Saturday, 11 July 2020

"Hapana" na "Samahani",Sitaweza........


Habari za wakati huu rafiki, muda ni rasilimali muhimu sana kwenye maisha yetu na Kila mmoja wetu kapewa muda Sawa na mwingine lakini wengine wamechaguwa kujipa sababu ya kwamba muda ni mchache kwa kufanya vitu visivyo na maana.......

Kila nikikumbuka swala la muda siwezi kukumbuka kanuni ya PARETO ya 20/80 na hapo ndipo naacha kujificha kwenye kichaka cha kwamba muda hautoshi, kanuni hii inatuambia kwamba ni asilimia 20 pekee ya vitu tunavyofanya ndio vinaleta matokeo yenye manufaa kwetu na 80 ni mambo yasiyo na maana kabisa na yanapoteza nguvu na muda wetu.

Watu tunaishi kwa kujipa matumaini hewa kwa kufanya mambo Yale yale tuliyozoea kufanya,Kila siku unajiambia umekosa muda hata wa kusoma kurasa tano za kitabu na kujifunza, lakini haipiti siku hujaangalia taarifa ya habari kuanzia inaanza mpaka utabiri wa hali ya hewa, ukitoka hapo utahitaji kuangalia tamthilia fulani nzuri unayoifuatilia na siku ukiikosa unaona kama umekosa sehemu fulani ya maisha yako, lakini jiulize ni tamthilia ngapi zimepita tangu umeanza kuangalia? Ni ipi ilikupa funzo linalokuingizia fedha? Iliyokupa hamasa ya kuanza biashara? Ni taarifa gani ya habari umekupa manufaa? Habari zote muhimu kwako zitakufikia bila kuzitafuta, lakini mtu huyu akitoka kwenye TV anakwenda kitandani na anaamka saa moja na kukimbizana kuelekea ofisini, akifika ofisini busy na simu yake, hivi ndivyo tunavyoishi na kuendelea kujipa matumaini ya kwamba ipo siku mungu atajibu maombi, maombi yapi hayo? Ingekuwa maombi bila kazi unafanikiwa hakuna ambaye angeenda kazini.

Baada ya kutafakari namna tunavyooendesha maisha yetu ndipo nikakubaliana na mwanafalsafa Seneca kwamba "siyo kwamba hatuna muda au muda ni kidogo bali ni mwingi mpaka tumeamua kuupoteza" kumkuta mtu akisema napoteza poteza muda ni kawaida na ndio maana anakubali Kila kitu anachoambiwa, anaweka matumaini hewa kwenye Kila fursa inayojitokeza, ukiambiwa fuga kwale wanalipa unafuga, kesho biashara ya chakula upo, keshokutwa biashara ya nguo upo lakini Kila unachojaribu ukiona kina ugumu fulani unaacha na kukimbilia fursa nyingine na hapo ndipo wanafalsafa wanatuambia maneno haya chini.

"No" and "sorry",I can't", Neno hapana,samahani na siwezi kufanya yakatumike kwenye mambo mengi ambayo hayana tija kwako,ondoa mazoea na ishi kwa kusudi na Fanya yale yanayotoa msaada kwa wengine na kwako na achana na mambo yasiyo muhimu, chagueni siku za kuzima TV kama unaona huwezi kuachana nayo kabisa na tumia muda huo kukaa na familia yako kuzungumza hatima na ndoto zenu.

Rafiki nenda kayaishi haya Mara moja na utajishukuru siku moja, siyo rahisi kuondoa mazoea lakini nimeshakuambia vitu vinavyokurudisha nyuma nenda kaviweke kwenye matendo.

Makala hii imeandikwa na Mimi Mwl.Kelvin Kinyaga, unaweza kuendelea kujifunza kwa kubonyeza maandishi haya hapa chini.


https://kinyagakelvin.blogspot.com

Kinyagakelvin162@gmail.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment