Friday, 31 July 2020
*Ustawi wa fikra* Wednesday 30,July 2020. _Hivi ndivyo wajanja wanavyoishi baada ya ongezeko la kipato chao_ Habari za wakati huu rafiki yangu, hongera kwa siku nyingine na tuna Kila sababu ya kumshukuru mungu..... Leo kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA tutaangalia dhana ya vipi utaweza kuzuia matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka. Rafiki kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba tabia moja unayopaswa kuwa nayo itakayokufikisha kwenye utajiri ni kuhakikisha matumizi yako ni kidogo kuliko kipato chako, kama kiasi unachopata unakitumia chote sahau kuhusu mafanikio. Mwandishi wa kitabu anasema kitu ambacho anakishangaa kwenye fedha hasa kwa waajiriwa ni hiki, japokuwa watu wanatofautiana vipato na mishahara wanayolipwa lakini Kila inapokaribia mwisho wa mwezi aliyepokea milioni moja na aliyepokea laki moja wote wanakuwa wameishiwa na kinachosababisha hili ni watu kuongeza matumizi Kila fedha inapoongezeka na kusababisha wawe watumwa kwenye fedha maisha yao yote lakini wajanja kwenye fedha hawaishi hivyo. Mwandishi anatoa mfano,pale kipato chako kinapoongezeka, jipe muda kidogo wa kuendelea na maisha yale ya kipato cha chini,tumia ongezeko hilo la kipato kuzalisha kipato cha zaidi. Baada ya kipindi cha miezi sita tangu upate ongezeko la kipato ndipo unaweza kuongeza matumizi yako kufikia nusu ya ongezeko na nusu kuendelea kuzalisha. Rafiki uwe umeajiriwa au kujiajiri au biashara hakikisha unakuwa mjanja kwa kuhakikisha huongezi matumizi yako Mara tu baada ya kuongezeka kipato chako. Asante na Leo nimekupa ujanja huu, nenda kautumie,biashara yako haitakua kama hutumii ujanja huu. Kinyagakelvin162@gmail.com https://kinyagakelvin.blogspot.com 0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment