Thursday, 20 August 2020

Ustawi wa fikra Thursday 20,August 2020 _Madeni ni utumwa_ Habari za wakati huu rafiki, Leo tuangalie elimu ya fedha kipengere cha madeni.... Kwanza kabisa mwandishi ameanza na kauli kwamba Madeni ni utumwa... Kauli hii inakera lakini ina ukweli ndani yake, watu wengi sana wana amini hawawezi kufanikiwa bila ya kukopa, pamoja na mikopo wanayochukua bado maisha yanakua magumu zaidi, wengi hawafahamu ni wapi wanakosea, Elimu ya fedha ndio suruhu ya tatizo hili, lazima ufahamu mkopo upi ni mbaya na upi ni mzuri kwako ndio uchukue. Madeni ni utumwa kwasababu anayekudai anakua na usimamizi mkubwa juu yako. Kile ulichowekea kama dhamana kinaweza chukuliwa muda wowote. Madeni ni utumwa kwasababu unawafanyia kazi wanaokudai, Kila unapofanya bidii kwenye kazi,malipo unayopata unatumia kulipa deni. Watu wengi wanajiambia isingekua mikopo wasingekuwa hapo walipo na mikopo imewasaidia, hili linakuja kwasababu wengi wanao chukua mkopo hawapigi hesabu za kiasi gani wanalipa kwa mkopo waliochukua. Pamoja na yote hayo mwandishi anatuambia madeni mengi ni utumwa wa kujitakia. Asante na siku njema.

No comments:

Post a Comment