ya palizi na kuondoa magugu ndivyo unavyopata mazao zaidi, uvivu ni magugu kwenye kazi,kiburi ni magugu,dharau ni magugu kwenye mafanikio.Ondokana na vitu  hivyo na utakuwa vyovyote unavyotaka.

Asante na nikutakie siku njema katika kuliendea wiki linaloanza kesho, katumie haya tunayoambiwa na mwanafalsafa EPICTETUS na kisha utaona matokeo utakayopata.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment