Monday, 13 July 2020
Tiba ya nne kwa mifuko iliyo sinyaa.....
Tumshukuru mungu wetu Kila tunapopata bahati kuianza siku tukiwa na afya tele, nikushukuru wewe rafiki yangu unayeanza kuona umuhimu wa kusoma makala hizi, hiyo ni hatua ya kwanza, nikupongeze wewe unayechukuwa hatua Mara moja na kufanyia kazi masomo haya, siwezi kuwa mjinga kukupatia masomo haya ikiwa sina uhakika kwamba yatakusaidia, karibu tuwe sote....
Leo kutoka kwenye chambuzi za kitabu chetu pendwa cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON tutaendelea kuangalia tiba kwa mifuko iliyosinyaa, kati ya tiba saba tutakazo jifunza tatu tumeshazichambuwa, tumeshafahamu kutenga asilimia kumi ya Kila kipato chako na kujilipa wewe kwanza, tumeshafahamu umuhimu wa kudhibiti matumizi yako,tukaona namna ya kufanya akiba yako izae zaidi na sasa tunakwenda kuangalia tiba ya nne LINDA HAZINA YAKO ISIPOTEE.
Utakapoanza kufanikiwa basi ndio unapaswa kuwa makini zaidi, kwani wengi ndipo huanza kuona kama changamoto nyingi zinajitokeza lakini ukiangalia kwa makini changamoto hizo zinasababishwa na mafanikio kidogo uliyopata. Na Arkadi alianza somo la nne kwa kuwaeleza kama hutolinda fedha zako basi zitapotea.
Sehemu kubwa inayowaangusha wengi ni pale wanapoanza kuona mafanikio ndipo Kila mtu kuwafuata na kuwapa ushauri wa wapi awekeze kutamlipa, na Mara nyingi humshauri kuwekeza ili apate faida ya haraka.Mwandishi anasema kama hutofikiri kwa makini utapoteza fedha zako.
Arkadi aliwauliza, Je ni vizuri kushawishika na faida kubwa wakati mtaji wote unaweza kupotea? Nadhani jibu ni hapana. Msingi wa kwanza wa uwekezaji ni usalama wa mtaji wako unaowekeza. Utapaswa kuweka umakini mkubwa na kuchunguza sehemu unayotaka kuwekeza fedha zako. Acha kutamanishwa na kupata faida kubwa kwa haraka.
Arkadi akitoa somo hili aliwakumbusha uwekezaji wake wa kwanza alivyopoteza kwa kutoweka umakini sehemu anayowekeza na akapata hasara hivyo aliwaeleza kwamba wasifanye makosa aliyofanya yeye.
Omba ushauri kwa wazoefu wa fedha na Fanya busara ndio ikuongoze katika uwekezaji, Kocha wetu huwa anapenda kutushauri kwamba kabla hujapokea ushauri wa mtu jiulize hiki anachonishauri kimemsaidiaje yeye kufika hapo alipo? Au amejifunza kwenye kitabu gani ili na Mimi nijifunze niweze kufanikiwa kwenye hili? Ukishapata majibu ndipo fanyia kazi ushauri huo.
Rafiki huwa tunapenda kupokea ushauri kwa Kila mtu, hasa watu tunao waheshimu, hata kama wamefanikiwa kifedha, swali la kujiuliza ni je hiki anachonishauri ndicho ambacho yeye kafanya na kufanikiwa? Au ndio ushauri wa madini kutoka kwa mfyatua matofari?
Nina imani unakwenda kufanyia kazi masomo haya, asante na uwe na siku njema rafiki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment