Sunday, 12 July 2020

Nini utakosa kwa kufanya nyumba kuwa uwekezaji wako wa kwanza?


Hongera sana rafiki yangu kwa kuweza kuanza wiki yako kwa kujifunza, ukifanya kujifunza kuwe muhimu kama chakula Nina hakika hapo ndipo utafahamu kuishi ni nini na nikukaribishe kwenye ukurasa huu wa USTAWI WA FIKRA tujifunze pamoja.......

Wiki iliyopita tuliangalia ni kwanini nyumba yako ya kuishi siyo Mali inayozalisha (assets) na kwanini elimu ya matumizi ndio muhimu kuliko elimu ya kutafuta fedha, wengi tunaweka bidii kutafuta fedha lakini kadri tunavyozipata ndivyo tunavyojitenga nazo, ni kwasababu hatufahamu tuwekeze wapi ili fedha ziweze kutuzalishia zaidi.

Baada ya wiki iliyopita kujifunza kwamba nyumba ya kuishi siyo asset nilipata maswali mengi sana na wengi walionyesha kulishangaa hilo kwasababu ni imani ya wengi kwamba nyumba zao za kuishi ndio asset zao kumbe hakuna kitu kama hicho, Leo tutaendelea na chambuzi kutoka kwenye kitabu chetu cha Rich dad, poor dad.

Kwanza napenda ufahamu kwamba mwandishi wa kitabu hiki ni muwekezaji mkubwa wa real estate, kwa kununua na kujenga nyumba,pamoja na kuziuza hivyo anafahamu matatizo mengi yanayotokana na watu kukimbilia kujenga nyumba au kuwekeza kwenye nyumba kabla ya kufanya uwekezaji mwingine.

_Haya hapa ndio mambo matatu unayokosa kwa kuwekeza kwenye nyumba_
1.Kwanza unapoteza muda;kinachofanya tunapata shida tulio wengi kwenye fedha ni uhakika, hatutaki kufanya biashara kwasababu tunataka uhakika wa kulipwa mshahara, na hili ndilo linatufanya tuogope kufanya uwekezaji mwingine tukimbilie kuwekeza kwenye nyumba, hivi hao matajiri unaowatetemekea ulishawauliza walianzaje? Chukuwa gharama ya mitaji walio anza nayo kisha ipime na thamani uliyojengea nyumba yako na riba uliyolipa benki kisha ona kama ungechaguwa kuwekeza fedha hiyo kwenye uwekezaji mwingine ungekuwa wapi?

2.Kupoteza mtaji; Ungeweza kutumia fedha uliyojengea nyumba kama mtaji wa kuwekeza maeneo mengine lakini unajipa jukumu la kupeleka fedha zako ambazo umekopa kwa riba kubwa kwa kukopa, hapo unakuwa umeamua kufukia fedha zako.

3.Kukosa elimu; Ukianza kuwekeza kwenye nyumba ina maana utasubiria mpaka deni benki liishe ndio uanze kufikiria kuwekeza maeneo mengine, hapo utakuwa umechukuwa muda wako wa kupata elimu ya kuwekeza maeneo mengine kwasababu huna fedha za kuwekeza huko na ukajifunza, kwani biashara zina faida nyingi na thamani yake inakuwa haraka lakini hatua za mwanzo ni ngumu na zimewaangusha wengi na hilo ndilo linawapa wengi hofu ya kuwekeza huko, ni ukweli kama huna elimu ya biashara unayotaka kufanya lazima upoteze fedha zako.

Hilo ndilo mwandishi anasema watu huendelea kuishi kwa chanzo cha mshahala na kupoteza elimu ya kujifunza kwenye uwekezaji, kwani hakuna elimu inayoizidi elimu ya kufahamu namna fedha itakavyokufanyia kazi na siyo wewe kuifanyia kazi fedha. Madeni yanaongezeka kwa kuongeza matumizi na siyo kwa kupata kipato kidogo.

*Fahamu maeneo ambayo masikini anafanyia kazi*
1.Mwajiri-Masikini yeyote lazima amfanyie kazi mwajiri na kadri anavyoongeza bidii kwenye kazi ndivyo mwajiri wake anavyonufaika, tambuwa hakuna anayekuajiri ili utimize ndoto zako bali ndoto zake yeye mwajiri kupitia bidii na ujuzi wako.

2.Serikali-Kadri unavyoongezewa kipato na mwajiri ndivyo na serikali wanavyopokea Kodi kubwa kutoka kwako, hivyo muda wako umempa mwajiri na fedha zako unailipa serikali kupitia kodi, Fanya tafiti mwajiriwa namfanyabiashara nani analipa kodi kubwa.

3.Unaifanyia kazi benki-Masikini wengi hupenda kukopa na kuwekeza maeneo ambayo hayazalishi kama kujengea nyumba na kunua viwanja na hili linawafanya kufanyia kazi benki kwa maisha yao yote.

Pengine rafiki ni miongoni Mwa watu unaye fanyia kazi maeneo hayo na sasa umefahamu, hebu kumbuka ile kanuni ya mashimo, ukijikuta kwenye shimo acha kwanza kuchimba na angalia unatokaje, Je upo kwenye shimo la madeni basi nafasi ni hii ya kujifunza na kuondoka huko.

Majina niliyopewa na Wazazi Wangu ni Kelvin Kinyaga. Mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya fedha na namna fedha itakavyonifanyia kazi. Karibu twende pamoja.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment